Shinyanga: Wananchi wachinja na kugawana nyama ya fisi aliyekuwa akizurura Kata ya Ngokolo

Sio njaa ni imani za watu ushirikina. Fisi akigogwa hata barabarani wasukuma watasafisha hadi unyoya na damu.Fisi kwa imani zao anasadikika kuwa na nguvu ,bahati.Hata baadhi wacheza ngoma za jadi nguli huwafuga na kwenda nao katika matamasha kama kivutio na nguvu za ziada.

Sent using Jamii Forums mobile app
Bado uko mulemule kwani wakisema wanna njaa Wana maanisha nini !
 
Fisi kuonekana shinyanga mbona ni Jambo la kawaida Sana sema huyo walimuhusisha na mabo yao ya kiimani sio kwa ujasiri huo
Interesting!
 
Kama simba mwenyewe anagwaya kula nyama ya fisi, binadamu wanagombania fisi kweli? hao watu kwa kweli wamebobea kwenye ushirikina..
 
Mkuu wacha kuongopa!

Haujaangalia chanel za wanyama kama Natgeo nk, fisi kwa simba ni 'sambusa'.

Analiwa hadi anaisha huku akipiga kelele za vitisho zisizomsaidia!

Simba naye akikaa vibaya analiwa na mbwa mwitu.

Mbwa mwitu akiingia kwenye anga za fisi, anafyagiliwa huku akibweka.

Hakuna aliye salama.

Nilidhania tembo hawezekani, kumbe kwa simba ni mswaki!

Mambo ya porini yaacheni jamani nyie.

Documentary 1 niliiona simba walikua watatu na wana njaa hatari mpk wamekonda,wakamuua Fisi wakaanza kumla ila simba mmoja na njaa yake aligoma kabisa kumla yule fisi akabaki na njaa yake tu(wanasema nyama ya fisi inanuka).

dodge
 
ndipo mmoja wa wananchi hao akampiga jiwe huyo fisi akaanguka. Jamaa aliyempiga jiwe akakata mguu wa mbele wenye hirizi, akaondoka zake...
Katika hali isiyo ya kawaida wakazi wa kata ya Ngokolo Mjini Shinyanga wamegombania nyama ya fisi waliyemuua baada ya kuonekana akiranda randa katika kata hiyo.

Tukio hilo la aina yake limetokea Ijumaa Februari 7,2020 majira ya mbili usiku katika mtaa wa Magadula kata ya Ngokolo ambapo mamia ya wananchi wameonekana wakisukumana huku wengine wakikata viungo vya mnyama fisi anayedaiwa kuwa na hirizi katika mguu wake wa mbele.

“Huyu fisi ametokea maeneo ya Seif Hotel, akaelekea maeneo ya Stendi ya mabasi Mjini Shinyanga, wananchi wamemkurupusha Stend, akatokezea eneo la Mapinduzi shule ya Msingi, kisha Mshikamano baadae akaingia kwenye kalavati/daraja lililopo mtaa wa Magadula karibu na barabara ya Mohamed Trans.

“Huyo fisi alivyoingia kwenye kalavati akatulia humo, wananchi wakachoma tairi upande wa pili, kutokana na moshi fisi akatoka, ndipo mmoja wa wananchi hao akampiga jiwe huyo fisi akaanguka. Jamaa aliyempiga jiwe akakata mguu wa mbele wenye hirizi, akaondoka zake na wananchi wakaendelea kugombania viuongo vya fisi, kila mmoja akikakata kiungo alichoona kinamfaa. Askari polisi wamefika ikashindikana kuondoa wananchi." Mashuhuda wamesema.

Tukio hili limehusishwa na imani za kishirikina kutokana na madai kwamba fisi huyo alikuwa na hirizi na siyo rahisi fisi kuonekana mjini kwani fisi mara nyingi hupendelea kwenye mapori/vichaka.

Habari kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa baada ya fisi huyo kuuawa na wananchi kugawana nyama,mwanamke mmoja ameonekana eneo alipouawa fisi huyo na kuanza kuangua kilio akidai fisi wake kauawa.

"Yaani huku ni vituko, kuna mama kaja mpaka eneo alipochinjiwa fisi akaangua kilio fisi wake wamemchinja akaanza kutafuta kichwa hajakipata, akawaambia watu fisi wangu alikuwa na kitu bora wangenirudishia tu. Kazoa mabaki yote kaondoka nayo alikuwa na bodaboda. Watu walivyoona hivyo wamemfuata na daladala na bodaboda kwa nyuma hadi wajue anakoelekea." amesema mmoja wa wakazi wa eneo hilo.
View attachment 1350642

Sent using Jamii Forums mobile app
Aliyeondoka na matumbo nampa pole sana... Akamakinike na nyongo

Jr
 
Hawana tofauti na wakanyanga mafuta

Acha kudanganya watu,nyie vijana wa mitandaoni mnashida sana,

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu unaona nasema uongo kuongea kuhusu hali ya umaskini Nchini?

Kama mtu nyama anakula Christmas hadi Christmas tena nusu kilo tu kutokana na umasikini utasema naongea uongo?

Kama Mjomba wako ungeweza kumudu kumtumia hela ya nyama angalau kilo 50 tu kwa mwaka asingehangaika kula hiyo nyama ya Fisi.
Hiyo yote inasadifu lundo la umasikini lilivyoshamiri kwenye jamii ya Watanzania.
 
Back
Top Bottom