Shivji: Mimi ni muumini serikali mbili

Shivji: Mimi ni muumini serikali mbili

Well analysed..!
Wengine huku mna-comment pasipo Kujua kuna Nini Nyuma ya Pazia. Ukiona msomi kaongea Ni JAMBO la kukaa kimya Na kuwaza au kutokuandika Chochote. Wasomi huongea Chini ya miamvuli miwili , Moja Ni nia Zao Za utashi unaotokana Na elimu zao Na pili Shinikizo la Watawala. Watawala wanatisha asikwambie Mtu!! Hakuna anaye penda Kifo, Ni rahisi ku-Sacrifice dignity yako Mbele ya jamii kuepusha mabalaa unayotishiwa Na watawala, Na frankly wasomi wengi sio majasiri Ni WAOGA sana.

Nikipima uzito wa Sentensi Za Mwanafalsafari huyu, utashi huu wa Kuongea sio WAKE. Lazima pana Shinikizo Nyuma Yake. NASEMA hivi kwa ushahidi wa Waziwazi Kwamba HAPANA Kati ya WANA-CCM au SERIKALI YA JMT Kiongozi yeyote ALIYE WAHI KUWA MUUMINI WA SERIKALI MBILI. Mwalimu Julius K. Nyerere HAKUWAHI Kuwa MUUMINI wa Serikali mbili. Msomi Na wasomi wote akiwemo Shimvi WANALIFAHAM HILI FIKA Kwamba Kwa wakati ule Ilimlazimu Mwalimu Na Cabinet zake kuridhia Muungano tata wa Serikali mbili lakini mchakato ukiwa kuelekea SERIKALI MOJA. Na Hii ndio Ndoto ambayo Mwalimu alipenda Itimie HATA kabla ya Umauti wake. Lakini Bado HATA Leo CCM wanaamini Ndoto Hii yaweza timia. So Mtu akisema Ni MUUMINI wa Serikali mbili ni Uongo Na WOGA tu Hakuna kitu Kama hicho. Ccm wote nadhani HATA wananchi Wote Ni Waumini wa SERIKALI MOJA.

Lakini TOKA Mwalimu atutoke tuwe wakweli tu michakato ya KUHARAMIANA kisiasa ikaanza kukua siku HATA siku within ourselves. Kuna UPANDE wa Muungano unaamini wakiwa wenyewe wanaweza Kufanya excellent kuliko Kuwa Na Muungano. Hali Hii ikapelekea UPANDE ule KUASI.. A COMPLETE open REBELLION. Hamwezi kujitengenezea Katiba Na Kujiita Nchi Na kusafirisha mamlaka Za Kidola huku Katiba mama IKIWEPO ISIYOWARUHUSU kutenda hivyo. Ni uvumilivu, utulivu Na Hekima Za Rais Wetu kuepusha Shari Na Umwagaji Damu ambao likely usinge Zuilika.

Wananchi kupitia TUME ya Mabadiliko ya Katiba tukasema, sisi Ni Ndugu kwanini Tugombane, embu Nyie kamateni fito hizi mjenge UPANDE wa kwenu Na sisi tujenge UPANDE huu wetu kisha wote tuweke PAA. Uamuzi huu una DHAMBI gani?!!???. Uamuzi wetu Wananchi hatutaki machafuko, hatutaki kugombana Na ndugu zetu, hatutaki kupoteza uhai wa Mtu yeyote. From point pai ya UASI Ninyi viongozi mlikuwa Na Uwezo wa kudhibiti lakini mliacha tuu kiasi Leo huwezi kuidhibiti. Kuendeleza Msemo wa Serikali moja au mbili Ni UCHOCHEZI wenye Lengo la kuvuruga Na Kiondoa AMANI ya Nchi Hii.

Hakuna ANAYE VUNJA MUUNGANO HAPA. Tunaimarisha MUUNGANO WETU.
 
Mhadhiri mwandamizi mstaafu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) na gwiji wa sheria nchini, Profesa Issa Shivji (pichani), amesema ni muumini wa muundo wa Muungano wa serikali mbili tangu zamani.

Alisema hayo jana kwenye kipindi cha Nipashe, kinachorushwa kila siku asubuhi na Radio One Stereo.

