NATAKA nionyeshwe tofauti ya CCM na CHADEMA kwenye mambo makubwa wanayoshutumiana. Kama chadema wanasema CCM ni chama cha watoto wa wakubwa kubebwa basi na CHADEMA wasiwepo!
Nisichotaka ni kuaminishwa kwamba kuna chama cha watakatifu kinaongozwa na watu wasio kosea wala wasio na rekodi mbaya za maisha yao ya nyuma wakati tunajua kwamba siyo kweli. Nyerere alishawahi kusema "Hatuhitaji malaika kuja kutuongoza" na hili ndilo ninalolipigania kwamba CHADEMA kisifanywe ni chama cha malaika chama ambacho watu wake wakikosea basi nchi nzima isujudu kutubu makosa yao.
njaa yako sasa inakuondolea utu wako.