Shule kumi ghali Tanzania

Shule kumi ghali Tanzania

Tukiwa hatuna uwezo ni utamaduni wetu kuponda.

Tutaponda IPhone na kusifia Tecno.
Tutaponda Range Rover na kusifia Vitz.

Lakini ikitokea tumepewa tuchague zawadi ya bure kati ya Iphone na Tecno au Range na Vitz ndio utajua mahitaji yetu halisi ya mioyo yetu.
Ni kweli japo sipendi iPhone,napenda Samsung
 
SHULE KUMI GHALI ZAIDI TANZANIA.

1- International School of Tanganyika (IST)
— Hii ndio shule ghali zaidi nchini. Iko jijini Dar Es Salaam na hufuata Mtaala wa IB. IST hutoza ada kuanzia shilingi za Kitanzania milioni 34 kwa chekechea hadi shilingi milioni 71 kwa sekondari, kwa mwaka.

2. Braeburn International School
—Hii ni shule ya kimataifa ambayo iko Dar Es Salaam na Arusha. Hufuata mfumo wa IB na ada yake kwa mwaka ni kuanzia shilingi za Kitanzania milioni 20 kwa shule ya msingi hadi shilingi milioni 43 kwa sekondari.

3. Dar Es Salaam International Academy (DIA)
—Hii ni shule ya tatu kwa kuwa na ada ghali zaidi nchini. Iko Dar Es Salaam na hufuata Mtaala wa IB. Ada yake kwa mwaka ni kuanzia Shilingi za Kitanzania milioni 23 kwa shule ya msingi hadi shilingi milioni 40 kwa sekondari.

4. Iringa International School (ISS)
— Iko mkoani Iringa na hufuata mitaala miwili ya IB na ule wa Cambridge. Hutoza ada kati ya Shilingi za Kitanzania milioni 17 kwa Chekechea hadi milioni 27 kwa sekondari.

5. Saint Constantine International School
—Inapatikana mkoani Arusha na hufuata Mtaala wa Cambridge. Ada yake ni kati ya Shilingi za Kitanzania milioni 8 kwa Chekechea hadi shilingi za Kitanzania milioni 23 kwa sekondari.

6. Kennedys House Schools
—Shule za Kennedys ziko maeneo mengi duniani. Nchini Tanzania iko katika mkoa wa Arusha wakiendesha Chekechea na Shule ya Msingi. Ada zao huanzia Shilingi za Kitanzania milioni milioni 8 kwa Chekechea hadi milioni 22 kwa Shule ya Msingi. Shule hii hufuata Mtaala wa Cambridge.

7. Haven of Peace Academy (HOPAC)
—HOPAC ipo katika Jiji la Dar Es Salaam. Hufuata Mtaala wa Cambridge na hutoza ada kati ya shilingi za Kitanzania milioni 16 hadi 22 kwa mwaka.

8. Aga Khan Primary & Secondary School
—Shule hii iko katika Jiji la Dar Es Salaam, na hufuata Mtaala wa IB kama ilivyo ISM. Hutoza ada kuanzia Shilingi za Kitanzania milioni 7 hadi milioni 20.

9. Internation School Moshi (ISM)/ UWC East Africa
— Hii ndio shule ghali zaidi katika mkoa wa Kilimanjaro. Hutoza ada kuanzia shilingi za Kitanzania milioni 16 kwa chekechea hadi shilingi za Kitanzania milioni 41 kwa wale wa kidato cha tano na sita. Shule hii hufuata Mtaala wa International Baccalaureate (IB).

10.Morogoro International School (MIS)
—Hii inapatikana mkoani Morogoro na hufuata mtaala wa Cambridge. MIS hutoza kuanzia Shilingi za Kitanzania milioni 6.4 kwa chekechea hadi shilingi za Kitanzania milioni 18 kwa sekondari. Hii ni ada peke yake, mbali na fedha ya usajili na boarding kwa wale wanaolala shuleni.

Huna hela wewe wenzako wanazo .....
Tafuta Pesa
 
Hapo bado tours za safu ya milima ya himalaya,na fukwe za maldives kuangalia waves features mbalimbali za fukwe,Gharama za kwenda hiroshima na nagasaki kushuhudia madhara ya Nuclear.Hawajaenda bdo siberia na ontario Canada ambako watapitia Arizona kuangalia baadhi ya vitu vya kijiografia na mwisho waende Amazoni kujifunza mambo mbali mbali ya kijamii na hasa kujifunza namna ambavyo msitu wa amazoni unavyobeba uhai wa viumbe duniani,halafu watatulia copa cabana kwenye tamasha la kimataifa kwa wanafunzi wenzao kutakuwa na mashindano mbali mbali katika viwanja vya maracana katikati ya jiji la rio de Janeiro Mzazi atachanga $40k...Hela hela,pesaaaa
 
Vimaskini vya humu JF vimekalia kuimba Imba tu tafuta hela tafuta hela wkt havijui hata vinaongea Nini.

