jsenyinah
JF-Expert Member
- Jan 25, 2012
- 249
- 339
Nipo hapa nyumbani naendelea kuisogeza siku hii ya tarehe 01.01.2017.
Ghafla nikaikumbuka shule hii ya sekondari Milambo iliyopo mjini Tabora,takribani kilomita 2 tu toka kituo kikuu cha mabasi Tabora,na ipo njiani kama unaelekea Urambo,nyumbani kwa marehemu Mh. Samweli Sitta (Mungu amrehemu). Shule hii pia alisoma Mh Edward Ngoyai Lowasa, Waziri Mkuu Mstaafu wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania.
Shule hii haina uzio (kwa sababu ni ya wanaume),na ipo karibu kabisa na mtaa maarufu Tabora uitwao Chemchemu.
Kando ya hiyo shule kuna canteen maarufu sana kwa ajili ya kununulia appetizer au chachandu unapotaka kulia NYALI au POLA.
Ni shule yenye mabweni matatu,mm nilikaa bweni la SOKOINE,floor ya kwanza.
Maji ya ile shule ni ya chumvi sana kiasi cha kuwafanya wanafunzi waende kuchota maji ya kunywa parokiani.
Nyuma ya shule upo uwanja mzuri sana wa mpira.
Waalimu ninaoweza kuwakumbuka n:-
1. Mwl Katondolaa (Marehemu)
2. Mwl Jubwa (Headmaster)
3. Mwl Zoma ( kwa fito balaa)
Nakimbuka pia kuna "Conco room",vyumba ambavyo wanafunzi hupenda kujifungia kama gheto kwa ajili ya kujisomea (hasa viongozi).
Ambavyo sitavisahau:
1. Sikuwahi kuitwa jina kwa miaka miwili
2. T-shirt zake zilikuwa kama blauzi. (ukivaa inasogea kifuani)
3. Foleni siku za nyali au ngema kwa nyama
4. Utamu wa pola (uji).
Milambo acha tu iitwe Milambo