Si jukumu la Watoto kukuhudumia uzeeni...

Noma sana yani . Na inakubid uwajibike tu no way out
Hapana mkuu, hawa wazee wetu ukiwadekeza watakirithisha umasikini wao, do what is right mbele za Mungu, usifanye kuwaridhisha binadamu wakati moyoni una manung'uniko, hata Mungu utakuwa unamkosea.
 
Hapana mkuu, hawa wazee wetu ukiwadekeza watakirithisha umasikini wao, do what is right mbele za Mungu, usifanye kuwaridhisha binadamu wakati moyoni una manung'uniko, hata Mungu utakuwa unamkosea.
Yaani hatari Sana , vp ww swala la ndugu mbali na wazaz wako. Huombwi kila wiki ?.
 
Yaani hatari Sana , vp ww swala la ndugu mbali na wazaz wako. Huombwi kila wiki ?.
Kinachonisaidia ndugu sikuwaga na mazoea ya kuwatembelea since nikiwa mdogo, hicho kimenisaidia sanaa.

Ila ndugu wa damu mizinga iko palepale, hasa ndugu wa kiume (mabroo).

Ila mimi nina formula 1, ukiniambia nikopeshe nakukopesha fresh kabisa, sasa ukijisahaulisha basi ndio ticket ya kuepuka mizinga.

Siku ukiniomba sikupi ng'oo hata iweje, labda iwe ni shida ya kiafya ama tatizo kubwa linalohitaji msaada kweli, ila sijui nina kinyumba changu nimekwama nipe 300k nitakurudishia sikupii.
 
I hope I die surrounded by the people who love me. Unakufa unaona sura ya nesi amekukunjia sura!!!

Halafu charity begins at home, kama mzazi wako mwenyewe huwezi kujitolea kumtunza uzeeni utasaidia wahitaji wowote kwenye hii dunia kweli!

Sema tu watu hawana mahusiano mazuri na wazazi wao, labda wazazi walikuwa too controlling, too demanding, too judgmental, they were absent parents etc, otherwise sio rahisi kuwaza unavyowaza kuhusiana na mtu unayempenda.

View attachment 2040637
Hata Kama walikuwa na tabia hizo, Kama una uwezo watunze wazee. Hakuna pride yoyote wewe upo unatumbua na Malaya wazee wako wanaombaomba kwa majirani au wanasaidiwa na watoto wa jirani kuchota maji.
What goes around comes around.
Unavyowatendea ndivyo utakavyotendewa.
 
Kinachonisaidia ndugu sikuwaga na mazoea ya kuwatembelea since nikiwa mdogo, hicho kimenisaidia sanaa.

Ila ndugu wa damu mizinga iko palepale, hasa ndugu wa kiume (mabroo).

Ila mimi nina formula 1, ukiniambia nikopeshe nakukopesha fresh kabisa, sasa ukijisahaulisha basi ndio ticket ya kuepuka mizinga.

Siku ukiniomba sikupi ng'oo hata iweje, labda iwe ni shida ya kiafya ama tatizo kubwa linalohitaji msaada kweli, ila sijui nina kinyumba changu nimekwama nipe 300k nitakurudishia sikupii.
Hata mm baadh ya ndugu siwajui lkn wao wananijua. Maana wakienda home wanapewa namba . Hapo mm huwa sitoi hela . Lkn madogo duuuh
 
…..
Ikitokea hivyo basi ni wao tu na Huruma zao waamue kunitunza mimi mzee ambae pengine nilishindwa kujiwekea Akiba ujanani kwangu.

Hakuna mzazi, au mwanadamu yeyote ambaye anatamani kesho yake iwe na ugumu.

Kuna sababu nyingi mzazi au wazazi wanashindwa kujiwekea akiba ya uzeeni, ikiwemo gharama za malezi na za kusomesha watoto wao.

Sidhani kama ni haki kumlaumu mzazi kwamba alikuwa mzembe kutojiwekea akib.
Mzazi aliwajibika usiku na mchana, alifikia hata kukopa na kujilimbikizia madeni ili mwanae asome na kuishi vizuri.

….wale utakao kuwa nao kwenye Shida na ata Raha ndio Ndugu zako wa kweli shikana nao.

?! mzazi au wazazi hawastahiki kuwa ndugu zako wa kweli?
Sikubaliani na hili.

Kwangu mimi binafsi,
Wazazi wangu walinilea, walinisomesha, na ndio wanastahiki kuwa 1st priority kushikamana nao.

(nikizeeka) siyo jukumu lako kunitunza, kuna walionileta ndio ulikuwa wajibu wao, labda ufanye tu kwa wema wako ila sio wajibu wala jukumu.

Waliokuleta wali play part yao, ndio maana ukafikia kwenye mafanikio yako.
It’s a circle.
Ni jukumu kuhakikisha na wao katika uzee wao kuwatunza na ni wajibu kuwasaidia, na hata watoto wajifunze kuwa what goes around comes around.

Watoto zetu wanamajukumu mengi, wana familia zao za kuwalea tusiwatwishe mizigo mizito ya kuwaelemea.

