Siasa za CHADEMA kama za CCM

Kigarama

JF-Expert Member
Apr 23, 2007
2,492
1,230
Aliyekuwa diwani wa kata ya kaloleni kupitia CHADEMA inasemekana anatafutwa na Polisi kwa tuhumu za kumtapeli mwekezaji mwenza kwenye biashara yao ya utalii. Charles David Mpanda (Rasta) anadaiwa kumtapeli Margaret Lema kiasi cha Dola 16,400 kutoka kwenye akaunti yao ya pamoja.

Hili jambo limenifanya nifikirie upya siasa za bongo. Margaret ni Mdogo wake God bless Lema Mbunge wa Arusha Mjini kwa maana nyingine yale yanayotokea CCM kwa watu wa ukoo mmoja kumiliki chama yanatokea na CHADEMA pia. Mbowe kaoa mtoto wa Edwin Mtei Muasisi wa CHADEMA, Lucy Owenya mbunge wa viti maalum ni mtoto wa Philimon Ndesamburo Mbunge wa Moshi Mjini.

Ukikutana na Rose Kamili Mbunge wa viti maalum ujue ni mzazi mwenzie Dr. Wilbroad Slaa pia ujue kwamba ukikutana na Christina LIssu ni Mdogo wake na Tundu Lissu, na Moulida au Anna Komu Mbunge Viti maalum ni Mke wa mkuu wa Idara ya fedha Makao Makuu CHADEMA, Anthony Komu. Hawa ni wale wanaohusiana kimapenzi na kiukoo hatujui wale wanaohusiana kimaslahi kama vile kibiashara wako wangapi na kwenye ngazi zipi. Lakini jambo hili kwa sababu limetokea CDM basi litatetewa weeee hadi mijasho itukauke.

Aliyekuwa mkuu wa upelelezi Kanda Maalum ya Dar es salaam Abdalah Zombe alidai kwamba Godbless Lema alikuwa ni mwizi wa magari. Sijaona mcharuko mkubwa angalau wa kumshinikiza Zombe aseme anavyojua wizi wa magari wa Lema wala wa kumshinikiza Lema kueleza historia yake ya nyuma kabla hajawa Mbunge inahusiana vipi na wizi wa magari. Wote tuko kimyaa kwa sababu ni mtoto wa nyumbani. Rage kuonyesha Bastola ilikuwa nongwa lakini la Lema ni "Uzushi' wa magamba.
 
Hilo la kuhusu Lemma kuwa mwizi wa magari, sidhani kama ni kweli. Jamaa alikuaga ni regular guy kabla ya kupata ubunge na alikua ana hustle kama watu wengine tu wa kawaida. Hiyo habari ya uwizi wa magari ni mpya kabisa Arusha. Labda kama alikua anahanja misele mingine.
 
Aliyekuwa diwani wa kata ya kaloleni kupitia CHADEMA inasemekana anatafutwa na Polisi kwa tuhumu za kumtapeli mwekezaji mwenza kwenye biashara yao ya utalii. Charles David Mpanda (Rasta) anadaiwa kumtapeli Margaret Lema kiasi cha Dola 16,400 kutoka kwenye akaunti yao ya pamoja.

Hili jambo limenifanya nifikirie upya siasa za bongo. Margaret ni Mdogo wake God bless Lema Mbunge wa Arusha Mjini kwa maana nyingine yale yanayotokea CCM kwa watu wa ukoo mmoja kumiliki chama yanatokea na CHADEMA pia. Mbowe kaoa mtoto wa Edwin Mtei Muasisi wa CHADEMA, Lucy Owenya mbunge wa viti maalum ni mtoto wa Philimon Ndesamburo Mbunge wa Moshi Mjini.

Ukikutana na Rose Kamili Mbunge wa viti maalum ujue ni mzazi mwenzie Dr. Wilbroad Slaa pia ujue kwamba ukikutana na Christina LIssu ni Mdogo wake na Tundu Lissu, na Moulida au Anna Komu Mbunge Viti maalum ni Mke wa mkuu wa Idara ya fedha Makao Makuu CHADEMA, Anthony Komu. Hawa ni wale wanaohusiana kimapenzi na kiukoo hatujui wale wanaohusiana kimaslahi kama vile kibiashara wako wangapi na kwenye ngazi zipi. Lakini jambo hili kwa sababu limetokea CDM basi litatetewa weeee hadi mijasho itukauke.

