Mimi dada FF huwa nakuheshim.sana Ustaadhat lakini leo dada'ngu umepotoka sana. Thaman ya fedha ikiwa vizuri hasa kwenye soko la ushindani wa matumiz ya dollar ni muhimu sana bila kujali raia mmoja mmoja ananufaikaje. Kuna mifano hutolewa humu kuwa Yen au Yuan ziko chini sana ya dollar karibia sawa na Rand ya SA, au Kshilling! Je tutasema Kenya wana uchumi bora kuliko Japan(Yen) au China( Yuan)? Jibu ni hapana. Lakin wao Wachina na Wajapan wanasababu zao kushusha thaman dhid ya dollar. Mojawapo ni kuwa wao bidhaa nyingi wanatengeneza na kuuza nje, hawaagizi. Kwa nchi zetu hizi ambazo bidhaa za kuagiza nje ni nyingi kuliko tunazouza/safirisha nje, ni muhimu tena ni LAZIMA hela yako ijitahidi kufukuzana na dollar , na ukiweza iwe tarakim 3 ni bora zaidi