Shule haikwepeki, hata kama hukwenda darasani, bila hivo utabaki maskini na Mungu atakukataa

Surya

JF-Expert Member
Jun 7, 2015
8,379
12,574
Nafungua ukurasa huu tujadiliane watu wote, wake kwa waume.
Wanasiasa, wafanyabiashara, Watumishi wa Mungu wote na hata wapagani Karibuni tuelekezane kwa upole na amani.
Hakikisha unamfundisha mwenzio kwa uwazi, kwa upendo wote bila makasiriko.

Nimesema shule nikimaanisha sehemu ya kujifunza, unaweza kujifunza kupitia vitabu mbalimbali, kumsikiliza mtu mwingine anachokuelekeza unaweza ukajifunza kupitia kuona jambo au matukio, kwa vitendo (practical) pia.
Mambo ya kujifunza ni mengi sana. Kwa kifupi hakuna mfanyakazi au mfanyabiashara asie jifunza.

Jambo gumu kujifunza na linalotumia muda mwingi ndio huleta mafanikio au faida kubwa pia.
Mada hii ni pana kwani mambo ni Mengi.
~ Kumjua Mungu
~ Biashara
~ Ufundi
~ Mahusiano, mtu na mtu
~ Mapenzi
~ Afya
~ Michezo

Kama ukitaka kuwekeza
Joel Nanauka anakwambia jambo la kwanza ni kuwekeza kwenye akili yako.
Usije ukasema mimi sina kazi na natamani siku moja niwe na pesa nyingi.. sasa acha nitulie nikae tu kwasababu kwa sasa bado sijapata mtaji.
Ukiwa na fikra hizi utakuwa ni mjinga kama wajinga wengine.

Nimechunguza nimegundua Mungu anatabia hii.. endapo utakataa kujifunza kwa kusoma na kusikiliza, Mungu huleta practical ujifunze kwa vitendo, utakapo angukia pua akili itakukaa 😁😁 Kwenye maandiko Utajifunza Saikolojia ya Mwanadamu na utaishi nae vizuri bila shida kabisa.

Twende kwenye neno(maandiko) watu wa Mungu, maana huko ndio kwenye kila kitu.

Hosea 4:6
Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako.

Yani sio maboss tu ndio wanatafuta watu wenye ujuzi na maarifa ya jambo fulani lakini pia hata Mungu, hachukui wavivu na wajinga.
Sitaeleza sana niende haraka kukaribisha mawazo na hoja za wengine.
uwa nasikitika sana kuona mtu ambaye anakurupuka kufanya kazi ya Mungu bila maelekezo ya kutosha kutoka kwa Mungu, Nyumba za ibada zimejaa Watumishi ambao hawajamaliza shule na Mungu then wanakurupuka kuanza huduma. Matokeo yake nikuwa na wao wanaingia kwenye taabu na tamaa nyingi.
Mussa alitamani kuwaongoza waisraeli akiwa na miaka 40, kazi ikamshinda akatoloka kumkimbia Farao akaenda kuchunga mifugo ya baba mkwe, kisha akaambiwa kazi ni sasa akiwa na Miaka 80.

Swala la Kutafuta utajiri
Ni uwe master mind kweli kweli.. ukiwa mtu wa kupuuza mambo huwezi toboa

Nyakati tulizopo ni hizi..
Kwasasa ili uweze kufanikiwa kiuchumi ni Lazima Uchague upande ambao utasimama kukutetea kuweza kupata huo utajiri na kufanikiwa.
Ni uchague Ufalme wa Nuru au Ufalme wa giza.
Mbali na hapo kwa sasa jiji limechafuka huwezi toboa.
Na nguvu hizi mbili hazifanani lakini waliowengi wameshindwa kabisa kuzitofautisha.
Unaweza kwenda kwenye Nyumba za Ibada ukifikiri utakutana na Mungu wa Nuru muumbaji lakini ukakutanishwa na Nguvu za giza.

Sasa akili kumkichwa.
ukienda kichwa kichwa utaumia.

Hata kwa shetani usipokua na kipawa au elimu yoyote, ukienda kwake atakugeuza kuwa mboga tu au kukutumia kufanya kazi zake chafu zilizojaa ukatili na uovu na uharibifu mwingi na mshahara wake anamalizia kwa kukuchukua na kwenda kuwa mtumwa katika kambi yake iliyojaa mateso, maumivu na kazi ngumu.

Lakini ukiwa msomi hata shetani anakuogopa, ukijua wewe ni nani na una mamlaka ipi na unanafasi ipi kwa Mungu hata jini linakuogopa.
Lakini ukiwa mjinga yani hata viganga uchwal vinakulisha mavi na hakuna kitu utafanya.

Msioamini hivi vitu kuwa vipo, poleni naomba mpite kimya.

Wafanyabiara wengi kwasasa wanatumia Nguvu za kiroho kuvuta wateja.
Matapeli na hata wezi karibia wote kwa sasa wanatumia nguvu ya giza kufanya kazi zao.
Watoto wa vyuo Karibuni Dar, kama unafikili matapeli wa Dar wanatumia maneno tu matupu, jichanganye sasa utajua dunia imekaaje.

Siku za Mwisho kutakua na Njaa, Sio njaa ya chakula ni njaa ya kulisikia neno la Mungu.

Ignore cause ignorance
 
Safi sana

Tuungane kuwasanua watu kila mmoja atumie akili tusonge

 
Back
Top Bottom