Should CHADEMA Fire Zitto?

Should Zitto get FIRED from CHADEMA?

  • YES

    Votes: 137 65.9%
  • NO

    Votes: 57 27.4%
  • May be

    Votes: 10 4.8%
  • I don't know

    Votes: 4 1.9%

  • Total voters
    208
Status
Not open for further replies.
Wachaga tutawaachia Chadema yenu mbaki peke yenu ndio mtafurahi! Zitto siasa hizi za kibaguzi kutumia ukabila hazitawafikisha Chadema mbali!
 

hivi kumbe mtu akitangaza nia ya urahisi ndio anapigwa majungu hivi? yaani hata ushahidi haujawekwa wazi wakina mushi wanataka ipigwe kura ya kumfukuza mtu aaaaah acheni ujinga huo siamini kaka chama makini km chadema kitafanya maamuzi bilia ushahidi wa uhakika.....
 
Kweli mkuu CCM nayo imepata fursa ya kufanya vyake pia. Kila chama itatumia nafasi hii kujiendeleza na kuangamiza washindani wake.
Kwangu mimi HAKI itendeke kwa Zito na kwa chama. Kama kweli bila shaka yoyote Zito amepokea rushwa atoswe na kama hakuchukua kitu chama kimsemee.
 

Ni kweli mkuu. Hata ZZK naye kashindwa kuwa mwangalifu katika hilo, rejea kauli yake mitandaoni kuwa shutuma za rushwa ni vita ya presidential aspirants na wapambe wao toka VYAMA VYOTE (meaning Chadema is also among those Parties). Hii ni kauli mbaya sana, kwasababu naamini hata baada ya yeye kuwa cleared na CC ya Chadema kuhusika na shutuma hizi, then litaibuka jingine na litashikiwa bango na wabaya wa Chadema kuwa ZZK alikuwa framed kuhusika na rushwa by his own party ili asigombee urais 2015 (iwapo katiba mpya itamruhusu).

So, ninachotaka ku-caution hapa ni ZZK na wenzake ndani ya chama kuwa makini na kauli zao wakati wakishughulikia sakata hili ili whatever the outcome, chama chao kibaki salama na united. Ni hayo tu wakuu!
 
Kweli mkuu CCM nayo imepata fursa ya kufanya vyake pia. Kila chama itatumia nafasi hii kujiendeleza na kuangamiza washindani wake.
Kwangu mimi HAKI itendeke kwa Zito na kwa chama. Kama kweli bila shaka yoyote Zito amepokea rushwa atoswe na kama hakuchukua kitu chama kimsemee ili kulinda na kuheshimu ukweli na imani potofu ya jamii.
 
Ninachoomba ni CDM kuendesha kesi ya Tuhuma za Zitto kwa uwazi wote,

Waende hatua kwa hatua,
namna alivyo omba rushwa,
na namna alivyopewa rushwa
zilikuwa pesa taslimu?
Cheki au zilihamishwa ndani kwa ndani katika mabenki?
Nani aliombwa rushwa,
siku gani wapi na Tshs au $ ngapi.
Alimwomba kwa sababu gani.
Na yeye alimpa kiasi gani?
Mtoa rushwa ahojiwe pia,

Kuna uwezekano mkubwa tu,
hizi ni propaganda za kisiasa,
kuwakipi buze CDM na mambo ya kutunga,
kwa nia ya kuwapunguzia kasi yao ya M4C.

CCM kwa asili yao ni mabingwa,
wa kutunga kusema na kusambaza uongo,
Wakibanwa na kubainika wameongopa,
siku zote hujificha nyuma ya mapazia,
ya ukimya,ubabe na kiburi.

Wakibanwa sana utawasikia,
wakitoa kauri za ukindakinda,
kwamba uongo ni sehemu ya siasa,
wapinzani hawako imara kukabiliana,
na kuutambua uzushi,
hivyo si watu makini.
CCM,Mvi pekee yake si busara

wao CCM wakituhumiwa jambo,
hata lile lenye ukweli wa wazi,
wanatumia vombo vyote vya habari,
na vya ulinzi kuhakikisha kwamba,
tuhuma zinachujushwa na kugeuzwa maneno ya mtaani.

CDM ni lazima wazingatie haki na sheria,
wafuate kanuni za chama chao,
katika kusikiliza na kutoa maamuzi katika jambo hili,
jiwe lolote lisiachwe kukaa juu ya jiwe jingine.

Kama huna matokeo sahihi ya utafiti wako, huna haki ya kuongea.
 
Sasa naona ukabila ndani ya Chadema waziwazi! Hakika ni Chadema ni chama cha Wachaga!
 
