Siasa nzito za CHADEMA zaendelea kuimaliza CCM (strategic and scientific politics) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siasa nzito za CHADEMA zaendelea kuimaliza CCM (strategic and scientific politics)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by George Maige Nhigula Jr., Nov 2, 2011.

 1. George Maige Nhigula Jr.

  George Maige Nhigula Jr. Verified User

  #1
  Nov 2, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 470
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ndugu wana JF,

  Sisi sote Ni mashuhuda jinsi Chama cha Demokrasia na Maendeleo KILIVYOBADILISHA SIASA ZA NCHI YETU KWA MIKAKATI YA KISAYANSI (SCIENTIFIC STRATEGY) na kinavyoendelea kukitesa chama cha mapanduzi na Vibaraka wake,

  Ni ukweli usiopingika kuwa nchi yetu na watanzania wengi walizoeshwa siasa nyepesi nyepesi na za ujanja ujanja kwa kuwa watanzania wengi walikuwa kwenye giza totoro kwa kukosa elimu ya kujitambua na umaskini uliofanya hata kutothamini haki zao za msingi. Hivi leo hali inaanza kutoa matumaini makubwa huko tuendako kwani Chama cha mapinduzi ambacho ni adui mkubwa wa maendeleo na ustawi wa Taifa letu kimejikuta matatani baada ya kuwekwa kwenye wakati mgumu wa kutetea rekodi yake ya miaka takribani 50 ya utawala wake, Tofauti na huko nyuma watu walikuwa wanalazimishwa kuimba sifa za chama ambazo haikustahili,

  Napenda kutoa pongezi za dhati kwa chama cha maendeleo chadema kwa kuwa so offensive towards the ruling party na kuwafanya wawe majeruhi wa kisiasa na hatimaye watanzania wengi kutambua uovu na uchakavu wa chama hicho kikongwe, ambapo sera zake zimeendelea kulifanya Taifa letu na wananchi wake kuwa maskini wa kutupwa duniani.

  Naomba Chadema na wanaharakati wote wasibweteke, tuendelea kupanga scientific strategy ya kummaliza adui wetu anaelipalangaya Taifa letu, CCM ni chama kilichozoea siasa nyepesi na legelege, siasa nzito na za kisayansi zinawapoteza taratibu kwenye ulimwengu wa siasa. Mapambano ya ukombozi wa fikra na mapinduzi ya kiuchumi kwa Taifa letu hayaepukiki, Tuungane pamoja na lengo litatimia.

  Mungu Ibariki Tanzania.
   
 2. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #2
  Nov 2, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,848
  Likes Received: 473
  Trophy Points: 180
  Hizi ni siasa za style ya kijerumani, mafunzo wanayopata CDM yanawafanya watumie strategical approaches kwa kila jambo na ndiyo maana wamekuwa mwiba kwa CCM ambao wanatumia mfumo wa Kirusi wa vitisho na kufunga watu jera na matumizi ya ziada ya majeshi, ubabe bila kutumia akili, leo tunashuhudia mauaji kila kona na kuwekeana sumu kwingi.Kamua CDM hadi kieleweke
   
 3. twahil

  twahil JF-Expert Member

  #3
  Nov 2, 2011
  Joined: May 31, 2011
  Messages: 3,590
  Likes Received: 1,971
  Trophy Points: 280
  Hizo siasa legelege ndizo zilizokiua CDM na CUF huko IGUNGA.Adui wa kwanza maendeleo ni CDM kwa kuwahamasisha watu waache kujishughulisha na shughuli za uchumi na washinde kwenye maandamano ya kijinga.mfano ni dhahiri huko Arusha,mbunge wa CDM amekua si mhamasishaji wa maendeleo bali vurugu na vituko kila kukicha ati anafuata nyayo za Mandela teh teh teh, ametufungia mwaka .
   
 4. CHIETH

  CHIETH Senior Member

  #4
  Nov 2, 2011
  Joined: Aug 15, 2011
  Messages: 179
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na wewe twahil vile vile nimekusamehe kwa kuwa huelewi unachokisema. Endelea kula raha ndani ya CCM wakati Watanzania walio wengi wanateseka iko siku tutafika tu. Sijui Kama CDM ndiyo inayokusanya kodi ya maendeleo na kuzidistribute kwa wananchi? Laiti kama CDM ndiyo ingekuwa inaamua mambo ktk central gvt na halmashauri zetu basi ningekuelewa kwa madai yako chakavu dhidi yake. Hata hivyo unayo haki kama mtanzania kuendelea kutupa mawazo yako fupifupi dhidi ya CDM hapa JF.
   
