Siasa nzito za CHADEMA zaendelea kuimaliza CCM (strategic and scientific politics)

Wakati umefika sasa tuweke itikadi za vyama pembeni ili kuwa na fikra huru zaidi, nadhani wanachopigania CDM, Lema akiwa kama mfano, kwa ujumla kina maana kubwa sana kwa wanachama wa vyama vyote irrespective of their political party differences. Ukiangalia anavyofanyiwa na polisi akiwa kama mbunge na watu wote wale anaowaongoza utagundua kuna ujumbe wanatupatia! Nadhani magamba na serikali yao wanalenga kupandikiza woga kwa watu, bila kujua kwamba watu wamechoka! Ipo siku, na nadhani i karibu, tutawafanyia ambacho hawakuwahi kuwaza!
Acha vitisho bwana watanzania hawajafikia mawazo hayo ya kishenzi. Hayo ni yako kwa vile umetumwa kusema hivyo. hiyo siku ikifika utafanyiwa wewe tena chunga mdomo wako usifikiri Mungu naye hakujui kama ambavyo unatumia jia feki hapa JF. Eee mungu na alaaniwe huyu muovu wa kutanguliza kauli zinazo ashiria uvunjifu wa amani. Tatizo mmeendekeza chuki binafsi, na hasa kwa lipi baya lililofanywa na Serikali. Hebu kalale bwana.
 
Na wewe twahil vile vile nimekusamehe kwa kuwa huelewi unachokisema. Endelea kula raha ndani ya CCM wakati Watanzania walio wengi wanateseka iko siku tutafika tu. Sijui Kama CDM ndiyo inayokusanya kodi ya maendeleo na kuzidistribute kwa wananchi? Laiti kama CDM ndiyo ingekuwa inaamua mambo ktk central gvt na halmashauri zetu basi ningekuelewa kwa madai yako chakavu dhidi yake. Hata hivyo unayo haki kama mtanzania kuendelea kutupa mawazo yako fupifupi dhidi ya CDM hapa JF.

kama hujaolewa ni pm tafadhali, natamani niwe mmiliki wako wa milele.....a joke!. Umeongea kwa ufahamu wa juu, congrats madam. Hako kapanya hakajui kanakoongea!
 
kwahiyo unakubali kuwa CDM inawatumia wananchi kufikia malengo yake ya kidhali ya kisiasa?.HALAFU ONDOENI FIKIRA POTOFU KUWA CCM HAISIKII PALE IKISHAURIWA.WASIOFAHAM CCM NI KWAMBA KILA BAADA YA UCHAGUZ HUFANYA TATHMINI NA KUWEKA MIKAKATI YA KUKIENDELEZA CHAMA.CCM HAISUBIRI KUPEWA TATHMIN YA UCHAGUZI NA MZEE BUTIKU ALIYEKO DSM.PILI WANAOIUA CDM NI WANAHABARI WANAIPA MATUMAINI KUWA ILISHINDA NA BAHATI MBAYA WENGI HUMU WANAJIFARIJI HIVYO.NDUGU ZANGU KUSEMA CCM HAIJAFANYA KITU TANGU UHURU NI SAWA NA KUJIKANA WEWE MWENYEWE.MKISEMA CCM HAISIKII,BASI NYINYI HAMUONI.
Hakuna chama duniani kisichotumia wananchi na wanachama wake kujiimarisha, yawe ni malengo mazuri au mabaya wananchi wenyewe wataamua. Museven alipoamua kwenda msituni wananchi wenyewe walimfuata, mwenyewe uta-judge kama yalikuwa malengo mazuri au mabaya. CCM na Chadema na vyama vingine vinagombea wananchi wale wale na vijana wale wale, vijana wanaokishabikia Chadema mnaowaita wahuni hawatoki Kenya wala Uganda, jiulize kwanini Chadema imekinyang'anya Chama cha mapinduzi vijana wake wengi nikiwemo mimi niliyecheza chipukizi ya CCM? jibu ni strategies tu.
Wengi hamjaona impact ya Lema (strategy) kujipeleka gerezani mnaita ni ujinga lakini kwa wenye akili hata ndani ya CCM wanajua impact yake. Utasema kuwa ni hiari yake au amependa mwenyewe 'yes' lakini kisiasa ni njia mojawapo ya kuwin mioyo ya watu. Hapa kwetu tunaona kama mbinu mpya lakini viongozi wengi mashuhuri wametumia mbinu hizo, juzi mwanaharakati Anna Hazare wa India ameitumia mbinu ya hunger strike kwenye scandal ya rushwa hadi akawin wananchi na bunge likabadilisha sheria, hizi ni baadhi ya scientifc strategies ambazo Chadema wanajaribu kuzi-apply. Watanzania na CCM hawajazoea siasa hizo CCM imezoea cheap politics za 'yes man' ambazo inataka mtu akitishwa ione ametishika.
 
