Shilingi yazidi kushuka, 1 USD = 2223Tsh

Nina tudola twangu kwenye kibubu, naomba ifike hata 3500 tu
 
Sasa kupata mkopo benk ni issue.
Benk zimejawa uogaa, wafanyabiashara nao waoga kukopaa.
Nani wa kumfunga Paka kengelee?
 
Mbona wachochezi nyinyi? Shilingi yetu ndiyo imepanda na pia njaa hakuna wala ukame maana mvua zilinyesha mwaka mzima.

Mwafaaa.....
 
hii dollar ipigwe marufuku tanzania.
yaani uchumi wetu unakua halafu inatuzingua.
 
Ngoja tuone speed ya kuporomoka. Niliangalia less than a week ago conversion rate ilikuwa ni U$ 1 = T shs 2,183.
Hali ya uchumi ni mbaya kwa kweli na huu ukame ukiendelea basi gharama za maisha zitakuwa hazishikiki kwa mfumuko wa bei.

Uchumi unaporomoka mdogo mdogo
 
Kwa mbali i can see the great depression in Tanzania.. GOD help us all

Watu bwana......eti depression.......waTanzania tuna depression kila Siku. Maisha yenyewe ni depression tosha. Uchumi wetu bado. Tuache kuongelea sijui inflation, sijui recession, na lugha pendwa za kwenye vitabu na majarida ya kiingereza. Huko hatujafika. Tufikirie namna ya kuwa na vyoo mashuleni, vitanda mahospitalini nk.
 
Alafu wewe Kijana tunakuonya acha kupingana na serikali ya chama tawala,rejea ripoti ya waziri wetu mtaalamu aliyebobea,alisema shilingi imeimarika.Kwanza unapinga mini wakati huna PhD!.Tutafuatilia IP address yako,eboo!
 
Mhh.... Mbona habari mbaya mapema hivi....naona BOT wanaripoti Ex ya 2227..
Loss of Forex kutaharibu sana biashara zetu ..
 
Ha aha ....
We jamaa wewe, kwa hiyo kipindi cha JK ambapo Dollar ilikuwa inashuka kwa kasi sana ilisababishwa na hayo ?
 
Ebu tuambie bajeti ambazo upinzani walishiriki Dollar ilishuka kwa kiasi gani ?
 
Alafu wewe Kijana tunakuonya acha kupingana na serikali ya chama tawala,rejea ripoti ya waziri wetu mtaalamu aliyebobea,alisema shilingi imeimarika.Kwanza unapinga mini wakati huna PhD!.Tutafuatilia IP address yako,eboo!
PhD za bongo nyingi ni feki ndiyo maana wanaojiita wasomi Tanzania wengi wamejaa vioja.
 
Nimeamini ID yako ni sahihi kwako.
 
Nakushangaa sana nchi tajiri kama Tanzania hatuwezi tegemea wafadhili baada ya muda tutaanza kuwa donar country we subiri tu six month to come wamarekani na wachina watakuja kukopa kwetu na kuomba msaada wa chakula.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…