Shocking! Nusu ya vifo hutokana na maelezo ya daktari

Dah mshana aisee sio kwa upafect huu I didn't expect this umenijibu haraka mnoooo I wish watanzania mahala pa kazi tungekuwa sharp hivi

Samahani kwa kuingilia Uzi huu ila imenisaidia
niko njiani naelekea kwenye uzi husika
 
Mwili wa binadamu hufika mahali ukapata shida fulani ya kiafya... Hii shida hujulikana kama ugonjwa, maradhi, kuumwa ama kuugua.... Utatuzi wake ni kupata kitu cha kuweza kupambana na hilo tatizo ili mwili uweze kurudi katika hali yake... Ufumbuzi wa tatizo unaitwa tiba na mtatua tatizo anaitwa tabibu

Kwa sehemu kubwa duniani kaliba ya uuguzi na tiba kwa ajili ya afya zetu... Inawezekana kabisa ndio taasisi nyeti inayopiga pesa ya kufuru na yenye mtandao mkubwa zaidi... Ni ndani ya taasisi hii
Kuna wakweli na kuna waongo
Kuna wajuzi na kuna wanaridhaa
Kuna matapeli na wapiga dill
Kuna waaminifu na wadanganyifu
Kuna wanaojali taaluma na wale wenye tamaa ya utajiri... Nknk

Ndani ya hilo kapu kubwa la mchanganyiko wote huo... Wote wamejivika koti la kuokoa afya yako... Kutibu tatizo lako na kukuokoa na kifo.... Na wote wakiaminika pakubwa na wewe mgonjwa!
Lakini je unajua kwamba kwa sehemu kubwa mwili wako hutumiwa kama majaribio ya dawa zisizo na uhakika wa kukuponya?
Je wajua kwamba tunatibiwa kwa sehemu kubwa na dawa zisizokuwa na uwezo wa kutusaidia matatizo yetu..
Je wajua kuwa pamoja na usahihi wa tiba lakini tabibu wengi huwa hawaangalii complications za dawa anayokupa kama zinaendana na mwili wako?
Je wajua kuwa matabibu wengi wenye nguvu na kwa ushawishi wa wanasiasa hushawishi Mataifa kutumiwa dawa zenye madhara makubwa lakini ya siri watumiaji?
Je wajua kuwa tabibu kamwe hawezi kukwambia ukweli kuwa kila dawa anayokupa ni kemikali inayopunguza selihai zako?

Kuna makosa makubwa ya wazi na ya kificho yanayofanywa na hii taasisi kubwa... Yanayofanywa kwa bahati mbaya ama kwa nia maalum ili kutimiza lengo fulani?
Hivi kama uzalishaji dawa kwenye taifa fulani ndio chanzo cha ajira na pato sehemu ya pato Lao la taifa... Watakubali kweli watu wasiumwe?
Hivi kweli kama sehemu fulani kuna mzigo wa dawa za ugonjwa fulani za zaidi ya dola million miamoja.... Kuna mtu atakubali hasara ya kupoteza kwa kuzitupa?

Mataifa mengi hasa ya dunia ya tatu ni
Vituo vikubwa vya majaribio ya dawa mbalimbali duniani
Ni vituo vikubwa vya kuuziwa dawa zilizo chini ya viwango
Ni vituo salama vya kuuza dawa zinazokaribia kikomo cha matumizi lakini zikiwa kwenye vifungashio vipya
Ni sehemu za kubet na maisha ya watu na chanzo cha utajiri na kipato
Ugua magonjwa ya kansa, figo na ini... Hutakuwa na tiba moja... Na kila ukienda utabalidiliwa dawa... Ukiuliza utambiwa hii imefeli ngoja tujaribu hii... Na kwakuwa unataka kupona utamwamini tabibu wako..... Kumbuka hizi dawa bei yake ni kichaa... Vipimo vyake navyo havikamatiki.... Ukishatumia pesa yako yote na ya ndugu na pengine kuuza hata baadhi ya mali zako... Mwili dhaifu unakuwa umechoka mno kwa kuumwa lakini pia kwa sumu za kutosha mwilini kutokana na madawa mengi na vipimo.... Baada ya hapo ni
Nenda sehemu tatu tofauti leo ukapime malaria tu... Halafu kashuhudie maajabu ya matokeo ya vipimo.....
Nipo Dunia ya kwanza na kwenye Field hii na yote ulioyaeleza ni 100% kweli.
 
Mshana Jr naomba niweke feedback kama nilivyoahidi hapo awali,

Sikwenda Hospital ya Wilaya ila jana nilienda kwenye Hospital au Zahanati ya mtu Binafsi na mambo yalikuwa kama ifuatavyo;

Kumuona daktari sh.5000/= pia vipimo vinaanzia hapo hapo mapokezi utapimwa uzito na BP, baada ya hapo ndo unapelekwa kwa Daktari,

Chumbani kwa Daktari;
Kule Daktari akachukua maelezo yangu kisha akaniandikia sindano na vipimo

Sindano;

Hii niliandikiwa ya Diclophenac kwa ajili ya kutuliza maumivu makali ya kichwa, sikuwahi kuchomwa hii sindano hivyo baada ya kama nusu saa hivi maumivu makali ya kichwa yaliacha ila Nikaanza kuvimba macho, Daktari akaniuliza kama nilishawahi kuchoma sindano ya Diclophenac nikamjibu hapana sijawahi,
(Nilijua ni sindano ya Diclophenac baada ya kuuliza chumba cha sindano nesi ndo akanijibu nimeandikiwa ili kutuliza maumivu ya kichwa)

Vipimo;

Niliandikiwa vipimo vya elf 15,
Malaria, Haja Ndogo, Damu (full blood picture + Blood Group) na vinginevyo

Baada ya majibu ya vipimo kutoka nikarudi kwa Daktari kule sikukutwa na tatizo lolote,
DAMU SAFI
MKOJO MSAFI
MALARIA SINA yaani kila kitu safi,
Hivyo nikaandikiwa kwamba naumwa HOMA ISIYOJULIKANA au ILIYOJIFICHA

Dawa;
Hapa nikaandikiwa dawa za aina nne ikiwemo PARACETAMOL zikajumlishwa Gharama ikatoka Tshs.55,500/=
Nikamwambia naomba za muhimu kwanza nyingine ntakuja kuzifuata kesho (leo), akaniuliza, "WEE UNASHILINGI NGAPI?", Nikamjibu hapa nimebaki na elf 10 tu! Akasema nimpe Elf 40,Nikamwambia niandikie gharama ya hizo dawa niipeleke ofisini akakataa akajua anaweza niandikia kila Dawa na bei yake kisha nikaenda kununua sehemu nyingine,

Hivyo nikamwambia,"ANDIKA KIASI CHA PESA KINACHOHITAJIKA CHA KUNUNUA HIZO DAWA" Ndo akaniandikia kwenye kijikaratasi kishingo upande

Nikaondoka zangu huku kimoyo moyo nikajisemea yaani alitaka kunipiga ELF 75 kirahisi rahisi tu!
 
Tukishatokomeza vyanzo vya malaria let's say kwa nchi kumi tu Africa ni viwanda vingapi ughaibuni vitakosa dili? Ni wafanyakazi wangapi huko kwao watakosa ajira? Ni wafanyabiashara wangapi wa madawa watayumba? Ni wanasiasa wangapi wataathirika?
Your disease is the state of welfare of others

Utanyunyizia dawa kutoka wapi?
Viwandani? Siyo?
Utanyunyiza Mara moja? Hapana ni zoezi endelevu. Then viwanda vitaendelea kuwapo.
Je magonjwa yote yanatibiwa kwa njio hiyo tu? Hapana. Zirahitajika nyingine.
Nyia za kukinga ni bora kuliko za tiba lakini ni very expensive at a given time kuliko za tiba. Je tunaweza kughatimia???

Na inapotolewa dawa sio lazima lengo liwe tiba kwa kila dawa na kila ugonjwa, wakati mwingine ni kutibu/ kupunguza dalili na hatimaye kupunguza maumivu, kurefusha na kuboresha maisha.
 
Na huu ujumbe uwafikie wale wanaopenda kupimapima magonjwa yasioyokua na tiba kama ukimwi cancer etc. Wengi wakishapima hasa cancer huwa hawachukui round wanapotea.

Jidanganye. Kuhusu ukimwi ukiwahi mapema kwanza hauwi ukimwi, unakuwa MTU anayeishi na VVU.

Kwa tiba na ushauri tumehama kutoka ugonjwa unaoua fasta na magonjwa nyemelezi kwenda kuwa tatizo tunaloweza kuli- control kama ulivyo Kisukari na Shinikizo LA juu LA damu. Kikubwa uwahi mapema. Kupima kwako ni muhimu sana oli kuweza kufikia malengo ya 90%, 90%, 90% na hatimaye kuzima ngebe za VVU.

Kuhusu cancer the earlier the better. Zipo stages ambapo inaweza kutibiks kabisa.
Don't be fool. Jenga utamaduni wa kufanya medical check up at least once per year.

Aaaaaaah!! When was the last time umekula dawa ya minyoo?? Am not saying that unakula sana kachumbari, mishikaki isiyoiva uzuri au undercooked pork, Aaaaah am just suggesting uende maabara inayoeleweka upime choo tu wanaweza kuta chochote.
 
Lakini pia kuna hili la national policies... Hizi za kisiasa.... Tangu miaka ile ya 60 tukitumia quinine kama tiba komesha ya malaria mpaka leo hii tuko kwenye mseto je rate ya malaria imeshuka ama imepanda?
Kila wakati inaletwa dawa mpya na pengine kwa majaribio na kutangaziwa kuwa ndio tiba bora baada ya ile ya kwanza kuwa sugu
Ni wangapi wamesahau mseto za kwanza zilivyowaumiza watu tena wengine wakiachwa na vilema vya kudumu!? Achilia mbali vifo

Bro kuhusu majaribio ya dawa kuna taratibu zake.
Kuna maazimio na miongozo kibao ya kimataifa inayohusu drug trials.
Hapa tuna taasisi nyingi pia zinazoratibu hayo.
Kwanza niseme sio rahisi dawa iingie kwenye market kwa majaribio. Zinazoingia kwenye market tayari trials zinakuwa zimeshafanyika ma kudhibitika ni salama na zina uwezo wa kuleta faida kwa TIBA ya igonjwa uliokusudiwa. Na kama kuna side effects zinawekwa kwenye leaflets na maelezo mengi kuhusu dawa husika.

Tofautisha dawa feki na dawa inayofanyiwa utafiti.
Dawa feki ni uharamia na upuuzi kama ulivyo ualifu na upuuzi mwingine katika sekta nyingine. Na mapambano yake ni endelevu.
 
Tiba itakuwepo tu. Na kadiri wanadamu tunavyozidi kuwa waongo ndio utapeli na ujanja ujanja unaongezeka.

Tanzania wanaofariki kwa sababu wamekosa huduma sahihi hospitali ni wengi.

Visabibishi!
Elimu

Elimu kwa wahudumiwa.
Ya darasani:
Watu ambao hawajaenda shule ni wengi na sekta ya afya inaingia gharama kubwa sababu ya hii.

Elimu ya jamii
Yaani kuna watu wengi wanofikiri madaktari wanatibu kama waganga.

Elimu ya afya
Hapa hata humu kuna watu anaamini akikosa malaria, uti, typhoid anaamini hawajaona ugonjwa. Kuna magonjwa mengi zaidi ya hayo sema hatuna uwezo wa kupima.

Elimu kwa watoa huduma.
Bado kuna watu wengi nchi hii ambao hawajawahi hudumiwa na MDs. Usitarajie makubwa.

Biashara.
Wajanja wameona fursa ya kupata pesa bila jasho wengi ukiweka na hao wa tiba za asili.

Vipaumbele na imani.
Yaani hata wasomi unakuta hana bajeti ya afya.
Kuna wasomi wengine hawajui hata UTI. Wanameza dawa nusu leo zimepata usugu tunalaumu viwanda.

Hatuko serious.
Akija mtu analalamika huduma amekaa sana kwenye foleni namwambia kasomeshe mwanao na wewe mwenyewe.

Watu wanafurahia vitambi halafu baadaye tatizo kiwe daktari kukupa dawa.