Profesa Shivji alisema amekuwa muumini wa muundo wa serikali mbili tangu mwaka 1983 na kwamba, wanaosema amebadili msimamo wake ni waongo, kwani katika kipindi hicho walikuwa bado hawajazaliwa.

Alisema hakuna siku, ambayo aliwahi kusema wala kushauri uwapo wa muundo Muungano wa serikali tatu.

“Wanaosema kuwa kuna chama kinachonisukuma na ambacho ninaegemea kwenye msimamo wao, kuhusu muundo wa serikali tatu hayo ni maoni yao binafsi,” alisema Profesa Shivji.

Kauli ya Profesa Shivji inakuja, huku kukiwa na shutuma kutoka kwa watu mbalimbali, ambao wamekuwa wakimlaumu kuwa ni kigeugeu, kwani huko nyuma aliwahi kusema kwamba, Zanzibar ina haki ya kuwa na mamlaka kamili.

Profesa Shivji akizungumzia Tume wa Warioba, alisema kuwa hakuwahi kutoa maoni yake kwenye Tume hiyo, isipokuwa aliitwa katika hatua za awali ili kutoa maelezo na mwongozo wa masuala ya kuzingatiwa katika kutengeneza katiba. Machi 30, mwaka huu, Profesa Shivji akizungumza kwenye kongamano la wasomi wa vyuo vikuu, lililoandaliwa na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, alisema Katiba ya Zanzibar ndiyo sababu kubwa ya mgogoro ndani ya Muungano.

Alisema marekebisho ya 10 mwaka 2010 ya Katiba ya Zanzibar yaliyoitambua Zanzibar kuwani nchi yenye mamlaka na mipaka yake na kumpa mamlaka rais wa Zanzibar kugawa maeneo ya mkoa, wilaya, na kupora madaraka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano ndiyo sababu ya matatizo katika Muungano.

Alisema pia kwamba, marekebisho mengine yaliyofanyika mwaka 1993 katika katiba hiyo yaliipa Zanzibar mamlaka ya kuwa na bendera na wimbo wa Taifa na kupendekeza kwamba, njia bora ya kulinda Muungano wenye muundo wa serikali mbili, ni kuondoa marekebisho hayo katika Katiba ya Zanzibar.

Profesa Shivji ambaye alikuwa mzungumzaji mkuu, alifafanua kuwa wanaotaka serikali tatu hawajui historia ya Muungano na ni wanasiasa, ambao ni wavivu kusoma na hawataki kufanya uchambuzi kabla ya kuzungumzia jambo linalowafikia.

Tume ya Jaji Joseph Warioba ilipendekeza muundo wa serikali tatu kwa maelezo kuwa ndiyo utakaokuwa mwarobaini wa kero za Muungano.

Jumatatu wiki hii, wajumbe wawili wa Bunge Maalumu la Katiba, Tundu Lissu na Jussa Isamail Ladhu waliitisha mkutano wa waandishi wa habari mjini Dodoma na kumtuhumu Prof. Shivji kuwa anasaliti msimamo na machapisho yake aliyoyasimamia kwa zaidi ya miaka 30 iliyopita kwa lengo la kuifurahisha serikali na CCM. Lissu na Jussa walisema wanamshangaa Prof. Shivji kwa matamshi yake na kutoamini kama aliyoyasema ilikuwa ni kwa akili yake au alishinikizwa.

Lissu alisema msimamo wa sasa wa Profesa Shivji kwamba Muungano wa serikali mbili unapaswa kudumishwa, umeshtua kwa kuwa unapingana na maandiko yake aliyochapisha kwenye vitabu mbalimbali yakipinga muundo wa serikali mbili.

Lissu alisema mwaka 1990 Prof. Shivji alitoa mhadhara wa kiprofesa uliosababisha apewe u-profesa akizungumzia misingi ya kisheria na uhalali wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kusema kuwa ili makubaliano ya Muungano yaweze kupata uhalali, ni lazima yatungiwe sheria ya kuridhia makubaliano hayo na mabunge ya nchi washirika.

Jussa alisema machapisho ya Profesa Shivji ndiyo yaliyochangia kuamsha vuguvugu la Wazanzibari kudai haki kwenye muundo wa Muungano, hivyo anashangazwa na kitendo cha Profesa Shivji kuyageuka machapisho yake na kutangaza hadharani kuunga mkono muundo ambao alikuwa akiukosoa kwa miaka mingi.

