Jamani hapa lazima tuwekane sawa na tuwe wawazi ili kukinusuru chama vinginevyo chadema itatufia mikononi kama ccm inavyoelekea kufa mikononi mwa rais kikwete. Mimi lazima niseme ukweli kwa manufaa ya chama atakayecheka acheke, atakayenuna anune, atakayelia alie ilimradi ujumbe umefika. Tukubali tusikubali, tutake tusitake uteuzi wa viti maalum kwa chadema ulikubwa na mizengwe fulani ambayo kwa namna moja au nyingine isipodhibitiwa siku zijazo chadema KITAKUFA! Nasema hivi kwa sababu kuna harufu ya undugunaization ambao umesababisha baadhi ya maeneo ambako chadema kimepata viti viwili au zaidi vya majimbo lakin yamekosa walau kiti 1 maalum. Kwa mfano, kulikua na sababu gani kwa mkoa wa singida kupata viti 2 na kilimanjaro kupata viti 3 hadi 4 maalum halafu mkoa kama shinyanga ambako chadema wamezoa majimbo 4 na kuibiwa la shy mjini na mbeya ambako wamezoa majimbo mawili kukosa walau kiti kimoja maalumu!? Pia kuna sababu gani zanzibar kupewa viti maalum 3 wakati chadema wanajua no matter what they do out there, the island will remain CUF-CCM dominated! Nadhan zanzibar kiti kimoja au 2 vingetosha walau kimoja kikaenda shinyanga! Katika mazingira kama haya kwa nini mtu asihoji wakati anaona jina la christina lissu (sijui uhusiano wake na tundu lissu) na la binti ndesa to mention but a few, yakiwa kwenye orodha!!? Viongozi wa chadema lazima walione hili na walifanyie kazi mapema wasituletee tabia za kubebana kama za ccm. Chadema ndo kwanza kinakua na hakijawa na wawakilishi wengi sana kwa hiyo basi wapinzani wake wanaangalia kila pungufu linalotokea na wanapata cha kusema na kuandika. Naomba tusiwape nafasi wapinzani wetu wasije sababisha chama chetu kife na wao ccm wakaendelea kutamba wakati wananchi wamesha wachoka!! TAKE CARE., LONG-LIVE CHADEMA..
Nilikuwa mmoja wa wagombea viti maalum toka mkoa wa Iringa, nimetoa mchango mkubwa kwa wagombea wote wa mkoa wa iringa na nje ya Iringa kama Ubungo, Segerea yalipo makazi yangu na Kilombero kwa dada Regia
Nilizunguka karibu kata zote za Isimani licha ya kutokuwepo mgombea ubunge ili kuhakikisha angalau tunapata kura wakati wa kampeni. niliomba likizo kazini na baadaye kuacha kazi ili nikafanye kampeni mkoani Iringa, Nina Digrii ya uchumi pia tukisema digrii ni vigezo. Bahati mbaya sikubahatika kuwa mmoja wa wateule, lakini mchango wangu nilikuwa nautoa kwa Chama, sikuwa nautoa ili nipate ubunge wa viti maalum, nimefurahi kwa walioteuliwa, nampongeza dada Yangu Chiku Abwao kwa kuteuliwa kuwa Mbunge viti maalum na kazi yangu ni kumsaidia, kushirikiana naye na kuchota uzoefu na uwezo toka kwake na siyo kupiga majungu.
Bahati nzuri mimi ni Muislamu na wakati wote siamini kama Kitila alitumia kigezo cha dini yangu kuniacha nje kwa sababu hata Chiku Abwao ni muislamu kwa hiyo wenye hoja kama hizo za udini ni wanasiasa waliofilisika kimawazo.
Sitaki kuzungumzia hoja ya kwa nini mbeya wamekosa mbunge wa viti maalum lakini napingana na wanaoendekeza majungu na kujaribu kujenga Taswira kwamba walitakiwa wawe wabunge wa Viti Maalum no Matter What????
Kazi ya kulikomboa taifa hili haiwezi kuletwa na wanasiasa ambao akili yao ni kuwa wabunge au wateule. Mtazamo wangu mara zote umekuwa mmoja. Tuungane pamoja , Tushirikiane na waliopata nafasi, lakini waliopata nafasi wafanye kazi kwa bidii ili tulio nje tusipate nafasi ya kusema "Hata mimi ningefaa kuliko yule" hizi hoja za kwa nini Christine Lisu kateuliwa au Kwa nini Lucy Owenya ni upuuzi. Tusubiri performance yao ndipo tuwaseme. Naamini Dr Kitila Mkumbo ni Mtu makini na alifanya kazi yake kwa vigezo. Namjua kitila kwa kuwa ni kiongozi wangu lakini yeye hanijui na sihitaji wala sikuhitaji kujipenyeza nijulikane kwani naamini wanaofanya kufanya hivyo ni wale wasiojua kuwa Siasa is a process, you need to start somewhere, you need to learn from others etc, siyo kulazimisha kupata nafasi za kuongoza.
Kama mtu ana vigezo hatuwezi kumkataa eti kwa kuwa anaitwa Kabwe au Mbowe au Slaa eti kuogopa undugunization
Undugunization ni kuteua watu wasio na vigezo kwa kuangalia majina, Naamini akila Owenya na Lissu wana vigezo na watatuwakilisha vema.
Narudia, sijibu hoja ya Shitambala lakini napingana na walalamikaji wenzangu kwani mimi pia nilikuwa mgombea na nimetoswa na nina furaha, amani na hapa nilipo napanga mikakati ya kuchangia chama ili 2015 tufanye vizuri zaidi
Nawasilisha