Jukumu la kwanza la asilia ni kwamba watoto walelewe na baba na mama, na sio boarding school au ndugu wengine, labda tu kwa shida/tatizo flani! Angalau mpaka form 4 mtoto asiwe boarding school. Ni kweli hali halisi kama mkazo wa maisha kifedha, jiografia, kazi na mazingira mengine yanafanya iwe ngumu. Ni vema kuwa na usawaziko (balanced) kwa hili jambo, fedha ni nzuri na watoto zaidi. Ukiona vipi ahirisha kuwa na watoto au usiwe nao kabisa! Haileti picha nzuri kuwa na watoto alafu wanagongwa, naniliwa... kimgongomgongo.
Pia nyakati (era), huu sio ule wakati tuliosoma boarding school za boys na girls na hayo mambo hayakuwepo. Mimi mwenyewe nilisoma Boys' Sec. na havikuwepo hivyo vinyamkela. Tuchukulie kwamba siku hizi shule zote zina hayo matatizo. Siku hizi elimu ni kubwa sana and easy to attain hasa ya uharibifu kupitia video, tv, internet, brochures, books, computers, simu zetu za viganjani etc. zote zimejaa ma modo, porn za aina zote, movies za uongo (fiction), mitandao ya kijamii, majivuno/kiburi, kusifia watu maarufu kama wacheza mpira, warembo, matajiri, matangazo mengi ya biashara aina zote yaliokolezwa chumvi etc.
Shule inatakiwa ziwe mchanganyiko. Sasa huko kutenga boys na girls sio asili yake. Anyway tujitahidi, ingawa hakuna expert wala wa kumnyooshea kidole mwenzake.
Siku njema