Shule za Dar es salaam ni pasua kichwa

Jul 29, 2014
55
32
Kwa wale wanaofundisha shule za Dar es salaam huu ni ujumbe kwenu. Fanya kazi sana lakini ujue hakuna bosi anayejali maslahi yako, utafanya kazi kama punda, sifa zote kwa mwenye shule.

Kuna shule hasa hizi kubwa kubwa wafanyakazi hawafanani na ukubwa wa shule, mfano unakuta waalimu wamechoka balaa.
Mikataba ya kilaghai (maarufu kama ya chief mangungo). Wanafukuza waalimu kama njugu yaani, hawalipwi stahiki zao
No overtime yaani unafanya kazi kwa ujira mdogo halafu kipimo chako ni ufaulu wa wanafunzi.

Sasa kuna hizi shule sitazitaja ni mabingwa wa kutafuta paper za nje, yaani kama wakitaka kukuondoa unatafutiwa paper ngumu balaa halafu wanafunzi wakifeli hakuna mazungumzo, unafungishwa virago hata stahiki zako hupewi na wanakuambia kashtaki popote.

In short hawafai na serikali wala haizimuliki maana wanaozimiliki ni kama giants hawagusiki. Mwisho kabisa wanatumia sana non professional teachers sijajua hawa wakaguzi wanakaguaga nini, very sad.
 
Ndo Tanzania hiyo ndugu, ni kuvumilia tu huku unatafuta fursa zingine, kwingine
 
Back
Top Bottom