SIAFIKI utaratibu wa watu kula msibani

SIAFIKI utaratibu wa watu kula msibani

We mtoa mada sema tu hao majirani zako hawashiriki kwenye misiba basiii, lakini msiba ukitokea majirani na marafiki ndio wanaohusika kufanya hizo shughuli, na unasema tusile? Hiyo ni big no kula ni sehemu ya ushirika wetu kama wanajamii husika, kwamba huyu marehemu na hawa walibaki ni washirika wenzetu after all chakula huwa kidogo sana huwezi sema naenda kushibia msibani no, wanaohangaika kufanya michango ni hao hao majirani na ndugu wengine, wanaochimba kaburi ni hao hao majirani
Hiyo ndo hali halisi kiukweli.
 
Inawezekana unaishi kwenye jamii ambayo haijastaarabika ndio maana mnawafanyia hvyo wafiwa

Kiufupi ww na jamii yako jitahidin kutembea mjifunze

Mm nijuavyo unapotokea msiba wafiwa wote hawafanyi kazi yoyote zaidi ya kutulia ndani na kuomboleza

Kazi zote zitafanywa na majiran ata kama kulikuwa na vyombo vichafu mlivyolia usiku wale majiran ndio wataosha , watafagia ndani na nje ya nyumba ninyi wafiwa mnaweza kuwa mnaelekeza tu kwamba kitu fulan Kiko hapa au kitunzwe pale kwa ajiri ya usalama na sio kufanya kazi tena
 
Hata Kiislamu haifai wafiwa kupika na kuandaa chakula bali inataki wapikiwe na wapewe chakula , shida Waislamu wengi hawalijui hili na kupelekea kufanya makosa kutengemeacwafiwa wafanye kazi na wawape chakula
Use common sense, sio kila kitu dini ikuelekeze.
 
Kipindi hicho bado najitafuta, nilifika Igurusi, Mbeya sina hata nauli ya kurudi Dar. Nikaukuta msiba wa maana hapo nikaenjoy siku 3. Yaani misosi na kulala na hakuna mtu aliniuliza wewe nani
 
Binafsi mi nimeachana na utaratibu huu wa kula misibani. Huwa nakula nyumbani au migahawani kama msiba uko mbali na nyumbani. Sioni ufahari kula msibani ni sehemu ya maombolezo/huzuni. Kwanza ni utaratibu mpya sijui nani alianzisha. Zamani ilikuwa hakuna chakula msibani, mkizika mnarudi nyumbani kwa msiba kunywa uji kikombe kimoja tu tena si wote ni baadhi ya watu tu na si lazima uji uwepo. Kwa mila na desturi za kabila letu chakula kilipikwa siku ya tatu kama tukio la kuanua matanga. Tena hapo kwenye kuanua matanga misosi hupikwa waombolezaji wale, waagane na kutawanyika kila mtu arudi alikotoka kuendelea na maisha yake kama kawaida
Unaishi mtaani hotelin
 
Kama mtu ana hali ngumu ya kifedha afuate utaratibu wa jamii ya wajaruo-ambapo unaacha mwili mochwari hata mwezi mnajipanga.

Wajaluo,kwao msiba ni sherehe.
 
Kuna watu tabia zao za ajabu hawana mshipa wa aibu, hicho chakula huenda mfiwa amekopa, maji n.k.

Kuna wengine wanategea mida ya chakula waingie...tabia mbaya sana.
 
bora tuendelee na utaratibu huo huo wa kupendana,

huko marekani wale jamaa wanaishi kama wanyama, kijana akifikisha miaka 18 tu anaanza kujitegemea na anawaacha wazazi wake wapambane na hali yao. hali kadhalika wazazi nao wakizeeka wanaishia kupelekwa kwenye care house za wazee, huko ni mwendo wa kuishi upweke utafkiri upo jehanamu. sasa si bora sisi wabongo tunaendelea kuishi kama binadamu wenye kujielewa.
Hao wazee wanaopelekwa kwenye care houses ni wale wenye uchumi wa chini sivyo? Ni wote
 
salaam,

Huenda wazo lilikua jema watu wanapofika kuwafariji wafiwa pia wale hapo ili kuweka mshikamano.

Lakini utaratibu huu binafsi naona haufai sana maana ni kama umekua mzigo kwa wafiwa hasa misiba ya familia za hali ya chini.

