Si kila Mtanzania ni kichwa cha panzi. We have made progress under Magufuli (For sure more needs to be done)

Bongolander

JF-Expert Member
Jul 10, 2007
5,062
2,000
Wakuu Great thinkers, napenda mijadala ya kwenye jukwaa hili maana wachangiaji na wakosoaji wanaotumia hoja na busara kuchangia, kukosoa, kushauri na kurekebisha. Watunga sera makini wanafuatilia sana jukwaa hili, kwa kuwa wachangiaji, hata kama si wote wenye weledi, walio wengi si mbumbumbu na vilaza. Kwa hiyo wanaweza kuiangalia nchi yetu kwa kioo cha jukwaa hili.

Nakumbuka sana wakati wa serikali iliyopita ni jukwaa hili ulikuwa unaanikwa uozo mwingi uliopo kimfumo na uliotudunisha kwa muda mrefu kama taifa. Kulikuwa hakuna kushambulia watu, ila kushambulia matendo na kauli zao. Tulishambulia ujinga ule, na wengi wenye akili walikuwa wanasema Tanzania, kwanza na utanzania kwanza. Na baada ya awamu ya tano kuingia madarakani, mengi tuliyokjuwa tunalalamikia huo yamefanyiwa kazi, na mengine hata yamezidi matarajio. (Kumbukeni madili yaliyokuwa yanapigwa kutokana na safari za rais nje ya nchi ambazo hadi leo hii gharama zake anajua Mungu- JPM Ametatua kabisa na kufanya maajabu) The point is hoja zetu zenye maana huwa zinasikilizwa na kufanyiwa kazi, hata kuliko zinazoongewa kwenye mikutano.

Ningependa turudi kwenye njia ile, ili manjuka wajue kuwa mijadala ni hoja zinazolenga issues, na sio mashambulizi ya wasifu binafsi. Au hata kuingia kwenye mambo cheap wakati nchi yetu inahitaji macho makali kwenye mambo makubwa.

Nimekuwa nafuatilia posts naona kama watu wanolalamikia sana serikali, wanawalenga watu, wakisema mambo yanayofanyika sasa yanafanya hali iwe ngumu. Lakini badala ya kueleza mibadala na kuchambua kwa picha kubwa, wanagusa vidone vodone na kuacha mbali picha kamili ya nchi yetu, na kuanza lugha za matusi.

Tujaribu kuangalia ni nini kilikuwepo before JPM, na sasa tukoje. Miaka minne iliyopita sio mbali sana. Kuna ukweli kuwa baada ya hela za dawa za kulevya kuondolewa mitaani, na baada ya hela za ufisadi kupungua sana mitaani, hali iko tofauti. Ndio maana baadhi ya watu wanasema bora wakati wa JK maana hela ilikuwa nje nje, lakini tunasahau kuwa ile hela ilikuwa chafu. Kumbukeni kuwa Eddo alikimbizwa U-PM kutokana na uozo wa madili ya ajabu, Mh Pinda alikuwa kwenye hati hati sababu kasi yake ya kudeal na mambo yanayogusa kutatua taabu za wananchi ilikuwa ndogo. Licha ya changamoto zilizopo sasa mambo yamebadilika sana.

Our country was in verge of becoming a banana republic, we averted that. So we need to do better than throwing cheap shots.
 

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
14,179
2,000
Mkuu naomba nizipitie hoja zako nilizozianisha kwa namba.

Kwanza, niweke wazi kuwa jamii yoyote kuanzia vijijini, mijini na majiji inakuwa ''vibrant'' kukiwa na mkinzano wa mawazo.

Mawazo mbadala hulazimu watu kuliangalia jambo kwa mtazamo mpana na tofauti.
Kuwa na mawazo ya aina moja hujenga ''confimation bias''
Hivyo ndivyo tulivyokuwa miaka michache iliyopita, lakini je, tupo hapo sasa hivi?
"Bongolander, post: 31766135, member: 3997"]
1.Serikali iliyopita ni jukwaa hili ulianikwa uozo mwingi uliopo kimfumo na uliotudunisha kwa muda mrefu kama taifa.
Ndiyo faida ya kuwa na uhuru wa mawazo.

Na wala hilo haliifanyi awamu iliyopita kuwa na uozo mwingi, inawezekana upo,hausemwi
Swali, ni kipi kimefanyika kubadili uozo wa mfumo ikiwa mfumo ni ule ule uliokuwepo?
Pengine ningeleewa kama tungekuwa na utaratibu mwingine kama ule wa katiba uliokwama
2. Tulishambulia ujinga na wenye akili walisema Tanzania, kwanza na utanzania kwanza.
Sidhani kama dhana ya Tanzania kwanza imekufa na sioni tatizo kwa dhana ile kama ilivyotumika.

Tofauti ni dhana ya Tanzania kwanza imefunikwa na hoja ya Uzalendo
Tanzania kwanza ni kusema kilichowazi, Uzalendo unachukuliwa kama ''kuhifadhiana'

Kuwa Mzalendo lazima uwe na ''mipaka'', ili kuweka Tanzania kwanza unasema kilicho na masilahi na nchi.Tunasikia fulani si Mzalendo kwasababu tu amesema kisichopendeza. Katika Tanzania kwanza, kusema hata kisichopendeza ndio ''ukwanza''
3. Na baada ya awamu ya tano kuingia madarakani, mengi tuliyokjuwa tunalalamikia huo yamefanyiwa kazi, na mengine hata yamezidi matarajio.
Mhh, sina uhakika yamefanyiwa kazi au la.Kutosikia yakisemwa haimaanishi yamefanyiwa kazi

Kuna kiongozi kasema '' wanaosema' watakatwa majina 2020.
Hao ni viongozi wanaambiwa, mwananchi wa kawaida atakuwa na ''guts' zipi za kusema?
Na kama yanafanyiwa kazi kwanini kuna hali ya kutishana kama alivyosema kiongozi huyo?
4. (Kumbukeni madili yaliyokuwa yanapigwa kutokana na safari za rais nje ya nchi ambazo hadi leo hii gharama zake anajua Mungu- JPM Ametatua kabisa na kufanya maajabu)
Hili nalo nina tatizo. Kuna tafsiri isiyo sahihi kuhusu gharama za kusafiri

Kwa ilivyoeleweka wakati ule, na tangu enzi za Mwalimu kiongozi kusaifiri ni sehemu ya kazi

Kilichozungumziwa awamu ya nne ni aina ya safari.Kwamba, ''itinerary'' haikuwa organized.

Haileti maana Rais asafiri ulaya mara mbili kwa wiki moja, au Rais aende Marekani kisha arudi Ulaya katika shughuli zinazoweza kufanywa katika msafara wa siku mfululizo

Tofauti na awamu ya nne, juzi Rais amekwenda South Afrika, Namibia na Zimbabwe katika ziara moja. kwa awamu ya nne huenda kungekuwa na ziara nne tofauti

Hoja kwamba gharama zinapungua kwa Rais kutosafiri nayo siikubali.
Faida za kusafiri haziwezi kuwekwa katika mizani na gharama

Kusafiri ni sehemu ya Diplomasia,viongozi wengi huitumia kama fursa ya kuchangamana na kutafuta ''deal'' za kitaifa kisiasa, kiuchumi na kijamii. Kumbuka ''out of sight out of mind''

Rais asiposafiri akamtuma VP au PM ni ngumu ku justify kuwa gharama zimepungua. Gharama hazipimwi kwa fedha bali umuhimu wa safari

Lakini pia VP na PM ni viongozi wenye uhitaji unaokaribiana na wa Rais
Wanapokwenda kama wawakilishi wa Rais hadhi zao zinapanda zaidi ki-protokali
Gharama zinapunguaje?

Ni kwa kiasi gani na ni kwa faida ipi ukiangali hadhi zao na mtarajio ya ziara zao?
Viongozi hawapaswi kuhudhuria mikutano tu, wanapaswa kutumia mikutano kujenga deal.

Kiprotokali viongozi wengi hupenda kukutana na counterpart wao na si wawakilishi.
Viongozi duniani hukutana na wenzao ili wafanye ''deal'' moja kwa moja na si wawakilishi wanaosubiri maamuzi kutoka kwa mamlaKa za juu yao.