CHADEMA ni chama cha sera na hoja yakinifu sana. Hakuna papara...!
 
Kumbe CHADEMA ni chama imara na makini?nilikuwa sijui hayo, teeeh teeeh napita tu humu
 
Hizo siasa legelege ndizo zilizokiua CDM na CUF huko IGUNGA.Adui wa kwanza maendeleo ni CDM kwa kuwahamasisha watu waache kujishughulisha na shughuli za uchumi na washinde kwenye maandamano ya kijinga.mfano ni dhahiri huko Arusha,mbunge wa CDM amekua si mhamasishaji wa maendeleo bali vurugu na vituko kila kukicha ati anafuata nyayo za Mandela teh teh teh, ametufungia mwaka .
Kwa faida ya nani? kama watu wamefanya kazi kwa bidii afu wajanja wanakula matunda huoni ni busara kuacha kazi na kumfukuza kwanza mwizi. Utajazaje ndoo iliyotoboka. Ziba ndoo ndo utie maji.
 
CDM itaweza kuleta mabadiliko makubwa kwenye Nchi iwapo CCM
wataelewa kwamba wote ni wajenzi wa nyumba moja ambao
wanachogombania ni fito tu na wala si kitu kingine cha kufanya
ni fursa za maendeleo bila hujuma ndio zitaleta mabadiliko
vinginevyo mambo yataharibika tu.
 
1. Ni makosa makubwa kusema sote ni mashuhuda, wakati inajulikana wazi kabisa member wa JF si watanzania wote , Aidha hakuna asiyejua kwamba JF ni mtandao ulioanzishwa na CDM mahsusi kwa ajili kuwapotosha watanzania juu ya maendeleo ya nchi yao.

2. Mikakati gani hiyo ya kisayansi? nadhani watanzania sasa wana fursa ya kutafakari hii mikakati na waipuuze kuwa haina tija kwa taifa. Na mfano mzuri umejionesha kule arusha, wamejaribu kushambuli madereva wa daladala wamepuuzwa. Big up wakazi wa arusha.

3. CDM wanaamini watanzania wako kwenye giza totoro na kwamba hawajui kuwa wanayoyafanya ni upotoshaji.

4. Watanzania wanatambua kuwa CDM ni adui mkubwa wa maendeleo na ndiyo maana wanabeza kila linalofanywa na Serikali, wanawapiga watu eti waache shughuli zao kumuunga mkono mtu ambaye ameamua kwenda gerezani kwa hiari yake, mtu mwenye uhakika kuwa familia yake inahudumiwa na Chama chake, lakini anataka watu waache shughulizi ili mradi tu wazidi kuwa maskini kwa vile muda mwingi wanautumia kumtafutia umaarufu LEMA. Nani adui wa maendeleo ya Watanzania , CCM au CDM?. Sdanganyiki, watanzania hawadanganyiki na hawatadanganyika.

5. Kila mtanzania anajua hili na wala haihitaji kuwaambia, kuwa CDM siku zote kipo kwa ajili ya kupinga CCM na siyo kuwaletea wananchi maendeleo. Siasa za chuki, hasira, kubeza, kutukana, kuchochea wananchi kuvunja amani ni alama tosha, ila najipa matumaini kuwa watanzania si wajinga kiasi hicho.

