Shy-Rose Bhanji Amwonya Msekwa

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,144
Shy-Rose Bhanji amvaa Msekwa

Shy-Rose Bhanji amvaa Msekwa

na Mwandishi wetu

amka2.gif

KADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Shy-Rose Bhanji, amemshutumu Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Pius Msekwa na kumtaka aache kukifanya chama hicho kama mali yake.
Shy-Rose ambaye aliwania ubunge katika Jimbo Kinondoni, jijini Dar es Salaam na kushindwa kwenye kura za maoni, alitoa kauli hiyo jana akijibu kauli ya Msekwa ya juzi akiwataka wanaotaka kuhama chama hicho baada ya kushindwa kwenye uteuzi wahame haraka.
Akizungumza na Tanzania Daima Jumatano kwa njia ya simu, Shy-Rose alisema ameshtushwa na kauli ya Msekwa kwani hakuwa na haki ya kutamka maneno mazito na yasiyo ya kiungwana hasa katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu.
“Kwa kweli nilivyosoma gazeti moja leo nimekutana na habari hii, ikanishtua kidogo. Nikajiuliza hivi huyu mzee Msekwa anasema maneno ya ajabu namna hii, hiki chama ni chake binfasi? Pengine amejisahau kwamba CCM ni chama chetu wote, sasa iweje yeye awe na ujasiri wa kujiamini kutoa maneo ya ajabu wakati hiki ni chama chetu wote au yeye anadhani ni chama chake?” alihoji Shy-Rose.
Shy-Rose alisema anaheshimu nafasi ya Msekwa kama kiongozi wa juu wa chama na vile vile kama mzazi wake, lakini nafasi hiyo haimpi uhalali wa kushabikia wanachama wanaotaka kuondoka kwenye chama hicho.
Alisema Msekwa alipaswa kujiuliza kwa nini wanachama hao wanaondoka na si kuzungumza maneno ambayo yanaonyesha wazi kwamba yana jazba ndani yake.
“Huu si wakati wa jazba, huu ni wakati wa kutafakari kwa nini watu wanaondoka CCM. CCM kazi yetu ilikuwa kupokea wapinzani, leo wanaondoka, lazima tujiulize hilo” alisema.
Kada huyo ambaye ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Mkoa wa Dar es Salaam na mjumbe wa Baraza Kuu la (UWT) Taifa, aliwataka viongozi wa CCM kwa sasa kuchunga kauli zao, vinginevyo hawatapata ushindi unaotarajiwa.
Alikumbushia uchaguzi mdogo wa ubunge Tarime, mkoani Mara mwaka juzi kwamba CCM ilishindwa kutokana na kauli za majigambo ya baadhi ya viongozi wa chama.
Akizungumzia msimamo wake baada ya kushindwa kwenye kura za maoni, Shy-Rose alisema hana mpango wa kuhama CCM kwa sasa.
“Kama kuondoka CCM, aondoke Msekwa na atuachie chama chetu, yeye hana mamlaka wala uhalali wa kuzungumza lugha za ajabu ambazo zitawafanya hata wale wasio na nia ya kuhama waondoke.
“Mimi sihami CCM, nimekulia ndani ya chama hiki na nitaendelea kubaki ndani ya chama lakini pale nitapoona kuna kasoro sitasita kukikosoa chama changu na nitasema kweli daima,” alisema.
Aliwapongeza walioamua kuondoka CCM kwani wametumia haki yao na kusisitiza kwamba kuondoka CCM si dhambi kama ambavyo wengine wanavyofikiria.