Alisema kitendo hicho kimemkwaza kwa kuwa yeye ni miongoni mwa Wazanzibar waliompatia ushirikiano mkubwa wakati akifanya utafiti wa masuala ya Muungano Visiwani Zanzibar.
CHANZO: NIPASHE

:yield:

Njaa mbaya sana,mkumbuke kuwa huyu Mzee kastaafu na pesa ndogo sana hana chochote alichojiwekea wakati akiwa chuo sasa inabidi awe mpiga debe wa ccm ili aweze kuishi.CCM kupitia costech hivi karibuni watamuandalia kongamano tena eti kutetea serikali 2
 
Watu wote ambao mnasema prof kawa kigeugeu, hembu toeni hapa ushahidi wa kunukuu machapisho yake ili sisi ambao hatukubahatika kufika kwenye elimu hiyo ya juu tuone!
 
Khaa!! Nyani wewe, Shivji >>> Lissu + Jussa + msigwa + ...+ vijibwa vyote kwenye mambo ya katiba. Katiba si siasa, katiba ni sheria.

Wewe acha tabia ya kutukana watu. hakuna aliyetukana hapa. Sasa nakwambia kijibwa ni mama yako, umezidi
 
Kuizuia Tanganyika isije ni sawasawa na mbuni kujifucha. Tanganyika itarudi hata kama si leo kesho yaja
MUNGU IBARIKI TANGANYIKA
 
Wanampinga Shivji waje na hoja zenye msingi...Uhindi ni rangi tu ile mbona hata nchi nyingine zina wahamiaji wa "races" tofauti? Hyo haiwez kuwa sababu ya yeye kutoa msimamo km huo!
 
Apande boti akawaeleze wale Wanzanzibari aliokuwa anawapa semina kuwa yeye ni muumini wa serikali 2.
 
Sasa matusi ya nini, sijamtusi mtu, wajinga ni waliokuzaa wewe unayetukana. mimi sijatukana mtu!
Khaa!! wewe vipi? Kuitwa mjinga si tusi. Ni sifa ya mtu asiyejua jambo fulani. Kama hujui kurusha ndege basi ni mjinga wakurusha ndege. Acha ujinga :rip:
 
Wewe acha tabia ya kutukana watu. hakuna aliyetukana hapa. Sasa nakwambia kijibwa ni mama yako, umezidi
Khaa!! wewe ukisikia neno kijibwa unapata picha ya mbwa mdogo. SIYO HIVYO!! Kasome upunguze ujinga wako :rip:
 
Wengine huku mna-comment pasipo Kujua kuna Nini Nyuma ya Pazia. Ukiona msomi kaongea Ni JAMBO la kukaa kimya Na kuwaza au kutokuandika Chochote. Wasomi huongea Chini ya miamvuli miwili , Moja Ni nia Zao Za utashi unaotokana Na elimu zao Na pili Shinikizo la Watawala. Watawala wanatisha asikwambie Mtu!! Hakuna anaye penda Kifo, Ni rahisi ku-Sacrifice dignity yako Mbele ya jamii kuepusha mabalaa unayotishiwa Na watawala, Na frankly wasomi wengi sio majasiri Ni WAOGA sana.

Nikipima uzito wa Sentensi Za Mwanafalsafari huyu, utashi huu wa Kuongea sio WAKE. Lazima pana Shinikizo Nyuma Yake. NASEMA hivi kwa ushahidi wa Waziwazi Kwamba HAPANA Kati ya WANA-CCM au SERIKALI YA JMT Kiongozi yeyote ALIYE WAHI KUWA MUUMINI WA SERIKALI MBILI. Mwalimu Julius K. Nyerere HAKUWAHI Kuwa MUUMINI wa Serikali mbili. Msomi Na wasomi wote akiwemo Shimvi WANALIFAHAM HILI FIKA Kwamba Kwa wakati ule Ilimlazimu Mwalimu Na Cabinet zake kuridhia Muungano tata wa Serikali mbili lakini mchakato ukiwa kuelekea SERIKALI MOJA. Na Hii ndio Ndoto ambayo Mwalimu alipenda Itimie HATA kabla ya Umauti wake. Lakini Bado HATA Leo CCM wanaamini Ndoto Hii yaweza timia. So Mtu akisema Ni MUUMINI wa Serikali mbili ni Uongo Na WOGA tu Hakuna kitu Kama hicho. Ccm wote nadhani HATA wananchi Wote Ni Waumini wa SERIKALI MOJA.