Kuna msiba umetokea hapa mtaani kwetu (Mungu awafariji wafiwa pia amrehemu marehemu) aise wafiwa hapa wanahangaika mara kijana anachimba mashimo ya kuweka mahema mara kapanda pikipiki amefuata kuni akirudi anaingia chumbani kwake analia uchungu wa kufiwa baba mzazh akitoka nje awahudumie wageni jamani daaah.

Nimeshuhudia misiba mingi ya familia za chini wafiwa ni kama huwa wanapata mzigo kwa watu kuja kutoa faraja.

Mara nyingi utaona wanapika chakula kikiiva wao ndio watazunguka kugawa chakula kwa wageni yote hii pia ni kutokana waTanzania tumezoea ukarimu kuwakarimu wageni jambo linalowafanya wafiwa kupewa mzigo wakati wanapitia kipindi kigumu.

Na hapo utakuta mimtu inaenda msibani inarundikana vikundi na kupiga story za siasa au simba na yanga huku wafiwa wakitarajiwa wawe wakarimu kwa kuwahudumia wageni hawa eti wamekuja "kufariji". HII SIO SAWA

Mara nyingine msiba ukiisha kuna vitu viliazimwa kama masufuria, sahani, maturubai, viti, na kutokana na ustaarabu mbovu wa "wageni wafariji" labda vimepotea au vimeharibika mzigo hua unaachwa kwa familia ya wafiwa
Mie pia sikubaliani na hambo hilo
 
Ukiwa na hadhi yako au umaarufu fulani na usile msosi wa msibani utasemwa sana, utaonekana unadharau....unaringa.

Ila ukiwa huna kitu, ule usile utajua wewe, hakuna anayekufuatilia..sanasana waombelezaji wenzio wasikika wakikusema
" Yaani huyu kaka kila msiba yeye yumo, halafu ni wa kwanza kuwahi plate"
 
Mkuu una umri gani na upo pande zipi za nchi hii?

Jamii ilishalimulika jambo hili tangia kitambo sana na kwa sasa linazidi kuboreshwa zaidi na kuwekwa katika mfumo wa sherehe.

Ndiyo maana sasa hivi utakuta kila sehemu kuna vikundi ama 'nzengo', yote haya ni kwa ajili ya kumsupport mfiwa, ingawa gharama za nsiba hazikwepeki 100%.

Kila mahali wamejiwekea kanuni zao namna ya kukabiliana na misiba yao, kwani inafahamika wazi kuwa, wakati wa kukumbwa na janga hilo si lazima mtu awe na ukwasi,lakini shughuli zinatakiwa zieende kwa ratiba kabisa.

Labda ninachotaka kusema hapa ni kushauri mfiwa kutuliza akili zake anapopata msiba, hasa kuhusu udhibiti wa vifaa mbali nbali kutokana na muingiliano wa watu wengi ghafla nyumbani kwake.
Kabla haujatangaza msiba kwako, tenga chumba, hamishia vitu muhimu na ukifunge.

Maana kuna wajanja ambao huona msiba kama fursa ya kunufaika binafsi, kula pamoja na kuondoka na vitu(wizi).
 
Binafsi mi nimeachana na utaratibu huu wa kula misibani. Huwa nakula nyumbani au migahawani kama msiba uko mbali na nyumbani. Sioni ufahari kula msibani ni sehemu ya maombolezo/huzuni. Kwanza ni utaratibu mpya sijui nani alianzisha. Zamani ilikuwa hakuna chakula msibani, mkizika mnarudi nyumbani kwa msiba kunywa uji kikombe kimoja tu tena si wote ni baadhi ya watu tu na si lazima uji uwepo. Kwa mila na desturi za kabila letu chakula kilipikwa siku ya tatu kama tukio la kuanua matanga. Tena hapo kwenye kuanua matanga misosi hupikwa waombolezaji wale, waagane na kutawanyika kila mtu arudi alikotoka kuendelea na maisha yake kama kawaida
Labda bado ni mtoto kwenye jamii/mtaa unaoishi hawakuchukulii kama mwananzengo mwenye mchango wowote kwao, hayo yafanye ukiwa mdogo kwenye jamii ila omba isifike zamu yako watu wakusanyike kwako! Siku hiyo ndo watataja tabia zako zoote na kukususia msiba wako. Imagine umefiwa na utatakiwa utoe faini ili watu wale msibani maana watakususia chakula chako utaambiwa huwa huli misibani na wao hawatakula na chakula umeandalia wafiwa na waombolezaji wote wanaofika pale. Jamii yenu hiyo nayo kiboko toka nimekuwa nahudhuria misiba sjawahi sikia vya vile, naonaga mwanzo mwisho lazima chakula kipikwe hadi watu wanasambaa msibani, jamii yenu ni ya nchi gani mkuu
 
Ukiwa na hadhi yako au umaarufu fulani na usile msosi wa msibani utasemwa sana, utaonekana unadharau....unaringa.

