Shillingi ya Tanzania hoi dhidi ya US $

Mipangomingi unaliza maswali mengi wakati unatakiwa kujibu maswali ya mleta mada kama unaweza kujibu
Swali Kwa nini US$1=2180Tsh sio blah market force blah central bank policy. Tuelimishe
Kuuliza ni kutaka kujua tu ndugu yangu, ingawa wakati mwingine hapa JF mtu kasoma kitabu chake cha Nyangwine, introduction to economics anataka kuja kufanya uchambuzi wa kiwango cha maprofesa wabobezi, ni shida kidogo. Mara nyingi uchumi hauna jawabu YES, au NO; kila policy ina kanuni zake ndipo itoe manufaa tarajiwa, wanasema "IT DEPENDS.."..
 
Asante Mkuu
 
1: Ifahamike kwamba kupanda au kushuka kwa thamani ya fedha yetu dhidi ya dola hakuna maana ya kuanguka kwa uchumi au kupanda kwa uchumi. Uchumi haupimwi kwa kaungalia kupanda au kushuka kwa thamani ya fedha, uchumi upimwa kwa kuangalia pato la taifa (GDP).

2: Sambamba na hilo hapo juu kupanda kwa thamani ya fedha yetu kunaweza kuathiri kukua kwa uchumi wetu kwa kusababisha bidhaa zetu zisiuzike (kumbuka kupanda kwa thamani ya fedha yetu manake ni kupanda kwa bei ya bidhaa zetu na hivyo kupata wanunuzi wachache assuming wanunuzi wako sensitive na bei zetu). Kinyume chake pia ni sahihi, shilingi ikishuka thamani inaweza kukuza uchumi maana unavuta wanunuzi wa bidhaa zetu kwenye soko la dunia ambalo liko reasonably competitive.

3: Ili uchumi ukuwe kwa nchi masikini kama Tz ambayo haiwezi ku-affect international market kupitia bidhaa zake lazima uzalishaji wa mazao ya export yaongezeke ili Tz iweze kuuza zaidi ili ku-offset impacts za currency appreaciation and depreciation.
MgonjwaUkimwi kama unavyojiita kwa kunielewesha:
1) Ni kwanini nchi zinakuwa concerned Sarafu zao zinaposhuka thamani?

2)Biashara kati ya nchi washirika za EAC zinahamasishwa, huoni kuwa Tanzania haitafaidika ikilinganishwa na Kenya
3) umesema sarafu za nchi maskini zinapoporomoka zinafaidika kwa kuuza zaidi nje. Tanzania inanunua kutoka nje mahitaji yake kuliko inavyouza; hilo likoje?
4) Kilimo (cha mkono) ni "uti wa mgongo wa uchumi" wetu. Tuko ktk jitida za ku-diversify uchumi. Wawekezaji wakubwa wanatoka nje. Waagiza mitambo na malighafi. Huoni kuwa nchi itazidi kakamuliwa?
 
MgonjwaUkimwi kama unavyojiita kwa kunielewesha:
1) Ni kwanini nchi zinakuwa concerned Sarafu zao zinaposhuka thamani?

Kushuka kwa thamani ya fedha, narudia, SIO KIPIMO cha kukua au kushuka kwa uchumi. Uchumi unapimwa kwa kuangalia pato la taifa (GPD) katika KIPINDI husika. Sasa moja ya vipande vinavyounda GDP ni mazao tunayouza nje (exports) dhidi ya mahitaji tunayoingiza kutoka nje (imports). Hivyo basi thamani ya safaru yetu inaposhuka manake mazao yetu yanakuwa cheaper kununuliwa na hivyo kipande cha exports-import kwenye mahesabu ya GDP kinakuwa. Vivyo hivyo sarafu ikipanda thamani manake wanunuzi ni wachache na exports-import inapungua. Concern za thamani ya safaru yetu kushuka inatokana na ukweli kwamba tunapunjwa bei ya exports zetu kwenye soko la dunia. Kwa maana kwamba kama tulipata dola 100 kwa kuuza gunia 2 za pamba sasa tutalazimika kuuza gunia 3 kupata hizo dola 100. Sasa kwasababu export ni kipande tu cha mahesabu ya GDP, hatuwezi kusema kushuka kwa sarafu ndio kushuka kwa uchumi.

2) Biashara kati ya nchi washirika za EAC zinahamasishwa, huoni kuwa Tanzania haitafaidika ikilinganishwa na Kenya
3) umesema sarafu za nchi maskini zinapoporomoka zinafaidika kwa kuuza zaidi nje. Tanzania inanunua kutoka nje mahitaji yake kuliko inavyouza; hilo likoje?
4) Kilimo (cha mkono) ni "uti wa mgongo wa uchumi" wetu. Tuko ktk jitida za ku-diversify uchumi. Wawekezaji wakubwa wanatoka nje. Waagiza mitambo na malighafi. Huoni kuwa nchi itazidi kakamuliwa?

Jibu la swali lako kipengele 2) juu ya biashara ndani ya EAC ni kwamba Tz haitanufaika kwa kuwa na sarafu ya thamani ya juu tu. Itanufaika kwa kuongeza uzalishaji na ubora wa bidhaa pamoja na mahitaji ya bidhaa katika soko. Nchi nyingi zimeingia kwenye economic integration zikiwa na utofauti mkubwa katika uthamani wa sarafu zao na bado kwa umoja wao kila nchi inafaidika. Uzalishaji, ubora, soko, miundombinu, mtaji nk ndivyo vinavyoinufaisha nchi inapoingia kwenye trade arrangements kama ilivyo EAC.

Jibu kwa swali lako kipengele 3, juu ya Tz ku import zaidi ya ku export ni kwamba hali hii ndio tatizo kubwa la nchi zote masikini za Africa na ndio chanzo za shirika la fedha duniani (IMF) kuzishauri nchi za Africa zishushe thamani ya sarafu zao (devaluation) kwenye miaka ya 80. Mzee Ruksa akawa wakwanza kuteremsha shilingi yetu akishirikiana na Prof Lipumba. Logic ni kwamba huwezi kuuza biashara yako pasipo kuangalia bei ya wenzako wanouza bidhaa kama yako. Sasa sarafu inapoteremka manake inavuta wanunuzi wa bidhaa zako, hivyo pamoja na kwamba unaingiza bidhaa nyingi muhimu kutoka nje, manake ukiuza sana unaweza kumudu zaidi kuingiza bidhaa kutoka nje.

Swali lako kipengele 4) juu ya kukamuliwa na wawekezaji wa nje jibu ni kwamba sisi tuna dhana potofu sana. Dhana ya kudhani faida za uchumi na uwekezaji zinaishia kwenye ela tu na sio vinginevyo. Tumekuwa watu wa ajabu, hatufikirii ajira, miundombinu, huduma za jamii ambazo zinaletwa na hao tunaowaita "wakamuaji", matokeo yake tunawawekea masharti magumu hadi wanakimbia na kutuacha na umasikini wetu.

Noeli njema.
 
Hongera wewe Shige2 umekuja na hoja yenye maana.....

sasa kuna baadhi wamekuja kisiasa wanasema natafuta kiki....ukiangalia comment yake ni pumba
Mkuu acha kumpa hongera huyo shinge, ingawa mimi si mchumi bado kuna vitu vinavyo nipa mashaka kwenye maelezo yake, anapo semea faida za kushuka kwa thamani ya shilingi dhidi ya dola, kule kwa wachina matokeo hayo yamepangwa na hapa kwetu haikupangwa iwe hivyo, ktk hali hiyo anadhani italeta effects sawa kwenye uchumi?. Alafu anasema watakao athirika ni wale wanao tegemea vitu vya ku import, huku akisahau kuwa tuna import hadi vipini.
 
Kushuka kwa thamani ya fedha, narudia, SIO KIPIMO cha kukua au kushuka kwa uchumi. Uchumi unapimwa kwa kuangalia pato la taifa (GPD) katika KIPINDI husika. Sasa moja ya vipande vinavyounda GDP ni mazao tunayouza nje (exports) dhidi ya mahitaji tunayoingiza kutoka nje (imports). Hivyo basi thamani ya safaru yetu inaposhuka manake mazao yetu yanakuwa cheaper kununuliwa na hivyo kipande cha exports-import kwenye mahesabu ya GDP kinakuwa. Vivyo hivyo sarafu ikipanda thamani manake wanunuzi ni wachache na exports-import inapungua. Concern za thamani ya safaru yetu kushuka inatokana na ukweli kwamba tunapunjwa bei ya exports zetu kwenye soko la dunia. Kwa maana kwamba kama tulipata dola 100 kwa kuuza gunia 2 za pamba sasa tutalazimika kuuza gunia 3 kupata hizo dola 100. Sasa kwasababu export ni kipande tu cha mahesabu ya GDP, hatuwezi kusema kushuka kwa sarafu ndio kushuka kwa uchumi.