Hata wazazi wetu walitulea, kutusomesha na ilhali na wao walijinyima katika hali ya majukumu mengi na mizigo mizito ya kuwaelemea mpaka nasi tumekua na leo hii tunajitegemea.

Sasa wao wamechoka!
Ni jukumu letu na wao kuwaangalia kwa jicho la huruma na fadhila.

Tujiwekee Akiba ujanani mwetu, tujiwekee akiba, tuache kula ujana tu kwa kutegema watoto watakulea.
Jiwekee akiba, hakika hautokuja kujuta
Ni Faraja tu ndio kitu kiwe cha kuomba ukizeeka.

Cc Zero IQ.

Hakika katika maisha ya taabu za uzeeni, hutakosa kulaumiwa kwamba ulikosea mwenyewe sababu ulikula maisha ujanani.

Hata ndugu yangu mwenye post hii, Mwenyezi Mungu akujaalie maisha na umri mrefu, uje uyaone ukweli wa maneno haya.

Katika umri wangu nimeyaona mengi.
Imagine maisha ya sasa;
(Mfano;)

Changamoto za usafiri kwenda na kurudi kazini,
changamoto za kodi iwapo ni nyumba ya kuoanga.
Changamoto za gharama za ujenzi.
Changamoto ya kipato kukidhi mlo wa kila siku.
Changamoto ya gharama za matibabu
Changamoto ya ada!
Changamoto ya michango ya kijamii, - harusi, misiba, matibabu, michango, michango, michango…

By the time mzazi anafika umri wa kustaafu, ameshindwa hata kujiwekea akiba. Anastaafu amechooooka,
Pengine hata kiinua mgongo atazungushwa weee!

Sote tunatamani kustaafu bila presha, ila reality haipo hivyo.

IMG_6858.jpg
 
Yani siwezi kula wala kulala kwa amani kama nikijua wazazi wangu wanalala njaa asee.

Wao ni sehemu ya familia yangu, wote wanatunzwa sawa na kwangu mimi kuwahudumia wazazi sio msaada ni wajibu wangu.

Alhamndullilah, sijaona hasara yyte ya kufanya hayo. Tuwahudumie hawa wazee na sio msaada. Yawezekana maisha yao duni ya uzeeni yametokana na wao kutupambania sisi tuwe hivi tulivyo sasa!
 
Pesa zitaajiri mtu wa kukuhudumia, tafuta pesa jiwekee Akiba Zitakutunza ukizeeka.

Acha watoto watunze familia zao, kitu pekee cha cha kuomba kwa wanao ukizeeka ni faraja yao pekee.
Mkuu inawezekana umri wako ni mdogo, hii hoja yako wala sio nzuri. Kama unawalea wakiwa wadogo,ukiishiwa nguvu watakulea pia. Pesa haifanyi kila kitu uyajue hayo kwanza. Lakini sio kila mmoja anaweza kuweka akiba za kumsaidia uzeeni, mtu akiba yake amewalelea watoto wake,wengine wamesomeshwa hizo zote ni akiba, mtu angezitumia uzeeni, tukifuata mtazamo wako ni kwamba ukizaa tu uondoke umwache mtoto usimlee kwa kuwa sio jukumu la mzazi, jukumu la mzazi ni kumleta duniani tu.

Yaani unamaanisha mzazi asilee mtoto na mtoto asimlee mzazi maana hawafungamani na hayo majukumu. Kila mtu apambane na changamoto zake.
 
Kama shughuli zako za kila siku zinakukutanisha na wazee ambao wako kwenye hali mbaya kiafya huwezi kuongea ujinga.
Ukishakuwa mzee ndugu, hela ni kitu cha ziada, cha kwanza ni uwe na watu karibu ambao wana upendo na wewe.... Kumbuka mwili wa mzee ni hekalu la magonjwa ya kila aina.. Kuna magonjwa ambayo hata ukimwajiri nesi lakini kama huna mtoto au ndugu wa kujitolea kukuhudumia basi utaozea kitandani maana hata manesi wenyewe siku hizi tunawajua walivyo kipesa zaidi.

Ila shida ni wale wazee ambao umri umeshaenda lakini bado anazalisha tu watoto ingali yeye nguvu kiuchumi zinapungua na maisha yenyewe kwa kiasi kikubwa anawategemea nyie watoto wake... Kwahiyo unahangaika naye na uhangaike na watoto tena.
 
Mzazi ukifa, mtoto wako ataitwa YATIMA, mtoto wako kifa, mzazi huna jina.
Tafsiri yake ni kwamba mtoto natakiwa kukutegemea wewe mzazi na sio mzazi kumtegemea mtoto hiyo ndio kanuni ishike maisha yako yote
 
Pesa zitaajiri mtu wa kukuhudumia, tafuta pesa jiwekee Akiba Zitakutunza ukizeeka.

Acha watoto watunze familia zao, kitu pekee cha cha kuomba kwa wanao ukizeeka ni faraja yao pekee.
Pesa itakutunza lakini haitakupa faraja wala utulivu. Watoto ndiyo!!
 
Back
Top Bottom