Si jukumu la Watoto kukuhudumia uzeeni...

Si jukumu la Watoto kukuhudumia uzeeni...

Zero IQ

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2016
Posts
13,985
Reaction score
25,204
Kwanza sizai watoto kwa sababu ya kunitunza uzeeni niweke wazi. Ikitokea hivyo basi ni wao tu na Huruma zao waamue kunitunza mimi mzee ambae pengine nilishindwa kujiwekea Akiba ujanani kwangu.

Tunawapa Mzigo mzito watoto zetu, na imekuwa kama wajibu wa wazazi wengi kuwaambia watoto zao kwamba nimekuzaa ili uje unitunze uzeeni"alikwambia nani kwamba utafika uzee wa kufikia kutunzwa"

Mi nazaa kama wajibu wangu, na Jukumu langu kuu ni kuwatunza ili kesho na kesho kutwa wakose cha kusema wakishindwa kufanikiwa kwenye maisha yao.

Nazaa wanangu na kuwaambia, nimewazaa siyo kwa sababu mje kunitunza uzeeni, Nimewazaa ili mje kuishi na kuzitimiza Ndoto zenu.

Ishini kwa matakwa ya mioyo yenu ili nanyi mje kuzitunza familia zenu. Mimi sio Ndugu yako, Ndugu zako ni hao uliozaliwa nao na wale wachache ambao watatambua shida zako, wale utakao kuwa nao kwenye Shida na ata Raha ndio Ndugu zako wa kweli shikana nao.

Mimi Nimetumika kama kiungo cha kukuleta kwenye ulimwengu huu hivyo, mimi ni kama gari tu na wewe abiria wajibu wangu ni kukuhudumia vyema na kukufikisha mpaka pale utakapokwenda,

Nikichakaa (nikizeeka) siyo jukumu lako kunitunza, kuna walionileta ndio ulikuwa wajibu wao, labda ufanye tu kwa wema wako ila sio wajibu wala jukumu.

Ndugu tusiwape majukumu mazito Watoto zetu mpaka kufikia hatua ya kujuta kuzaliwa. Watoto zetu wanamajukumu mengi, wana familia zao za kuwalea tusiwatwishe mizigo mizito ya kuwaelemea.

Tujiwekee Akiba ujanani mwetu, tujiwekee akiba, tuache kula ujana tu kwa kutegema watoto watakulea. Jiwekee akiba, hakika hautokuja kujuta. Ni Faraja tu ndio kitu kiwe cha kuomba ukizeeka.

Cc Zero IQ.

Cc Zero
 
You talk nonsense saivi unaongea sababu ni kija unanguvu Ila uzeeni huwezi sema ayooo wanao kukutunza siyo lazima wakupe pesa jua kun na kuumwa na ndyo vitu vinavyowasumbua wazee wengi sana upweke na magonjwa na labda mkeo au mmeo kafariki tayrii jukumu la kukuudumia litabaki Kwa wanao
 
Ni kweli,hili jambo limejikita ktk mizizi ya jamii nyingi za kiafrika, lakini hili somo linapaswa lianze kufundishwa sasa kwa ajili ya wazee wa hapo baadae,kwa sasa wazee waliopo wasaidiwe wamalizie maisha kwanza maana itakuwa hatari!
 
Hii pumba tupa dust bin, kwani kutunzwa ni hela peke yake? Unaweza ukafika uzeeni ukashindwa kuona, hela zitakuhudumia?
Pesa zitaajiri mtu wa kukuhudumia, tafuta pesa jiwekee Akiba Zitakutunza ukizeeka.

Acha watoto watunze familia zao, kitu pekee cha cha kuomba kwa wanao ukizeeka ni faraja yao pekee.
 
You talk nonsense saivi unaongea sababu ni kija unanguvu Ila uzeeni huwezi sema ayooo wanao kukutunza siyo lazima wakupe pesa jua kun na kuumwa na ndyo vitu vinavyowasumbua wazee wengi sana upweke na magonjwa na labda mkeo au mmeo kafariki tayrii jukumu la kukuudumia litabaki Kwa wanao
Ukijiwekea akiba kuumwa, na matatizo ya uzee yanajitatua kwa sababu utakuwa na Akiba yako itakayotumika kukuhudumia,
Ajiri mtu wa kuhudumia kwa akiba uliyojiwekea unanani.

Achia watoto watunze familia zao, ndio maana wazee wengi wanakufa kabla ya uzee wao kamili kwa sababu ya mawazo, na stress za kutokutunzwa na watoto zao.