h.sep3.gif

juu
blank.gif

na Mwandishi wetu

amka2.gif

KADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Shy-Rose Bhanji, amemshutumu Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Pius Msekwa na kumtaka aache kukifanya chama hicho kama mali yake.
Shy-Rose ambaye aliwania ubunge katika Jimbo Kinondoni, jijini Dar es Salaam na kushindwa kwenye kura za maoni, alitoa kauli hiyo jana akijibu kauli ya Msekwa ya juzi akiwataka wanaotaka kuhama chama hicho baada ya kushindwa kwenye uteuzi wahame haraka.
Akizungumza na Tanzania Daima Jumatano kwa njia ya simu, Shy-Rose alisema ameshtushwa na kauli ya Msekwa kwani hakuwa na haki ya kutamka maneno mazito na yasiyo ya kiungwana hasa katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu.
“Kwa kweli nilivyosoma gazeti moja leo nimekutana na habari hii, ikanishtua kidogo. Nikajiuliza hivi huyu mzee Msekwa anasema maneno ya ajabu namna hii, hiki chama ni chake binfasi? Pengine amejisahau kwamba CCM ni chama chetu wote, sasa iweje yeye awe na ujasiri wa kujiamini kutoa maneo ya ajabu wakati hiki ni chama chetu wote au yeye anadhani ni chama chake?” alihoji Shy-Rose.
Shy-Rose alisema anaheshimu nafasi ya Msekwa kama kiongozi wa juu wa chama na vile vile kama mzazi wake, lakini nafasi hiyo haimpi uhalali wa kushabikia wanachama wanaotaka kuondoka kwenye chama hicho.
Alisema Msekwa alipaswa kujiuliza kwa nini wanachama hao wanaondoka na si kuzungumza maneno ambayo yanaonyesha wazi kwamba yana jazba ndani yake.
“Huu si wakati wa jazba, huu ni wakati wa kutafakari kwa nini watu wanaondoka CCM. CCM kazi yetu ilikuwa kupokea wapinzani, leo wanaondoka, lazima tujiulize hilo” alisema.
Kada huyo ambaye ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Mkoa wa Dar es Salaam na mjumbe wa Baraza Kuu la (UWT) Taifa, aliwataka viongozi wa CCM kwa sasa kuchunga kauli zao, vinginevyo hawatapata ushindi unaotarajiwa.
Alikumbushia uchaguzi mdogo wa ubunge Tarime, mkoani Mara mwaka juzi kwamba CCM ilishindwa kutokana na kauli za majigambo ya baadhi ya viongozi wa chama.
Akizungumzia msimamo wake baada ya kushindwa kwenye kura za maoni, Shy-Rose alisema hana mpango wa kuhama CCM kwa sasa.
“Kama kuondoka CCM, aondoke Msekwa na atuachie chama chetu, yeye hana mamlaka wala uhalali wa kuzungumza lugha za ajabu ambazo zitawafanya hata wale wasio na nia ya kuhama waondoke.
“Mimi sihami CCM, nimekulia ndani ya chama hiki na nitaendelea kubaki ndani ya chama lakini pale nitapoona kuna kasoro sitasita kukikosoa chama changu na nitasema kweli daima,” alisema. Aliwapongeza walioamua kuondoka CCM kwani wametumia haki yao na kusisitiza kwamba kuondoka CCM si dhambi kama ambavyo wengine wanavyofikiria.

h.sep3.gif

juu
blank.gif
 
Shy-Rose mawenge, Msekwa yuko right. Chama ni sera na uongozi. Ukiwa hujaridhika na sera au uongozi ni haki yako kuhama.

Sasa Shy-Rose anacholialia nini ? Alitaka Msekwa alazimishe wanaotaka kuondoka CCM wabaki ? Ndiyo idea yake ya demokrasia hiyo ?

Au maneno yamemgusa binafsi kwa kuwa na yeye kashindwa ubunge alitegemea kubembelezwa ?
 
Tena hata ukihama ccm chadema usije kabisa yani labda uhamie tlp kwa mapepe mwenzio.
 
Ms Banji anataka kujifanya mtu wa diplomasia kivile.............wakati yeye alirusha ngumi!

wanasiasa vijana bongo wengi hamna kitu.
 
Hivi kwani Shy-rose alikuwa na mpango wa kuihama CCM?
Inawezekana alikuwa na mpango huo kwani maneno ya msekwa yanamchefua zaidi MwanaCCM ambaye ameshindwa kura za maoni na aanataka kuihama CCM.
By the way swala la Msekwa kukifanya chama kama ni mali yake binafsi ni point.
 