Lakini TOKA Mwalimu atutoke tuwe wakweli tu michakato ya KUHARAMIANA kisiasa ikaanza kukua siku HATA siku within ourselves. Kuna UPANDE wa Muungano unaamini wakiwa wenyewe wanaweza Kufanya excellent kuliko Kuwa Na Muungano. Hali Hii ikapelekea UPANDE ule KUASI.. A COMPLETE open REBELLION. Hamwezi kujitengenezea Katiba Na Kujiita Nchi Na kusafirisha mamlaka Za Kidola huku Katiba mama IKIWEPO ISIYOWARUHUSU kutenda hivyo. Ni uvumilivu, utulivu Na Hekima Za Rais Wetu kuepusha Shari Na Umwagaji Damu ambao likely usinge Zuilika.

Wananchi kupitia TUME ya Mabadiliko ya Katiba tukasema, sisi Ni Ndugu kwanini Tugombane, embu Nyie kamateni fito hizi mjenge UPANDE wa kwenu Na sisi tujenge UPANDE huu wetu kisha wote tuweke PAA. Uamuzi huu una DHAMBI gani?!!???. Uamuzi wetu Wananchi hatutaki machafuko, hatutaki kugombana Na ndugu zetu, hatutaki kupoteza uhai wa Mtu yeyote. From point pai ya UASI Ninyi viongozi mlikuwa Na Uwezo wa kudhibiti lakini mliacha tuu kiasi Leo huwezi kuidhibiti. Kuendeleza Msemo wa Serikali moja au mbili Ni UCHOCHEZI wenye Lengo la kuvuruga Na Kiondoa AMANI ya Nchi Hii.

Hakuna ANAYE VUNJA MUUNGANO HAPA. Tunaimarisha MUUNGANO WETU.

Umeandika mengi lakini nashindwa kupata point ya mahubiri yako! Kwamba muungano ni wakulazimishwa au muungano ni mzuri?
 
Wanampinga Shivji waje na hoja zenye msingi...Uhindi ni rangi tu ile mbona hata nchi nyingine zina wahamiaji wa "races" tofauti? Hyo haiwez kuwa sababu ya yeye kutoa msimamo km huo!

Waje na hoja wakati yeye hakutoa hoja? Hoja ni kwamba wengi wanataka serikali tatu! Sasa yeye aje na hoja kuonyesha vingine!
 
Rohonzuri uelewe wewe ni Mtanganyika tuu usidanganywe...BABA NI BABA hata kama hujamuona, asilani huwezi jitungia baba mwingine..
Khaa!! Usiwe na akili fupi
Mtanganyika = mchaga + Msukuma+ mhehe+ muha + ...+...
Mchaga = Mrombo + Mmarangu + ...+..
Mmarangu = Mtui + Tarimo +...+...
Sasa Mtanganyika yuko wapi??? Acha ulevi :rip:
 
Kwanini kuwe na serikali mbili au tatu au moja?

Si kila mtu awe na nchi yake na Serikali yake apendavyo mwenyewe.

Huu Muungano una siri gani kubwa hata uwepo?
 
Wengine huku mna-comment pasipo Kujua kuna Nini Nyuma ya Pazia. Ukiona msomi kaongea Ni JAMBO la kukaa kimya Na kuwaza au kutokuandika Chochote. Waisomi huongea Chini ya miamvuli miwili , Moja Ni nia Zao Za utashi unaotokana Na elimu zao Na pili Shinikizo la Watawala. Watawala wanatisha asikwambie Mtu!! Hakuna anaye penda Kifo, Ni rahisi ku-Sacrifice dignity yako Mbele ya jamii kuepusha mabalaa unayotishiwa Na watawala, Na frankly wasomi wengi sio majasiri Ni WAOGA sana.