Aliyekuwa mkuu wa upelelezi Kanda Maalum ya Dar es salaam Abdalah Zombe alidai kwamba Godbless Lema alikuwa ni mwizi wa magari. Sijaona mcharuko mkubwa angalau wa kumshinikiza Zombe aseme anavyojua wizi wa magari wa Lema wala wa kumshinikiza Lema kueleza historia yake ya nyuma kabla hajawa Mbunge inahusiana vipi na wizi wa magari. Wote tuko kimyaa kwa sababu ni mtoto wa nyumbani. Rage kuonyesha Bastola ilikuwa nongwa lakini la Lema ni "Uzushi' wa magamba.

Natoa Tamko: Kuanzia LEO mimi nakupiga BAN!! ya kufa mtu!! Hatutaki wambea huku, wala wazushi, wala waropokaji... kama una ushahidi uweke bayana sio kuropokaropoka tu. watu hao nawafaham fika, majina mengine umeyachonga wala hayapo, mengine umeyajumlishajumlisha wala hayana uhusiano.. BANNNNN!!!
 
Bado hujuaeleweka mkuu, katika dunia wote tuna mahusiano,kwanza wote ni BINADAMU,pili tumezaliwa na binadamu so labda utupe ushahidi wa wazi kuwa kuna upendeleo katika kupata nafasi fulani, ikiwa mtu katimiza vigezo na masharti kuna kosa gani?ieleweke kwamba kumpendelea mtu kutokana na unasaba ni jambo lisilofaa na huenda na ndivyo ilivyo huzorotesha maendeleo ya sehem husika hebu tupe ushahidi kuwa kuna upendeleo halaf HATUA ZICHUKULIWE
 
hebu taja sehemu ambayo huwezi kuta watu wengi katika jamii au taasisi yenye maslahi ya umma then wenye nasaba hawapo, nenda CUF na vyama vingine. Mfano U.S.A Raisi alianza baba na mtoto akawa raisi hawa ni kina Bush, Clinton alikuwa raisi mkewe nawe alitaka kuwa raisi na leo mke ndio waziri wa mambo ya nje, Uganda Museveni raisi mke waziri so haina shida sana as long as ana fit sio kupeana kama huko CCM
 
Aliyekuwa diwani wa kata ya kaloleni kupitia CHADEMA inasemekana anatafutwa na Polisi kwa tuhumu za kumtapeli mwekezaji mwenza kwenye biashara yao ya utalii. Charles David Mpanda (Rasta) anadaiwa kumtapeli Margaret Lema kiasi cha Dola 16,400 kutoka kwenye akaunti yao ya pamoja.

Hili jambo limenifanya nifikirie upya siasa za bongo. Margaret ni Mdogo wake God bless Lema Mbunge wa Arusha Mjini kwa maana nyingine yale yanayotokea CCM kwa watu wa ukoo mmoja kumiliki chama yanatokea na CHADEMA pia. Mbowe kaoa mtoto wa Edwin Mtei Muasisi wa CHADEMA, Lucy Owenya mbunge wa viti maalum ni mtoto wa Philimon Ndesamburo Mbunge wa Moshi Mjini.

Ukikutana na Rose Kamili Mbunge wa viti maalum ujue ni mzazi mwenzie Dr. Wilbroad Slaa pia ujue kwamba ukikutana na Christina LIssu ni Mdogo wake na Tundu Lissu, na Moulida au Anna Komu Mbunge Viti maalum ni Mke wa mkuu wa Idara ya fedha Makao Makuu CHADEMA, Anthony Komu. Hawa ni wale wanaohusiana kimapenzi na kiukoo hatujui wale wanaohusiana kimaslahi kama vile kibiashara wako wangapi na kwenye ngazi zipi. Lakini jambo hili kwa sababu limetokea CDM basi litatetewa weeee hadi mijasho itukauke.

Aliyekuwa mkuu wa upelelezi Kanda Maalum ya Dar es salaam Abdalah Zombe alidai kwamba Godbless Lema alikuwa ni mwizi wa magari. Sijaona mcharuko mkubwa angalau wa kumshinikiza Zombe aseme anavyojua wizi wa magari wa Lema wala wa kumshinikiza Lema kueleza historia yake ya nyuma kabla hajawa Mbunge inahusiana vipi na wizi wa magari. Wote tuko kimyaa kwa sababu ni mtoto wa nyumbani. Rage kuonyesha Bastola ilikuwa nongwa lakini la Lema ni "Uzushi' wa magamba.

