Kufuatia TEC kutoa waraka wa kupinga uwekezaji wa DP katika bandari yetu.
1. Serikali inapaswa isimamie msimamo wake kwa masilahi mapana ya Taifa letu.
2. Wabunge wetu ambao ndio wawakilishi wa wananchi tayari walishapitisha makubaliano hayo na kuridhia mchakato uendelee.
Hatua hii iliyo fanywa na chombo chetu cha Bunge letu tukufu ni muhimu na inapaswa iheshimiwe na kila mtu na kila taasisi.
3. Serikali yetu inaongozwa na mihimili mikuu mitatu;
Baraza
Bunge na
Mahakama. Sio TEC wala BAKWATA.
TEC au BAKWATA sio miongoni mwa mihimili ya Serikali, hivyo tusiruhusi baadhi ya watu kutumia taasisi hizo za kidini kupenyeza mambo makubwa ya Kiserikali, Serikali isikubali kuendeshwa na taasisi hizo za kidi, kamwe tusikubali kuyumba wala kuyumbishwa.