Shule ya sifa: Shule ya Sekondari Milambo, Tabora

Mie nilimaliza hapo 1983 combination ya French . Nilikuwa Kennedy no. 10. Nakumbukia Sana maembe ya kule mawiti. Maji tulikuwa tunachota Bwawa la igombe. Nakumbukia father kalumanzira wa parokia ya makokola. Classmates ninaowakumbuka ni kama Shewere, Ben Mwangonda, Felix Lubuva, Revocatus Msokane, Julius Mganga , Philip assey n.k. Mkuu alikuwa ni Mr. Msemakweli.
Umenikumbusha mbali mkuu. Father Kalumanzira au Fr. Gabriel, Shewere alikuwa mwalimu Kazima Sekondari. Kwa sasa sijui wako wapi? Siku ziiiileeee.... kama naziona hivi!
 
Nilimaliza form four 2005 mpaka Leo sijaona head master kama majubwa Mzigua yule alikuwa kiboko alikuwa anatukana matusi ya nguoni hadharani mbele ya walimu na wafanyakazi wa kike mpaka wanakimbia wenyewe na akitaka kuongea mpaka mnahamu nae
 
Daaah nilikuwepo hapo nikipiga PCB,yan uongoz wa shule hauna habar ni mwendo wa utawala binafsi tuu alaf watu wanapasua pepa kama kawaidaa!!!!!!.
 
Nmemaliza apo 2012, maji kwa muda uo tulikuwa tunachota kachelema, maisha matamu sana apo kwa pola na nyali ya mzee msangi
 
Daah ss tulikua hapo 2009/2011 pgm sokoine room no4
Wewe kumbe class mate wangu hapo



Basi kama ni huo mwaka utakumbuka yafuatayo


1. Disco vumbi kwa wanyamwezi na akina Nkunu Elisha,
2. Samaki zilizosambazwa katika taasisi za serikali tulikula mpaka basi

3. Mbwa mkali, hapa tunajipatia kila vinavyotuhusu,

4. Safati za kwenda kachelema.

5. Siku ya miss KAMNA warambo walishiriki karibia nusu ya shule.




Wimbo wetu na hasa ukutwapo na magumu popote ukiuimba utapata mrambo tiii


""Warambo mko wapi, warambo mko wapiii.....
Kwa nguvu utasikia yeaaaaaa.....""

Tulifukuzwa siku ya mwenge baada ya kukosa mahali pa kukaaa


Aseeee nakumbuka mengi uramboni jamaniii


Zoma,
Katondolaa
Kabejaa.
 
Nipo hapa nyumbani naendelea kuisogeza siku hii ya tarehe 01.01.2017.

Ghafla nikaikumbuka shule hii ya sekondari Milambo iliyopo mjini Tabora,takribani kilomita 2 tu toka kituo kikuu cha mabasi Tabora,na ipo njiani kama unaelekea Urambo,nyumbani kwa marehemu Mh. Samweli Sitta (Mungu amrehemu). Shule hii pia alisoma Mh Edward Ngoyai Lowasa, Waziri Mkuu Mstaafu wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania.

Shule hii haina uzio (kwa sababu ni ya wanaume),na ipo karibu kabisa na mtaa maarufu Tabora uitwao Chemchemu.

Kando ya hiyo shule kuna canteen maarufu sana kwa ajili ya kununulia appetizer au chachandu umapotaka kulia NYALI au POLA.

Ni shule yenye mabweni matatu,mm nilikaa bweni la SOKOINE,floor ya kwanza.

Maji ya ile shule ni ya chumvi sana kiasi cha kuwafanya wanafunzi waende kuchota maji ya kunywa parokiani.

Nyuma ya shule upo uwanja mzuri sana wa mpira.

Waalimu ninaoweza kuwakumbuka n:-

1. Mwl Katondolaa (Marehemu)

2. Mwl Jubwa (Headmaster)

3. Mwl Zoma ( kwa fito balaa)

Nakimbuka pia kuna "Conco room",vyumba ambavyo wanafunzi hupenda kujifungia kama gheto kwa ajili ya kujisomea (hasa viongozi).

Ambavyo sitavisahau:

1. Sikuwahi kuitwa jina kwa miaka miwili

2. T-shirt zake zilikuwa kama blauzi. (ukivaa inasogea kifuani)

3. Foleni siku za nyali au ngema kwa nyama

4. Utamu wa pola (uji).

Milambo acha tu iitwe Milambo
Nimeipenda sana hii ukizingatia nimesomea Uyui na nimeishi Ng'ambo huko tulifuata materials.Hongereni mliosoma Shule kongwe kama Milambo inayoshabihiana na jina LA timu maarufu sana huko Ally Hassan Mwinyi
 
Ila madogo wa Tabora Boys huwa wanawakimbiza sana kitaaluma.

Tatizo nini wazee?Hata Tabora Girls tu wanawashinda jamani
Usifananishe tabora boys na mirambo ni vitu viwili tofauti, kwanza katika malengo ya watu wanachokifuata

1.Tabora boys wanaenda shule kusoma ili wapate vyeti, millambo wanaenda shule kujifunza ili wapate elimu


Ukiujua huo utofauti hutoifananisha milambo na shule yeyote tanzania au na A. Mashariki

Ni mwanafunzi wa Milambo pekeee anaanza kidato mpaka anamaliza hamjui mwalimu wa somo wala darasa zaidi ya mwalimu wa usafi na chakula
Lakini abaingia kwenye ushindani wa mitihani ya kitafa

Ni mwanafunzi wa milambo pekeee anaenza shule mpaka anamaliza shule anafanya mtihani wa mock anakujakumaliza na NECTA basi lakini matunda utayaona.


Ni mwanafunzi wa milambo pekee anaehudhuria shughuri za kijamii mf. Misiba na sherehe na kujamiiana na jamii inayomzunguka kwa kujifunza maisha halisi watu wanayoishi na yeye atakayoishi pindi amaluzapo masomo yake


Ni mwanafunzi wa milambo pekeee anaejua yupi ni adui yupi ni ndugu na kipi nifanye na kipi nisifanye, pia ni huyuhuyu pekeee ambaye siku zote wakiwa shule huishi kwa kuchukuliana na kuteteana kama familia, hata muwe na tofauti zenu mkiwa pale ikitokea ukafanyiwa ndivo sivyo mnaweka tofauti zenu chini mnaungana na kutoa maamuzi kwa pamoja.

MILAMBO SIO SHULE YA KAWAIDA KATIKA UKANDA HUU WA A. MASHARIKI NA KATI
 
Enzi zeta tulikuwa na FUPA (Msemakweli) kama Headmaster akisaidiwa na MWANAKONDOO (sikumbuki jinale ila alikuwa mwalimu French. Mzee wa Fito alikuwa SIR Njile ( mwalimu pekee aliyeitwa SIR)
usinikumbushe enzi za fupa, dadadeki, tulimng'oa mwaka 1994 na mwalimu Mabuye akaja kuwa mwalimu mkuu akitokea kazima, RIP mwalimu Mabuye, mwanakondoo nadhani unamsema mwalimu Mwilu ndio alikuwa mwalimu wa kifaransa, mwalimu Njile yupo Kaliua shule 1 ya kata huko,
 
Back
Top Bottom