Watu wengine sijui huwa mnafikiri kwa kutumia akili gani.

Rasta na Margareth walipofungua akaunti pamoja na biashara yao chadema ndio iliwashawishi? Kama wamedhulumiana kwenye biashara zao hilo ni lao wenyewe chadema haihusiki. Kama chadema ingekuwa inahusika basi polisin wangeitafuta chadema na si rasta.

Hizi njaa zenu msizitumie kupandikiza chuki na mafarakano kwa watu wasiohusika.

Bandiko lako linaonekana umetumwa kuja kuwashambulia viongozi wa chadema wala si kutapeliana kwa wafanyabiashara hao unaowataja.

Jitahidini kuimarisha matawi mliyoyafungua jana kwani rizi anakuja kuyafunga, msitafute ugomvi msiouweza bado magamba hayajavuka.
 
Aliyekuwa diwani wa kata ya kaloleni kupitia CHADEMA inasemekana anatafutwa na Polisi kwa tuhumu za kumtapeli mwekezaji mwenza kwenye biashara yao ya utalii. Charles David Mpanda (Rasta) anadaiwa kumtapeli Margaret Lema kiasi cha Dola 16,400 kutoka kwenye akaunti yao ya pamoja.

Hili jambo limenifanya nifikirie upya siasa za bongo. Margaret ni Mdogo wake God bless Lema Mbunge wa Arusha Mjini kwa maana nyingine yale yanayotokea CCM kwa watu wa ukoo mmoja kumiliki chama yanatokea na CHADEMA pia. Mbowe kaoa mtoto wa Edwin Mtei Muasisi wa CHADEMA, Lucy Owenya mbunge wa viti maalum ni mtoto wa Philimon Ndesamburo Mbunge wa Moshi Mjini.

Ukikutana na Rose Kamili Mbunge wa viti maalum ujue ni mzazi mwenzie Dr. Wilbroad Slaa pia ujue kwamba ukikutana na Christina LIssu ni Mdogo wake na Tundu Lissu, na Moulida au Anna Komu Mbunge Viti maalum ni Mke wa mkuu wa Idara ya fedha Makao Makuu CHADEMA, Anthony Komu. Hawa ni wale wanaohusiana kimapenzi na kiukoo hatujui wale wanaohusiana kimaslahi kama vile kibiashara wako wangapi na kwenye ngazi zipi. Lakini jambo hili kwa sababu limetokea CDM basi litatetewa weeee hadi mijasho itukauke.

Aliyekuwa mkuu wa upelelezi Kanda Maalum ya Dar es salaam Abdalah Zombe alidai kwamba Godbless Lema alikuwa ni mwizi wa magari. Sijaona mcharuko mkubwa angalau wa kumshinikiza Zombe aseme anavyojua wizi wa magari wa Lema wala wa kumshinikiza Lema kueleza historia yake ya nyuma kabla hajawa Mbunge inahusiana vipi na wizi wa magari. Wote tuko kimyaa kwa sababu ni mtoto wa nyumbani. Rage kuonyesha Bastola ilikuwa nongwa lakini la Lema ni "Uzushi' wa magamba.

Mkuu, hii thread yako imenipa somo sana, ni kweli kabisa Magwanda na Magamba wote wanafanana
 
Aliyekuwa diwani ndo leo siyo hata mwanachama wa CDM ...mfate mwenyewe akupe mambo,Margreth ni mwekezeji kama ulivyomsema na wamezinguana na 'aliyekuwa'diwani,sie kama chama inatuhusu nini?

Ulitaka nini hasa kutoka kwetu sie wananchi wa Tanganyika??
 
kwa hiyo kwa akili zako unafikiri mimi na wewe tunafanana kwa lolote?
magamba siku hizi ni wauaji.
magwanda ni makamanda(che guavara,fidel castro,samora machel nk.)
 
