Siasa za utakatifu!

Siasa za utakatifu!

Baada ya hapo huyo mleta taarifa aliuwawa ?
Nitanenda kusoma hiyo 2 Samweli 2
Nitakuletea mrejesho nimeona nini

Asante kwa kifungu hicho
Yaa! aliuawa, soma mpaka sura ya tanno yupo na mwingine alimuua afsa wa jeshi la marehemu Sauli nao akasema wauawe baada ya kutoka kwenye maombi ya mfungo. Pale Kuna siasa ya utakatifu imetamalaki
 
Asante sana😍
 
Unahisi watawala au viongozi wengine wa siasa wameacha mlango wazi kukoselewa ikiwa wanaenda kinyume na maadili na sheria ?
Au wamevaa vazi la utakatifu ?
Au wakosoaji wanaonekana kuvuka mipaka ?
kwa hapa nchini hata maeneo mengine dunia hilo linaweza kutofautiana mfumo wa kisiasa, taasisi zilizopo, na hata utamaduni wa jamii husika. Katika mazingira yenye taasisi imara kama nchi za wenzetu walio na utamaduni wa uwajibikaji, viongozi mara nyingi hukubali kukosolewa kwa sababu kwa wenzetu ukosoaji huonekana kama sehemu ya kuboresha utendaji na kuimarisha imani ya wananchi.

ila sasa kibongobongo changamoto hutokea pale ambapo viongozi kama vile Rais wa nchi au wafuasi wao ambao huwa wanaitwa nyumbu hujenga taswira kwamba viongozi hawawezi kukosea, au ukosoaji wowote unaonekana kama shambulio binafsi, ukosefu wa heshima, au usaliti. Hapo ndipo inaweza kujitokeza kile ambacho kwenye huu uzi wetu umekiita “siasa za utakatifu,” ambapo hadhi ya mtu inaanza kuwa muhimu kuliko mjadala wa hoja inayozozaniwa na uwajibikaji. kwa hiyo auntie yangu, ni muhimu kutambua kwamba ukosoaji wenyewe pia una mipaka ya maadili na sheria. Ukosoaji wenye hoja, ushahidi usio na mashaka na heshima huchangia demokrasia yenye afya, lakini matusi, uzushi, taarifa zisizo sahihi au uchochezi vinaweza kuharibu maana nzima ya mjadala.
Kwa hiyo, swali lingine muhimu si tu kama viongozi wamevaa “vazi la utakatifu,” bali pia kama jamii yetu ina nafasi salama ya kuuliza maswali, kutoa maoni tofauti, na kujadili hoja kwa uwazi na heshima bila hofu ya kutekwa na uvccm
 
Hakika hakika ni kweli tupu

Mpwa wangu mzurii ndio maana nakupenda namna unajenga hoja kwa utulivu

Nimekuelewa mnoo tena sana

Sasa ni nani muasisi wa huu utakatifu ambao ki msingi sio mzuri kabisa kwa ustawi wa taifa

Huu utakatifu na uspesho ambao baadhi ya watawala na baadhi ya wanasiasa wanaojivika utakomeshwa na akina nani?

Maana wanaopinga huu utakatifu na us pesho naona baadhi yao nao wakiingia
Kwenyee huu huu mtego 🤔

Tunaona watu wana acha kujenga hoja na kupokea maoni tofauti

Na hili swala bila kuficha wala kumngunya maneno sio chama tawala wala upinzani hawa watu hawataki kupata maoni tofauti na misimamo yao je hii si ni dalili ya ubabe na kuvaa hili vazi la utakatufu kwa wote ?

Umesema upande wa chama tawala wanatumia UVCCM kufifisha wanaotoa maoni haya tuseme ni kweli

Je Huku upande wa upinzani nako ukienda kinyume na maoni yao inakuaje ni matusi kwa sana si ndio

Je wanatumia matusi kwa sababu huenda labda hawana power
Kama ilivyo kwa CCM

Kwa maana wangekua na power wangekua like UVCCM

Mada hewani ni utakatifu kweny siasa✍️
 
Ni kweli kwamba wenye mamlaka wanaweza kutumia nguvu za dola au taasisi kuwanyamazisha wakosoaji, lakini pia ni sahihi kukosoa wafuasi wa upinzani wanapotumia matusi au kuwashambulia wanaotoa maoni tofauti. Makosa yakifanywa na upande wowote yanapaswa kukemewa kwa kipimo kilekile.
Mwisho wa siku, hatupaswi kuhukumu kwa misingi ya nani anafanya, bali kwa misingi ya kanuni. Ikiwa tunapinga ubabe, basi tuupinge bila kujali unatoka CCM, upinzani, au mtu mwingine yeyote.
 
