Shule kumi ghali Tanzania

Shule kumi ghali Tanzania

Kwa sasa elimu ni ubishoo tu, na ndo mana utawaona ni matajiri, mtu wa kawaida wapo wanao weza na wana mishahara ya million 7 au 8 lakini wametoka familia masikini tu, milioni 71 per year nikiiweka Kwa akili ya huyo mtoto kiuwekezaji, na Kisha akasoma elimu ya kawaida, bado anaweza kifika mbali kielimu na akamaliza akiwa na mali pia ambayo wewe kama mzazi umeitengeneza, na inawezekana kabisa wale wenzie wa ada ya million 71 wakaja kuajiriwa naye

Msitujengee ujinga vichwani ilihali uhalisia tunaujua
Umekosea kusema "elimu in ubishoo" ungeweka "mtaala wa elimu ya bongo ni ubishoo".

Hao watu wanaosomesha watoto hiyo mitaala mostly ni watu wanaoijua dunia na wameteka takribani kila nyanja katika dunia halafu sio watu wa show off.
 
Hizo shule ndiyo wanaosoma watoto wa vigogo na wafanya biashara wakubwa nchini,, ambao wakimaliza mpaka mavyuoni, tayari wana nafasi zao serikalini huko,,
Wapi shule za kata????
Na huko kazini lazima wakwibe sana maana hiyo ada kuifidia siyo.
 
Hahaha hamna boss ni ujasiriamali tu. Tulifundishwa entrepreneurship pale KH.
hahahahah hongera mkuu kama waliwapa mbinu za kubinu mbwinu za kujikwamua ada haikwenda Bure Lima tu maana vijana wa kigoma wanakimbilia daslam kutembeza vyombo huko wameacha maekari ya kutosha yamekua mapori tu!
Mbinu za kilimo zero na hili li CCM letu no support!
 
Tukiwa hatuna uwezo ni utamaduni wetu kuponda.

Tutaponda IPhone na kusifia Tecno.
Tutaponda Range Rover na kusifia Vitz.

Lakini ikitokea tumepewa tuchague zawadi ya bure kati ya Iphone na Tecno au Range na Vitz ndio utajua mahitaji yetu halisi ya mioyo yetu.
Alisikika tajiri mmoja wa JF ambae anamiliki wa Aston Martin one,Koenigsegg, Bugatti na Pagani huayra akiongea kwa sauti ya juu wkt akikata gogo.
 
hahahahah hongera mkuu kama waliwapa mbinu za kubinu mbwinu za kujikwamua ada haikwenda Bure Lima tu maana vijana wa kigoma wanakimbilia daslam kutembeza vyombo huko wameacha maekari ya kutosha yamekua mapori tu!
Mbinu za kilimo zero na hili li CCM letu no support!
Wakati tukiwa level ya primary nilikuwaga na machalii zangu wao walikuwa wanasoma Sombetini Primary School tukikutanaga wakawa wananiambia wamesoma kitabu cha kiswahili kuna mashairi sijui yanaitwa "kama mnataka mali mtaipata shambani" kwani huko Kigoma shule zao hazikufundisha?😂😂
 
Hapo limerudi likizo baada ya form 6 halafu limevalia linakwambia linatoka na boyfriend wake.
Pumbavu, wache wakanunue visheti vya Ticha Manka huko Kayumba lakini wabaki marijali.

View attachment 2080147
Waache Hawa maskini wa JF wanaojifanya mafogo wkt Ni choka mbaya wajifanye wanashobokea hizo shule Kuna siku watajionea hayo majibu kwa watoto wao.
 
Mtu ana lipa ada kimilioni ana anza mishoboko mala ooh mtoto shule! Hahahahaa una zijua shule wewe
 
Kuna binadamu wanajua kutumia akili. Kwahiyo hii mashine inakwangua nyasi zisizo na tija na kuacha mazao. Je kama nyasi imeota kwenye shina la mmea sahihi inafanyaje!?.
Hapo ndio sijui sasa. Ila kuna watu wamepiga hatua sana yan kuanzia kuandaa shamba had kupeleka mazao sokoni wao wanatumia mashine tu
 
Vimaskini vya humu JF vimekalia kuimba Imba tu tafuta hela tafuta hela wkt havijui hata vinaongea Nini.

