ShyRose amuomba radhi Rais Magufuli kwa ujumbe uliosambaa kutokea kwenye akaunti yake ya Instagram. Asema alidukuliwa

Status
Not open for further replies.

Mongoiwe

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
524
263
Kada maarufu wa CCM na aliyewahi kuwa mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki(EALA), ShyRose Bhanji kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram ameandika kuwa Hakubaliani na Utawala wa Rais JPM, na yuko tayari kwenda jela

7864c934-f69b-4966-bccc-184e9e16fa91.jpeg

Ikumbukwe kuwa Mwanasiasa huyo siku kadhaa zilizopia aliandika kupitia ukurasa wake huo kuwa ''Serikali ya chama changu CCM haiwezi kukwepa lawama kwa namna yoyote ile kufuatia kupigwa risasi kwa binti ambaye hakuwa na hatia hata kidogo.

Imekuwa ni siku mbaya sana kwangu; nimeshindwa kula na nashindwa kupata usingizi kutokana na kifo cha huyu binti. Nafsi yangu inanisuta. Mungu wangu naomba unisaidie ''

1f4a32ee-dcfd-4172-bdd6-55f60fbf69de.jpeg

=====
UPDATES

ShyRose Bhanji ajitokeza na kukanusha taarifa zilizosambaa kuwa hakubaliani na utawala wa Rais Magufuli

Kupitia akaunti yake hiyo ya Instagrama, Shyrose amemuomba radhi Rais Magufuli na watanzania wote kwa ujumbe huo kwani akaunti yake ilidukuliwa

db0b4fbe-720a-4d8b-845f-fc9a74e12b39.jpeg
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom