LOSEJMASAI
JF-Expert Member
- Feb 18, 2013
- 332
- 849
Kwa mtazamo wangu naona NI VIZURI sana sana kushuka kwa thamani ya pesa yetu katika SOKO la fedha la KIMATAIFA.
Uzuri ni kuwa watanzania Wafanya BIASHARA wanao EXPORT/ uza nje watapata FAIDA kubwa zaidi na hivyo kuweza KULIPA kodi/ushuru wa serikali bila shida na hivyo nchi kufanikiwa.
Kama una habari, Rais mteule wa Marekani AMEIONYA China kuwa ina MCHEZO wa MAKSUDI wa KUISHUSHA thamani ya pesa yake ili NCHI YAKE IFAIDIKE!
Na ni kweli China ni MANIPULATORS wa currency yao wakubwa sana.
Kwa hivyo mkuu hakuna kitakacho panda bei. Isipokuwa kwa vituVINAVYOAGIZWA toka nje ya nchi. Na Mtanzania wa kawaida saa ngapi ataenda kununua imported goods si wale tu WALIONAZO nao ni WACHACHE?
Itafika wakati itabaki katika kiwango hitajika.
Hasa kama watu wengi HAWAINUNUI DOLA kwa PUPA!
Labda kwa sasa kuna watu WANAONUNUA DOLA SANA na kwa PUPA.basi lazima tu thamani ishuke. Mpaka hapo BANKI kuu ITAKAPOGUTUKA!
Sina lengo la kusema shillinng imepanda ama imeshuka lakini natoa maelezo kidogo tu kuhusu concept ya exchange rate na impact yake kwenye uchumi na maendeleo
Shige, Kuna jambo moja unatakiwa ulielewe. Kinachotokea China huwezi ukakifananisha na Bongo. the exchange rate market ni complex lakini nitajaribu kulifanya atleast simple kama ifuatavyo.
Kuna kitu knaitwa Purchasing Power Parity (PPP), Kuna Nominal Exchange rate (NER) na Kuna Real Exchange Rate (RER).
NER = Kwenye pesa
RER = kwenye product
Kwenye uchumi lengo kubwa la importation ni exportation and the other way around (Yaani tunatoa bidhaa nje tulizo nazo kwa lengo la kubadirishani kupata bidhaa tusizonazo).
yaani tunawapa pamba ambayo sisi tunayo ili watupe nguo ambazo sisi hatuna (a very simple explanation of exchange rate, importation and exprotation) sasa badala ya kuziita pamba na nguo (PPP and RER) tunizipa majina ya pesa (NER) pamba iwe shilling na nguo iwe dollar.
NOTE: kwenye maelezo yanayokuja pamba itakuwa inarefer shilling na nguo itakuwa inarefer dollar
Sasa unahitaji pamba(shilling) 2100 ili kupata nguo(dollar) 1.
sasa ikitokea samahani ya nguo(dollar) ikaongezeka and ikawa zinahitajika pamba(shiling) nyingi basi kununua nguo(dollarr) 1 basi badala ya kuexport pamba 2100 kupata nguo 1 itabidi uexport pamba nyingi 2300 kupata nguo 1. kwenye uchumi hapa umekuwa umeincrease export yako.(Kuna notion kwamba export is a good thing for a country) Lakini hii increase inakuwa haikuongezi idadi ya pesa za kigeni nchi and inaleta development ndogo or not at all.
Kina chotokea china ni something different.
China ana over-capacity and overproduction sasa anakuwa na bidhaa nyingi sasa,, kwa kutumia concept ya hapo (tutumie huo huo mfano wa pamba na nguo).. China kadhalisha pamba nyingi kweli lakini hana pa kuipeleka lakini thamani ya nguo ipo pale pale.,, anachofanya anashusha thamani ya pamba yake (kutoka pamba 10 kununua nguo 1 anashusha thamani ya pamba ili atumie pamba 50 kununua nguo 1, ili kupunguza overproduction na kuendelea kuongeza ajira zake) kwa mtindo huo anakuwa anatumia pamba (pesa ya kichina) nyingi ambayo yeye hata hana shida nayo ili kupata nguo (dollar) ambayo anashida nayo sana.
Madhara kwa marekani yake ni nini,,
Mchina anakuwa na Export kubwa, kutokana na overproduction and overcapacity yake aliyo nayo and hence anaongeza ajira na kukuza uchumi.
Another thing mchina anakutwa anakuwa na nguo (dollar) nyingi sana kiasi kwamba Mmarekani hata akitakaa kucontrol idadi ya dollar kwenye circulation wanashindwa..
Economic crisis ya 2008, moja ya sababu ya wamerakani kushindwa kuidhuia mapema, wakati marekani anajitahidi kudhui circulation ya dollar kwenye mzunguko kwa kupandisha interest kwenye bond zake,, china akajitokeza akawa anatoa dollar kwa interest ndogo tofauti na Marekani.
Sasa Kwetu kinachotokea huwezi ukakifananisha na mchezo wanaucheza china. sasa increase yetu of export haituongezi dollar (foreign goods) maana shilling yetu ndo inayukuwa inatumika sasa.