Hakuna bureaucracy siku hizi, kama hupo watu wanaendelea na deal na waliopo
Hoja kubwa si kusafiri kwani ni sehemu ya kazi, bali aina ya safari, sababu za safari na mpangilio wa safari ''itinerary'', hayo ndiyo muhimu
5. Ningependa turudi kwenye njia ile, ili manjuka wajue kuwa mijadala ni hoja zinazolenga issues, na sio mashambulizi ya wasifu binafsi
Hili naweza kusema ni matokeo ya kutuma vijana mitandaoni kutetea hoja kwa viroja, kuvuruga hoja na kuwatisha watu kuwa ''uzalendo'' si kueleza mbadala ni kukubaliana na kila kinachosemwa.

Na hapa CCM inahusika. Ikiwa ni chama tawala pekee inashangaza vijana wake wanaotumwa, kwanza, hawajui kujenga hoja,kutetea hoja au kufanya hata kiutafiti cha hoja

Katika mazingira ya kawaida, chama tawala kingekuwa mfano, kina mengi mazuri ya kueleza kuliko inavyoonekana sasa. Kwasababu hawana uwezo wa kujenga, kubomoa au kutetea hoja, siku hizi kuna kauli za ''siyo mzalendo, anatumiwa na mabeberu'' Ina udhi na kukera
7...Badala ya kueleza mibadala na kuchambua kwa picha kubwa, wanagusa vidone vodone na kuacha mbali picha kamili ya nchi yetu, na kuanza lugha za matusi.
Tumewajenga vijana kuamini kuwa mawazo tofauti ni kukosa uzalendo. nimelieza hapo juu

Na hapa ndipo dhana ya uzalendo inapopotoshwa na kupoteza maana yake
8.Tujaribu kuangalia ni nini kilikuwepo before JPM, na sasa tukoje. Kuna ukweli kuwa baada ya hela za dawa za kulevya kuondolewa mitaani, na za ufisadi kupungua sana mitaani, hali iko tofauti.
Wengine tulizungumzia hili, kwamba, pesa zilizokuwepo mitaani ni zilikuwa nje ya mfumo rasmi wa mzunguko wa pesa.
Na kwa maana hiyo hata inflation ilikuwa ni kubwa

Inflation ya juu inaumiza zaidi kuliko ongezeko la mshahara.
Inflation inagusa kila kitu mtu anachotumia iwe bidhaa au huduma.

Hivyo, inflation ilikuwa zao la kuzagaa pesa bila mpango
Nchi zilizoendelea mfumo wa pesa unadhibitiwa kuondoa pesa zilizo nje ya mfumo rasmi.

Wanaosema pesa zikiwa mitaani hali ni nzuri, well,ni burungutu lisilo na thamani.

Ni bora kudhibiti inflation kuliko kuongeza mishahara.

Kwa hoja dhaifu za mitaani na zisizo za kiuchumi, ongezeko la mshahara kwa 100,000 hakulingani na inflation ndogo tu ya 5%.

Hiyo 5% inagusa kila kitu, kila huduma ya maisha ya mtu. Mwisho, 100,000 haina maana kabisa
 

Bongolander

JF-Expert Member
Jul 10, 2007
5,062
2,000
Mkuu Nguruvi3,

Ni kweli unayosema, ndio maana nasema we still have a long way to go. Unajua ni kweli kuna watu wanaogopa kumwambia JPM hali halisi ya baadhi ya mambo, au wanaamua kukaa kimya kwa hofu ya kutumbuliwa, au kum-mislead kwa kujilinda wenyewe. Yote matatu hayajengi. Lakini uzuri ni kwamba JPM akiambiwa na akielewesha kupitia proper channels anachukua hatua, au hata akijua mwenyewe anachukua hatua.

Mfano mzuri ni issue ya kikokotoo. Nadhani kila mtu alikaa kimya na kuacha wastaafu waumie. Lakini JMP alisimama nataka itafutwe njia mbadala. Kwa kuwa kilio kilisikika na kimifikia.

Kuna changamoto nyingine zipo hatuwezi kukataa, maana tunaziona, lakini tusitregemee kuona uozo wa miaka 30 unarekebishwa kwa miaka mitatu, will take more than that. Mfano ni issue ya liquidity uliyotaja, hiyo kweli ni mtihani mgumu. We are damn when we are lack of it, more so when we have it in eccess from illegitimate sources (Inflation). Sasa muziki wake upo kwenye kuweka uwiano, hapo ndio naona BOT bado wanahangaika. Unajua hii issue ya uchumi wa "madili" ndio imeharibu maana ya uchumi halisi. Hata thamani ya kazi kidogo imepungua kwa kuwa madili machafu yalikuwa yanalipa zaidi. So here it will be changing the whole mindset yetu.

Hili la Rais kusafiri mkubwa it pains me like hell. In fact linaweza kupimwa. Tunaweza kuomba watu watusaidie kufanya cost benefit analysis. What did we as a country spent on them, toka ngazi ya Rais, mawaziri, makatibu ...tuone tulitumia dola ngapi, and what did those travel brought to us. So far naona nyingi zilikuwa mbaya. Kibaya zaidi watu wanaangalia ziara za JK peke yake, ukweli zilikuwa nyingi sana na gharama zilikuwa inflated. So, kuzipunguza ni jambo jemba. Lakini that alone hatuwezi kuita mafanikio makubwa. Unajua kama sikosei enzi ya JK safari moja ya economy class Asia Ulaya na America ilikuwa ni zaidi ya dola 7000 (sina hakika) kwa kuwa ununuaji wa tiketi ulikuwa unafanywa kupita agents, na wasafiri walikuwa wanapishana angani (Refer to former FM). Lakini sasa idadi ya safari imepungua, tickets zinanunuliwa moja kwa moja kwa airline companies, kile cha juu tulichokuwa tunaibiwa na agents hakipo tena. Tatizo ni kuwa serikali haitwaambii wananchi wazi ni vipi hatua za kupunguza safari za nje zimefanyika na zimeokoa kiasi gani. Na watu wanafikiri ni JPM peke yake hasafiri safiri.

Mawazo mbadala sio uadui. Ila kuna mdudu mmoja mbaya sana, akitoa mawazo mbadala mtu wa CCM anaonekana ana nia mbaya, akitoa mawazo mbadala mtu wa upinzani anapuuzwa. Nadhani we need to be better than that, tuangalie quality ya maoni na sio nani ametoa. Lakini hata mtindo wa utoaji maoni wenyewe pia una-matter, ili maoni yakubalike. Kwa hiyo iwe ni mtu anayelipwa na CCM au anayelipwa na Upinzani kuja kupost lolote hapa, kama ni ujinga lisemwe wazi kuwa ni ujinga, kama ni la maana lipongezwe, na kuhimizwa.

Mkuu sina maana kuwa sasa mambo ndio mazuri saaaaaana. Changamoto bado zipo, na kweli uozo tuendelee kusema ili serikali ichukue hatua. Am sure watawala na watunga sera wetu wana nia njema, lakini miongoni mwao bado kuna watu ambao kidogo ni tatizo.
 

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
11,305
2,000
JPMi ni kiongozi mzuri ingawa siyo politician au economist mzuri. Anachofanya inaitwa a bitter pill that heals. Unfortunately mtoto akizaliwa huwa haanzi kukimbia papo hapo; itachukua miaka kabla ya watu kuona matunda ya juhudi hizo. Inaweza kuwa ni muda ambapo JPM hatakuwa madarakani tena.
 

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
14,179
2,000
"
Bongolander, post: 31790845, member: 3997"] Unajua ni kweli kuna watu wanaogopa kumwambia JPM hali halisi ya baadhi ya mambo, au wanaamua kukaa kimya kwa hofu ya kutumbuliwa, au kum-mislead kwa kujilinda wenyewe. Yote matatu hayajengi.
Swali, katika mazingira kama hayo , je, tunapiga hatua ''we have made progress''
Tunawezaje kusema '' si kila Mtanzania ni kichwa cha panzi''

Lakini uzuri ni kwamba JPM akiambiwa na akielewesha kupitia proper channels anachukua hatua, au hata akijua mwenyewe anachukua hatua.Mfano mzuri ni issue ya kikokotoo. Nadhani kila mtu alikaa kimya na kuacha wastaafu waumie.
Lakini JMP alisimama nataka itafutwe njia mbadala. Kwa kuwa kilio kilisikika na kimifikia
Kikokotoo ni mswada uliopelekwa Bungeni na Serikali. Miswada hupitiwa na vyombo husika ikiwemo Cabinet. Je, unataka kusema hilo halikutokea?
Kwa utaratibu wa kawaida, miswada hushirikisha wadau ambao hapa ni Wafanyakazi.
Je, walishirikishwa kikamilifu? Sarakasi za kutowasikiliza zilitengenezwa za nini?

