Shule kumi ghali Tanzania

Shule kumi ghali Tanzania

SINA SWALI. Mtoto kazi kwake akija kuwa mlalamishi atakuwa kajitakia.
Ila math sio extra curricular bali ni mainstream curriculum.
Mtaala tarajiwa wa serikali usipocheza humo itakuwa wametumia pesa za serikali vibaya.

hawatumii mtaala wa serikali, they learn math darasani but kama kuna mtoto anataka more math, anapewa watoto wengi husoma chuo nje na wengi ndoto zao ni Ivy League baada ya DP
 
Ubora unakuwepo lakini sio technical, ada inakuwa kubwa kutokana na gharama za uendeshaji, mfano watachukua mwalimu kutoka uingereza/ Kenya na watamlipa mshahara wa milioni 6,watakula chakula kizuri labda kuku n.k, wataenda mbuga za wanyama, n.k wakati hizi shule za vumbi mshahara wa mwalimu ni laki 3. Kwa hiyo gharama kubwa aimaanishi ubora, bali inatokana na kuwa na gharama kubwa za uendeshaji.
Kimlipa mwalimu mil 6 ambae ni bora ndio ubora. Kula chakula balanced diet ndio ubora. Ni sahihi kulipa hizo hela pengine nj nfogo.
Niligogo ubso mmoja wa smart board una range mpaka milioni 20 ambao ni nchi 40. Shilr bora inahitaji smartboard kama hizo ngapi
Elimu ni gharama sana na ukitaka kujua hilo angalia vyio vya nje zina fika dola 100.000. Ina maana bila nfadholi husomi chuo kama hicho kwa sisi walala hoi .
Kuwepo shule 10 tu jama hizo ina maana bado tupo nyuma na hata wenye hela TZ bado hawaoni kipaumbele kulipa ada kubwa wanaona bora wapekeke kwenye private za milioni 2 ambazo ni kama kayumba za english ambazo hazina extra curricula.
 
NIMEPITIA HUU UZI WOTE MAFOGO WA JF SIJAWAONA, AU HUKU NI KINA KIREFU KWAO
 
Tukiwa hatuna uwezo ni utamaduni wetu kuponda.

Tutaponda IPhone na kusifia Tecno.
Tutaponda Range Rover na kusifia Vitz.

Lakini ikitokea tumepewa tuchague zawadi ya bure kati ya Iphone na Tecno au Range na Vitz ndio utajua mahitaji yetu halisi ya mioyo yetu.
😁😁😁😁
 
68914361-4027-4F34-B2D1-28B69070D82E.jpeg
 
Daaaa kuna jamaa yangu mmoja alikuwa anasomesha watoto wake 4 wote kwenye shule number 2 hapo.Ila maisha anayopitia sasahivi ni huruma.Na yule mtoto mkubwa yupo tu ameshindwa kumpeleka hata chuo Nairobi(Mana malengo ilikuwa S.A au Europe)
 
Na Kuna watoto wanasoma humo, nasemaje mkisema Mimi maskini sawa, cha muhimu afya. Na kufanya kazi kwani kitu Gani bwana 😢
 
SHULE KUMI GHALI ZAIDI TANZANIA.

1- International School of Tanganyika (IST)
— Hii ndio shule ghali zaidi nchini. Iko jijini Dar Es Salaam na hufuata Mtaala wa IB. IST hutoza ada kuanzia shilingi za Kitanzania milioni 34 kwa chekechea hadi shilingi milioni 71 kwa sekondari, kwa mwaka.

2. Braeburn International School
—Hii ni shule ya kimataifa ambayo iko Dar Es Salaam na Arusha. Hufuata mfumo wa IB na ada yake kwa mwaka ni kuanzia shilingi za Kitanzania milioni 20 kwa shule ya msingi hadi shilingi milioni 43 kwa sekondari.

3. Dar Es Salaam International Academy (DIA)
—Hii ni shule ya tatu kwa kuwa na ada ghali zaidi nchini. Iko Dar Es Salaam na hufuata Mtaala wa IB. Ada yake kwa mwaka ni kuanzia Shilingi za Kitanzania milioni 23 kwa shule ya msingi hadi shilingi milioni 40 kwa sekondari.

4. Iringa International School (ISS)
— Iko mkoani Iringa na hufuata mitaala miwili ya IB na ule wa Cambridge. Hutoza ada kati ya Shilingi za Kitanzania milioni 17 kwa Chekechea hadi milioni 27 kwa sekondari.

5. Saint Constantine International School
—Inapatikana mkoani Arusha na hufuata Mtaala wa Cambridge. Ada yake ni kati ya Shilingi za Kitanzania milioni 8 kwa Chekechea hadi shilingi za Kitanzania milioni 23 kwa sekondari.

6. Kennedys House Schools
—Shule za Kennedys ziko maeneo mengi duniani. Nchini Tanzania iko katika mkoa wa Arusha wakiendesha Chekechea na Shule ya Msingi. Ada zao huanzia Shilingi za Kitanzania milioni milioni 8 kwa Chekechea hadi milioni 22 kwa Shule ya Msingi. Shule hii hufuata Mtaala wa Cambridge.

7. Haven of Peace Academy (HOPAC)
—HOPAC ipo katika Jiji la Dar Es Salaam. Hufuata Mtaala wa Cambridge na hutoza ada kati ya shilingi za Kitanzania milioni 16 hadi 22 kwa mwaka.

8. Aga Khan Primary & Secondary School
—Shule hii iko katika Jiji la Dar Es Salaam, na hufuata Mtaala wa IB kama ilivyo ISM. Hutoza ada kuanzia Shilingi za Kitanzania milioni 7 hadi milioni 20.

9. Internation School Moshi (ISM)/ UWC East Africa
— Hii ndio shule ghali zaidi katika mkoa wa Kilimanjaro. Hutoza ada kuanzia shilingi za Kitanzania milioni 16 kwa chekechea hadi shilingi za Kitanzania milioni 41 kwa wale wa kidato cha tano na sita. Shule hii hufuata Mtaala wa International Baccalaureate (IB).

10.Morogoro International School (MIS)
—Hii inapatikana mkoani Morogoro na hufuata mtaala wa Cambridge. MIS hutoza kuanzia Shilingi za Kitanzania milioni 6.4 kwa chekechea hadi shilingi za Kitanzania milioni 18 kwa sekondari. Hii ni ada peke yake, mbali na fedha ya usajili na boarding kwa wale wanaolala shuleni.

Huna hela wewe wenzako wanazo .....
Hii inakusaidia nini, ndiyo maana mnakufa maskini.
 
Back
Top Bottom