Naunga mkono ila kuna sehemu hujajibu

Wewe umesema kwamba CCM wanatumia kundi la UVCCM kunyamanzisha sauti za wanaohoji

Ni kasema tufanye ni kweli wanafanya hivyo

Swali langu nikakuuliza 👇

Hawa wapinzani wao wanatumia matusi kuwanyamanzisha kuwa kebehi wanao hoji au walio kinyume na mawazo yao

Je hii ni kwa sababu hawana option nyingine?

Je wanatumia matusi kwa sababu hawana power kama walionayo CCM?

Kwa maana matusi ni silaha ya mwisho
Kwamba wangekua na nafasi ,Power kama ya CCM na wao wangefanya yale yale ?
 
Mbona it is very obvious, hawa wanaotoka vyama vingine nje ya CCM nao wangekuwa na mamlaka wangefanya yaleyale ya Ccm au wangefanya mabaya zaidi.
Kwa mfano kwa sasa kama tunavyoona hawana nguvu ya kudhuru mwili ila wanadhuru hisia kwa kutumia matusi, wakizidiwa sana wanatumia block option.

Mtu anayeku block ili msi interact, siku akipata power atakuweka gerezani ili usimsumbue.
 
Huu ndio ukweli na uhakika hili taifa linataka zaidi ya upinzani
Taifa linatakiwa kutakaswa
 
Uhalisi ni kwamba haliwezi kutakasika.

Kumbuka wakati ule Chadema wale waliokuwa viongozi wakuu wa kiume, karibia wote wake zao walikuwa bungeni kwenye viti maalumu.

Unafikiri hawa siku wakishika dola, watashindwa kuwapa teuzi za kiserikali wajomba zao na watoto wao?
 
Taifa haliwezi kutasika si ndio?
Kwa sababu taifa limejaa watu wenye fikra zile zile?

Tulete watu wapya?
Wakulitakasa kutoka wapi sasa?

Au tu format bongo zetu?

Hapo mwisho akuunga mkono
Watu wachama tawala ukiongea kitu kikawagusa kwa maumivu wataona wewe ni upinzani

Watu wa upinzani nao ukiongea wasio taka kusikia unaitwa chawa mindset zile zile 🙌

Na ndio maana ni kasema tatizo sio upinzani wala CCM tatizo lipo kwenye maslahi mpwa
 
Ndio tatizo ni cash.

Na kwa hapa Tanzania tutaendelea tu kushuhudia mabadiliko madogo madogo, hakutakuwa na issue serious za kuhakikisha malalamiko yaliyopo sasa yanakoma.
 
Sawa aunt karibu tena
 
Kama Title inavyosema

Wengi tuna amini kuwa utakatifu ni hali ya usafi maadili mema na kutokuwa na dosari

Lakini je, nini hutokea pale ambapo dhana ya utakatifu inapohusishwa na siasa

Mimi naamini hasara zake zinaweza kuwa kwa kiwango kikubwa sana

Pale ambapo mtu au kundi la watu linaonekana kuwa watakatifu, kiasi kwamba jamii inaanza kuamini hawawezi kukosea, kukosolewa au hata kuhojiwa, matokeo yake huwa mabaya

Kwa upande mwingine, je, tatizo ni utakatifu wenyewe, au ni namna ambavyo binadamu anaweza kutumia dhana hiyo kwa maslahi yake binafsi, akijiona kuwa bora kuliko wengine?

Kwa sababu historia imeonyesha kuwa pale ambapo mtu anaaminiwa kupita kiasi na kupewa nafasi ya kuonekana hakosei, wakati mwingine inakuwa vigumu kwa jamii kuhoji maamuzi yake. Hata pale anapokosea, inaweza kuwa ngumu kuwajibishwa kwa sababu tayari kuna kundi kubwa la watu linalomwamini na kumwekea kinga

Swali la mjadala👇

Je, dhana ya utakatifu kwa binadamu ni mbaya yenyewe?

Au tatizo hujitokeza pale ambapo utakatifu unapogeuzwa kuwa kinga ya kukwepa uwajibikaji na kuzima sauti za wanaohoji?

Mnalionaje suala la siasa za utakatifu?

Unadhani linaweza kuwa chachu ya kujenga jamii yenye maadili au linaweza kuwa chanzo cha changamoto pale linapotumiwa vibaya?

Mwisho wa yote tujiulize

Je, utakatifu unapokuwa sehemu ya siasa unabaki kuwa mwongozo wa maadili au unaweza kugeuka kuwa chombo cha nguvu au ngao?

ShesRise_1 ✋️
Kwa maoni yangu,
siasa sio utakatifu wala ushetani, Ila mwanasiasa anaweza kua mtakatifu au shetani kulingana na mawazo, maneno au matendo yake yake akiwa kwenye siasa. Kwa mfano mwanasiasa na mpigania uhuru wa taifa letu hayati Nyerere hivi sasa yupo kwenye hatua za kutangazwa mtakatifu na dhehebu lake la dini.

Na kuna chama fulani cha siasa humu nchini cha watakatifu fulani wanatukana na kuporomosha matusi mbaya sana hasa ikiwa unajieleza kinyume na maoni ya utakatifu wao.

haijulikani wanatafuata utakatifu wa kutukana katika siasa au wanajaribu kutengeneza falsafa ya kutukana na kuporomosha matusi na kua kama utambulisho wa siasa zao, maana kwao kila kitu ni kibaya na kila mwenye maoni tofauti na yao ni adui yao na zawadi atakayopewa ni matusi tu.

Sense of perfections miongoni mwa wanasiasa humu nchini, imeharibu kwa kiasi kikubwa uelewa wa vijana na wanasiasa wengi sana, na imefikia mahali kwamba, badala ya mtu kujenga hoja, anashia kutukana tu, kwa vile labda unampinga au una maoni tofauti na muanzilishi wa falsafa ya kutukana

huenda tukawa na siasa za ushetani tuendako:NoGodNo:
 
Nyerere wanataka kumpa hadhi ya utakatifu wao wenye dhehebu lake ila sio yeye kajivika utakatifu si ndio?

Hao wanaotukana wanaonesha utovu wa nidhamu wamekosa maadili na hawana heshima wala hawawezi kujenga hoja si ndio
Hapo tumekubaliana

Sasa vipi kuhusu malalamiko kuhusu chama tawala kunyamanzisha watu kuwafunga mdomo kuzima sauti za wanaohoji ni ya kweli?

Kuna ushahidi waliowahi kukosoa watawala hadharani wamepotea /kupotezwa
Mf: Soka, Dude,Pole pole, Lissu aliponea chupu chupu

Haya madai vipi?
 
YES,

nashukuru kukubaliana hapo kwenye utovu wa maadili katika siasa,

lakini hapo kwingine eti sijui chama tawala kinanyamazisha watu?
kwa maoni yangu nadhani si kweli, hizo ni hisia binafsi na dhana tu za walioshindwa kufanya siasa au kukosa agenda na kujaribu kugain au kuatract public sympathy kwa sad na emotional theories kama hizo.
Nina hakika wanaodai hivyo hawana ushahidi wowote kama ambavyo mimi ninae eleza haya nisivyo na ushahidi wa dhana hiyo.

hakuna anaenyamazishwa nchi hii wala, hakuna anae zuiwa kusema chochote nchi hii ndio maana hata humu jukwaani wadau wanatukana mapaka viongozi wa kitaifa wa chama na serikali na tuko nao jukwaani na tunasonga mbele pamoja kama taifa lakini pia kama watoto wa mama Tanzania :1Head:
 
Kwahiyo unasema kwamba hata wewe huna uhakika na dhana hiyo ya kupotezwa kwa wanaopaza sauti ?

Basi tuseme wenye uhakika ni vyombo vya ulinzi na usalama lakini mbona hawatoi majibu ya kueleweka
Majibu yao sasa yalipaswa kua kwa vitendo wanaoteka watu wangefunguliwa mashtaka na
Kuwajibishwa ila hii tuhuma itoke juu utawala si ndio?
 
Back
Top Bottom