Shiranga la Mashoga wa Baa ya Stonewall! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shiranga la Mashoga wa Baa ya Stonewall!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Apr 16, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Apr 16, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280

  stonewall.jpg

  Inadaiwa kwamba tukio la awali la serikali yoyote duniani kupambana na ushoga ni lile lililotokea kule Marekani Julai 6, 1969. Mapambano kati ya Polisi wa nchi hiyo yalitokea kwenye kitongoji cha Greenwich jijini New York, kwenye baa iliyokuwa ikifahamika kama Stonewall. Baada ya kuwepo kwa taarifa ya baa hiyo kuwafuga mashoga, polisi waliandaa shambulizi kwa kisingizio cha kumkamata mwenye baa na wanywaji kwa kuendesha biashara ya pombe bila leseni.

  Shambulizi dhidi ya baa hiyo lilifanywa saa 6:00 usiku hadi saa 8:00 ikiwa ni saa mbili za kamata kamata. Polisi wa awali ambao walikuwa ni wachache walikaribia kuzidiwa nguvu na mashoga ambapo ilibidi waombe msaada wa kuongezewa nguvu, vinginevyo mashoga hao huenda wangewaumiza au kuwadhuru zaidi. Katika mpambano huo Polisi wanne walijeruhiwa na mashoga kadhaa pia ambapo 13 walikamatwa. Ndani ya baa hiyo inadaiwa kwamba kulikuwa na zaidi ya mashoga au mashoga na wapenzi wao wapatao 200. Baa hiyo inadaiwa kwamba ilikuwa ikiendeshwa na kundi la kigaidi la Mafia.

  Habari za shambulizi hilo iliandikwa kwenye gazeti la New York Daily News, la Julai 6 hiyo hiyo, lilinukuu baadhi ya kauli za mashoga hao. Baadhi ya wale walionukuliwa ni pamoja na Erick na Jackson ambao walikuwa ni wachumba na Bruce na Nan ambao pia walikuwa ni mke na mume. Mashoga hao walinukuliwa na gazeti hilo wakilaani shambulio hilo kwani walisema lilikuwa limevuruga harusi iliyokuwa ifanyike Julai 7, yaani siku inayofuata kati ya Erick na Jackson.

  Mama mmoja anayeishi jirani na eneo hilo, Shirley Evans aliliambia gazeti hilo kwamba, mashoga kwenye baa hiyo walikuwa ni watu waungwana sana na kamwe hakuwahi kusikia vurugu au ugomvi ndani ya baa hiyo. Kwa hiyo kuvamiwa kwao na Polisi alikuona kama uonevu tu.

  Kumbuka hiyo ilikuwa ni mwaka 1969, wakati huku kwetu hata uchangudoa lilikuwa ni jambo la aibu sana na la kushangaza.
   
 2. Mkaa Mweupe

  Mkaa Mweupe JF-Expert Member

  #2
  Apr 16, 2012
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 654
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35

  Kwani Sodoma na Gomorah ilikuwa ni mwaka gani? Haya mambo yapo tangu zama hizo! Tangu Adam na Hawa walipomuasi Mungu...
   
 3. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #3
  Apr 16, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  NImezungumzia kwa huku kwetu Tanzania, jambo hilo la ushoga lilikuwa ni jambo la kufikirika..........................
   
 4. BAGAH

  BAGAH JF-Expert Member

  #4
  Apr 16, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 4,523
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  kaka MTAMBUZI...siku zote nakwambia "yako ndefu lakini imenyooka"...HAYA TUAMBIE STONEWALL YA DASLAMU IKO WAPI?...lmao!
   
 5. Kunta Kinte

  Kunta Kinte JF-Expert Member

  #5
  Apr 16, 2012
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 3,660
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Kwa hiyo mazee hadithi yako inatufundisha nini?
   
