Siasa za Dkt. Mwigulu Nchemba zinadidimiza huduma nzuri za afya Hospitali ya Wilaya Iramba

Lyambalyetu

JF-Expert Member
Apr 6, 2021
265
240
Nimefanya utafiti wangu kwa kuitembelea Hospitali ya Wilaya yetu tangu Machi, 2021 mpaka mara ya mwisho jana.

Wagonjwa wengi waliokuwa wakiletwa wakiwa katika hali ya kuhitaji huduma ya haraka na ya dharura (emergency) wanakataliwa kupokelewa kwa kuambiwa huduma husika haiwezi kutolewa pale. Mgonjwa anapofikishwa pale anachelewesha Zaidi ya saa 5 na kisha anaambiwa apelekwe hospitali ya mkoa Singida ambapo ni takribani kilomita 80.

Juzi kuna mgonjwa amabaye inaonesha alipata ajali kutoka Kata ya Ulemo akafikishwa pale akacheleweshwa na hamna huduma yeyote aliyopata a mwishowe akaelekezwa kupelakwa Singida. Hali yake ingekuwa taabani sichelei sema yule bwana angekata roho.

Majuma mawili yaliyopita takribani wagonjwa watatu wamefikishwa pale wakiwa na hali ya kuumwa sana lakini walielekezwa Singida na mmoja alikataliwa na kuambiwa ni bora arudishwe nyumbani hali yake haikuruhusu kuendelea na matibabu pale.

Hospitali hii imeingiliwa na siasa. Vikao vya madiwani havijaldili kabisa uzo uliopo katika Hospitali hii kwani Mwenyekiti wa Halmshauri ni Swaiba wa Dr. Mwigulu. Huyu anatumika na Dr. Mwigulu pale inapotokea ukosoaji wowote wa watendaji wa Halmshauri.

Dr. Mwigulu anawatumia viongozi wa Halmshauri kuimarisha sehemu anazozitaka yeye - amepeleka Kata ya Kyengege na Ulemo anayotoka na alikojenga kila kitu. Viongozi wa Wilaya hususan DED ni swaiba wake wamekumbatiana kwa uovu na ufujaji wa fedha za Halmsharui na wamekithiri vitendo vya upendeleo.

Dr. Gwajima (acha mpinga chanjo) ambaye amewahi kuwa Mganga Mkuu wa Wilaya hii anashindwa kuisadia hospitali hii kwa sababua ya kuogopa kuchukiana na Mamba Mwigulu aliyeko kwenye kina kirefu. Dr. Kitila Mkumbo alipoulizwa kusaidia amedai ndiyo hata kutembelea Jimbo hili hataki kabisa kwa kuhofia kuleta chuki kati yake na Dr. Mwigulu.

WaNyiramba sijui tukoje? Yaani hawa mawaziri wote wameshindwa hata kutengeneza affiliation ya pamoja kwa ajili ya kusaidia maendeleo ya Jimbo lao. Hamna asiyejua kuwa Dr. Kitila Mkumbo moo wake upo Iramba lakini kiwiliwili ndiyo kipo Ubungo.

Hata Dr. Gwajima kutokana na maneno ya watu wake wa karibu kwa sasa anatamani kusaidia jimbo alikozaliwa (Iramba) lakini kikwazo ni Dr. Mwigulu ambaye mtu kipeleka hata mchango wa mifuko mitatu ya simenti kijijini kwao anamwandika kwenye Black Book yake. Hatutafika mbali kwa kweli!
 
Mnamfugaje Mwigulu huku mkijua mchawi wa maisha yenu.Kwa hiyo hata wenzake wanamuogopa kwa ushirikina.

Dorothy Gwajima atawasaidia anaonekana kuyajua maisha ya huko na ameyaishi.

Mwigulu ni genge la wahuni.

Kitila kigeugeu na hana utulivu.
 
Mnamfugaje Mwigulu huku mkijua mchawi wa maisha yenu.Kwa hiyo hata wenzake wanamuogopa kwa ushirikina.

Dorothy Gwajima atawasaidia anaonekana kuyajua maisha ya huko na ameyaishi.

Mwigulu ni genge la wahuni.

Kitila kigeugeu na hana utulivu.
Inaweza kuwa kweli huu mtazamo!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom