Shinyanga: Wananchi wachinja na kugawana nyama ya fisi aliyekuwa akizurura Kata ya Ngokolo

Sio njaa ni imani za watu ushirikina. Fisi akigogwa hata barabarani wasukuma watasafisha hadi unyoya na damu.Fisi kwa imani zao anasadikika kuwa na nguvu ,bahati.Hata baadhi wacheza ngoma za jadi nguli huwafuga na kwenda nao katika matamasha kama kivutio na nguvu za ziada.

Sent using Jamii Forums mobile app
bila kusahau chatu wa kule makurugusi.

NB:
daladala ifahamike kuwa zimeongelewa baskeli za kubeba abiria. wenyeji wa dar msije kutafsiri ni Toyota Hiace

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tusije shangaa baada ya siku kadhaa watakao kuwa na nyama ya fisi huyo /wahusika kupatwa na madhila ya ajabu ajabu.
 
Wasukuma bana, wacha tuitwe washamba tu, yaani badala ya kugombania yale ma-diamond, ma-gold, ma-platinum na ma-copper tumeishia kugombania nyama ya fisi yenye hirizi?!
Wacha wakina Barrick na Petra au Wiliamson Diamond wajizolee mali tu...
Bure kabisa
 
Katika hali isiyo ya kawaida wakazi wa kata ya Ngokolo Mjini Shinyanga wamegombania nyama ya fisi waliyemuua baada ya kuonekana akiranda randa katika kata hiyo.

Tukio hilo la aina yake limetokea Ijumaa Februari 7,2020 majira ya mbili usiku katika mtaa wa Magadula kata ya Ngokolo ambapo mamia ya wananchi wameonekana wakisukumana huku wengine wakikata viungo vya mnyama fisi anayedaiwa kuwa na hirizi katika mguu wake wa mbele.

“Huyu fisi ametokea maeneo ya Seif Hotel, akaelekea maeneo ya Stendi ya mabasi Mjini Shinyanga, wananchi wamemkurupusha Stend, akatokezea eneo la Mapinduzi shule ya Msingi, kisha Mshikamano baadae akaingia kwenye kalavati/daraja lililopo mtaa wa Magadula karibu na barabara ya Mohamed Trans.

“Huyo fisi alivyoingia kwenye kalavati akatulia humo, wananchi wakachoma tairi upande wa pili, kutokana na moshi fisi akatoka, ndipo mmoja wa wananchi hao akampiga jiwe huyo fisi akaanguka. Jamaa aliyempiga jiwe akakata mguu wa mbele wenye hirizi, akaondoka zake na wananchi wakaendelea kugombania viuongo vya fisi, kila mmoja akikakata kiungo alichoona kinamfaa. Askari polisi wamefika ikashindikana kuondoa wananchi." Mashuhuda wamesema.

Tukio hili limehusishwa na imani za kishirikina kutokana na madai kwamba fisi huyo alikuwa na hirizi na siyo rahisi fisi kuonekana mjini kwani fisi mara nyingi hupendelea kwenye mapori/vichaka.

Habari kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa baada ya fisi huyo kuuawa na wananchi kugawana nyama,mwanamke mmoja ameonekana eneo alipouawa fisi huyo na kuanza kuangua kilio akidai fisi wake kauawa.

"Yaani huku ni vituko, kuna mama kaja mpaka eneo alipochinjiwa fisi akaangua kilio fisi wake wamemchinja akaanza kutafuta kichwa hajakipata, akawaambia watu fisi wangu alikuwa na kitu bora wangenirudishia tu. Kazoa mabaki yote kaondoka nayo alikuwa na bodaboda. Watu walivyoona hivyo wamemfuata na daladala na bodaboda kwa nyuma hadi wajue anakoelekea." amesema mmoja wa wakazi wa eneo hilo.
View attachment 1350642



Sent using Jamii Forums mobile app
Wakifuatilia asili ya huyo fisi wanaweza kukuta wamchinja binadamu mwenzao
 
Nani kakudanganya eti fisi hawaji mjini... kwetu pale misitu ilipo na mjini center ni kitambo kabisa tena mbali hasa lakini kila jioni fisi kama wote wanajisogeza machinjioni basi lakini cha ajabu

1.ikifika swalaa hutamsikia hata mmoja (mlinzi wa machinjio ambaye yeye ndo anayashuhudia kupitia kijumba chake cha ulinzi kila siku yanapokuja na kuondoka anasema ikifika saa 12 na kigiza tu ndo wanaanza kumiminika na haivuki saa 6 wote wamesepa

2.mpaka kufika machinjioni nyumba zimeshona lakini hayupo mtu anayesema leo nimekuta fisi sehemu (fisi wanakuja/ondoka kwa timing ya kiwango cha daktari wa falsafa tena mwenye digrii 4)

3.Hakunaga kesi za kushambuliwa na fisi labda mojamoja sana kwa mifugo kwa wale wanaofuga ng'ombe na mbuzi(pamoja kwamba fisi hao wanazurura pia muda wote wanapokwepo mjini)


4.
 
Back
Top Bottom