Hawa maskini wamesoma kayumba ambako kwny civics types za family walikua wanafundishwa ziko Aina Tatu.
1.Nuclear family
2.Extended family
3.Single parent family

Leo hizi shule za kitajiri, types of family wanazofundishwa Ni hizo Tatu hapo juu pamoja na hizi nyingine ambazo wameweka na picha kabisa kwny hivyo vitabu:

4.Mwanaume na Mwanaume na mtoto wakisema hio Ni Aina nyingine ya familia.

5.Mwanamke na Mwanamke na mtoto wakisema hio ni Aina nyingine ya familia.

6.Shemale na shemale wakiwa na mtoto wakisema hio Ni type nyingine ya familia.

Sasa maskini wa JF endeleeni kushobokea msivyovijua huku mkisema tafuta hela.
Una uthibitisho?
 
Usagaji na ushoga unaanzia nyumbani.

Tz mashoga wengi wametoka familia za ngumbaru. Na hata huko sekondari za serikali, ushoga njenje.
Nilishangaa hata vijijini mashoga wapo...
 
Nenda kawaulize wanaofuata hio mitaala watakwambia Nini maana ya 'Creating an inclusive LGBT Inclusion Curriculum'

Nyie endeleeni kuimba tu ooh tafuta hela tafuta hela.Mtafurahishwa.
Thibitisha kuwa kuna shule yoyote kati ya hizo inafundisha hayo uloyataja
 
Vimaskini vya humu JF vimekalia kuimba Imba tu tafuta hela tafuta hela wkt havijui hata vinaongea Nini.

Hawa maskini wamesoma kayumba ambako kwny civics types za family walikua wanafundishwa ziko Aina Tatu.
1.Nuclear family
2.Extended family
3.Single parent family

Leo hizi shule za kitajiri, types of family wanazofundishwa Ni hizo Tatu hapo juu pamoja na hizi nyingine ambazo wameweka na picha kabisa kwny hivyo vitabu:

4.Mwanaume na Mwanaume na mtoto wakisema hio Ni Aina nyingine ya familia.

5.Mwanamke na Mwanamke na mtoto wakisema hio ni Aina nyingine ya familia.

6.Shemale na shemale wakiwa na mtoto wakisema hio Ni type nyingine ya familia.

Sasa maskini wa JF endeleeni kushobokea msivyovijua huku mkisema tafuta hela.
Bro una hasira kinoma au utakua umempeleka dogo kwenye shule anayosoma form 1-4 ada ya miaka yote minne laki 4 na 60 Nini?
Kama ni hvyo lazma uwe na hasira na watu wanaolipa 71M kwa mwaka mmoja
 
Wakati tukiwa level ya primary nilikuwaga na machalii zangu wao walikuwa wanasoma Sombetini Primary School tukikutanaga wakawa wananiambia wamesoma kitabu cha kiswahili kuna mashairi sijui yanaitwa "kama mnataka mali mtaipata shambani" kwani huko Kigoma shule zao hazikufundisha?😂😂
kyeee!kyee!kyee!
E bwana eee kusema ule ukwerii wa ndani kabisaaa Hilo shairi liliandikwa na mhenga mmoja wa CCM kipindi Cha ujamaa Hata yeye aliyeandika hakuwahi miliki Hata shamba la mihogo Huko Kisarawe au Rufiji Lile lilikua ni shairi la motivation speaker wa enzi za ujamaa na kujitegemea kiuhalisia hamna kitu!

(In Brother K voices)
😁😁😁😁
 
Bro una hasira kinoma au utakua umempeleka dogo kwenye shule anayosoma form 1-4 ada ya miaka yote minne laki 4 na 60 Nini?
Kama ni hvyo lazma uwe na hasira na watu wanaolipa 71M kwa mwaka mmoja
😄😄😄 Kwahio na ww ambae ulipelekwa police baada ya kusingiziwa mwizi na walinzi wkt Ukitoka kuangalia Mpira kwny Banda umiza ukaishia tu kusema Mungu atawalipa unataka kuniambia nitafute hela sio?Hahah aiseee
 
Mtoto aliepitia hizi shule ana nafasi ya kuajiriwa haraka kuliko hizi zingine? Au nae lazima ahangaikie?
 
Tukiwa hatuna uwezo ni utamaduni wetu kuponda.

Tutaponda IPhone na kusifia Tecno.
Tutaponda Range Rover na kusifia Vitz.

Lakini ikitokea tumepewa tuchague zawadi ya bure kati ya Iphone na Tecno au Range na Vitz ndio utajua mahitaji yetu halisi ya mioyo yetu.

Hata kama mkuu kwa mwezi niingzie billion bado sijalipa ad ya milioni 70 yani haiwezekani sio tu kwasababu huo uwezo sina hata nikiwa nao iyo hela silipi niamini
 
Back
Top Bottom