Miswada hupitishwa na Bunge ambalo majority ni CCM. Je, nao walitaka kum-mislead kiongozi na serikali yao? Kwanini hawakuliona hilo lililpopigiwa kelele na Wapinzani!

Na mwisho, ili mswada uwe sheria lazima utie saini na Mh Rais.
Mswada huo ulikuwaje sheria bila Rais kuuona au kuupitia au Washauri wake kuupitia?
Kuna changamoto nyingine zipo hatuwezi kukataa, maana tunaziona, lakini tusitregemee kuona uozo wa miaka 30 unarekebishwa kwa miaka mitatu, will take more than that.
Ipi ni njia bora, kufanya mabadiliko ya mfumo, au kufuma sehemu zilizoharibika kwa njia za reja reja. Kwanini tunaendelea kutumikia mfumo ule ule unaotuletea matatizo bila kufikiria njia mbadala ya kutafuta suluhu ya kufumua mfumo na kuusuka upya
Hili la Rais kusafiri mkubwa it pains me like hell. In fact linaweza kupimwa. Tunaweza kuombaLakini sasa idadi ya safari imepungua, tickets zinanunuliwa moja kwa moja kwa airline companies, kile cha juu tulichokuwa tunaibiwa na agents hakipo tena.

Tatizo ni kuwa serikali haitwaambii wananchi wazi ni vipi hatua za kupunguza safari za nje zimefanyika na zimeokoa kiasi gani. Na watu wanafikiri ni JPM peke yake hasafiri safiri.
Tatizo ni wapiga debe wasiojua wanachoongelea, wasioweza kujenga hoja, wanaotafuta kiki na wasiojua mkakati hasa wa mawasiliano

Hoja hapa si Rais kusafiri bali ujumla wa kupunguza safari kwa kuangalia maeneo haya
1. Umuhimu wa safari
2. Wahusika wanaotakiwa kusafiri
3. Logistic za kusafiri na itinerary
4. Kutumia resource nyingine zilizo karibu kama ofisi za ubalozi
5. Idadi ya wahusika na majukumu yao katika umuhimu wake

Haya ndiyo yanayotakiwa kuelezwa na kutolewa hesabu ikibidi ili kuona tija za kubana matumizi

Wapambe hawaoni, hoja yao ni kusema Rais hasafiri na hilo ni kupunguza gharama

Matokeo yake hoja nzima inakuwa katika mgongo wa 'Rais' kwamba ndiye sehemu ya gharama

Rais kusafiri halijawa tatizo. Ndiyo maana anapewa rasilimali zote
Tatizo ni uratibu wa safari kama ilivyoelezwa hapo juu (namba 1-5)
Hayo ndiyo mapungufu ya awamu ya nne

Kuna tatizo jingine linalopewa nafasi bila kujua athari zake.
Kuna mtindo umezuka sijui ni makusudi au bahati mbaya au kutokujua.

Viongozi wanajishughulisha na vitu 'trivial sana'' hata kama kuna makubwa yanafanyika

Ingekuwa vema watu wakaongelea kilimo au viwanda na ubishi ukawa hapo kwa hoja

Kwanini tusiunganishe miundo mbinu kama reli, kwanini usafiri rahisi wa treni umekufa

Tunatumiaje gesi ya Mtwara kuondoka katika kuni. n.k n.k

Kinyume chake utasikia malumbano yasiyo na tija, leo kijana kakamatwa na bendera, kesho kuna mtu kavaa t-shirt, keshikutwa fulani kaitwa kituoni halafu kanyimwa dhama kwa hofu ya kukimbia hata kama amekwenda mwenyewe, Ijumaa mshahara unatosha kutoka na mchepuko, j'mosi waandishi wa habari ni machinga, J'pili utasikia RC ameagiza madaktari waandike dawa fulani, jumatatu DC kasweka watu ndani n.k n.k.

Hutasikia kiongozi anashangilia watu wake kupata maji safi, utasikia anashangilia mpinzani kurudi huku. Hawa wote ndio wanatakiwa kumsaidia Rais , ndio wenye ajenda ya viwanda
Katika hali hiyo tutafanikiwa kwa miujiza gani?
 

Bongolander

JF-Expert Member
Jul 10, 2007
5,062
2,000
Mkuu Nguruvi3 wewe mwenyewe unaona karibu kila kona ni mess, where do we start? What do we start with? Where would you start if you wore JPM shoes? Tuanze sekta ya Kilimo? usafiri? hata hiyo ya usafiri tuanze kwa reli? barabara? tusubiri kununua ndege mpya mwaka 3000? Tuanze sekta ya fedha? afya? tuanze kuboresha administration system, tuanze wapi? Ni vigumu sana kwa kuwa tumevuruga mambo mengi sana kwa muda mrefu. Uozo uko kila kona, tunatakiwa tuendelee kusema na kuweka mambo wazi ili serikali iyafanyie kazi. Kumbuka JPM alivyoingia madarakani....at some point alikiri mwenyewe kuwa "Kikwete umeniachia kazi ngumu".

Kama mtu anajua kuwa urais ni kazi ngumu, basi kwa busara ndogo tu ni kuwa the person is serious with the job. Lakini kama anauchukulia urais ni fursa ya kujipatia misifa na utukufu, hawezi kutusaidia. I believe kuwa JPM na timu yake wana nia ya kuiendeleza Tanzania at heart. (Licha ya kuwa dosari na changamoto zipo)

Ninaposema sio kila mtanzania ni kichwa cha panzi, maana yangu ni kuwa si kweli kama katika miaka mitatu hakuna la maana lililofanyika contrary to what opposition parties are trying to have us believe. There are lots of tangible outcomes, some of which directly touch our lives (Tuangalie kazi za TAMISEMI). Na pia sio kweli kuwa Tanzania tayari ni nchi ya asali na maziwa kama baadhi ya watu wa CCM wanaokuja hapa jamvini na kujaribu kutuaminisha, (there is no way uozo wa miaka mingi ukaondolewa kwa miaka mitatu). Sipendi notion ya baadhi ya watu kuwa CCM iko sahihi siku zote na wapinzani hawako sahihi. Au CCM haiko sahihi siku zote na wapinzani wako sahihi. Hili haliwezekani.

Nadhani cha muhimu ni kuwa tuendelee kutoa sauti kwa mambo ya msingi, tusiwe pawns wa wanasiasa. Kama hatuana imani na wanasiasa tukumbuke kuwa tuna civil service...so it is a matter of how to channel out thoughts.
 

Bongolander

JF-Expert Member
Jul 10, 2007
5,062
2,000
JPMi ni kiongozi mzuri ingawa siyo politician au economist mzuri. Anachofanya inaitwa a bitter pill that heals. Unfortunately mtoto akizaliwa huwa haanzi kukimbia papo hapo; itachukua miaka kabla ya watu kuona matunda ya juhudi hizo. Inaweza kuwa ni muda ambapo JPM hatakuwa madarakani tena.

Mkuu it is very unfortunate kuwa matunda ya kazi yake, yatakuwa wazi baada ya yeye kuondoka. Labda ni machache sana atayashuhudia akiwa madarakani. Nikiangalia stiglers Gorge najua huu ni mwimba mchungu sana kwa wenye nia mbaya (has ukizingatia kuwa WB na IMF hawawezi kupata faida kutokana na jinsi serikali ya JPM inavyougharamia mradi huu), lakini ukienda vizuri utakuwa na manufaa makubwa kwa Tanzania na watanzania. Gharama za umeme zitashuka, itakuwa big plus kwa Tanzania kama tukiwa tunalipa bili za umeme ndogo, sio kama sasa hata kutumia AC au majiko ya umeme tunaogopa. Na kama ndege zitaweza kusafiri moja kwa moja kutoka Mtwara hadi Kagera, toka Tanga hadi Rukwa, iwe kwa ndege au kwa gari, kwa mimi litakuwa jambo la maana sana.
 

