Shule nikiwa kazini je inawezekana.

MAGAMBA MATATU

JF-Expert Member
Jul 2, 2011
646
1,174
Wakuu mie ni mwajiliwa wa kampuni ya madini hapa bongo , na mshahara wangu kwa mwezi ni laki 7.3,nina miaka miwili nikiwa kazini, nini diploma ya Environmental Engineering nina first class ya GPA ya 4.8 kwa ufupi nina sifa zote za kujiunga na chuo, lakini napenda kujiendeleza zaidi kielimu na kuna wakati nawaza niache kazi ili niende chuo, lakini pia naona nikiacha kazi nikasome nikimaliza nitakuta wigo wa ajira umepungua halafu nikasota mtaani, ila imefikia hatua nikaona kuwa sisi tulio na diploma za vyuo serikali imetunyima mkopo tangia mwaka jana sasa kuacha kazi nikasome naona ada itakuwa mzigo.
sasa naomba ushauli wenu wakuu, niache kazi ili niende chuo au nisome online chuo kikuu huria nikiwa kazini?? na nisomee course gani???

Nawasilisha wakuu.
 
mbona wengi tu tunasoma tukiwa makazini me binafsi nasoma pia natoka job sa 11 then naenda chuo kupiga book sema ndio unakuwa umebanwa vibaya mana shule ya jioni ngumu usipime lkn kama una nia unasoma tu.
 
mbona wengi tu tunasoma tukiwa makazini me binafsi nasoma pia natoka job sa 11 then naenda chuo kupiga book sema ndio unakuwa umebanwa vibaya mana shule ya jioni ngumu usipime lkn kama una nia unasoma tu.

mkuu si unajua makampuni ya madini hayako mjini kama dsm au mwanza sasa hiyo jioni nitakuwa nasomaje huko chuo???
 
Mbona ni rahisi sana...chuo kikuu huria..unasomea nyumbani au kazini....masomo wanakutumia kwa Posta.
 
pole......ndiyo reality za maisha hizo zikichangiwa na sera za MAGAMBA.

nadhani kama unataka kubaki na ajira basi usome chuo kikuu huria(open University) hapo utamudu kubaki na ajira lakini pia gharama ni nafuu ingawa changamoto ya kusoma peke yako nayo ni kubwa.
 
i heard that UDSM-Business school wanampango wa kutoa B.com ya evening program...i think itakufaa sana..jarib ufatilia..
 
mkuu usiache kazi nakushauri soma masomo ya jioni ni vema usome OUT mbona wengi tuppo kazini na tunasoma open, kazi muhim ndugu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom