Shibuda: Wanaopinga posho ni madomokaya na wahuni

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Katika hali ya kushangaza mbunge wa maswa John Shibuda-chadema amewalaani vikali watu wote wanaopinga nyongeza ya posho ya wabunge na kuwafananisha wote hao wanaopinga na madomokaya na wahuni.

Shibuda ameendelea kusema kwamba nyongeza hiyo ni kidogo sana na watanzania waendelee kuiomba serikali iwajali wabunge wake.Shibuda amesema wanaopinga ni wanafiki wakubwa,wasaliti na waropokaji.

Source: Shibuda aliongea na waandishi jana na kunukuliwa na baadhi ya magazeti leo kama Tanzania daima na majira
 
Kati ya watu CDM imechemsha ndo huyu,hivi hata haon huruma ya wananchi wa jimbo lake walivyo na maisha magumu?Shibuda akapimwe akili na apelekwe Mirembe
 
Dah, lazima nisema kuwa hapa cdm tuliokota garasha hatufai kabisa huyu kama ni kweli kayasema haya!

mh shibuda kweli ni zigo. Taabu anaona maisha ni magumu na yeye kawekeza kwenye posho tu. Mbona anaifedhehesha familia yake. Kila siku baba anaongea offpoint tu
 
Yuda alikuwa mwanafunzi wa Yesu kati ya wale thenashara
 
Shibuda ni Taahira so sishangai.
I second this.
Mlishasikia akichangia kitu gani cha maana bungeni?
Yule lazima utetezi wa haki za binadamu unaopigiwa kifua na Cameroon, Clinton na Obama utakuwa unamhusu sana yule.
 
Wakati ule anawatukana Wabubge wenzake eti bado ni vijana Bungeni hawajui mambo ya kibunge, ambapo pia alikataa kutoka nje ya Bunge, CDM walimsamehe. Lakini katika hili, nafikiri CDM wamfukuze tu. Tuone kama hatarudi tena CCM. Ni afadhali kumkosa Shibuda kuliko kuwa naye. Hana msaada kwetu, siyo mzalendo, hana utu, hathamini wananchi wake, anafanyia tumbo lake tu na familia yake.
 
Nadhani muda umefika sasa kwa vyombo vya habari kuacha kutuchosha sisi wananchi kusoma habari za huyu dalali wa CCM uchwara. Shibuda anajulikana ni mchumia tumbo na CCM wanapenda watu wa namna hiyo maana wakimpa hela atanya chochote wanachotaka ili mradi tu anapata pesa.

CHADEMA wameshapata walichotaka - kura nyingi kwenye jimbo la huyu bwana ambazo zimesaidia kuinua ruzuku ya chama (ruzuku inategemea % ya presidential vote). Kwa sasa hivi Shibuda ni karai, zege limeisha hana kazi tena. Aongee, akae kimya it does not matter.Ila jambo moja ni dhahiri, vizazi vijavyo vitashangazwa sana na historia ya Shibuda. Sio nzuri and I hope familia yake itamsaidia kutambua hili!
 
I wanna kill right now!??!!!? Life tight kuna mtumishi analipwa 146,000 Kwa mwezi afu ye posho ya laki mbili kwa siku haitoshi na huku bidhaa na huduma tunapata kwa bei moja. Yaani niko tayari kuwa recruited kwa wapambanaji watakaotaka kuingia msituni sanduku la kura halitatuokoa ikiwa wabunge wenyewe ndo hawa na vyama venyewe ndo hivyo Damn it
 
Huyu hatufai kabisa na alikuja CDM kwa ajili ya manufaa yake lakn sio kwa wananchi,lakn hili liwe fundisho kwa CDM sio kila mwanachama ajae huku ana upendo wa dhati na CDM
 
mi napenda mtu mwny siasa za kweli kama shibuda anasema analoamini si hawa wanaongata na kupuliza.japo siungi mkono wabunge kuongezewa posha
 
Nadhani imefika mahali sasa Mbowe,Dr Slaa na Zitto waonyeshe mamlaka yao ya kiungozi dhidi ya Shibuda.
 
Hakuna cha ukweli anaosema Shibuda, domokaya no 1, ndo yeye. Ni mnafiki kubwa sana huyo hana lolote. Kama sio mnafiki kwanini amejificha kwenye magwanda wakati yeye ni gamba namba one? Apotee zake mnafiki huyo.
 
tuliwaambia suala la posho halina itikadi sasa huyu ni mbunge wa chadema analilia posho. chadema fukuza huyu kama ccm walivyothubutu kumfukuza Rostam Aziz na kuingia kwenye uchaguzi
 
Mhe. Shibuda, kama unasoma humu, nakushauri uwe na shukrani katika madogo ili uwe na shukrani katika makubwa!.

Kuendekeza njaa kupindukia kutakulisha visivyo liwa!.

Kwa msiomfahamu Mhe. Shibuda, huyu si wa kulaumiwa ni wa kuhurumiwa tuu kwa maana hajui asemalo wala atendalo!.
 
shibuda ni mamluki afukuzwe mbona ccm walithubutu kumwondoa akakimbilia chadema kwa nini chadema wanashindwa kuchukua maamuzi magumu.
 
Back
Top Bottom