"Bongolander, post: 31908412, member: 3997"]Nilifikiri kwa kutoa mifano hiyo unaweza kupata undani wangu kuwa ni nini nakijali zaidi, baada ya kuwa frustrated na demokrasia tunayodanganywa kila siku.
Hivi unapataje watu wa kusukuma mbele gurudumu la maendeleo kama si kwa njia ya demokrasia? Tunadanganywa na nani kuhusu demokrasia?
Demokrasia ni kitu kigeni nchini?
Nimekuwa naona kama ni mchezo wa wanasiasa kupata wanachotaka, na sisi kura washangiliaji wakati hatuna umeme, maji, shule, hospitali...
Hapa unalaumu uwepo wa bunduki.
Sidhani Bunduki na mabomu ni tatizo. Tatizo ni jinsi watu wanavyotumia vitu hivyo.
Badala ya kutumia bunduki responsibly watu wanatumia kushambuliana katika hadhara
Badala ya kutumia mabomu kulipua miamba ya madini na njia za usafiri, watu wanalipuana
Kwa nchi nyingine demokrasia nakuwa practiced bila tatizo hata kidogo
Hatuwezi kusema sasa ndio mwisho wa demokrasia , kwa kigezo na utaratibu gani
Nakubaliana na wewe kabisa kuwa viongozi waliotangulia walitoa kipaumbele kwa vyote maendeleo na demokrasia, walikuwa na busara.
Halafu soma hapa chini unavyojichanganya .
What do facts tell us, they tells us Democracy to us is just fantasy.
!!
Chaguzi tunafanya kupoteza hela na muda, kwa kuwa matokeo yanakuwa predetermined long before election. So why waste our money and our time? Kuwafurahishwa watu wa magharibi? or just to have the label that we are a "democratic" country?
Sijui kama unafuatilia mjadala, demokrasia si uchaguzi ndugu yetu!!.
Uchaguzi ni moja ya element za demokrasia, nyingine ni utawala bora na haki za binadamu.
Unapokataa demokrasia kwa maneno mengine unakataa rule of law and human rights.
Demokrasia ndiyo inatupa ushirikishwaji wa wananchi katika maendeleo yao
Bila demokrasia unaishia kuwa na utawala la kiimla.
Sifa ya utawala la kiimla ni kuamua mambo na kuya impose kwa watu wake.
Hilo ndilo linazaa neno IMLA ambalo kwa kiingereza ''dictate''
Mtu anaye dictate ni Dictator. Labda utusaidia mfumo upi utakuwa mbadala wa demokrasia
Just look at mchezo wa kilichoitwa mkutano wa katiba, how much time and money have we wasted? Zile hela zingetumika kujenga shule au hospitali, leo tungekuwa na kitu tangible. All what we have now is "we had a democratic process". My point here, is ideas and facts do not match.
Katiba haikuwa na tatizo hata kidogo.
Tatizo ni CCM waliokataa maoni ya wananchi wakihofia katiba mpya kuwa mwiba kwao
Hivyo hakuna uhusiano kati ya demokrasia na uhuni wa CCM ambao wewe hutaki kuusema
Kwa taarifa yako,CCM walioko madarakani ndio walikuwa ndani ya Bunge la katiba
Ni nani miongoni mwao alifikiri kuwa mchakato ule ulikuwa wa ujinga na kusema!!
Bongolander: Kimsingi nakubali kuwa demokrasia ni jambo la muhimu, ni muhimu sana.
halafu
Bongolander :Nimekuwa naona kama ni mchezo wa wanasiasa kupata wanachotaka, na sisi kura washangiliaji wakati hatuna umeme, maji, shule, hospitali..
anamalizia
Bongolander: democracy to us is just fantasy
!!!
I'm out, good luck