Balantanda
JF-Expert Member
- Jul 13, 2008
- 12,484
- 4,825
Mudi...Na hili ni pigo baya sana kwa ccm na vibaraka wake. Wamesababisha wananchi wa kata husika wamekosa uwakilishi kwa siasa za hadaa na ghiriba.
Hao Madiwani ni watu hatari sana...Hawafai kuwemo kwenye chama aina ya CHADEMA ambacho kinaamini kwenye dhana ya Usaliti...Hao Madiwani tayari wameonesha udhaifu mkubwa sana na sio wa kuwaamini...Mlipaswa kuwaadhibu kwa hatua waliyoichukua...Na adhabu pekee waliyostahili ni kutowapokea ama kuwafukuza kabisa uanachama...Hawakustahili kupokelewa kama hivi (CCM style)....
Kwa kweli hawa ni wasaliti wa CHADEMA....Sikuona umuhimu wa kufanya hata mkutano wa kuwapokea 'kishujaa' kama hivi...Hawa ilitakiwa waachwe wasote mtaani ili wapate funzo....Kwa tukio hili sijaona tofauti ya CHADEMA na CCM...Hawa waliisaliti CHADEMA na kwenda kujiunga na CCM kwa mbwembwe zote kiasi cha kuitukana na kuikashifu CHADEMA...Leo wanaonekana ni mashujaa kisa tu wametoka CCM na kurudi walikotoka...
Nini kimeisibu CHADEMA mpaka mmeamua kuwapokea wasaliti hawa walioamua kuwatelekeza wananchi waliowachagua kwa tamaa??...