Nikipima uzito wa Sentensi Za Mwanafalsafari huyu, utashi huu wa Kuongea sio WAKE. Lazima pana Shinikizo Nyuma Yake. NASEMA hivi kwa ushahidi wa Waziwazi Kwamba HAPANA Kati ya WANA-CCM au SERIKALI YA JMT Kiongozi yeyote ALIYE WAHI KUWA MUUMINI WA SERIKALI MBILI. Mwalimu Julius K. Nyerere HAKUWAHI Kuwa MUUMINI wa Serikali mbili. Msomi Na wasomi wote akiwemo Shimvi WANALIFAHAM HILI FIKA Kwamba Kwa wakati ule Ilimlazimu Mwalimu Na Cabinet zake kuridhia Muungano tata wa Serikali mbili lakini mchakato ukiwa kuelekea SERIKALI MOJA. Na Hii ndio Ndoto ambayo Mwalimu alipenda Itimie HATA kabla ya Umauti wake. Lakini Bado HATA Leo CCM wanaamini Ndoto Hii yaweza timia. So Mtu akisema Ni MUUMINI wa Serikali mbili ni Uongo Na WOGA tu Hakuna kitu Kama hicho. Ccm wote nadhani HATA wananchi Wote Ni Waumini wa SERIKALI MOJA.

Lakini TOKA Mwalimu atutoke tuwe wakweli tu michakato ya KUHARAMIANA kisiasa ikaanza kukua siku HATA siku within ourselves. Kuna UPANDE wa Muungano unaamini wakiwa wenyewe wanaweza Kufanya excellent kuliko Kuwa Na Muungano. Hali Hii ikapelekea UPANDE ule KUASI.. A COMPLETE open REBELLION. Hamwezi kujitengenezea Katiba Na Kujiita Nchi Na kusafirisha mamlaka Za Kidola huku Katiba mama IKIWEPO ISIYOWARUHUSU kutenda hivyo. Ni uvumilivu, utulivu Na Hekima Za Rais Wetu kuepusha Shari Na Umwagaji Damu ambao likely usinge Zuilika.

Wananchi kupitia TUME ya Mabadiliko ya Katiba tukasema, sisi Ni Ndugu kwanini Tugombane, embu Nyie kamateni fito hizi mjenge UPANDE wa kwenu Na sisi tujenge UPANDE huu wetu kisha wote tuweke PAA. Uamuzi huu una DHAMBI gani?!!???. Uamuzi wetu Wananchi hatutaki machafuko, hatutaki kugombana Na ndugu zetu, hatutaki kupoteza uhai wa Mtu yeyote. From point pai ya UASI Ninyi viongozi mlikuwa Na Uwezo wa kudhibiti lakini mliacha tuu kiasi Leo huwezi kuidhibiti. Kuendeleza Msemo wa Serikali moja au mbili Ni UCHOCHEZI wenye Lengo la kuvuruga Na Kiondoa AMANI ya Nchi Hii.

Hakuna ANAYE VUNJA MUUNGANO HAPA. Tunaimarisha MUUNGANO WETU.

Tumeshindwa kuelewana tukiwa wawili halafu tutegemee tukiongeza wa tatu tutaimarisha mahusiano, bado sijawa convinced, tunaelekea kuuvunja Muungano na kwa kweli tuseme wazi tumeshachokana sasa basi, kila mtu aende zake.

Wale wanaoshabikia serikali tatu, hizo hazitakuja sasa, labda huko mbeleni.
 
Namuunga mkono kabisa hata mimi ni muumini wa serikali mbili pia.
 
Tumeshindwa kuelewana tukiwa wawili halafu tutegemee tukiongeza wa tatu tutaimarisha mahusiano, bado sijawa convinced, tunaelekea kuuvunja Muungano na kwa kweli tuseme wazi tumeshachokana sasa basi, kila mtu aende zake.

Wale wanaoshabikia serikali tatu, hizo hazitakuja sasa, labda huko mbeleni.
Wadau wa serikali tatu ni uroho wa madaraka tu kutaka kugawana vyeo hii haikubaliki kabisa.
 
Bahati mbaya kundi linalorengwa eti ndiyo maoni ya watanzania ni wanasiasa, wananchi wa kawaida wako busy na shughuli za kujitafutia mlo wa kila siku.

Ningewaona wa maana sana kama wangechukuwa muda mrefu kujadili namna nchi yetu inaweza kuwakwamua wananchi na maisha duni regardless nani yuko madarakani.
 
Back
Top Bottom