Uchaguzi 2020 Si Magufuli, si Humphrey Polepole waliojaribu hata ku-tweet kushukuru wapiga kura au kusherehekea ushindi mpaka sasa

Mkuu ukweli wa walichokifanya ili kupora uchaguzi wanakijua sana ndiyo sababu wamepiga kimya wahuni hawa.
Kasome jinsi Hussein Bashe alivyoshambuliwa baada ya kuandika tweet ya kumpongeza Magu na kusema miaka mingine mitano kwa Magu.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
CCM 3 TANZANIA 0

Ajabu kuna mama alikuwa anaiombea kura ccm nyumba kwa nyumba leo analia kwa uchungu haamini nini kimetokea!
Anasema mwenyewe hali itakuwa mbaya jamani kuliko ilivyokuwa!

Nimeshangaa kuona hata ccm wanasikitika
 
Kama nilivyosema katika uzi wangu wa asubuhi ya leo,mpaka muda huu viongozi hawa wako kimya kabisa licha ya Magufuli kutangazwa mshindi wa kitu cha urais.

Inawezekana chama kinajiandaa kutoa tamko rasmi wakati wowote ule, ila bado nilitarajia kutokana na furaha ya ushindi, mmoja wa viongozi hawa angeshasema lolote kupitia mitandao na hasa mtandao wa Twitter kuhusu ushindi huu wa asilimia zaidi ya 80 ila cha ajabu wako kimya kabisa.

Ni vijana wao wa mitandaoni tu wakiwemo kina Pascal Mayalla ndio wanaojikakamua kusherekea na kusifu na kukejeli wapinzani ila wenye chama mpaka sasa kimya utadhani wao ndio wametangazwa kushindwa.

Anyway,labda nao wao hawana access na internet ndio maana wako kimya.

All in all, hii ni dalili kuwa hata wenyewe hawana raha na matokeo haya na huenda hawakutarajia mambo yangeenda yalivyoenda.

Tunawasubiri mjikaze kutoa taarifa ya ushindi na kupongezana.Nasubiri tweet ya Mwenyekiti (Mgombea)na Polepole.
Mtu wa mwisho kushukuriwa ni wewe. Polepole alikuwa live kwa wananchi wa Tanzania na Wana CCM:

 
Pole pole unapoongea unazidi kutia watu jazba.
Ni muhimu sana mkae chini na kujiuliza, kwanini kuna chuki dhidi ya! kwa kiasi hicho

-Kama mlitaka kufanya halali kwanini mlifunga internet? Kuna nini mlichoogopa
-Masanduku ya kura feki zikiwa na mihuri ya NEC imepatikana ikiwa na watu wa CCM
Mhuri wa NEC unapatikana wapi!
-Kwanini mliwatia ndani wapinzani
-Kwanini mliwazuia mawakala
-Hivi kura za Ubunge zinakuwaje chache kuliko za Urais? hujaona hayo katika vituo
-Kubwa zaidi , Polisi walishaanza kutangaza matokeo kabla ya kura (OCD Hai)

Waangalizi wa kimataifa wa EA ni akina Kagame na Museveni, Burundi na Congo.
Hao ndio unaosema wamesema uchaguzi ni wa haki. Hawa ndio wanasimamia haki! real?
Yaani hao ndio waangalizi. Umesahau mlipiga marufuku waaangalizi wa kimataifa.

Mataifa makubwa yamezungumza na mengine yatazungumza.
Hakuna kupongezwa bali kutuhumiwa tu. Leo siku ya 3 kila Taifa linajiuliza, hamuoni tatizo ?

Disco linachezwa katika ukumbi si makaburini. Taifa lina huzuni si kwa uchaguzi bali mlicholifanyia.
Kuna chuki kubwa ! ingieni mtaani mtabaini .Mkiona nchi ina ganzi jueni lipo tatizo. Hivi mnaishi wapi?

JokaKuu Mag3
 
Nyuzi zinazofata za Salary Slip ziwe zinahamishiwa jukwaa la Jf Doctor maana nachokishuhudia siku mbili tatu hizi kwa huyu member ni mtu ambae kama hatapata msaada wa haraka wa wataalam wa afya ya akili anaweza kujidhuru. Ana dalili zote za mtu anaechanganyikiwa na hii huenda inatokana na jinsi anvozidi kutokubaliana na kitu ambacho hana uwezo nacho.
Mkuu jitahidi kujichanganya na watu mbadilishane mawazo japo kwa spana ulizo pondwa psychologically unaweza kuhisi jamii yote inakuzomea ila jitahidi hivo hivo. Ila chonde chonde usijaribu kupambana na hiyo hali mawazoni kwa kutumia vilevi, ukijaribu tu tutaletewa habari hapa member maarufu wa bavicha kawehuka, kajidhuru au kajitoa uhai kwa sababu ya kijinga kabisa(mambo ya siasa). Na kwa taratibu ya jamii nyingi za nchi hii kama hilo la tatu litatokea(kujitoa uhai) kabla ya kukuzika tunakuchapa kwanza viboko ili huo mkosi usihamie kwa ndugu wengine.
Nirudie tu kukupa pole kamanda, ila jifunze kupokea matokeo yote kama yalivo. Kuendelea kutoamini na kukataa haikusaidii wewe wala haiwasumbui CCM.
 
Back
Top Bottom