Hawa maskini wamesoma kayumba ambako kwny civics types za family walikua wanafundishwa ziko Aina Tatu.
1.Nuclear family
2.Extended family
3.Single parent family

Leo hizi shule za kitajiri, types of family wanazofundishwa Ni hizo Tatu hapo juu pamoja na hizi nyingine ambazo wameweka na picha kabisa kwny hivyo vitabu:

4.Mwanaume na Mwanaume na mtoto wakisema hio Ni Aina nyingine ya familia.

5.Mwanamke na Mwanamke na mtoto wakisema hio ni Aina nyingine ya familia.

6.Shemale na shemale wakiwa na mtoto wakisema hio Ni type nyingine ya familia.

Sasa maskini wa JF endeleeni kushobokea msivyovijua huku mkisema tafuta hela.
 
SHULE KUMI GHALI ZAIDI TANZANIA.

1- International School of Tanganyika (IST)
— Hii ndio shule ghali zaidi nchini. Iko jijini Dar Es Salaam na hufuata Mtaala wa IB. IST hutoza ada kuanzia shilingi za Kitanzania milioni 34 kwa chekechea hadi shilingi milioni 71 kwa sekondari, kwa mwaka.

2. Braeburn International School
—Hii ni shule ya kimataifa ambayo iko Dar Es Salaam na Arusha. Hufuata mfumo wa IB na ada yake kwa mwaka ni kuanzia shilingi za Kitanzania milioni 20 kwa shule ya msingi hadi shilingi milioni 43 kwa sekondari.

3. Dar Es Salaam International Academy (DIA)
—Hii ni shule ya tatu kwa kuwa na ada ghali zaidi nchini. Iko Dar Es Salaam na hufuata Mtaala wa IB. Ada yake kwa mwaka ni kuanzia Shilingi za Kitanzania milioni 23 kwa shule ya msingi hadi shilingi milioni 40 kwa sekondari.

4. Iringa International School (ISS)
— Iko mkoani Iringa na hufuata mitaala miwili ya IB na ule wa Cambridge. Hutoza ada kati ya Shilingi za Kitanzania milioni 17 kwa Chekechea hadi milioni 27 kwa sekondari.

5. Saint Constantine International School
—Inapatikana mkoani Arusha na hufuata Mtaala wa Cambridge. Ada yake ni kati ya Shilingi za Kitanzania milioni 8 kwa Chekechea hadi shilingi za Kitanzania milioni 23 kwa sekondari.

6. Kennedys House Schools
—Shule za Kennedys ziko maeneo mengi duniani. Nchini Tanzania iko katika mkoa wa Arusha wakiendesha Chekechea na Shule ya Msingi. Ada zao huanzia Shilingi za Kitanzania milioni milioni 8 kwa Chekechea hadi milioni 22 kwa Shule ya Msingi. Shule hii hufuata Mtaala wa Cambridge.

7. Haven of Peace Academy (HOPAC)
—HOPAC ipo katika Jiji la Dar Es Salaam. Hufuata Mtaala wa Cambridge na hutoza ada kati ya shilingi za Kitanzania milioni 16 hadi 22 kwa mwaka.

8. Aga Khan Primary & Secondary School
—Shule hii iko katika Jiji la Dar Es Salaam, na hufuata Mtaala wa IB kama ilivyo ISM. Hutoza ada kuanzia Shilingi za Kitanzania milioni 7 hadi milioni 20.

9. Internation School Moshi (ISM)/ UWC East Africa
— Hii ndio shule ghali zaidi katika mkoa wa Kilimanjaro. Hutoza ada kuanzia shilingi za Kitanzania milioni 16 kwa chekechea hadi shilingi za Kitanzania milioni 41 kwa wale wa kidato cha tano na sita. Shule hii hufuata Mtaala wa International Baccalaureate (IB).

10.Morogoro International School (MIS)
—Hii inapatikana mkoani Morogoro na hufuata mtaala wa Cambridge. MIS hutoza kuanzia Shilingi za Kitanzania milioni 6.4 kwa chekechea hadi shilingi za Kitanzania milioni 18 kwa sekondari. Hii ni ada peke yake, mbali na fedha ya usajili na boarding kwa wale wanaolala shuleni.

Huna hela wewe wenzako wanazo .....
 
Back
Top Bottom