Mwiso, watoa huduma nao ni watu. Si mapepo au miungu.
 
Hapo kwenye madawa nakubaliana na wewe asilimia 1000, yani dokta anakuandikia dawa lakini haulizi historia yako au kama una allergy yeye anaandika tu, ukifika nyumbani ukasoma kile kikaratasi kinachowekwa ndani ya boksi ya dawa utachoka, kuna vitu vingi vimeelezwa ambavyo dokta alipaswa kuuliza maswali kabla hajakuandikia, sasa jiulize wale wanatumiaga tu bila kusoma vile vikaratasi vya ndani wanazulika kiasi gani? dawa inaandika ukiwa hivi au vile usitumie hii dawa au tumia kwa jinsi hii na hii, vitu ambavyo ni kazi ya dokta lakini wapi, alafu wote wako hivyo sio hospitali za serikali wala bianafsi, hawana muda wa kujua historia za wagonjwa kabla ya kuwaandikia dawa, najiuliza na nchi yetu tu au dunia nzima ndo tabia ya madokta
 
Jidanganye. Kuhusu ukimwi ukiwahi mapema kwanza hauwi ukimwi, unakuwa MTU anayeishi na VVU.

Kwa tiba na ushauri tumehama kutoka ugonjwa unaoua fasta na magonjwa nyemelezi kwenda kuwa tatizo tunaloweza kuli- control kama ulivyo Kisukari na Shinikizo LA juu LA damu. Kikubwa uwahi mapema. Kupima kwako ni muhimu sana oli kuweza kufikia malengo ya 90%, 90%, 90% na hatimaye kuzima ngebe za VVU.

Kuhusu cancer the earlier the better. Zipo stages ambapo inaweza kutibiks kabisa.
Don't be fool. Jenga utamaduni wa kufanya medical check up at least once per year.

Aaaaaaah!! When was the last time umekula dawa ya minyoo?? Am not saying that unakula sana kachumbari, mishikaki isiyoiva uzuri au undercooked pork, Aaaaah am just suggesting uende maabara inayoeleweka upime choo tu wanaweza kuta chochote.
Hawa wanawaleta watu hospitali dakika ya mwisho wamezidiwa halafu waseme mgonjwa wao alifia hospitali hawakuona ugonjwa.
Kana kwamba hospitali zinatoa miujiza.
 
Hawa wanawaleta watu hospitali dakika ya mwisho wamezidiwa halafu waseme mgonjwa wao alifia hospitali hawakuona ugonjwa.
Kana kwamba hospitali zinatoa miujiza.

Wanaanzia kwenye maombi, then Songoma, wanakuja hospital too late. Na hapo hospital watafanya kinachowezekana kwa wakati, kwa hali ya ugonjwa au uwezo walio nao ( huwezi ambiwa upewe rufaa kutoka chunya kwenda Ocean road DSM wakati inajulikana kansa ishakula mitaa ya kutosha na death ni inevitable na huna hela ya kufika huko). Unapata counselling then you die kwa peace.
 
Mshana Jr naomba niweke feedback kama nilivyoahidi hapo awali,

Sikwenda Hospital ya Wilaya ila jana nilienda kwenye Hospital au Zahanati ya mtu Binafsi na mambo yalikuwa kama ifuatavyo;

Kumuona daktari sh.5000/= pia vipimo vinaanzia hapo hapo mapokezi utapimwa uzito na BP, baada ya hapo ndo unapelekwa kwa Daktari,

Chumbani kwa Daktari;
Kule Daktari akachukua maelezo yangu kisha akaniandikia sindano na vipimo

Sindano;

Hii niliandikiwa ya Diclophenac kwa ajili ya kutuliza maumivu makali ya kichwa, sikuwahi kuchomwa hii sindano hivyo baada ya kama nusu saa hivi maumivu makali ya kichwa yaliacha ila Nikaanza kuvimba macho, Daktari akaniuliza kama nilishawahi kuchoma sindano ya Diclophenac nikamjibu hapana sijawahi,
(Nilijua ni sindano ya Diclophenac baada ya kuuliza chumba cha sindano nesi ndo akanijibu nimeandikiwa ili kutuliza maumivu ya kichwa)

Vipimo;

