Rawasen
Senior Member
- Aug 11, 2014
- 182
- 74
Hivi hii sheria mpya haitawahusu?
Inawahusu Mkuu
Hivi hii sheria mpya haitawahusu?
mbona unaandika kwa kufichaficha maneno, unamwogopa nani?
Hawa GPL wanafanya makosa sana, nashangaa na serikali nayo iko kimya! Haki ya faragha inapotezwa kabisa!
namalizia process nipate cha moto a.k.a mguu wa kuku wakinikuta faragha tu masikio yao halali yangu
yaani inakua ny.ege ni zangu umbea ni wao roho zao ni halali yangu
Naam hiyo ndio dawa yao wapumbavu wale.kwanin wasijikite kwenye kufuatilia mafisadi,?
Faragha na wake za watu.. ??? Au waume za watu??. Hivi kama wewe ukiona wamekukamatia mgoni wako utaawachukia kweli?
Zunguka duniani kote hakuna sheria inayoruhusu faragha ya mtu kuingiliwa labda kuwa na special order from the court!!
Je hawa GPL wametumwa kufanya hayo wanayofanya, hapo tujiulize.
Faragha na wake za watu.. ??? Au waume za watu??. Hivi kama wewe ukiona wamekukamatia mgoni wako utaawachukia kweli?
Habari wanaJF
Kuna hii kampuni inaitwa Global Publishers ikiwa chini ya Bw. Erick Shingongo, kiukweli sidhani kama alisajili kampuni hii kwa ajili ya kuingilia faragha za watu lakini ndiyo kazi ambayo Global Publishers wanayoifanya kwa sasa.
Hapo awali Global Publishers walikuwa wakijikita zaidi katika uandishi wa majarida na vitabu lakini naona hiyo kazi wameona haiwalipi na hivi sasa wanazunguka kwenye nyumba za kulala wageni walipoweka kambi zao ili kudakua faragha za watu wanaofika katika nyumba hizo za kulala wageni wakiwa katika starehe zao.
Sitetei uzinifu lakini faragha ya mtu iheshimiwe, na siyo kazi ya Global Publishers kuwapiga chabo na kupiga picha bila idhini ya wahusika, huu ni udhalilishaji unaofanywa ma Global Publishers.
Wizara ya habari na utamaduni wakishirikiana na Brela waimulike tena hii kampuni huenda imesahau majukumu yake au imeshindwa kujiendesha kihalali.
Kuingiza hela kupitia udhalilishwaji wa watu fulani haikubaliki.