 5. Bob Lee Swagger

  Bob Lee Swagger JF-Expert Member

  #5
  Nov 2, 2011
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,367
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Wakati umefika sasa tuweke itikadi za vyama pembeni ili kuwa na fikra huru zaidi, nadhani wanachopigania CDM, Lema akiwa kama mfano, kwa ujumla kina maana kubwa sana kwa wanachama wa vyama vyote irrespective of their political party differences. Ukiangalia anavyofanyiwa na polisi akiwa kama mbunge na watu wote wale anaowaongoza utagundua kuna ujumbe wanatupatia! Nadhani magamba na serikali yao wanalenga kupandikiza woga kwa watu, bila kujua kwamba watu wamechoka! Ipo siku, na nadhani i karibu, tutawafanyia ambacho hawakuwahi kuwaza!
   
 6. A

  ARKADI MAKONA Member

  #6
  Nov 2, 2011
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Usimtaje Mungu kwenye kelele zako za kihuni hizo.Utaishia kushabikia MAWAZIRI VIVULI kazi yao ni fujo na unafiki wa kimasilahi and never shall they think of eradicating poverty in Tanzania and Africa at large.Be a wise thinker "TUMIKA USITUMIKISHWE".
   
 7. Bob Lee Swagger

  Bob Lee Swagger JF-Expert Member

  #7
  Nov 2, 2011
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,367
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hujui usemalo, hatukuwahi kuwa na maandamano kama hayo unayoita ya kijinga kwa karibia miaka 40 na zaidi ya uhuru,tulikuwa na maandamano ya kuunga mkono hoja na fikra za viongozi! tumefika wapi unapoweza kupatolea mfano?! huo uchumi na maendeleo kwa ujumla yako wapi!?!
   
 8. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #8
  Nov 2, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  hahaaa hivi igunga nan alionekana legelege....ccm bwana
   
 9. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #9
  Nov 2, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,696
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Angekuwa karibu ningemuuliza, are you listening to yourself? Tatizo la CCM hawataki kabisa kuface reality. Ni kama dereva wa pikipiki anaelekea kugongana na lori halafu anafumba macho. Utakufa tu!
   
 10. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #10
  Nov 2, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  Makosa ya CCM ni kutotaka kukubali makosa na kujiona kuwa wao huwa hawakosei, utawasikia ndani ya CCM hakuna mgogoro wakati kila mtu anaona, same Igunga watu wenye akili zao kina Butiku wamewaambia kulikuwa na tatizo kule viongozi badala ya kukiri ndio wa kwanza kuzunguka na kupongezana, hapo ndipo Chadema inapowazidia. Mfano Chadema ilikubali mgogoro wake wa madiwani Arusha kuwa upo na ikaahidi kuushughulikia kweli ilifanya hivyo. Huu mgogoro wa Arusha (Lema) guess who is going to benefit, Chadema leo wako kimya kazi yao ni kutoa matamko tu serikali na CCM zinacheza mziki, leo kuna polisi kibao mitaani Arusha hapo wananchi hawailaumu polisi tu bali pia CCM on the other hand sympathy inakwenda kwa Chadema. Hizo ni baadhi tu ya strategies za Chadema ambazo zinaifanya inufaike kwa kutumia watu wachache na nguvu kidogo iliyonayo kuiyumbisha serikali na chama chake.
   
 11. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #11
  Nov 2, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  That's what am' trying to advocate and it is where the CCM big problem is.
   
 12. ikizu

  ikizu JF-Expert Member

  #12
  Nov 2, 2011
  Joined: Oct 26, 2011
  Messages: 431
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nimekubali
   
 13. T

  Topical JF-Expert Member

  #13
  Nov 2, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Unafaa kuwa political analyst wa ccm..
   
 14. twahil

  twahil JF-Expert Member

  #14
  Nov 2, 2011
  Joined: May 31, 2011
  Messages: 3,590
  Likes Received: 1,971
  Trophy Points: 280
  kwahiyo unakubali kuwa CDM inawatumia wananchi kufikia malengo yake ya kidhali ya kisiasa?.HALAFU ONDOENI FIKIRA POTOFU KUWA CCM HAISIKII PALE IKISHAURIWA.WASIOFAHAM CCM NI KWAMBA KILA BAADA YA UCHAGUZ HUFANYA TATHMINI NA KUWEKA MIKAKATI YA KUKIENDELEZA CHAMA.CCM HAISUBIRI KUPEWA TATHMIN YA UCHAGUZI NA MZEE BUTIKU ALIYEKO DSM.PILI WANAOIUA CDM NI WANAHABARI WANAIPA MATUMAINI KUWA ILISHINDA NA BAHATI MBAYA WENGI HUMU WANAJIFARIJI HIVYO.NDUGU ZANGU KUSEMA CCM HAIJAFANYA KITU TANGU UHURU NI SAWA NA KUJIKANA WEWE MWENYEWE.MKISEMA CCM HAISIKII,BASI NYINYI HAMUONI.
   
 15. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #15
  Nov 2, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  You are not on your senses, please go back to your senses before your put your fingers on the keys again. Pole maana hujui utendalo labda kwa kuwa unafaidika na huu mfumo, but we are sorry we are against this exploitive system and we want change and will never calm until you are all gone!
   