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
14,179
2,000
Mkuu kuna maswali yangu niliuliza, sijui una maoni gani. Mjadala ni mzuri ukiwa endelevu
"Bongolander, post: 31805002, member: 3997"]unaona karibu kila kona ni mess, where do we start? What do we start with? Where would you start if you wore JPM shoes? Tuanze sekta ya Kilimo? usafiri? hata hiyo ya usafiri tuanze kwa reli? barabara? tusubiri kununua ndege mpya mwaka 3000? Tuanze sekta ya fedha? afya? tuanze kuboresha administration system, tuanze wapi? Ni vigumu sana kwa kuwa tumevuruga mambo mengi sana kwa muda mrefu. Uozo uko kila kona, tunatakiwa tuendelee kusema na kuweka mambo wazi ili serikali iyafanyie kazi. Kumbuka JPM alivyoingia madarakani....at some point alikiri mwenyewe kuwa "Kikwete umeniachia kazi ngumu".
Hapa kuna tatizo kubwa la mfumo. Kila mwaka tunasomewa mipango ya maendeleo .

Tunasomewa ilani za uchaguzi ambazo nyingi zimelenga katika kuondoa uozo.
Kwa bahati nzuri hatujawahi kuwa na chama kingine tawala ni CCM
inakuwaje basi kuna uozo na kurithishana uozo?

Nadhani jibu ni rahisi, ni mfumo na waliopewa dhamana ambao si watu bali CCM kwa ujumla

Hatuna sababu ya kuchagua wapi tuanzie, tunasababu za kujilaumu kushindwa kuwa na dira ya Taifa.

Hayo unayoeleza yanaeleza kwa kina kwamba hatuna mfumo sahihi unaotuongoza kwa mwaka, miongo au miaka. Tulichonacho ni maono ya nani yupo madarakani

Tulikuwa na elimu kwa wote ya Mkapa, tukaja na elimu kwa kila mwanafunzi ya Lowassa, ghafla ikaja kilimo kwanza ya Pinda na sasa ni Viwanda kwanza

Hivi lini tulifanyia tathmini ya kimoja kabla ya kuhamia kingine?
Tofauti ya Lowassa na Pinda ni ipi katika utawala mmoja ?

Yote hayo yanaeleza kuwa hatuna mfumo unaotuongoza, tunaamka na kubahatisha
Hatuishi kwa hesabu tunaishi kwa maono ya kila mmoja, kwa dunia ya leo huko si sahihi
Kama mtu anajua kuwa urais ni kazi ngumu, basi kwa busara ndogo tu ni kuwa the person is serious with the job. Lakini kama anauchukulia urais ni fursa ya kujipatia misifa na utukufu, hawezi kutusaidia. I believe kuwa JPM na timu yake wana nia ya kuiendeleza Tanzania at heart. (Licha ya kuwa dosari na changamoto zipo)
Kuhusu ugumu wa kazi ya Urais, Mwl Nyerere alisema ''...nimekaa pale Ikulu miaka 23, ni kazi ngumu kweli. Kila jambo ni mzigo wako'' Sasa nani hajui uzito wa kazi hiyo ?
Ninaposema sio kila mtanzania ni kichwa cha panzi, maana yangu ni kuwa si kweli kama katika miaka mitatu hakuna la maana lililofanyika contrary to what opposition parties are trying to have us believe. There are lots of tangible outcomes, some of which directly touch our lives (Tuangalie kazi za TAMISEMI). Na pia sio kweli kuwa Tanzania tayari ni nchi ya asali na maziwa kama baadhi ya watu wa CCM wanaokuja hapa jamvini na kujaribu kutuaminisha, (there is no way uozo wa miaka mingi ukaondolewa kwa miaka mitatu). Sipendi notion ya baadhi ya watu kuwa CCM iko sahihi siku zote na wapinzani hawako sahihi. Au CCM haiko sahihi siku zote na wapinzani wako sahihi. Hili haliwezekani.
Bila kuwa na mfumo sahihi unaotuongoza tutaendelea kuishi katika hali ya uozo kama ilivyokuwa.

Swali, hebu tupe tangible outcome za TAMISEMI tuzijadili

Kuhusu Wapinzani, sidhani kama unawatendea haki.

Hivi si hawa ndio waliopigia kelele fao la kujitoa la mifuko ya jamii hadi kubadilishwa?

Je, walikuwa waongo na kama ndivyo wapi walitudanganya.

Kazi ya opposition ni kuwa mbadala, inawezekana kabisa wanapotosha lakini suala la kuwazuia wasiseme linawapa upper hand.
Kama hakuna tatizo kwanini hoja isijibiwe kwa hoja?

Kwanini serikali ya CCM haiwezi kutetea hoja kama Stigler gorge, SGR na mengine mazuri tu kwa hoja bali kuwashambulia na kuwaandama Wapinzani?

Wengi wanaamini kwa dhati kuimarisha usafiri wa anga ni jambo jema kabisa.

Kinachoongelewa si ndege bali namna ya tunaendesha shirika bila kurudi kwa ATC

Na katika hili tayari kuna tatizo linajitokeza ambalo wananchi hawaambiwi

Ukiacha taratibu za uendeshaji ambazo bado zinafanyiwa kazi, mbinu za kuua mashirika mengine inaanza kuwagharimu wananchi. ATCL inatumia monopoly kwa namna isivyo

Kuimarisha usafiri wa anga hakumaanishi kutengeneza monopoly wananchi.

Kuimarisha kuna maana moja, kuufanya usafiri wa anga uwe affordable and reliable kwa wananchi katika kuendesha shughuli za kawaida na kibiashara

Ni nani ndani ya CCM iliyopoteza nguvu za chama anaweza kusimama na kusema kuna tatizo limejitokeza kutokana na monoply? Wapinzani wakisema wanakosea wapi?

Hatuwezi kusema tunapiga hatua za kuondoa uozo bila kuwa na mfumo utakaohakikisha uozo unaondoka bila kujali nani yupo madarakani.

Kama hatutakaa chini na kujitathmini kisha kutengeneza mfumo imara, kinachoonekana ni ''kumpa mgonjwa aspirin kutibu malaria''
Nadhani cha muhimu ni kuwa tuendelee kutoa sauti kwa mambo ya msingi, tusiwe pawns wa wanasiasa. Kama hatuana imani na wanasiasa tukumbuke kuwa tuna civil service...so it is a matter of how to channel out thoughts.
Mkuu civil service hazitakiwi kwa sasa.
Yule mwenezi wa chama anasema ''ukisema tutakata jina 2020''

Kuna missed opportunity kwa awamu ya tano, kuua uhuru wa mawazo, kuzuia uhuru wa mawazo, kuzuia uhuru wa habari n.k. Kwasasa hakuna civil service inayoweza kusema lolote
Ikiwa media haziwezi, ni civil society gani yenye mtima

Awamu ya nne iliruhusu sana uhuru wa maoni na kupata fursa nzuri ya kuelewa nini kinaendelea katika jamii.
Tatizo likawa kuchukua hatua za kushughulikia taarifa zinazopatikana

Laiti awamu ya tano ingetumia fursa hiyo, kungekuwa na fursa kubwa sana

Matatizo yote ynayoshughulikiwa sasa hivi ni yale yaliyosemwa katika awamu ya nne

Hakuna tatizo , ufisadi, wizi au deal mpya iliyoibuliwa. Ni yale yale tofauti ikiwa kuyashughulikia

Uhuru wa mawazo na habari una faida moja, ni kioo cha waliopo madarakani kuelewa nini kinaendelea huku mitaani katika maisha ya kila siku.
 

