Shukrani toka kwa Sheikh Ponda Issa Ponda

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,015
SHUKRANI KUTOKA KWA SHEIKH PONDA ISSA PONDA!

Nilipigiwa simu na Sheikh Ponda Issa Ponda alipotoka kizuizini. Alipiga kwa lengo la kushukuru kwa ajili ya sauti zilizopazwa kwa ajili yake. Aliambiwa kuwa mimi nilikuwa ni miongoni mwa waliopaza sauti kwa ajili yake.

Nilisumbuka sana moyoni! Kwa nini mimi nipokee shukrani kwa kazi ambayo kwa kiasi kikubwa ilifanywa na wengine? Nilijaribu kukataa shukrani zile, lakini alivyosisitiza kumaanisha, ilibidi nijitahidi kumuelewa! Lakini baada ya kukata simu na kutafakari nikakumbuka jambo. Kwamba kupitia kwangu, shukrani zile zingewafikia pia watu wengine wengi ambao Ponda asingeweza kuwapata wakiwemo wale waliotumika kusambaza ujumbe wangu na wale walioandika maoni yao katika ujumbe ule. Wapo pia ambao waliandika katika kurasa zao nao pia wangelitiwa moyo kusikia kuwa hatua walizochukua zilimtia moyo na zilisaidia pakubwa!

Sheikh Ponda ni mtu wa shukrani. Hakulazimika kunitafuta mimi kwa lengo la kunishukuru. Pengine uungwana wake ndio uliomsukuma kufanya vile. Alitumia nafasi ile pia kuwashukuru watu wote waliopaza sauti kwa ajili yake pasipo kujali dini, itikadi, kabila, ukanda nk.

Mimi ni mtetezi wa uhuru wa kutoa maoni. Tunaweza tusikubaliane na maoni ya wengine, lakini ni wajibu wetu kutetea uhuru wao na haki yao ya kutoa maoni. Mimi ni mtetezi wa haki ya kila mtu kusikilizwa na kujitetea. Hatulazimiki kufuata maoni ya watu wote, lakini pia hatupaswi kuyazuia au kuyakandamiza maoni tusiyoyapenda!


Jamii isiyoheshimu maoni ya wengine itaendelea kwa kasi ndogo sana kuliko ile inayoheshimu maoni ya wengine na kutoa nafasi kwa maoni tofauti kusikika! Kuna kipindi maoni ya Galileo Galilei yalionekana kama uhaini, lakini baadaye maoni yale yakaja kushangiliwa kama ugunduzi mkuu!

Kuna aina mbalimbali za maoni. Kuna maoni ya kusifia na ya kukosoa! Yapo maoni ya kulalamika na kupongeza! Yapo maoni ya kuamsha hisia na mitazamo na ya kufifisha hisia. Kuna maoni yanayoweza kuleta ugunduzi na mengine kudumaza ugunduzi. Watoa maoni wasilazimishe maoni yao yafuatwe. Vivyo hivyo, wapokea maoni wasiwapangie watoa maoni ni aina gani ya maoni watoe ambayo wao wanataka kuyasikia!

Mwisho wa siku, maoni yaliyo na hoja ndiyo huheshimiwa katika jamii. Vivyo hivyo, maoni mabaya au yasiyofaa hunyamazishwa kwa hoja! Kuzuia maoni ni sawa na kuzuia kuhubiri Neno la Mungu. Tunahubiri kwa watu walio huru kusikia na walio huru kufuata au kutofuata tunachohubiri! Tukipambana na kutumia nguvu kwa lengo la kuzuia maoni, ipo siku tutajikuta tunapambana na kutumia nguvu kwa lengo la kuzuia Neno la Mungu lisihubiriwe pia.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula - Mwamakula - Moravian Revival Church in Tanzania & East Africa
 
Kila cinema ikiletwa wapinzani wanacheza, mara paap, mgombea urais kapata kura laki tisa
 
Kwa hiyo, ndo kusema Shehe Ponda yuko nje kwa dhamana baada ya kuwa ndani kwa sababu ya waraka was maoni ya waislamu wenzake?
 
Huyu ndio Askofu kwa maana halisi ya uaskofu.
Utakuwaje au inakuwaje uitwe Askofu huku unashindwa kusema ukweli na kuipigania haki?
Hongera sana Askofu pia hongera sana Shehe Ponda kwa kusimamia ukweli bila woga
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Kabisa Mkuu kwani matendo yao na kauli zao zinagusa/yanagusa mioyo ya Watanzania wengi sana.
Kabisa lkn wanaosema ukweli ndio wanaoitwa wachochezi lk wake wahuni wanaomsifia rais kinafiki ndio wanapewa vyeo ila mmoja tu ndo amebaki nagundu gani cjui anaitwa musiba japo nasikia analipwa na tiss
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Back
Top Bottom