Show za kibabe

Show za kibabe

Shukrani Mkuu kuna watu humu wakiamua kuonyesha ujuha wao humu hadi unashangaa! Duh! Nadhani tunaweza kuchukua ushindi kwa kuwa nchi yenye majuha wengi duniani.
Always huwa nikishaona dalili naquite the earliest
 
Kwani huyu mama alikua kiongozi wa nini?... Kama upendo tu, mbona mama Jannet au mama Salma walikua wazuri tu, walikua wanatoa maneno mazuri na hotuba mzuri, Juz juz mama Salma kupewa zawadi
Sijabahatika kuziona hotuba zao nitafurahi ukiziweka hapa...! Nawaheshimu sana
 
Huyo mama na mumewe wote wastaarabu sana halafu vichwa. Huko ndiko kwenda shule kwa maana ya kupata elimu na kuelimika sio kusoma bila kuelimika na kustaarabika
Haters don't like this
 
Najaribu kuwaza tuu, jee Michelle angekuwa ni 1st mamaa wa kwetu kwa sasa ni mabadiliko gani yangekuwepo kwa 1st gentleman wetu?
Maana wanasema ukiona mafanikio ya mwanamume ujue nyuma yake kuna mwanamke.
cc; Evelyn Salt
Wanasemaga soseji ya Los Angeles si ya Manzese midizini wala Tandale kwa Bibi nyau
 
Viongozi wa Afrika kama tulivyo waafrika wenyewe, tunaishi nyakati hizi lakini kwa fikra na tabia za kipindi cha kabla ya Yesu. Wakati ambapo hakukuwa na viongozi bali watawala. Watawala ambao waliamini ni wakuu wa kila kitu, hata hewa wanayoivuta watu wao.

Mtume Paulo alishtakiwa kwenye mahakama za Kiyahudi na kuhukumiwa lakini Paulo akasema anakata rufaa Roma, utawala wa kiyahudi uliheshimu kauli ya Paulo, akasafirishwa mpaka mjini Roma. Hiyo ilikuwa karne ya kwanza. Lakini ndani ya Afrika, karne ya 21, watu wanatengenezewa kesi, watu wananyimwa dhamana bila sababu za msingi, watu wanawekwa vizuizini, watu wanatekwa na kupotea, watu wanapigwa na Polisi bila hata sababu, etc. Halafu kuna Waafrika wanaamini kuwa nasi ni jamii ya binadamu sawa na wa mataifa ambako utu wa mtu una thamani kuliko kitu chochote.

Uonevu huleta laana, Afrika imelaanika kwa sababu ya dhuluma dhidi ya watu wake. Taifa la waliolaanika, midomoni mwa watawala hutoka maneno ya chuki na vitisho, na mikono yao huzalisha mateso na manung'uniko kwa watu wao.

Katika Afrika, badala ya viongozi kuwa kama vivuli kwenye jangwa kwaajili ya kujikinga watu wao, wao hugeuka na kuwa mapanga ya kuondoa vivuli. Badala ya viongozi kuwa kama vijito vya kutiririsha maji katika ardhi kame, wao huwa kama moto uchomao majani yaliyokauka. Badala ya wao kuwa tulizo kwa wanaowatawala hugeuka kuwa chukizo kwa watu wao. Badala ya viongozi kuwa daraja la kuwaunganisha watu wao, hugeuka na kuwa korongo la utengano.
 
View attachment 465950 Nimeangalia video ya Michelle Obama wakati akiwaaga wamarekani kupitia wanafunzi wa chuo kikuu...Hotuba ile aliyoitoa yule mwanamama maneno aliyoongea ni wachache sana duniani hata wenye elimu kiwango change phd wake kwa waume wanaweza kuitoa (nikijaaliwa nafasi nitaweka tafsiri yake hapa kwa tafsiri ya kikwetu.

Ni mojawapo ya hotuba bora kabisa kuwahi kutokea miaka ya hivi karibuni duniani, hotuba ya kutia hamasa kutia moyo kuamsha uzalendo na matumaini kujiamini na kujenga uwezo wa kutenda na kufikiri kwa njia chanya zaidi. Uhuru wa kujieleza matamanio ndoto mitazamo na hata maono
Niliwaona wazungu wakitokwa na machozi, ni hotuba inayopinga kunyanyapaa na kujinyanyapaa.

Nikakukumbuka hotuba za viongozi wetu wa kiafrika zilizojaa ubabe vitisho na kuwajenga watu kuishi kwa woga na kutojiamnini.

Tunajenga Taifa gani hili? Hatuwezi kuiga kwa Michelle?
Umeeeleza vizuri sana nikadhani nitapata cha maana kutoka kwako kumbe shida yako ni kuonyesha rangi yako ni ipi!!!Jogoo akiwika na asipowika kutakucha tu acheni chuki zenu hizo!!!
 
Huyo na mmewe achana nao kabisaaa!!

Angalia ile hotuba ya Obama kule Michigan siku ya kuwaaga wamarekani.
Obama anawa aga wananchi,na kuishukuru familia yake; wanae na mkewe kwa hisia kali na kwa maneno matamu ya kusifu mkewe hatimae machozi kumtoka.

Zile sifa Obama alizozitoa Obama kwa michelle ukizifanya hapa Bongo wanawake wote watakuona Malaika kwao.
 
Ndugu Mshana hotuba zina akisi kile mtu anachokiamini na kukisimamia kutoka moyoni. Nadhani huyu mama alikuwa akielezea hisia za moyoni mwake. Hata waafrika wanaweza kuelezea hisia zao nakushauri usikilize hotuba za Prof. P. L. O. Lumumba wa Kenya. Huyu alikuwa ni mkuu wa taasisi ya kupambana na Rushwa Kenya kabla hajatumbuliwa.
Siku izi plo Lumumba ameanza kuwa kanjanja mkubwa
 
Siku izi plo Lumumba ameanza kuwa kanjanja mkubwa
Unaweza kutoa ushahidi kuhusu ukanjanja wa huyu Professor msomi wa sheria? Mimi najua kanjanja ni mtu ambaye anafanya kazi ambayo hajaisomea - yaani anatumia uzoefu tu. Au nitajie Professor wa kitanzania ambaye unaweza kumlinganisha kwa uwezo wa kuchambua na kuwasilisha mada na huyu unayemwita ni kanjanja.
 
Huyo mama na mumewe wote wastaarabu sana halafu vichwa. Huko ndiko kwenda shule kwa maana ya kupata elimu na kuelimika sio kusoma bila kuelimika na kustaarabika

Unafananisha na wasomi wa hapa kwetu ambao wanaPHD lakini sana walichofanya ni kujua kusoma na kuandika na kuongeza makaratasi
 
Back
Top Bottom