Bongolander

JF-Expert Member
Jul 10, 2007
5,062
2,000
Mkuu maswali yako nimeyaona. Yana mantiki sana, naomba nijaribu kuyatolea maoni polepole

Kuna baadhi ya mambo ni lazima tukubali. CCM kama chama idara yake ya habari imeshindwa kuandaa hoja za kumuunga mkono Rais na serikali kwenye miradi inayotekelzwa sasa. Mpaka sasa mbali na cosmetic statements za wanasiasa, bado hakuna organised and systematic efforts to communicate na watanzania umuhimu na ulazima wa miradi kama Stiglers Gorge au SGR. Unajua mpaka sasa hata ukitoka mtaani muulize mtanzania mwenye elimu kiasi, haiwezi kukupa jibu la maana. Hii ina maana idara ya uenezi ya CCM ikubali kuwa kuna dosari mahali fuilani kwenye kazi zake, Mr. POLEPOLE ni member hapa, sijui kama anaweza kuja na kutueleza. Tunasikia tu watu wanasema “haijawahi kutokea Afrika, haijawahi kutokea tangu Uhuru” and so on and so forth, hizo kabisa sio hoja zenye akili kuisemea na kutetea miradi mikubwa kama hiyo, na ku-rally support behind....... So tunaweza kusema kuna mambo makubwa yanafanywa na JPM as individual, CCM as Party, and the Government as whole, lakini chama tawala chenyewe hakina mechanism makini ya kutetea yale yanayofanywa na chama na serikali. Labda wanaona kuwa sisi watanzania ni mbumbumbu hakuna sababu ya kuambiwa. (May be)

Hili la kusema mtu akizungumzia 2020 atakatwa jina naona ni cheap talk, haya mambo yanatakiwa kuongelewa na kukemewa kwa umakini sana. Iwekwe wazi kuwa licha ya uzuri na umuhimu wa demokrasia na uhuru wa kuongea, maendeleo ni namba moja. We should not be a country where the focus is only on politics and elections, not on development. Utamaduni wa miaka 10 kwa CCM ni bora ukiheshimiwa, na katika miaka hiyo 10 concentration iwe kwenye maendeleo, kama kukosoana tukosoane kwa lengo hilo. Bahati mbaya hilo ni kama halipo, kuna watu wanalofikiria 2020, wengine wanafikiria kukata majina na wengine kukatwa majina, (wote wawili hawafikirii maendeleo, this is tragedy) Hii naweza kusema ni internal power struggle ya CCM, na haitakiwi kuathiri maendeleo ya nchi, au kuwa kisingizio cha kuwaadhibu wanaotoa genuine alternative opinion.

Tumefika mahali ni kwamba hata priorities hatuna. Ndio maana umesema kulikuwa na kilimo kwanza, kuliko na elimu kwanza, ndani ya serikali moja. Serikali yenyewe ya JK chini ya ma-PM tofauti ilikuwa na vipaumbele tofauti. Leo tukisema tupime matokeo yake jibu ni 0, labda watakuja watu wa spin watasema ilikuwa na mafanikio sana. Kwa hiyo kuna tatizo Chama tawala hakijaweka wazi priority ni ipi, serikali nayo haijaweka wazi, maana vipaumbele vinabadilika kutokana na Rais. Sina hakina kama hili ni sahihi. Moja ambalo naweza kusema nimelipenda ni barabara, ambalo kidogo linaonekana kuwa endelevu, toka Mkapa, JK na sasa JPM linaonekana ninazingatiwa.

Hili la kumfikishia ujumbe Rais nakubaliana na wewe. Unajua hata ukisikia hotuba za Rais, unaweza kuona kuwa kuna watu kama wanaogopa kusema. Ni kama wanataka kuonekana kwa rais kuwa wanafanya kazi nzuri kwenye maeneo yao, hence rais ajisikie kuwa mambo yanaenda vizuri, lakini ukienda kwenye ground the situation is not as it is being said. Na Rais mwenyewe akijua anatumbua.

Mimi bunge mara nyingi nimekuwa na mashaka sana na muundo wake. Maana inaonekana kama bungeni maslahi ya vyama na ya wabunge yanakuwa mbele kuliko maslahi ya taifa. Wana CCM kama hoja ikiletwa na CCM hata kama sio nzuri, basi wataunga mkono kwa asilimia zote bila hata kuipitia kwa kina na kuijua kiundani, (KIKOKOTOO). Hata kama wanajua kwa kina na wanaona dosari, just for the sake of collective responsibility wataunga mkono. Same applies kwa wapinzani, hata kama wanaunga mkono hoja, just because wako upinzani watapinga for the sake of collective responsibility. Hili ni tatizo. Binafsi ningependa bunge liwe la chama kimoja, au lisiwe na vyama kabisa…. Lakini nakumbuka kuna siku Rais JPM alimsifia wazi Bw. Kafurira kwa kukemea wizi kwenye sekta ya madini, and that is unprecedented.


Kuna mahali umeuliza kuwa kipi bora kufanya mabadiliko ya kimfumo, au tuendelee na mfumo huu na kuweka viraka kwenye matatizo. Ugumu wa swali hili ni kuwa sisi wenyewe hatujui vizuri tunafuata mfumo gani. Ujamaa na kujitegemea? Ubepari na kuendeleza mfumo wa mtaji? Uliberali na kutegemea misaada? Tukiwa na jibu, ndio tunaweza kuanza kazi ya kubadilisha mfumo. Au tunazungumzia mfumo wa utendaji wa civil service kutoka kuangalia tatizo, kulifanyia majadiliano, kufanya maamuzi, kutoa maigizo na utekelezaji? Still not very clear. Hiyo ni challenge.

Ni kweli pia kuna baadhi ya watu wanapenda kujionesha kuwa wanatumia madaraka, nadhani hiyo imeanza kuonekana na akusema. Mtu anataka kuytoa maagizo tu au amri aonekane kwenye media, lakini the actual fact ni kuwa kazi hawafanyi, but pretending to work. Au kuna wengine wanafanya uozo wanasema hapa kazi tu kama alivyosema Rais juzi. Hapo tunakubaliana kabisa kuwa these guys are doing more harm to the country than good. Kweli kwa mtindo huo hata hiyo sera ya viwanda itakuwa kwenye hatihati. 

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
14,179
2,000
"Bongolander, post: 31816213, member: 3997"]CCM kama chama idara yake ya habari imeshindwa kuandaa hoja za kumuunga mkono Rais na serikali kwenye miradi inayotekelzwa sasa. Mpaka sasa mbali na cosmetic statements za wanasiasa, bado hakuna organised and systematic efforts to communicate na watanzania umuhimu na ulazima wa miradi kama Stiglers Gorge au SGR.
Hapa ninapata tatizo la kukuelewa. Kwa nchi yetu, Chama huteua mgombea na hapa ni CCM.

Mgombea huuza sera za chama kwa wapiga kura.
Mgombea akishinda anaunda serikali inayotokana ili kutekeleza ilani ya chama, again CCM

Sasa mkanganyiko unatoka wapi?

Unasababishwa na nini ikiwa sera zimeandaliwa na chama chake?
Chama kinashindwaje kueleza sera zake kwa kumshauri Rais mwenye kuunda serikali?
Kwa maelezo yako hakuna coordination kati ya chama na serikali
Binafsi ningependa bunge liwe la chama kimoja, au lisiwe na vyama kabisa….
Tunawezaje kuwa na Bunge lisilotokana na vyama?

Unaposema ni afadhali Bunge la chama kimoja, ni kwa mantiki gani!
Kwamba Bunge tulilokuwa nalo wakati wa chama kimoja lilikuwa effective zaidi ya sasa

Lakini pia tujiulize, katika Bunge la sasa 2/3 majority ni CCM wanaoweza kufanya jambo lolote bila kuhitaji kura hata moja ya mpinzani.
Kuna tofauti gani ya Bunge la chama kimoja na la sasa

Labda utusaidie kuelewa Wabunge wa upinzani wamekwamisha nini hadi sasa kwa 1/4 minority
Kuna mahali umeuliza kuwa kipi bora kufanya mabadiliko ya kimfumo, au tuendelee na mfumo huu na kuweka viraka kwenye matatizo. Ugumu wa swali hili ni kuwa sisi wenyewe hatujui vizuri tunafuata mfumo gani. Ujamaa na kujitegemea? Ubepari na kuendeleza mfumo wa mtaji? Uliberali na kutegemea misaada? Tukiwa na jibu, ndio tunaweza kuanza kazi ya kubadilisha mfumo. Au tunazungumzia mfumo wa utendaji wa civil service kutoka kuangalia tatizo, kulifanyia majadiliano, kufanya maamuzi, kutoa maigizo na utekelezaji? Still not very clear. Hiyo ni challenge.
Hili la mfumo ninaliongelea kwa maana ya utaratibu wa kujitawala. Huko nyuma umeongelea uozo wa kila mara unaojitokeza

Tatizo letu ni kutokuwa na utaratibu unaotuhakikishia kuwa tunajitawala kimfumo mahususi, tunabahatisha tu. Mfumo ni KATIBA
 

Bongolander

JF-Expert Member
Jul 10, 2007
5,062
2,000
Mkuu hapa ni kuangalia reality za nchi yetu. Ukiangalia utendaji wa JPM anaonekana angalia zaidi nchi. Kimsingi ukiangalia utendaji wa Magufuli unaweza kuona wazi kuwa ni kama aliingia madarakani kwa tiketi ya CCM lakini kinaongoza chama kingine, mambo yalivyo si biz as usual kabisa. Kuna mabadiliko sana. Tunaweza kusema CCM ya Magufuli ni tofauti kabisa na CCM ya Kikwete. Sidhani kama issue kwa Tanzania ni sera, naona kama sera za vyama vyote zinafanana, labda tofauti ziko ndogo ndogo. Wapinzani bado hawajashika dola kuona watatekeleza vipi. Lakini tumeona kabisa kuwa CCM awamu na nne na awamu ya tano, ni CCM mbili tofauti kabisa, japo sera ni zile zile. Na kama ukiangalia kwa undani unaweza kuona kuwa JPM hataki kukwamishwa na politics kwenye utendaji wake. Kwa hiyo kufikiri kuwa hakuna muunganiko mkubwa kati ya CCM na serikali ni sahihi.