Sioni kuna relation gani kati ya hii kauli ya Msekwa na kutaka kukifanya chama mali yake binafsi. Chama chochote kinachofuata demokrasia kitaruhusu wanachama wake wasioridhika kuondoka.

Kinyume cha hapo utaleta mambo ya street gangs na mafia, ambako unaweza kuambiwa "ukiingia hutoki".
 
Dada yangu Shy-rose asubiri tu hurma ya mbayuwayu maana ana siti 100.

Lakini ni mpaka ashinde..... nafasi ni finyu kwa mbayu...
 
Dada Shy-Rose Leo hii ndiyo umegundua haya? mi naona Usimlaumu Msekwa jilaumu wewe na CCM yako. Nakuomba usihame, bakia humo humo mmalize matatizo yenu mnajuana ninyi. tutawaokoa wachache werevu kama sisi waje CHADEMA tuunde serikali.
 
Dada yangu Shy-rose asubiri tu hurma ya mbayuwayu maana ana siti 100.

Lakini ni mpaka ashinde..... nafasi ni finyu kwa mbayu...

Mbayuwayu atahurumia wangapi wakati mida hii anajihurumia mwenyewe kwanza? Hata kama mbayuwayu anajifanya machoni pa watu kuwa hatishiki na mwamko wa wananchi, anawaza na kuwazua sana. Tatizo anapanga mbinu chafu za kuiba
 
Shy-Rose Bhanji amvaa Msekwa

“Kama kuondoka CCM, aondoke Msekwa na atuachie chama chetu, yeye hana mamlaka wala uhalali wa kuzungumza lugha za ajabu ambazo zitawafanya hata wale wasio na nia ya kuhama waondoke.
“Mimi sihami CCM, nimekulia ndani ya chama hiki na nitaendelea kubaki ndani ya chama lakini pale nitapoona kuna kasoro sitasita kukikosoa chama changu na nitasema kweli daima,” alisema. Aliwapongeza walioamua kuondoka CCM kwani wametumia haki yao na kusisitiza kwamba kuondoka CCM si dhambi kama ambavyo wengine wanavyofikiria.
Sasa yeye anamkosoa mzee msekwa wakati huo huo yeye anawapongeza waliokimbia chama. Na mie nadhani msekwa kamgusa huyu dada yetu Shyrose .sasa yeye ana mamlaka gani ya kuwapongeza wanaondoka.

Huyu dada akae mbali na vyomba vya habari. atauza magazeti kwa pumba zake wakati yeye anaposhikilia tawi linazidi kukauka.
 
tatizo la baadhi ya vijana ni wao kujiona ni wa2 wa ndani ya chama(ccm)wanajidanganya!!!! wakati ukweli ni kwamba wanashindwa kuona mbele kutakuwaje ili waanze kujiandaa kupitia vyama vingine!!!!!!ninavyoona mimi hali itaendelea kuwa hivyo ndani ya ccm kwa muda mrefu kwani hakuna mzee mwenye nia ya kung'atuka ili kuwaachia akina shy-rose & co.Sauti zao zitasikika iwapo watakuwa tayari kuzisema nje ya mfumo wa ccm!!!!
 
shy-rose mawenge, msekwa yuko right. Chama ni sera na uongozi. Ukiwa hujaridhika na sera au uongozi ni haki yako kuhama.

Sasa shy-rose anacholialia nini ? Alitaka msekwa alazimishe wanaotaka kuondoka ccm wabaki ? Ndiyo idea yake ya demokrasia hiyo ?

Au maneno yamemgusa binafsi kwa kuwa na yeye kashindwa ubunge alitegemea kubembelezwa ?

unaona ni sawa kwa mwanasias mkongwe kutamka maneno kam ahaya chini?

samsonmfalila said:
akijibu kauli ya msekwa ya juzi akiwataka wanaotaka kuhama chama hicho baada ya kushindwa kwenye uteuzi wahame haraka.
 
Back
Top Bottom