 6. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #6
  Apr 16, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Mh ulizia mwanayamala kuna movement ya mashoga na inakuja juu

  Soon utagundua kuwa TZ kulikuwa na mashoga 2000 kila mkoa mwaka 1969
   
 7. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #7
  Apr 16, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,578
  Likes Received: 543
  Trophy Points: 280
  hahahah NATA Bwana
   
 8. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #8
  Apr 16, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  najua walikuwepo lakini ilikuwa ni kimya kimya....................Lakini siku hizi.............Mweh!
   
 9. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #9
  Apr 16, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,129
  Likes Received: 6,617
  Trophy Points: 280
  Asante kwa kutujuza hili.

  Naomba unitumie ile ya yule
  mwanamke wa kibongo aliyemuua mwenzie
  sikuwa nimemaliza kuisoma, niwekee hata kwenye PM.
  heshima sana kwako kijana wangu.
   
 10. Mkaa Mweupe

  Mkaa Mweupe JF-Expert Member

  #10
  Apr 16, 2012
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 654
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Hii inatokana na kukua kwa njia ya upashana habari kuwa rahisi. Siku hizi tukio linatokea unapata taarifa hai (live story) ila enzi hizo mpaka uwe wa ndani(inner circle) ndo ujue...

  Hata hivyo hawa jamaa zako kitambo wapo mbali... Just Imagine Titanic ilizama 14/04/1912, huku Tanganyika hata Nyerere Hajazaliwa... si mambo ya ajabu haya...

  Na kwenye hiyo Titanic kulikuwa na mashoga eebboooh!...
   
 11. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #11
  Apr 16, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Sehemu za kuzifanyizi kama stonewall

  1. Ni salenda briji- Njenje jumamosi
  2.
   
 12. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #12
  Apr 16, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Ukweli ndio huo first lady hawa watu wapo muda mrefu sana hasa pwani hii ya EA
   
 13. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #13
  Apr 16, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Kuna stori moja tulikuwa tunasimuliana, eti shoga kamuona mwizi akikimbizwa yeye akam-mwagia shombo ya samaki, wale waliokuwa wakimfukuza mwizi wakamuuliza kwa nini hakumkamata yule mwizi yeye akasema, "Nimemwagia shombo ya samaki, akaliwe na paka huko mbele ya safari......." LOL
  Najaribu kujiuliza wakati huku kwetu mashoga walionekana laini laini, lakini hawa wenzetu walimudu kupambana na Polisi kwa mtiti wa nguvu hadi ikabidi Polisi waombe msaada wa vikosi zaidi........kumbuka walikuwa hawana silaha!
   
 14. TaiJike

  TaiJike JF-Expert Member

  #14
  Apr 16, 2012
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 1,475
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Hivi kuna hisia ipi hapo kati mwanaume na mwanaume kupaishana? duh.... kinyaa sana aise nashindwa hata kuchangia.
   
 15. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #15
  May 29, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  Acha kusoma historia za kibongo na za mashariki ya kati..Mombasa na zenj km miji ilianza lini?Mercury alikuwa ndiye shoga maarufu kujitangaza wazi ktk vyombo vya habari na kupata support ya mataifa makubwa.Ila hivi vizee vijavyojisifia kwa ubasha along the coast vina miaka mingapi?
   
 16. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #16
  May 29, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Kati ya mashoga si kunawengine ni madume na mengine majike hapo?
  Naona yale madume ndiyo yaliyopambana na maaskali.lol!
   
 17. kadoda11

  kadoda11 JF-Expert Member

  #17
  May 29, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 16,379
  Likes Received: 8,505
  Trophy Points: 280
  kw hiyo mkuu kwa thread hii unataka kutuambia kuwa unaunga mkono hoja ya barack obama....:ranger:
   
 18. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #18
  Jul 5, 2016
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  kumbe hawa jamaa wakiungana kinanuka.
  Naogopa yasije kutukuta
   
 19. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #19
  Jul 5, 2016
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,230
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  Kweli Marekani wametutangulia kwa mengi!
   
 20. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #20
  Jul 5, 2016
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  wenzetu walijaribu wakaangukia pua wakakubali yaishe
   
Loading...