Ninachokiona in regard to CCM, serikali ya sasa ya CCM inajaribu kukirudisha chama kwa wananchi na wanachama, baada ya serikali mbili zilizopita kukiuza kwa matajiri.

Tatizo halipo kwa wabunge wa upinzani, maana mpaka sasa wao hawana nguvu ya kusukuma utekelezaji wa maamuzi. Tatizo lililopo ni kukosekana kwa uwiano wa wabunge, kunakofanya bunge lisiwe na msukomo makini kwa serikali. Ingekuwa 50% kwa 50% tungeweza kuwa na msingi wa kulaumu, kwa sasa kinachoamuliwa na CCM kinapita bungeni moja kwa moja bila hata kuchujwa ipasavyo, simply because ni cha CCM. Hapa ndio tatizo. Kama tungekuwa na utaratibu wa kuchagua wabunge wa kujitegemea labda tungekuwa na bunge huru na lene nguvu ya kuisukuma serikali, kwa sasa sherif zetu zinalazimisha mbunge awe na chama.

Kama kweli unafikiri tatizo la kimfumo ni katiba, you are very wrong. Nitakubali kuwa katiba ni tatizo, kama hii iliyopo ikitekelezwa kikamilifu. Kuanza kuilaumu katiba wakati dosari ni za kiutendaji, hasa kutosimamia sheria za sasa, ni kumiss point. Bora tutekeleze katiba kikamifu, halafu tuangalie ni papi kuna dosari, then ndio tubadilishe. Kenya walifikiri issue ni katiba, lakini hatuoni tofauti kubwa kati ya katiba ya sasa na iliyopita. Na pia kama utawala wa Mkapa, JK na JPM zinakuwa tawala tatu tofauti sana wakati chama ni kile kile, na katiba ya nchi ni ileile, ile basi ina maana kuwa tatizo liko pengine, sio kwenye katiba.
 

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
14,179
2,000
"Bongolander, post: 31827986, member: 3997"]Tunaweza kusema CCM ya Magufuli ni tofauti kabisa na CCM ya Kikwete. Sidhani kama issue kwa Tanzania ni sera, naona kama sera za vyama vyote zinafanana, labda tofauti ziko ndogo ndogo.
Nilidhani kuwa mipango inaongozwa na sera. Kama hukuna sera si ndio mwanzo wa kuwa na kilimo kwanza, elimu kwanza viwanda kwanza n.k.

Huoni kuna tatizo kwamba hatujatathmini kimoja tunahamia kingine.
Lakini pia sera zinaeleza mengi kuhusu elimu, afya na jamii kwa ujumla
Ni wapi wanakoendelea bila kuwa na sera kama mwongozo?
Lakini tumeona kabisa kuwa CCM awamu na nne na awamu ya tano, ni CCM mbili tofauti kabisa, japo sera ni zile zile. Na kama ukiangalia kwa undani unaweza kuona kuwa JPM hataki kukwamishwa na politics kwenye utendaji wake.
Hapa unatueleza kuwa ''nguruwe ni haramu lakini mchuzi wake ni halali''.

Urais ni mamlaka yanatotokana na siasa, na uongozi uliowekwa kisiasa hauwezi kukwepa shughuli za siasa.

Kama ni hivyo kwanini tusivunje taasisi zinazohusiana na siasa kama Bunge tuwe na serikali tu inayofanya kazi bila kujishughulisha na siasa?
Ninachokiona in regard to CCM, serikali ya sasa ya CCM inajaribu kukirudisha chama kwa wananchi na wanachama, baada ya serikali mbili zilizopita kukiuza kwa matajiri.
Unaweza kusema kwa dhati kabisa CCM ya leo na ya Mwalimu au Mwinyi au Mkapa zinalingana kwa ukaribu wa chama na Wananchi

Ingalikuwa ni ukaribu unaosema hawa akina Bashe, Nape na wengine wasingetishwa kukatwa majina kwa kzungumza yale yanayowagusa wananchi. Kwanini watishwe?

Ile nguvu ya CC na Halmashauri kuu ya CCM unaiona zama hizi?

Ukimya hauna maana ya kuridhika, ukimya unaweza kueleza zaidi kuliko 'ukimya' uliopo
Nadhani mtu aliyejitahidi kuirudisha CCM kwa wananchi ni Mzee Kinana na Nape
Kama tungekuwa na utaratibu wa kuchagua wabunge wa kujitegemea labda tungekuwa na bunge huru na lene nguvu ya kuisukuma serikali, kwa sasa sherif zetu zinalazimisha mbunge awe na chama.
Well said, kwa ufupi unaunga mkono hoja ya mfumo hasa Katiba ni tatizo kama ambavyo inatunyima Wabunge wa kujitegemea.
Kwa hili umejibu hoja ya umuhimu wa katiba vema
Kama kweli unafikiri tatizo la kimfumo ni katiba, you are very wrong.
Nitakubali kuwa katiba ni tatizo, kama hii iliyopo ikitekelezwa kikamilifu.
Kuanza kuilaumu katiba wakati dosari ni za kiutendaji, hasa kutosimamia sheria za sasa, ni kumiss point. Bora tutekeleze katiba kikamifu, halafu tuangalie ni papi kuna dosari, then ndio tubadilishe.
Nimesimama na hoja ya katiba kwa muda wote nikiwa JF, na nasimama nayo
Kila siku kuna proof kuhusu katiba

Kutotekelezwa katiba si bahati mbaya wala si makusudi.
Ni mapungufu ya katiba yenyewe yanayotoa loophole ya kutotekelezwa

Hoja kwamba tusimamie sheria ili kutekeleza katiba ina tatizo.

Sheria zinasimamiwa zikiwa huru .
Kwa mfumo wetu uliopo kwa katiba hii ya 1977 kuna loophole nyingi za kui-abuse

Hapa nikuulize kuna chombo gani au vyombo gani huru vinavyoweza kusimamia katiba hii hii tuliyo nayo? Ukinijibu hili tutaweza kujadili zaidi kwasababu zipo hoja za msingi sana
Kenya walifikiri issue ni katiba, lakini hatuoni tofauti kubwa kati ya katiba ya sasa na iliyopita. Na pia kama utawala wa Mkapa, JK na JPM zinakuwa tawala tatu tofauti sana wakati chama ni kile kile, na katiba ya nchi ni ileile, ile basi ina maana kuwa tatizo liko pengine, sio kwenye katiba.
Tanzania tulikuwa ''gold standard' za mambo ya kujitawala sijui hilo limeishia wapi.

Kuna msemo mmoja kwamba, idea zinatoka Tanzania, zinakuwa developed Uganda na zinatekelezwa Kenya.

Mapungufu ya Kenya huenda yanatokana na msingi mbovu. Vipi sisi tukijaribu utaratibu wetu?

Tawala au awamu zinakuwa tofauti sana kwasababu moja, kwamba, hatuna muongozo wa nchi unaotuweka katika njia moja.

Kwa maana hiyo kila dereva ilimradi amekalia usukani anatupeleka anakotaka si kule tunakotaka

Maderava wa kisiasa hupatikana katika vyama kwa taratibu zao.

Muhimu, wanapopewa usukani kuwe na mwongozo tunaokubali wote kwamba huku ndiko tunakotaka kuelekea

Mwongozo hutangenezwa na sheria mama Katiba.

sera zoote lazima ziakisi Policy za nchi si za vyama.