Ila ukiwa huna kitu, ule usile utajua wewe, hakuna anayekufuatilia..sanasana waombelezaji wenzio wasikika wakikusema
" Yaani huyu kaka kila msiba yeye yumo, halafu ni wa kwanza kuwahi plate"
Hata kama hana....ogopa walimwengu mkuu! Utafanya vile hata hawakuulizi wanasikilizia zamu yako ifike maana hii misiba ni kupokezana tu leo kwangu kesho kwako! Siku hiyo ndo utaorodheshewa yoote na hata kama hauna faini ndiyo utatoa ili watu washiriki kawaida msibani na wakule chakula chako, la sivyo unasusiwa msiba kama unavofanya misiba ya wengine eti "sili msibani, kazi sifanyi, ohooo chunga likukute
 
Thubutu, labda kama hakuna nyama.
Ni dagaa tu zinaweza kususiwa.
Wakishaona ng'ombe kaangushwa chini ile asubuhi...
Hiyo misimamo inayeyuka.
Kuna watu wa mtaa wa nne watajipitisha hapo, kama wanacheza karata hivi kumbe wanasubiri menyu.
 
Labda kwenye jamii yenu ndo wana njaa za hivyo, watu wanasusiwaga kila kitu mpaka faini itolewe, nimezunguka katika jamii nyingi Tanzania likimkuta mtu wa hivyo kwenye nzengo lazima kimrambe haijalishi kawapikia nini, kwanza anaanza kususiwa hakuna wa kupika, haya jamii nyingi mfiwa haruhusiwi kuingia kupika hasa siku ngumu huwa ya mazishi ndiyo inakuwaga na watu wengi na mfiwa asikanyage jikoni, unatoa huyo ng'ombe nani anachinja? Haya utachinja utaingia kumpikia nani ilihali unaona hakuna anayeshughulika na wewe? Omba yasikukute umefiwa afu jamii ikususie kila kitu. Utaleta watu wa catering na vyakula vyao ila nzengo ikisusa imesusa na wao hawali kwako kama unavofanyaga lazima utoe faini na uombe msamaha wananzengo ndiyo mambo yataenda.....jamii inayokuzunguka inahifadhi sana matukio yako kuliko unavyofikiria
 
Mbona wagalatia walishaanza kufanya hivyo zamani tu
Nimesha hudhuria misiba kama mitatu ya rafiki niliosoma nao shule kabisa, na tulikuwa na ukaribu lakini baada ya kuzika tukaenda kutoa pole kwa wazazi, na ilikuwa kavu kavu
Acheni kuweweseka, huu ni utaratibi wetu waislamu na hautaachwa
Lazima tuwakarimu walikuja kushiriki mazishi
 
Labda kwenye jamii yenu ndo wana njaa za hivyo, watu wanasusiwaga kila kitu mpaka faini itolewe, nimezunguka katika jamii nyingi Tanzania likimkuta mtu wa hivyo kwenye nzengo lazima kimrambe haijalishi kawapikia nini, kwanza anaanza kususiwa hakuna wa kupika, haya jamii nyingi mfiwa haruhusiwi kuingia kupika hasa siku ngumu huwa ya mazishi ndiyo inakuwaga na watu wengi na mfiwa asikanyage jikoni, unatoa huyo ng'ombe nani anachinja? Haya utachinja utaingia kumpikia nani ilihali unaona hakuna anayeshughulika na wewe? Omba yasikukute umefiwa afu jamii ikususie kila kitu. Utaleta watu wa catering na vyakula vyao ila nzengo ikisusa imesusa na wao hawali kwako kama unavofanyaga lazima utoe faini na uombe msamaha wananzengo ndiyo mambo yataenda.....jamii inayokuzunguka inahifadhi sana matukio yako kuliko unavyofikiria
Huo ni ugalatia
 
Back
Top Bottom