Shinyanga: Wananchi wachinja na kugawana nyama ya fisi aliyekuwa akizurura Kata ya Ngokolo

Roving Journalist

JF-Expert Member
Apr 18, 2017
421
1,000
Katika hali isiyo ya kawaida wakazi wa kata ya Ngokolo Mjini Shinyanga wamegombania nyama ya fisi waliyemuua baada ya kuonekana akiranda randa katika kata hiyo.

Tukio hilo la aina yake limetokea Ijumaa Februari 7,2020 majira ya mbili usiku katika mtaa wa Magadula kata ya Ngokolo ambapo mamia ya wananchi wameonekana wakisukumana huku wengine wakikata viungo vya mnyama fisi anayedaiwa kuwa na hirizi katika mguu wake wa mbele.

“Huyu fisi ametokea maeneo ya Seif Hotel, akaelekea maeneo ya Stendi ya mabasi Mjini Shinyanga, wananchi wamemkurupusha Stend, akatokezea eneo la Mapinduzi shule ya Msingi, kisha Mshikamano baadae akaingia kwenye kalavati/daraja lililopo mtaa wa Magadula karibu na barabara ya Mohamed Trans.

“Huyo fisi alivyoingia kwenye kalavati akatulia humo, wananchi wakachoma tairi upande wa pili, kutokana na moshi fisi akatoka, ndipo mmoja wa wananchi hao akampiga jiwe huyo fisi akaanguka. Jamaa aliyempiga jiwe akakata mguu wa mbele wenye hirizi, akaondoka zake na wananchi wakaendelea kugombania viuongo vya fisi, kila mmoja akikakata kiungo alichoona kinamfaa. Askari polisi wamefika ikashindikana kuondoa wananchi." Mashuhuda wamesema.

Tukio hili limehusishwa na imani za kishirikina kutokana na madai kwamba fisi huyo alikuwa na hirizi na siyo rahisi fisi kuonekana mjini kwani fisi mara nyingi hupendelea kwenye mapori/vichaka.

Habari kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa baada ya fisi huyo kuuawa na wananchi kugawana nyama,mwanamke mmoja ameonekana eneo alipouawa fisi huyo na kuanza kuangua kilio akidai fisi wake kauawa.

"Yaani huku ni vituko, kuna mama kaja mpaka eneo alipochinjiwa fisi akaangua kilio fisi wake wamemchinja akaanza kutafuta kichwa hajakipata, akawaambia watu fisi wangu alikuwa na kitu bora wangenirudishia tu. Kazoa mabaki yote kaondoka nayo alikuwa na bodaboda. Watu walivyoona hivyo wamemfuata na daladala na bodaboda kwa nyuma hadi wajue anakoelekea." amesema mmoja wa wakazi wa eneo hilo.
View attachment Shuhudia Live w-1581151982752.mp4Sent using Jamii Forums mobile app
 

Patroman

JF-Expert Member
Nov 12, 2018
519
1,000
shy town tena kwa mauzauza ndio mwenyewe...kuna mzee mmoja marehemu (aliuwawa) alikuwa anaitwa Jikolile alishi mshikamano....alikuwa anatembea huku akifuatana na mbuzi mnyama...kifo chake kilisababishwa na kipigo kutoka kwa wananchi wenye hasira...baada ya mbuzi wake kumnusa mtoto mdogo alikuwa anacheza.... na baadaye mtoto huyo alifariki.
 
Top Bottom