Kwa maana hiyo kuna sera zinazobadilika lakini kama Taifa lazima tuwe na sera za kitaifa na thamani zake ''values''

Mfano, sera ya nchi inaweza kusema ''mfumo wetu wa elimu kuanzia chekechea hadi chuo kikuu uwe abcd'' Bila kujali nani yupo madarakani huo ndio utaratibu wa nchi

Katika vyama ndiko kuna sera za namna gani ya kutekeleza sera hiyo ya kitaifa

CCM wanaweza kusema mfumo na sera ya elimu ya nchi iwe ''public funded'
Chadema wanaweza kusema mfumo na sera ya elimu ya nchi iwe ''private'
Wajamaa ACT wakasema wanataka mfumo uwe wa '' public lakini pia uchangiwe private''

Hizo ndizo sera zinazoweza kuuzwa kwa wananchi lakini lengo ni kuwa na sera ya nchi ya elimu iliyokubaliwa kwa pamoja na wananchi
 

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
14,179
2,000
"Bongolander, post: 31816213, member: 3997"]
Utamaduni wa miaka 10 kwa CCM ni bora ukiheshimiwa, na katika miaka hiyo 10 concentration iwe kwenye maendeleo, kama kukosoana tukosoane kwa lengo hilo.
Hayo ya muda ndani ya uongozi ni tatizo lenu CCM. Tafuteni suluhu, siyo suala la kitaifa
 

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
11,818
2,000
Nadhani cha muhimu ni kuwa tuendelee kutoa sauti kwa mambo ya msingi, tusiwe pawns wa wanasiasa. Kama hatuna imani na wanasiasa tukumbuke kuwa tuna civil service...so it is a matter of how to channel out thoughts.
Bongolander, tatizo lako la msingi ni kwamba ama kwa kukusudia au kwa bahati mbaya, umeamua kutuita sisi ndugu zako Watanzania ama tusiokubaliana nawe au tuaothubutu kumkosoa JPM...ama ni vichwa panzi au ni wasaliti wa taifa.

Pia kwa makusudi mazima umeamua kupotosha msimamo wa watu kama mimi niliyekuwa mkosoaji mkubwa wa awamu iliyopita na bado naendelea kuwa mkosoaji mkubwa wa awamu hii...ama hufahamu au huelewi msingi wa huo ukosoaji kutoka kwa baadhi yetu.

Vyovyote vile kwa ufupi sana nitaeleza ili kama ulikuwa hujui uweze kufahamu na kama ulikuwa huelewi uweze kujua ni kwa nini msimamo wa baadhi yetu umebakia kama ulivyo. Bongolander, tunacholilia ni uongozi unaoheshimu, unaotetea na unaolinda Katiba, period.

Tulililia uongozi huo wakati wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete na bado tunaulilia uongozi kama huo wakati huu wa Rais John Pombe Magufuli, utawala unaoheshimu sheria. Katiba ni msingi, na nyumba bila msingi imara, ingawa awali itasimama haiwezi kubaki salama.

Ni kweli uongozi wa Kikwete ulikuwa dhaifu na hivyo kutomudu utawala unaozingatia sheria tofauti na uongozi huu wa kibabe wa Magufuli ambapo uongozi unaonekana uko juu ya sheria na matokeo yake ni kama vile sheria ndiyo inatakiwa kuzingatia utawala.

Athari za aina hizi mbili ya uongozi zinafanana ila hiyo ya pili ni hatari zaidi kwa mshikamano na maendeleo kama taifa na historia ni mwalimu mzuri sana kwa hatma ya taifa uongozi unapokuwa juu ya sheria. Kiongozi kuwa juu ya Katiba si uongozi, ni udikteta.

Naomba nikuulize swali Bongolander, je unakubaliana na madai ya baadhi ya Watanzania kuwa ni sawa tu Rais kutofuata Katiba kama nia yake ni nzuri? Sisi wengine tunasema, hapana, kama kweli nia ya Rais John Pombe Magufuli ni nzuri, kwa nini aogope kufuata Katiba?
 

Bongolander

JF-Expert Member
Jul 10, 2007
5,062
2,000
Bongolander, tatizo lako la msingi ni kwamba ama kwa kukusudia au kwa bahati mbaya, umeamua kutuita sisi ndugu zako Watanzania ama tusiokubaliana nawe au tuaothubutu kumkosoa JPM...ama ni vichwa panzi au ni wasaliti wa taifa.

Heshima yako mkubwa, kwanza niweke vizuri. Kutokubaliana kimawazo hayta siku moja si usaliti. na ukiangalia kwa auandani unaweza kuona kuwa hata kama tunatofautiana kimawazo, lengo letu ni moja, kuiona Tanzania yetu inakuwa bora.

Mimi sioni kama ni vibaya kumkosoa Magufuli. Hata yeye mwenyewe huwa anajikosoa, na pale anapoona amekosea anajaribu kubadilisha. Kwa hiyo kumkosoa sioni kama ni jambo baya. The whole point of my post ni kuwa tunatakiwa tu ackonwledge kuwa tangu aingine madarakani, kuna mambo tumepiga hatua, Hili tukubali. Kuna mambo tumerudi nyuma pia that is fact too. Lakini tuangalie realities za nchi yetu.

Uongozi wa kufuata sheria na unaoheshimu katiba kweli unafaa sana, kama haufanyi usanii. Nadhani wengi tunapenda tufike huko, ambako bado hatuajafika. Iwe ni sababu ya kuwa na mashaka na katiba yenyewe, au iwe ni sababu ya mianya ndani ya katiba, au kukosa muundo imara wa kulinda na kutetea katiba. Tatizo langu mimi kwenye issue hii ni kuwa, kuna wale ambao wanatumia katiba kutuibia au kutufanya tuwe duni, na wengine wanatumia katiba kwa maslahi binafasi na sio maslahi makuu ya taifa. Hapa ni wote wana CCM na wapinzani.

Lakini kuna wengine ambao ndio nawalaani zaidi, wanapenda kujionyesha (kwa nchi za magharibi) kuwa wanafuata katiba lakini gharama yake kwa taifa ni kubwa, ni kama tunagharamia mchezo wao. Hawa nawachukia. Kwangu mimi binafasi maendeleo ni kitu cha kwanza na cha msingi kabisa. Mengine yanafuata. Nadhani hapa jamvini tofauti yetu iko kwenye mawazo ya namna ya kufikia maendeleo hayo.

Swali na mwisho uliloniuliza kama naweza kusema ni swali gumu kwangu. "Kukiuka katiba kwa nia nzuri??" MImi binafsi kutokana na kiwango cha maendeleo ya nchi, nisingependa kitu chochote kinizuie kuleta maendeleo ya nchi, iwe katiba, iwe chama au hali yoyote. Kipaumbele ni Maendeleo. Lakini nachukia watu wanaojaribu kutumainisha kuwa JPM anavunja katiba as if Mwalimu, Mzee Ruksa, Mkapa na JK hawakufanya hivyo. Ukiangalia kuna cases nyingi tu ziliwahi hata kufikishwa mahakani kuhusu ukiukaji wa katiba. That is not the issue for Tanzanians. Issue kwa sasa ni maendeleo.
 

Bongolander

JF-Expert Member
Jul 10, 2007
5,062
2,000
Naomba utuongoze katika kujadili hili la mafanikio ya TAMISEMI

Tafdhali sana
Mkubwa kwanza nijikusanye kidogo, haya ya TAMISEMI sinayo karibu lakini yapo. Will get back.

Lakini naoamba wewe na wana JF wengine msinielewe vibaya. Sina maana kuwa Tanzania sasa chini ya JPM taabu zote au matatizo yote yameisha. Yapo mengi sana, itachukua muda mrefu sana kwa matatizo ya Tanzania na watanzania kwisha. Tusiiangalie nchi kwa picha ndogo ya mtu mmoja au chama kimoja.

Tukiangalia kwa undani na mapana, tunaweza kuona kuwa kuna mwelekeo tofauti wa utendaji, mambo yatabadilika, tuombe mwelekeo uwe hivi ili tuweze kuwa na matokeo ya haraka.
 

Bongolander

JF-Expert Member
Jul 10, 2007
5,062
2,000
Hayo ya muda ndani ya uongozi ni tatizo lenu CCM. Tafuteni suluhu, siyo suala la kitaifa

Mkubwa unajua ni kwamba ndani ya CCM yenyewe, kama ailivyo kwenye vyama vingine vya siasa na hata jamii nzima ya Tanzania, kuna matatizo yake. Kwa kuwa CCM imeshikata hatamu, uozo wake unaonekana zaidi na unaathiri taifa. Tukiwa na kiongozi wa CCM fisadi, bila shaka ufisadi wake unaathiri taifa. Lakini mtu wa ACT akiwa Fisadi au Chadema Fisadi, ufisadi wake ni limited kwa chama chake. Kwa hiyo kinachotokea CCM bila shaka kinawahusu hata wasio wanaCCM, maana kwa sasa CCM ndio iko madarakani, na mambo ya CCM yanalihusu taifa.
 