Kitu pekee cha kuomba uzeeni ni faraja tu kutoka kwa watoto
 
Ni kweli,hili jambo limejikita ktk mizizi ya jamii nyingi za kiafrika, lakini hili somo linapaswa lianze kufundishwa sasa kwa ajili ya wazee wa hapo baadae,kwa sasa wazee waliopo wasaidiwe wamalizie maisha kwanza maana itakuwa hatari!
Kabisa kabisa mkuu
 
Kiasili kuna kitu kinaitwa familia na inajumuisha vizazi ambavyo ni watoto, vijana, watu wazima na wazee. Huu mzunguko unategemeana kwa kila kitu. Mtoto akizaliwa anakuwa hajiwezi na uhudumiwa na wazazi mpk atakapojitegemea na hivyo hivyo kwa wazee na vikongwe

Familia ni asili ya mamalia wote ndio maana hata Simba au wanyama wengine wanatunzana kuanzia watoto, vijana na wazee. Simba vijana wakiwinda wanaua na kuwakaribisha wazee wale ili waweze ku survive, ni kanuni ya maisha

Pia hata ukiwa na hela kiasi gani kuna vitu utaishia kuibiwa tu na kufilisika vikifanywa na mtumishi ambaye huna vinasaba nae.

Chukulia umezeeka huwezi kwenda hata benki au ATM au TigoPesa, utaishia kupigwa tu. Pia familia ni upendo unaokutoa kwenye upweke.

Wazee sio tu watunzwe bali waheshimiwe siku zote. Vimeandika vitabu vya dini zote
 
Kwanza sizai watoto kwa sababu ya kunitunza uzeeni niweke wazi,
Ikitokea hivyo basi ni wao tu na Huruma zao waamue kunitunza mimi mzee ambae pengine nilishindwa kujiwekea Akiba ujanani kwangu.

Tunawapa Mzigo mzito watoto zetu, na imekuwa kama wajibu wa wazazi wengi kuwaambia watoto zao kwamba nimekuzaa ili uje unitunze uzeeni"alikwambia nani kwamba utafika uzee wa kufikia kutunzwa"

Mi nazaa kama wajibu wangu, na Jukumu langu kuu ni kuwatunza ili kesho na kesho kutwa wakose cha kusema wakishindwa kufanikiwa kwenye maisha yao.

Nazaa wanangu na kuwaambia, nimewazaa siyo kwa sababu mje kunitunza uzeeni, Nimewazaa ili mje kuishi na kuzitimiza Ndoto zenu.

Ishini kwa matakwa ya mioyo yenu ili nanyi mje kuzitunza familia zenu.
Mimi sio Ndugu yako, Ndugu zako ni hao uliozaliwa nao na wale wachache ambao watatambua shida zako, wale utakao kuwa nao kwenye Shida na ata Raha ndio Ndugu zako wa kweli shikana nao.

Mimi Nimetumika kama kiungo cha kukuleta kwenye ulimwengu huu hivyo, mimi ni kama gari tu na wewe abiria wajibu wangu ni kukuhudumia vyema na kukufikisha mpaka pale utakapokwenda,

Nikichakaa(nikizeeka) siyo jukumu lako kunitunza, kuna walionileta ndio ulikuwa wajibu wao, labda ufanye tu kwa wema wako ila sio wajibu wala jukumu.

Ndugu tusiwape majukumu mazito Watoto zetu mpaka kufikia hatua ya kujuta kuzaliwa,
Watoto zetu wanamajukumu mengi, wana familia zao za kuwalea tusiwatwishe mizigo mizito ya kuwaelemea.

Tujiwekee Akiba ujanani mwetu, tujiwekee akiba, tuache kula ujana tu kwa kutegema watoto watakulea.
Jiwekee akiba, hakika hautokuja kujuta
Ni Faraja tu ndio kitu kiwe cha kuomba ukizeeka.


Cc Zero IQ.


Cc Zero
I am sorry man, zile amri 10 za Musa, Amri ya nne inahusika. Ndio Amri pekee yenye If...,Then...
 
I hope I die surrounded by the people who love me. Unakufa unaona sura ya nesi amekukunjia sura!!!

Halafu charity begins at home, kama mzazi wako mwenyewe huwezi kujitolea kumtunza uzeeni utasaidia wahitaji wowote kwenye hii dunia kweli!

Sema tu watu hawana mahusiano mazuri na wazazi wao, labda wazazi walikuwa too controlling, too demanding, too judgmental, they were absent parents etc, otherwise sio rahisi kuwaza unavyowaza kuhusiana na mtu unayempenda.

images (24).jpeg
 
Back
Top Bottom