Zitto ni muhimu sana Chadema lakini hii haimfanyi asichukuliwe hatua pale itakapothibitika alipokea rushwa. Mwali Nyerere aliwahi kutoa mfano wa mfalme mmoja ambaye alimuacha mke wake(malkia) kwa sababu ALITUHUMIWA TU kula rushwa. Kama mfalme huyo aliweza kumuacha kipenzi chake Chadema wasiache kumchukulia hatua AKITHIBITIKA, japo kwa mtu kama Zitto KUTUHUMIWA TU ilitosha kumuwajibisha!
 

Uko makini sana kaka......!
 
yeye ni mbunge, ametoa wapi hela za kununulia hummer, na lile gorofa anajenga mbezi beach?...jamaa ni mnafiki sana, anajifanya anaongea sana kumbe ananunulika tu. wengi wanamtuhumu kuwa amekula bilioni mbili wengine tatu za sisiemu ili aiangushe chadema kabla ya 2015.
 
Kwa utaratibu wako Zitto is a virus, no doubt, lakini hiyo ni kujikaanga kama watamfukuza kwa chuki. Zitto hajahongwa hata kidogo! Subirini midomo itakuwa wazi, lazima Lissu angemtaja kama angechukua rushwa but haikuwezekana hata kidogo. Najua CDM wanahangaika sana kumtoa Zitto but kama ni chama cha haki hawataweza lakini kama ni chamfukoni they will do that! and they will see what happens baada ya hapo.
kila jambo lina sababu zake zitto kashatimiza wajibu wake sasa aende tu ,do u knw how much one virus can damage miilion of good cells?
 
Zitto siamini kama kachukua rushwa kwa Mhando,tena eti yeye ndio kaomba sidhani....ila kinachofanya watu wawe na vimashaka ni yale matukio yaliyokuwa yanalipotiwa juu ya mikutano yake ya siri na watu wachafu....ili litapita ila litaacha doa kubwa sana sio tu kwa Zitto bali kwa Chadema yote...

Alafu kuna kitu nime-note kwenye ili sakata...kumbe Chadema kuna mpasuko mkubwa sana tofauti na tunavyochukulia...nimeona watu wanachukiana mpaka wako tayari kufanya lolote lile....kila kundi linafanya kitu kukomoa kundi lingine lakini hawaangalii mustakabali wa chama...kwa waelevu watakuwa wameliona ilo...sijui wazee wa chama wanalichukuliaeje ili au labda ndio demokrasia....!!

Mie namshauri Zitto atulie japo kidogo,aache kiburi na majivuno ya kitoto ni moja ya vitu vinavyommaliza kila kukicha....na vijana kwenye chama watulie waache kukomoana hawakomoani bali wanakiaribia chama...hii ishu imewavunja moyo sana vijana uku mtaani kuhusu hamasa ya kisiasa na vijana ndio mtaji wa CDM...Wekeni mambo sawa MAKAMANDA.
 
Last edited by a moderator:
Mtaendelea kuchemka sana, lakini hakuna facts ni maneno ya kwenye kahawa, wangapi wana magorofa na hawajaiba? we unafikiri ghorofa hadi uibe? look at you! hata mimi mtumishi wa kawaida najenga gorofa kwa hela yangu mwenyewe,hakuna hata senti ya kuiba, hayo ni mawazo mgando sana, tanzania ni virgin kabisa lots of opportunities unaweza jenga ghorofa bila kuiba.
 

Wanaodai hivyo si ni CCM cuz CDM hawakutoa hizi tuhuma........in any case binafsi sijamuelewa anachomsapoti Mhando ni nn
 
Zitto pole sana, anyway unaweza kusema unaonewa ni sawa. Ila kumbukumbu zangu zinaonyesha uliwahi kuwa na mawasiliano ya muda mrefu sana na Rostam, na mwanahalisi liliansika kwa uwazi na hukuwahi kukanusha.

Rostam baadae alienda voda na kumtafuta aliyetoa data. Hii binafsi inanionyesha wewe ni wa mlengo usiojulikana.

Kwa hili nashauri ufukuzwe maana ni hatari sana ndani ya chama na taifa kwa ujumla.
 
Wanaodai hivyo si ni CCM cuz CDM hawakutoa hizi tuhuma........in any case binafsi sijamuelewa anachomsapoti Mhando ni nn
Ni kweli unachosema,hatujajuwa bado ni kwanini anamsapoti Mhand😵n the other hand,yeye anaelekeza tuhuma kuelekea huko huko kwamba ni siasa za urais.
 
Umezungumza pointi za maana sana,je hata kama haya yakipita,na let's say Zitto didn't get fired,unadhani hatalitumia hilo kama mtaji wa kisiasa ukizingatia ameshayahusisha na urais?amelikoroga kinyama yani,let's wait and see,ila nimependa maoni ye wengi.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…