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
11,818
2,000
Heshima yako mkubwa, kwanza niweke vizuri. Kutokubaliana kimawazo hata siku moja si usaliti.
Naona unaishi dunia ya peke yako ndugu yangu, dunia ya kufikirika na si hii Jamhuri yetu ya Muungano, Tanzania! Je umejiuliza na kutafakari kwa nini baadhi ya wananchi wenzetu, ndugu zetu na rafiki zetu wanatekwa, kuteswa, kumiminiwa risasi na kuokotwa kwenye viroba wakiwa maiti?
...na ukiangalia kwa auandani unaweza kuona kuwa hata kama tunatofautiana kimawazo, lengo letu ni moja, kuiona Tanzania yetu inakuwa bora.
Hakuna jambo la hatari katika awamu hii kama kutofautiana kimawazo na utawala na hali hii imefanya wananchi waishi kwa woga kuliko wakati wowote toka tupate uhuru. Kwa mara ya kwanza serikali imekiri kuwa kuna kundi la watu wasioonekana wala kujulikana linaloteka, kutesa na hata kuwaua wenye mawazo tofauti na hasa wapinzani.
Mimi sioni kama ni vibaya kumkosoa Magufuli. Hata yeye mwenyewe huwa anajikosoa, na pale anapoona amekosea anajaribu kubadilisha. Kwa hiyo kumkosoa sioni kama ni jambo baya.
Bila shaka hujawahi kujiuliza hatma ya kijana mwanaharakati, Ben Saanane, ambaye alipata ujasiri wa kumkosoa Magufuli. Mbunge na kiongozi mwandamizi wa Upinzani Bungen, Mh. Tundu Lissu, sasa ni mwaka wa pili akiwa kwenye matibabu nje ya nchi baada ya kumiminiwa risasi zilizotosha kumwangusha tembo mchana kweupee katika eneo lenye ulinzi 24/7, kisa? Kuukosoa utawala wa Rais Magufuli!
The whole point of my post ni kuwa tunatakiwa tu ackonwledge kuwa tangu aingine madarakani, kuna mambo tumepiga hatua, Hili tukubali. Kuna mambo tumerudi nyuma pia that is fact too. Lakini tuangalie realities za nchi yetu.
It is also a fact kwamba hakuna Rais hata moja ambaye wakati wa uongozi wake taifa halikupiga hatua yoyote kimaendeleo! Hata hivyo kama walivyowahi kusema wahenga, good is never enough where better is possible. Katika awamu hii na bila kumung'unya maneno hatua za kurudi nyuma zimefunika hatua za kusonga mbele na huo nao ndio ukweli mchungu.
Uongozi wa kufuata sheria na unaoheshimu katiba kweli unafaa sana, kama haufanyi usanii. Nadhani wengi tunapenda tufike huko, ambako bado hatuajafika. Iwe ni sababu ya kuwa na mashaka na katiba yenyewe, au iwe ni sababu ya mianya ndani ya katiba, au kukosa muundo imara wa kulinda na kutetea katiba.
@Bongolander, koleo liite kwa jina lake...tafadhali sana usiliite kijiko! Kwa tulipofika tatizo si Katiba, tatizo ni kiongozi kuamua kutofuata Katiba. Kama tatizo lingekuwa Katiba, ndani ya Katiba hiyo hiyo ziko njia za kuifanyia marekebisho au maboresho bila kuvunja sheria. Wanaoamua kwa makusudi kutofuata Katiba ni mafashisti au madikteta uchwara. Dikteta anayejiamini hasiti kutumia Katiba hiyo hiyo kujipa uhalali wa kuwa dikteta lakini dikteta uchwara hujitwalia madaraka haramu kimabavu. Huu ni woga na si ujasiri na kiongozi kama huyo hujificha nyuma ya maendelao hewa.
Tatizo langu mimi kwenye issue hii ni kuwa, kuna wale ambao wanatumia katiba kutuibia au kutufanya tuwe duni, na wengine wanatumia katiba kwa maslahi binafasi na sio maslahi makuu ya taifa. Hapa ni wote wana CCM na wapinzani.
Acha kudanganya watu ndugu yangu, hakuna Katiba inayoruhusu vitendo vya kihalifu, hakuna kipengele chochote ndani ya Katiba yetu pamoja na mapungufu yake inayoruhusu wizi. Wenye ujasiri wa kufanya hivyo ama wanavunja sheria au wanajiona wako juu ya Katiba na kwa utawala wa awamu hii wametamalaki kila moja kwa ngazi yake. Swali ni je aliyeapa kuheshimu, kutetea na kulinda hiyo Katiba na Katiba hiyo hiyo ikampa mamlaka na vyombo vyote vya kuilinda yuko wapi?
Lakini kuna wengine ambao ndio nawalaani zaidi, wanapenda kujionyesha (kwa nchi za magharibi) kuwa wanafuata katiba lakini gharama yake kwa taifa ni kubwa, ni kama tunagharamia mchezo wao. Hawa nawachukia.
Bila shaka hapa unajaribu kuwalaani wale wanaopigia kelele uvunjifu wa Katiba ama siyo? Kwamba kudai utawala unaozingatia sheria (Katiba) ni jambo la kulaaniwa na linalolitea taifa matatizo, fedheha na gharama? Masikini Tanzania, kweli tumefikia hapa!
Kwangu mimi binafasi maendeleo ni kitu cha kwanza na cha msingi kabisa. Mengine yanafuata. Nadhani hapa jamvini tofauti yetu iko kwenye mawazo ya namna ya kufikia maendeleo hayo.
Naomba nikukumbushe tu msingi wa Katiba yetu, nanukuu...

"KWA KUWA SISI Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tumeamua rasmi na kwa dhati kujenga katika nchi yetu jamii inayozingatia misingi ya uhuru, haki, udugu na amani:

NA KWA KUWA misingi hiyo yaweza tu kutekelezwa katika jamii yenye demokrasia ambayo serikali yake husimamiwa na Bunge lenye wajumbe waliochaguliwa na linalowawakilisha wananchi, na pia yenye Mahakama huru zinazotekeleza wajibu wa kutoa haki bila woga wala upendeleo wowote, na hivyo kuhakikisha kwamba haki zote za binadamu zinadumishwa na kulindwa, na wajibu wa kila mtu unatekelezwa kwa uaminifu."


Bila shaka Bongolander, huu msingi wa Katiba yetu hauna maana yoyote kwako.
Swali na mwisho uliloniuliza kama naweza kusema ni swali gumu kwangu. "Kukiuka katiba kwa nia nzuri??" MImi binafsi kutokana na kiwango cha maendeleo ya nchi, nisingependa kitu chochote kinizuie kuleta maendeleo ya nchi, iwe katiba, iwe chama au hali yoyote. Kipaumbele ni Maendeleo.
Hata kama Watanzania, wananchi wenzako, ndugu zako, jirani zako, marafiki zako wenye mawazo mbadala wanatekwa, wanateswa na wanauawa twende tu, tutafika...kipaumbele ni maendeleo! Swali linalozuka hapa ni je kwa nini tunahitaji maendeleo?
Lakini nachukia watu wanaojaribu kutumainisha kuwa JPM anavunja katiba.
Je wewe? Unajaribu kutuaminisha kuwa JPM havunji Katiba? Je Katiba inaruhusu wananchi wenye mawazo mbadala kunyamazishwa kwa namna yoyote ile? Je Katiba inamruhusu JPM kutwaa madaraka ya Bunge? Je Katiba inamruhusu JPM kuwa juu ya sheria? Je, je , je?
as if Mwalimu, Mzee Ruksa, Mkapa na JK hawakufanya hivyo. Ukiangalia kuna cases nyingi tu ziliwahi hata kufikishwa mahakani kuhusu ukiukaji wa katiba. That is not the issue for Tanzanians. Issue kwa sasa ni maendeleo.
Tuseme Mwalimu, Mzee Rhuksa, Mkapa na JK walifanya hivyo, je inahalalisha huu utawala wa kikatili? Ah, unasema issue ni maendeleo, sawa...utadhani wakoloni hawakuleta maendeleo yoyote.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions
Thread starter Title Forum Replies Date
Mlenge Mkopo wa Elimu ya Juu kwa Kila Muombaji Great Thinkers 2

Similar Discussions

Top Bottom