Ship Chartering - Biashara ya ukodishaji meli

Offshore Seamen

JF-Expert Member
Mar 9, 2018
4,947
12,517
Ship Chartering ni biashara ya ukodishaji meli baina ya mmiliki na mkodishaji kwa makubaliano maalumu.Charterer huyu ni mtu ambaye anaenda kukodisha meli.Charter Party huu ni mkataba wa makubaliano ya kukodisha meli kati ya mmiliki na mkodishaji.

Biashara ya kukodisha meli kuna madalali(Ship Brokers) hawa ndio kiunganishi kati ya wamiliki na wakodishaji. Ship Broker yeye uwasiliana na pande zote mbili na kufanya makubaliano pande zote na kusikiliza hitaji la kila mmoja.

Tuangalie aina za Ship Chartering
1.Time Charter
Huu ni ukodishaji wa meli kwa kipindi fulani cha muda, inaweza ikawa wiki,mwezi. Meli gharama za wafanyakazi na kuendesha meli kipindi chote cha mkataba zitakuwa za mmiliki na mkodishaji yeye atalipa gharama za kukodi meli,bandari,mafuta.
Hapa mmiliki atakuwa na mamlaka yote kwenye meli yake.

2.Voyage Charter
Huu ni ukodishaji wa meli kwa safari husika kutoka sehemu moja kwenda nyingine.Mfano meli inaweza ikakodiwa kwa safari ya kutoka Dar es Salaam itapopakia mzigo kwenda China itapoenda kushusha mzigo.

Kwenye ukodishaji huu gharama za kuhudumia meli na wafanyakazi wote hubaki chini ya mmiliki wa meli husika mkodishaji ulipa gharama za kusafirisha mzigo kwa tani.

Kwenye mkataba kuna makubaliano katika muda wa kushusha na kupakia mzigo(Laytime) endapo mkodishaji atawahi kufanya kwa wakati atalipwa pesa kama bonasi kwa kuwahi(Despatch). Na kama mkodishaji atachelewa kutokana na muda waliokubaliana itabidi amlipe mmliki gharama za uchelewaji(Demurrage Cost)

3.Demise/Bareboat Charter
Huu ni ukodishaji wa meli ambao mkodishaji ukodisha meli kwa kipindi fulani na umiliki uamia kwake na anakuwa na mamlaka ya kuhudumia meli,kusajili kwa utaifa anaotaka,kuwahudumia wafanyakazi.

Huu mfumo unatumika sana kwa wakodishaji meli za mafuta(Tankers) na shehena kichele(Bulk Cargo) mizigo isiyo wekwa kwenye kontena kama ngano,mahindi na makaa ya mawe.
Matajiri wa mashariki ya mbali na Asia wao huenda kwa watengeneza meli na hukodi meli ikiwa mpya (Hire and Purchase) ambapo hukubaliana kuikodi huku wakilipa kuinunua kipindi cha mkataba.

Angalizo: Kwenye biashara hii ya ukodishaji meli au boti wakodishaji wamekuwa wahanga maana kwenye mkataba huu vipengele vya masharti wamiliki wamekuwa wakiweka katika maandishi madogo sana na uwia vigumu mtu kusoma. Hii imepelekea kesi nyingi sana kwa wakodishaji pale wanapokosea kutokana na kutosoma vizuri vipengele vya mkataba.
 
Ziwa Victoria inawezekana kama kuna watu wana hizo meli. Kwa baharini ni rahisi maana vyombo ni vingi na unaweza ukakodi hata nje ya nchi.

Hizi ngalawa za Uvuvi hivi zinauzwaje bei yake na biashara ya kukodisha kwa wavuvi huwa inafanyikaje pale feri kiongozi...?

Naskia inalipa sana sana. Tupe muongozo angalau tupate ABC kiongozi.

Thanks a lot.
 
Mkuu bei za kukodisha boti za uvuvi pale ferry sizijui?
Ila bei ya kukodisha injini ya boti kwa Dar kwa siku huwa kati ya 15000-20000/= mafuta juu ya mtumiaji na gharama ya kuileta na kurudisha kwako.

Tanga boti/Ngalawa/Dau ndogo unaweza ukakodisha kuanzia elfu 10,000 na kuendelea kulingana na ukubwa.
 
Ngalawa ndogo inachongwa kutokana na gogo la mti mkubwa hizi ukiwa na kuanzia laki 7 unaoata iliyokamilika.

Boti za mbao itabidi utengeneze na mbao pamoja na ufundi andaa kuanzia million 2 au 3 unaweza ukapata boti hata ya mita 7.
 
Mkuu bei za kukodisha boti za uvuvi pale ferry sizijui?
Ila bei ya kukodisha injini ya boti kwa Dar kwa siku huwa kati ya 15000-20000/= mafuta juu ya mtumiaji na gharama ya kuileta na kurudisha kwako.
Sawasawa kiongozi na hiyo 15/20k inakuwa kwa siku na vipi bei ya engine husika ni kiasi gani inauzwa kiongozi...?

Tanga boti/Ngalawa/Dau ndogo unaweza ukakodisha kuanzia elfu 10,000 na kuendelea kulingana na ukubwa.
Hiyo ni bei ya boti/ngalawa yenye engine au inakuaje kiongozi...?

Na vipi suala la kutokomea nayo uaminifu unakuaje kiongozi...?
 
Ngalawa ndogo inachongwa kutokana na gogo la mti mkubwa hizi ukiwa na kuanzia laki 7 unaoata iliyokamilika.

Boti za mbao itabidi utengeneze na mbao pamoja na ufundi andaa kuanzia million 2 au 3 unaweza ukapata boti hata ya mita 7.

Hii inabidi ichongwe au inakuwa tayari imeshachongwa unachofanya ni kununua tu...?
 
Sawasawa kiongozi na hiyo 15/20k inakuwa kwa siku na vipi bei ya engine husika ni kiasi gani inauzwa kiongozi...?

Hiyo ni bei ya boti/ngalawa yenye engine au inakuaje kiongozi...?

Na vipi suala la kutokomea nayo uaminifu unakuaje kiongozi...?
Injini inauzwa kivyake bei zinatofautiana kulingana na ukubwa wa nguvu (HP) zipo za kuanzia million 2.

Boti hizo za mbao hazitengenezwi na injini wewe ndio unaweka. Unaweza ukakuta iliyotengenezwa au ukatoa oda wakuchongee utakayo.
 
Ukikodisha mtu unayempa ni wale wavuvi wanao aminika na mnaandikishana.

Ngalawa ni ndogo yenyewe inatumia tanga kuendeshwa kwa nguvu ya upepo au kupiga kasia.
 
Back
Top Bottom