Jibu la swali lako kipengele 2) juu ya biashara ndani ya EAC ni kwamba Tz haitanufaika kwa kuwa na sarafu ya thamani ya juu tu. Itanufaika kwa kuongeza uzalishaji na ubora wa bidhaa pamoja na mahitaji ya bidhaa katika soko. Nchi nyingi zimeingia kwenye economic integration zikiwa na utofauti mkubwa katika uthamani wa sarafu zao na bado kwa umoja wao kila nchi inafaidika. Uzalishaji, ubora, soko, miundombinu, mtaji nk ndivyo vinavyoinufaisha nchi inapoingia kwenye trade arrangements kama ilivyo EAC.

Jibu kwa swali lako kipengele 3, juu ya Tz ku import zaidi ya ku export ni kwamba hali hii ndio tatizo kubwa la nchi zote masikini za Africa na ndio chanzo za shirika la fedha duniani (IMF) kuzishauri nchi za Africa zishushe thamani ya sarafu zao (devaluation) kwenye miaka ya 80. Mzee Ruksa akawa wakwanza kuteremsha shilingi yetu akishirikiana na Prof Lipumba. Logic ni kwamba huwezi kuuza biashara yako pasipo kuangalia bei ya wenzako wanouza bidhaa kama yako. Sasa sarafu inapoteremka manake inavuta wanunuzi wa bidhaa zako, hivyo pamoja na kwamba unaingiza bidhaa nyingi muhimu kutoka nje, manake ukiuza sana unaweza kumudu zaidi kuingiza bidhaa kutoka nje.

Swali lako kipengele 4) juu ya kukamuliwa na wawekezaji wa nje jibu ni kwamba sisi tuna dhana potofu sana. Dhana ya kudhani faida za uchumi na uwekezaji zinaishia kwenye ela tu na sio vinginevyo. Tumekuwa watu wa ajabu, hatufikirii ajira, miundombinu, huduma za jamii ambazo zinaletwa na hao tunaowaita "wakamuaji", matokeo yake tunawawekea masharti magumu hadi wanakimbia na kutuacha na umasikini wetu.

Noeli njema.
Asante MgonjwaUkimwili kwa elimu uliyonipa.

Nikikukariri ni kuwa kipimo cha ukuaji wa uchumi ni GDP: exports -- imports ukimaanisha tofauti kati ya exports na imports. Nchi inatakiwa kuuza nje zaidi kuliko kununua kutoka nje ili kupata pesa za kigeni zaidi ya inavyotumia kununua bidhaa kutoka nje.

Aidha, kushuka kwa thamani ya sarafu kunapelekea kuongezeka kwa mauzo nje japo kunamaanisha kupunjika. Pamoja na kupunjika, nchi hufaidika kwa kuboreka kwa miundo mbinu, huduma, halikadhalika maarifa, ujuzi, nk. Kutokana na uwezekezaji.
 
Upo sahihi kabisa, isipokuwa sijasema GDP = export minus import. Sijasema hivyo na nisieleweke hivyo. Kwa urahisi wake GDP = Private investment + government expenditure + consumption + (export-import). Sasa utaona export-import ni sehemu tu ya GDP.
 
Ni Ukweli kuwa nchi imeshindwa kuzalisha bidhaa bora za export

A - Mazao ya Biashara kama Kahawa, Katani

B- Viwanda kuzalisha bidhaa bora na kuuza nje

Note: Serikali inapiga wimbo tu Viwanda viwanda, hawajatafuta chanzo cha viwanda kufa

---Hawajabadilisha sera na kuvutia ujenzi wa viwanda (ondoa utitiri wa kodi) Example Dangote crisis

Tourism: Tourism ilikuwa njia rahisi nchi kupata forex nyingi sana

Matokeo yake serikali imeshindwa kuchochea ukuaji wa utalii

A - Matangazo mengi (adverts)

B- Landing fee na Jet fuel kupunguza bei ili ndege nyingi zije direct Tanzania na bei za ticket zitapungua
Kununua ndege pekee haitoshi....Bado ATCL italipa landing fee na bado bei ya mafuta ni juu, ATCL hawataweza kutoa cheap tickets

C - VAT za ghafla (Destination inakuwa ghali sana) na wakati bado miundo mbinu ni duni..Why?

D - Kuboresha sehemu na makazi ya watalii matajiri--- bado
 
Weka numbers, siyo maneno tu.
 
Back
Top Bottom