6. Eti kummaliza adui wetu anaelipalaganya Taifa letu. Siasa si uadui bwana, watu wanaingia majukwaani kwa hoja. Tuambieni watanzania mtatufanyia nini na tupeni mifano hai kwamba nchi fulani ya kiafrika ilifanya mabadiliko haya na ndani ya mwaka mmoja mambo yakawa hivi, si kutudanganya. Mambo ya shule bure, hospitali bure, saruji 5,000/= , hadithi za abnwasi hizo, mawazo ya mfame JUHA, au la katika nchi ya KUFIKIRIKA?
kwa hiyo wewe ni mwanachadema kulingana na maelezo yako hapo namba moja, au umejiunga na mtandao wa wanachadema kama anti-chadema
 
Hapo kwenye red sijakuelewa bado.
Ina maana hata wewe umejiunga na JF kwa vile wewe ni Chadema mahsusi ili kuwapotosha watu juu ya maendeleo makubwa ya nchi yao?
 
Siasa maji taka?

Mngekuwa kweli na siasa za maana mngechukuwa japo Igunga.
 
1. Ni makosa makubwa kusema sote ni mashuhuda, wakati inajulikana wazi kabisa member wa JF si watanzania wote , Aidha hakuna asiyejua kwamba JF ni mtandao ulioanzishwa na CDM mahsusi kwa ajili kuwapotosha watanzania juu ya maendeleo ya nchi yao.

2. Mikakati gani hiyo ya kisayansi? nadhani watanzania sasa wana fursa ya kutafakari hii mikakati na waipuuze kuwa haina tija kwa taifa. Na mfano mzuri umejionesha kule arusha, wamejaribu kushambuli madereva wa daladala wamepuuzwa. Big up wakazi wa arusha.

3. CDM wanaamini watanzania wako kwenye giza totoro na kwamba hawajui kuwa wanayoyafanya ni upotoshaji.

4. Watanzania wanatambua kuwa CDM ni adui mkubwa wa maendeleo na ndiyo maana wanabeza kila linalofanywa na Serikali, wanawapiga watu eti waache shughuli zao kumuunga mkono mtu ambaye ameamua kwenda gerezani kwa hiari yake, mtu mwenye uhakika kuwa familia yake inahudumiwa na Chama chake, lakini anataka watu waache shughulizi ili mradi tu wazidi kuwa maskini kwa vile muda mwingi wanautumia kumtafutia umaarufu LEMA. Nani adui wa maendeleo ya Watanzania , CCM au CDM?. Sdanganyiki, watanzania hawadanganyiki na hawatadanganyika.

5. Kila mtanzania anajua hili na wala haihitaji kuwaambia, kuwa CDM siku zote kipo kwa ajili ya kupinga CCM na siyo kuwaletea wananchi maendeleo. Siasa za chuki, hasira, kubeza, kutukana, kuchochea wananchi kuvunja amani ni alama tosha, ila najipa matumaini kuwa watanzania si wajinga kiasi hicho.

6. Eti kummaliza adui wetu anaelipalaganya Taifa letu. Siasa si uadui bwana, watu wanaingia majukwaani kwa hoja. Tuambieni watanzania mtatufanyia nini na tupeni mifano hai kwamba nchi fulani ya kiafrika ilifanya mabadiliko haya na ndani ya mwaka mmoja mambo yakawa hivi, si kutudanganya. Mambo ya shule bure, hospitali bure, saruji 5,000/= , hadithi za abnwasi hizo, mawazo ya mfame JUHA, au la katika nchi ya KUFIKIRIKA?

Mungu akusamehe kwani hukijui ulichokiandika!
 
Acha vitisho bwana watanzania hawajafikia mawazo hayo ya kishenzi. Hayo ni yako kwa vile umetumwa kusema hivyo. hiyo siku ikifika utafanyiwa wewe tena chunga mdomo wako usifikiri Mungu naye hakujui kama ambavyo unatumia jia feki hapa JF. Eee mungu na alaaniwe huyu muovu wa kutanguliza kauli zinazo ashiria uvunjifu wa amani. Tatizo mmeendekeza chuki binafsi, na hasa kwa lipi baya lililofanywa na Serikali. Hebu kalale bwana.
Wa tz wote tungekua na akili kama za TAHIRA HILI hii nchi sasa hv ingekua imeisha.Inaonyesha unatabia kama za ile jamii ambayo Serikali Uingereza wanataka tuwa support.Ovyooo....!
 