 16. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #16
  Nov 2, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  1. Ni makosa makubwa kusema sote ni mashuhuda, wakati inajulikana wazi kabisa member wa JF si watanzania wote , Aidha hakuna asiyejua kwamba JF ni mtandao ulioanzishwa na CDM mahsusi kwa ajili kuwapotosha watanzania juu ya maendeleo ya nchi yao.

  2. Mikakati gani hiyo ya kisayansi? nadhani watanzania sasa wana fursa ya kutafakari hii mikakati na waipuuze kuwa haina tija kwa taifa. Na mfano mzuri umejionesha kule arusha, wamejaribu kushambuli madereva wa daladala wamepuuzwa. Big up wakazi wa arusha.

  3. CDM wanaamini watanzania wako kwenye giza totoro na kwamba hawajui kuwa wanayoyafanya ni upotoshaji.

  4. Watanzania wanatambua kuwa CDM ni adui mkubwa wa maendeleo na ndiyo maana wanabeza kila linalofanywa na Serikali, wanawapiga watu eti waache shughuli zao kumuunga mkono mtu ambaye ameamua kwenda gerezani kwa hiari yake, mtu mwenye uhakika kuwa familia yake inahudumiwa na Chama chake, lakini anataka watu waache shughulizi ili mradi tu wazidi kuwa maskini kwa vile muda mwingi wanautumia kumtafutia umaarufu LEMA. Nani adui wa maendeleo ya Watanzania , CCM au CDM?. Sdanganyiki, watanzania hawadanganyiki na hawatadanganyika.

  5. Kila mtanzania anajua hili na wala haihitaji kuwaambia, kuwa CDM siku zote kipo kwa ajili ya kupinga CCM na siyo kuwaletea wananchi maendeleo. Siasa za chuki, hasira, kubeza, kutukana, kuchochea wananchi kuvunja amani ni alama tosha, ila najipa matumaini kuwa watanzania si wajinga kiasi hicho.

  6. Eti kummaliza adui wetu anaelipalaganya Taifa letu. Siasa si uadui bwana, watu wanaingia majukwaani kwa hoja. Tuambieni watanzania mtatufanyia nini na tupeni mifano hai kwamba nchi fulani ya kiafrika ilifanya mabadiliko haya na ndani ya mwaka mmoja mambo yakawa hivi, si kutudanganya. Mambo ya shule bure, hospitali bure, saruji 5,000/= , hadithi za abnwasi hizo, mawazo ya mfame ****, au la katika nchi ya KUFIKIRIKA?
   
 17. j

  jigoku JF-Expert Member

  #17
  Nov 2, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Ingelikuwa humu ni lazima kuweka picha yako halisi nadhani ingependeza maana tunakosa nafasi ya kuwaona watu ambao kwa maandishi yao humu jamvini wanathibisha ni mataahira,wala si watu wanye fikra kibinadamu na hasa ya amasaburi huenda yakawa ni ya kweli.
  Hivi unawezaji kusimama au kuandika japo hatukuoni kwamba CCM imefanya jambo ndani ya hii nchi kwa kulinganisha na resources tulizonazo?hivi wale mnaosema hivyo mnaishi wapi,au ni wale mnaofaidika na ufisadi unaofanywa na wana-CCM? for sure ninyi ni sehemu ya matatizo,na hakika laana ya kudhulumu,kukandamiza,kuwanyonya wavuja jasho wizi wa kila aina zimewafanya hamwezi hata kufikri,hamoni kitu wala hamsikii kitu,lakini nawahakikishia ya kwamba nchi hii lazima tupate mabadiliko ya kweli hata kama kwa kumwaga damu.maana hamtaki kwa amani tutapambana,siku itafika japo mnajidai mna jeshi,mna silaha,mahakama,magereza yote hayo si kitu mbele ya nguvu ya umma.
   
 18. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #18
  Nov 2, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  lema ana mwaka 1 sasa je nimaendeleo yapi aliyoyakwamisha..
   
 19. j

  jigoku JF-Expert Member

  #19
  Nov 2, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Mnaona upuuzi wenu sasa,haya ahadi za JK mwenyekiti wa CCM taifa zimeshaanza kutekelezwa?hivi ninyi mnajiona mko right sio,lakini nadhani kwa maneno nini hatuwawezi ngojeni dawa yenu inachemka,maana mnaonekana ni matahira,hivi kweli unaijua hii nchi?unayajua matatizo ya watanzania kwa kusoma kwenye vyombo vya habari?hivi kweli mnaona mko right na maendeleo yamepatikana?unajua rasilimali zilizoko TZ?hivi wewe una akili kweli?hivi hayo maendeleo mlioyaleta yako wapi?UFISADI NA MAWAZO YA KIFISADI NI LAANA KUBWA.TENA WATU KAMA NINYI MTAUMBUKA VIBAYA.
  Hivi wizi uliofanywa na unaofanywa na CCM hauoni?au na wewe ni mmoja wao?
   
 20. i

  ibange JF-Expert Member

  #20
  Nov 2, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 1,545
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Pumbaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
   
Loading...