Geita: Watu 10 wajeruhiwa na fisi

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,115
Screenshot 2023-03-30 at 14-06-01 BLUE BOY WA KISHUA (@millardayo) • Instagram photos and videos.png


Screenshot 2023-03-30 at 14-09-47 BLUE BOY WA KISHUA (@millardayo) • Instagram photos and videos.png
Watu 10 katika Kijiji cha Nyamalimbe Kata ya Nyamalimbe Wilayani Geita Mkoani Geita wamejeruhiwa na Fisi muda mfupi baada ya Fisi hiyo kumuua ng’ombe katika Kijiji hicho.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Bethaneema Mlayi amesema kuna Watoto walikuwa wanachunga ng’ombe wakamuona Fisi akimshambulia ng’ombe na kupiga kelele na Wananchi walipofika kuanza kumwinda Fisi huyo akawajeruhi.

Kamanda Mlayi amesema baada ya kupata taarifa za Fisi huyo walifika eneo la tukio na kukuta Wanakijiji wamekusanyika kwa ajili ya kumuua Fisi huyo ndipo walichukua uamuzi wa kuwatafuta Mamlaka ya Hifadhi ya Wanyamapori na Misitu Geita (TFS) kufika eneo hilo na wamefanikiwa kumuua Fisi huyo.

“Fisi amewajeruhi Watu 10 wakiwemo watano wa Familia moja na kwa ujumla wao wanaendelea vizuri kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Teule ya Rufaa ya Mkoa wa Geita na kama hali zao zitaimarika jioni wataruhusiwa kwenda nyumbani”

Chanzo: Millad Ayo
 
Kwa Geita uyo atakua mtu, wafuatilie Kama itatokea msiba wowote apo kijijini au Kijiji Cha jirani, fisi mtu wachawi sana uko
 
Huko Geita pa kishamba sana mpaka mafisi yanatawala yanavyotaka
 
Back
Top Bottom