Aliyekuwa diwani wa kata ya kaloleni kupitia CHADEMA inasemekana anatafutwa na Polisi kwa tuhumu za kumtapeli mwekezaji mwenza kwenye biashara yao ya utalii. Charles David Mpanda (Rasta) anadaiwa kumtapeli Margaret Lema kiasi cha Dola 16,400 kutoka kwenye akaunti yao ya pamoja.

Hili jambo limenifanya nifikirie upya siasa za bongo. Margaret ni Mdogo wake God bless Lema Mbunge wa Arusha Mjini kwa maana nyingine yale yanayotokea CCM kwa watu wa ukoo mmoja kumiliki chama yanatokea na CHADEMA pia. Mbowe kaoa mtoto wa Edwin Mtei Muasisi wa CHADEMA, Lucy Owenya mbunge wa viti maalum ni mtoto wa Philimon Ndesamburo Mbunge wa Moshi Mjini.

Ukikutana na Rose Kamili Mbunge wa viti maalum ujue ni mzazi mwenzie Dr. Wilbroad Slaa pia ujue kwamba ukikutana na Christina LIssu ni Mdogo wake na Tundu Lissu, na Moulida au Anna Komu Mbunge Viti maalum ni Mke wa mkuu wa Idara ya fedha Makao Makuu CHADEMA, Anthony Komu. Hawa ni wale wanaohusiana kimapenzi na kiukoo hatujui wale wanaohusiana kimaslahi kama vile kibiashara wako wangapi na kwenye ngazi zipi. Lakini jambo hili kwa sababu limetokea CDM basi litatetewa weeee hadi mijasho itukauke.

Aliyekuwa mkuu wa upelelezi Kanda Maalum ya Dar es salaam Abdalah Zombe alidai kwamba Godbless Lema alikuwa ni mwizi wa magari. Sijaona mcharuko mkubwa angalau wa kumshinikiza Zombe aseme anavyojua wizi wa magari wa Lema wala wa kumshinikiza Lema kueleza historia yake ya nyuma kabla hajawa Mbunge inahusiana vipi na wizi wa magari. Wote tuko kimyaa kwa sababu ni mtoto wa nyumbani. Rage kuonyesha Bastola ilikuwa nongwa lakini la Lema ni "Uzushi' wa magamba.

Katika swala la UKOMBOZI wa aina yeyote tunaangalia msaada wa karibu na sio mahusiano,ukiangalia uhuru wa tanzania waliokuwa wameanzisha ni waislam lkn hakuna aliyesema hayo unayotaka kuyaonnyesha kwa sasa.Nyerere alipoonyesha interest walimkaribisha kwa moyo mkunjufu. kwa hiyo ktk vita hatuchagui silaha.
 
TAFAKARI CHUKUA HATUA. Ujumbe umefika maana hakuna ata mtu anayepinga kwa ushahidi kama ulivyofanya wewe.
 
Aliyekuwa diwani wa kata ya kaloleni kupitia CHADEMA inasemekana anatafutwa na Polisi kwa tuhumu za kumtapeli mwekezaji mwenza kwenye biashara yao ya utalii. Charles David Mpanda (Rasta) anadaiwa kumtapeli Margaret Lema kiasi cha Dola 16,400 kutoka kwenye akaunti yao ya pamoja.

Hili jambo limenifanya nifikirie upya siasa za bongo. Margaret ni Mdogo wake God bless Lema Mbunge wa Arusha Mjini kwa maana nyingine yale yanayotokea CCM kwa watu wa ukoo mmoja kumiliki chama yanatokea na CHADEMA pia. Mbowe kaoa mtoto wa Edwin Mtei Muasisi wa CHADEMA, Lucy Owenya mbunge wa viti maalum ni mtoto wa Philimon Ndesamburo Mbunge wa Moshi Mjini.

Ukikutana na Rose Kamili Mbunge wa viti maalum ujue ni mzazi mwenzie Dr. Wilbroad Slaa pia ujue kwamba ukikutana na Christina LIssu ni Mdogo wake na Tundu Lissu, na Moulida au Anna Komu Mbunge Viti maalum ni Mke wa mkuu wa Idara ya fedha Makao Makuu CHADEMA, Anthony Komu. Hawa ni wale wanaohusiana kimapenzi na kiukoo hatujui wale wanaohusiana kimaslahi kama vile kibiashara wako wangapi na kwenye ngazi zipi. Lakini jambo hili kwa sababu limetokea CDM basi litatetewa weeee hadi mijasho itukauke.