Usimtaje Mungu kwenye kelele zako za kihuni hizo.Utaishia kushabikia MAWAZIRI VIVULI kazi yao ni fujo na unafiki wa kimasilahi and never shall they think of eradicating poverty in Tanzania and Africa at large.Be a wise thinker "TUMIKA USITUMIKISHWE".

another CRAP!
 
Hizo siasa legelege ndizo zilizokiua CDM na CUF huko IGUNGA.Adui wa kwanza maendeleo ni CDM kwa kuwahamasisha watu waache kujishughulisha na shughuli za uchumi na washinde kwenye maandamano ya kijinga.mfano ni dhahiri huko Arusha,mbunge wa CDM amekua si mhamasishaji wa maendeleo bali vurugu na vituko kila kukicha ati anafuata nyayo za Mandela teh teh teh, ametufungia mwaka .
Inaonekana umeathirika kifikra maana hata yaliyotokea Igunga hukubaliani nayo bali unjiaminisha kuwa ccm ilishinda, swala la nani kikwazo cha maendeleo lipo wazi kabisa halihitaji maelezo wala elimu ya chuo kikuu, hivi sasa wananchi wanajua nani tatizo ila wale waathirika tu wa kifikra (ambao mtazamo wao ni zidumu fikra za...) ndio bado wanajiaminisha kuwa kikwazo ni cdm, swali rahisi ujiulize miaka 50 ya uhuru wetu na miaka 15 ya upinzani kipi kilipaswa kuwa na tija...
 
Hizo siasa legelege ndizo zilizokiua CDM na CUF huko IGUNGA.Adui wa kwanza maendeleo ni CDM kwa kuwahamasisha watu waache kujishughulisha na shughuli za uchumi na washinde kwenye maandamano ya kijinga.mfano ni dhahiri huko Arusha,mbunge wa CDM amekua si mhamasishaji wa maendeleo bali vurugu na vituko kila kukicha ati anafuata nyayo za Mandela teh teh teh, ametufungia mwaka .
Natumaini umeshirikisha ubongo hadi ufikie hatma hii, na kama hii ndo level yako ya kufikiri basi sina mchango ktk hili.
 
Kwa faida ya nani? kama watu wamefanya kazi kwa bidii afu wajanja wanakula matunda huoni ni busara kuacha kazi na kumfukuza kwanza mwizi. Utajazaje ndoo iliyotoboka. Ziba ndoo ndo utie maji.
Nakubaliana na ww, lakini kuna hakika gani tutamtoa mwizi na tusije ingiza jambazi sugu? Tusije ruka mkojo tukatumbukia kwenye kinyesi eeeh? Mfano wa ndoo ni sawa kuziba kisha ujaze maji, lakini tunachokiona ni harakati za kuongeza matundu kwenye ndoo badala ya kushirikiana kuziba. Je tutafika? Tunagombea fito wakati tunajenga nyumba moja kweli itakamilika hiyo nyumba? Tutafakari kwa makini badala ya kutoa majibu ya mkato.
 
CCM chama mfu wanaipata tangu uchaaguzi uishe mwaka jana wako kwenye defensive ooh CCm chama KUbwa ooh maendeleo ooh hakuna chama kama hiki ukweli wanarushwa kichura nadhani pale pana think tanks wengi wenye dira undercover
 
ALL in ALL tunahitaji Siasa za amani, watu wapingane kwa hoja, wawe na umoja, upendo, mshikamano, ushirikianao, utu wema
 
Hizo siasa legelege ndizo zilizokiua CDM na CUF huko IGUNGA.Adui wa kwanza maendeleo ni CDM kwa kuwahamasisha watu waache kujishughulisha na shughuli za uchumi na washinde kwenye maandamano ya kijinga.mfano ni dhahiri huko Arusha,mbunge wa CDM amekua si mhamasishaji wa maendeleo bali vurugu na vituko kila kukicha ati anafuata nyayo za Mandela teh teh teh, ametufungia mwaka .

Pole sana. Arusha imekaa na mbunge wa CCM miaka yote 48 ya uhuru. kama wambunge wenu kwa kipindi chote hicho wangekuwa wanahamasisha shughuli za maendeleo basi hiyo Arusha ingekuwa kama Ulaya. Acha kulaghai umma kawatumikie mafisadi tuache sisi tunaohitaji maendeleo tupiganie haki yetu.
 
Back
Top Bottom