kuna siku alfajiri tukawa tunakimbia mchakamchaka, sasa kufika pale 4 ways karibia na mihayo sekondari, tukakutana na tabora boys nao wanakimbia mchakamchaka, dadadeki, ulitembea mkono hapo, sie tusio na nguvu vinyoya tukalala mbele kurudi shule, wababe wakanyukana, na kuna siku tena tulikutana na tabora boys nadhani lilikuwa ni kombe la mgulunde pale kazima, mechi kwisha tu ngumi zikaanza mpunga wa kazima sec wote ulilazwa chini, na kuna siku wakakosea behewa la treni tukawekwa pa1 na tabora boys, kuingia tunakuta tabora boys wametuna wanapiga story, mkono ulitembea hapo mpaka tabora boys ikabidi warudi kwa station master wakapewa behewa lingine