Aliyekuwa mkuu wa upelelezi Kanda Maalum ya Dar es salaam Abdalah Zombe alidai kwamba Godbless Lema alikuwa ni mwizi wa magari. Sijaona mcharuko mkubwa angalau wa kumshinikiza Zombe aseme anavyojua wizi wa magari wa Lema wala wa kumshinikiza Lema kueleza historia yake ya nyuma kabla hajawa Mbunge inahusiana vipi na wizi wa magari. Wote tuko kimyaa kwa sababu ni mtoto wa nyumbani. Rage kuonyesha Bastola ilikuwa nongwa lakini la Lema ni "Uzushi' wa magamba.

Tokea CDM ianzishwe hao uliowataja ndio waliokuwa wakiangaika nayo mpaka kuwa chama kkuu cha upinzani. Sasa ulitaka kwa kuwa wameifikisha CDM kuwa cha kkuu cha upinzani basi watoswe tu. Kinachokataliwa na watoto na jamaa wa viongozi kubebwa katika nafasi za uongozi kama invyofanyika ndani ya CCM. Hivi ulikuwepo wakati wa Mwalimu wewe, ile Ikulu na JWTZ walijaa watu kutoka Musoma tu. Hoja yako haina matiki mpaka pale utakapoweza kuonyesha nani kati yao kabebwa. Hivi mtu kama Nape ndani ya CCM utasema kabebwa kwa kuwa alikuwa mtoto wa kigogo au anastahili nafasi aliyonayo?
 
Pamoj na kutofahamu lengo lako hata upotshaji unaouonyesha kwenye hoja yako. Niseme hivi, inawezekana wewe ni mtot wa juz au umesahau jinsi wakati wa utawala wa Mkapa Watnzania walivyokuwa wnaambiwa kwamba wapinzani ni wahuni. Na kwa maeneo ya vijijini vilitumika na bado vinatumika vitisho kuwazuia watu kujiunga na upinzani. Kwa hiyo watu walioingia upinzani ni wale waliokuwa karibu na wale ambao tayari walikuwa ndani ya upinzani ndiyo maana si ajabu kukuta humo mtu na dada, mume, mke, shangazi, mjomba na wengine. Tatizo sio la vyama vya upinzani bali ni la serikali kukubali mfumo wa vyama vingi kwa shingo upande na haikuishia hapo bali vyombo vya dola vilitumika na bado vinatumika kuhujumu vyama vya upinzani.
Ila habari njema ni kwamba Watanzania hawadanganyiki tena na soon mabadliko ya kweli yatatokea Tanzania, GOD IS WITH US
 
Natoa Tamko: Kuanzia LEO mimi nakupiga BAN!! ya kufa mtu!! Hatutaki wambea huku, wala wazushi, wala waropokaji... kama una ushahidi uweke bayana sio kuropokaropoka tu. watu hao nawafaham fika, majina mengine umeyachonga wala hayapo, mengine umeyajumlishajumlisha wala hayana uhusiano.. BANNNNN!!!
Nilijua watu kama nyie mtaibukia na BANNNNN! Sasa wewe akili unazo, lakini hata kuzitumia tuu hutaki?

Ni jina gani ambalo nimelitumia halipo, na yapi niliyoyajumlishajumlisha ambayo hayana uhusiano?

Tumia japo akili kidogo aliyokupa mwenyezi mungu.
 
Tokea CDM ianzishwe hao uliowataja ndio waliokuwa wakiangaika nayo mpaka kuwa chama kkuu cha upinzani. Sasa ulitaka kwa kuwa wameifikisha CDM kuwa cha kkuu cha upinzani basi watoswe tu. Kinachokataliwa na watoto na jamaa wa viongozi kubebwa katika nafasi za uongozi kama invyofanyika ndani ya CCM. Hivi ulikuwepo wakati wa Mwalimu wewe, ile Ikulu na JWTZ walijaa watu kutoka Musoma tu. Hoja yako haina matiki mpaka pale utakapoweza kuonyesha nani kati yao kabebwa. Hivi mtu kama Nape ndani ya CCM utasema kabebwa kwa kuwa alikuwa mtoto wa kigogo au anastahili nafasi aliyonayo?