Niliandikiwa vipimo vya elf 15,
Malaria, Haja Ndogo, Damu (full blood picture + Blood Group) na vinginevyo

Baada ya majibu ya vipimo kutoka nikarudi kwa Daktari kule sikukutwa na tatizo lolote,
DAMU SAFI
MKOJO MSAFI
MALARIA SINA yaani kila kitu safi,
Hivyo nikaandikiwa kwamba naumwa HOMA ISIYOJULIKANA au ILIYOJIFICHA

Dawa;
Hapa nikaandikiwa dawa za aina nne ikiwemo PARACETAMOL zikajumlishwa Gharama ikatoka Tshs.55,500/=
Nikamwambia naomba za muhimu kwanza nyingine ntakuja kuzifuata kesho (leo), akaniuliza, "WEE UNASHILINGI NGAPI?", Nikamjibu hapa nimebaki na elf 10 tu! Akasema nimpe Elf 40,Nikamwambia niandikie gharama ya hizo dawa niipeleke ofisini akakataa akajua anaweza niandikia kila Dawa na bei yake kisha nikaenda kununua sehemu nyingine,

Hivyo nikamwambia,"ANDIKA KIASI CHA PESA KINACHOHITAJIKA CHA KUNUNUA HIZO DAWA" Ndo akaniandikia kwenye kijikaratasi kishingo upande

Nikaondoka zangu huku kimoyo moyo nikajisemea yaani alitaka kunipiga ELF 75 kirahisi rahisi tu!
Asante sana kwa mrejesho vipimo viko ok lakini ukaandikiwa na doze ya 55elfu God is watching...! Ishu ya kuumwa kichwa mapumziko kunywa maji mengi na panadol vingesaidia... Ila watakula wapi?
 
Utanyunyizia dawa kutoka wapi?
Viwandani? Siyo?
Utanyunyiza Mara moja? Hapana ni zoezi endelevu. Then viwanda vitaendelea kuwapo.
Je magonjwa yote yanatibiwa kwa njio hiyo tu? Hapana. Zirahitajika nyingine.
Nyia za kukinga ni bora kuliko za tiba lakini ni very expensive at a given time kuliko za tiba. Je tunaweza kughatimia???

Na inapotolewa dawa sio lazima lengo liwe tiba kwa kila dawa na kila ugonjwa, wakati mwingine ni kutibu/ kupunguza dalili na hatimaye kupunguza maumivu, kurefusha na kuboresha maisha.
China wamewezaje? Nchi nyingine zote wamewezaje? Tunahofia gharama ya maramoja huku tukikubali gharama ya kila siku inayoondoka pamoja na maisha ya watu? Uhujumu uchumi ni dhana pana ila mpaka uijue vema
 
Sio rahisi kama unavyoiweka.
Inaanzia kwenye kuwakomboa watu kifkra na kielimu kabla ya hizo interventions.
Kama mpaka Leo kunawa tu mikono kama public health measure ya kupunguza magonjwa ya kuhara na mengineyo ni kizungumkuti je kuwaambia watu wanyunyize dawa let say after every 4 months kuuwa mazalia ya umbu itawezekana??
Choo tu mpaka tupelekane kwa mtendaji na fine juu hayo mengine vipi??
OK. Tunapopata chakula chetu kila siku huko migahawani how often tumekomaa tuhudumiwe na waliovaa mavazi rasmi kama unavyotakiwa?? Achana na kujua kama wamepima typhoid periodically kama inavyoelekezwa. Hayo ni baadhi ya vitu kwenye public health ambavyo ni wajibu wetu sisi watumiaji kuvisimamia kabla ya law enforcers na wengine to come into play.
Ni mwendo mrefu, hatua kwa hatua huku na sisi tukifanya / timiza yetu kabla ya government
 
Tuna miaka 50 ya uhuru nini kimeshindikana? Tutaweza lini tusipojaribu? Ugumu uko wapi? Tatizo ni moja tu... Tumeacha taaluma na kuipa siasa kipaumbele na thamani kubwa
 
Kwaiyo unashauri watu wakiumwa wasiende hospital?

Waende kwa waganga wa kienyeji kusikokua na chemicals?

Poor poor poor
 
Back
Top Bottom