Mwalimu kwa mfano alimkuta Jenerali Musuguri tayari akiwa jeshini. Hili la kuhangaika na chama linatofauti gani na kina Vita Kawawa kuwa wabunge kwa sababu baba yao alihangaika sana na chama?
 
Pamoj na kutofahamu lengo lako hata upotshaji unaouonyesha kwenye hoja yako. Niseme hivi, inawezekana wewe ni mtot wa juz au umesahau jinsi wakati wa utawala wa Mkapa Watnzania walivyokuwa wnaambiwa kwamba wapinzani ni wahuni. Na kwa maeneo ya vijijini vilitumika na bado vinatumika vitisho kuwazuia watu kujiunga na upinzani. Kwa hiyo watu walioingia upinzani ni wale waliokuwa karibu na wale ambao tayari walikuwa ndani ya upinzani ndiyo maana si ajabu kukuta humo mtu na dada, mume, mke, shangazi, mjomba na wengine. Tatizo sio la vyama vya upinzani bali ni la serikali kukubali mfumo wa vyama vingi kwa shingo upande na haikuishia hapo bali vyombo vya dola vilitumika na bado vinatumika kuhujumu vyama vya upinzani.
Ila habari njema ni kwamba Watanzania hawadanganyiki tena na soon mabadliko ya kweli yatatokea Tanzania, GOD IS WITH US

Majibu yako ndiyo yanaonyesha kile nilichokisema mwanzoni kwamba linapokuja swala la CHADEMA kukosea inatafutwa njia ya kutokea.
Unakumbuka kwenye uchaguzi wa mwaka jana jinsi CHADEMA walivyokuwa wanasema kwamba gari moja la Mkuu wa Wilaya thamani yake ni sawa na zahanati nne zikijengwa.

Ni wabunge wangapi wa CHADEMA ambao baada ya kushinda wamenunua magari kama yaleyale ya wakuu wa Wilaya au yenye thamani kubwa zaidi na ile? Jee magari yao si sawa na Zahati Nne zikijengwa au ni mpaka magari hayo yamilikiwe na CCM ndiyo tuone kwamba thamani yake inafaa kujenga Zahanati Nne?

Unakumbuka jinsi Dr. Slaa alivyokuwa anasema akiingia Ikulu yuko tayari kula Mihogo na atayauza Mashangingi yote ya Serikali na kununua au kubakiza yale Hard Board peke yake. Kweli kwa haya mashangingi yaliyonunuliwa na wabunge wa CHADEMA ahadi hiyo ingetekelezwa au vingetafutwa visingizio?
 
Aliyekuwa diwani ndo leo siyo hata mwanachama wa CDM ...mfate mwenyewe akupe mambo,Margreth ni mwekezeji kama ulivyomsema na wamezinguana na 'aliyekuwa'diwani,sie kama chama inatuhusu nini?

Ulitaka nini hasa kutoka kwetu sie wananchi wa Tanganyika??
Mwaka jana wakati anagombea tabia zake zilikuwa zinafaa kwa yeye kuwa diwani? Chekeche la chama lilifanya kazi yake ipasavyo?
 
hebu taja sehemu ambayo huwezi kuta watu wengi katika jamii au taasisi yenye maslahi ya umma then wenye nasaba hawapo, nenda CUF na vyama vingine. Mfano U.S.A Raisi alianza baba na mtoto akawa raisi hawa ni kina Bush, Clinton alikuwa raisi mkewe nawe alitaka kuwa raisi na leo mke ndio waziri wa mambo ya nje, Uganda Museveni raisi mke waziri so haina shida sana as long as ana fit sio kupeana kama huko CCM
NATAKA nionyeshwe tofauti ya CCM na CHADEMA kwenye mambo makubwa wanayoshutumiana. Kama chadema wanasema CCM ni chama cha watoto wa wakubwa kubebwa basi na CHADEMA wasiwepo!

Nisichotaka ni kuaminishwa kwamba kuna chama cha watakatifu kinaongozwa na watu wasio kosea wala wasio na rekodi mbaya za maisha yao ya nyuma wakati tunajua kwamba siyo kweli. Nyerere alishawahi kusema "Hatuhitaji malaika kuja kutuongoza" na hili ndilo ninalolipigania kwamba CHADEMA kisifanywe ni chama cha malaika chama ambacho watu wake wakikosea basi nchi nzima isujudu kutubu makosa yao.
 
Back
Top Bottom