Shibuda: Wanaopinga posho ni madomokaya na wahuni

Shibuda achafua hewa CHADEMA
• Atoa shutuma nzito kwa viongozi wake

na Bakari Kimwanga (tanzania Daima)

amka2.gif
MBUNGE wa Maswa Magharibi (CHADEMA), amechafua hali ya hewa ndani ya chama hicho baada ya kuwaita viongozi wake na watu wa kada mbalimbali wanaopinga ongezeko la posho za wabunge kuwa ni domokaya wanaotafuta umaarufu wa kisiasa mbele ya jamii.

Shibuda ambaye maelezo yake yaliwashangaza baadhi ya waandishi wa habari aliokutana nao jana jijini Dar es Salaam, alidai kuwa viongozi wa siasa wanaopinga ongezeko hilo la posho ni makuwadi wa watu wa nje ambao wameanza na suala hilo lakini si ajabu kesho wataunga mkono ushoga.
Alisema tangu lilipotangazwa jambo hilo, kumekuwa na msukumo kwa baadhi ya wanaharakati, viongozi wa vyama vvya siasa pamoja na baadhi ya wabunge kutaka kuligeuza jambo hilo kuwa la kisiasa, ilhali ilani za vyama hazizungumzii jambo lolote kuhusu posho.

Mbunge huyo alisema hivi sasa kuna kundi la watu linafanya kampeni inayoweza kuchochea chuki kwa wananchi dhidi ya serikali na wawakilishi wao bungeni, huku wakitumia shida za wananchi kwa maslahi yao.

Shibuda alisema baadhi ya wanasiasa wamekuwa mabingwa wa kutuhumu upande mwingine, wakati wao wenyewe hawajitazami usafi wao mbele ya jamii.Katika kauli iliyoonekana kumwelekea zaidi Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Freeman Mbowe, Shibuda aliongeza kuwa wapo wanasiasa waliojidai kukataa kutembelea magari waliyopewa na serikali, hata kufikia hatua ya kuyarudisha, lakini wanaonekana wakitamba na magari ya kifahari.
 
Nimemsoma vizuri SHIBUDA sasa hivi. Kujiunga Chadema licha ya ubunge alitarajia kupata nafasi nyingine katika uongozi wa chama kitaifa. Kama mtakumbuka ndoto zake tangu bunge lililotangulia alitaka kugombea urais kumtelemsha Kikwete. Alipogonga mwamba na kuishia kutiwa kapuni huko Maswa kwenye ubunge, tegemeo lake lilikuwa Chadema angeweza kuibuka na kuwa pekee mwenye kauli na hivyo kuwa na tegemeo la kupata nafasi ya uongozi kitaifa na kisha kuteuliwa kugombea urais. Kwa sasa hali inavyoonyesha ndoto hizo zimeyeyuka na kinachoendelea ni kutapatapa kwa mfa maji.
 
tuliwaambia suala la posho halina itikadi sasa huyu ni mbunge wa chadema analilia posho. chadema fukuza huyu kama ccm walivyothubutu kumfukuza Rostam Aziz na kuingia kwenye uchaguzi
wewe ni muongo wa kutupwa, CCM hawakumfukuza Rostam Azizi, alijiuzuru kwa hiari yake. Hivyo na Shibuda atajiondokea kwa hiyari yake.
 
Huenda kuna mtu ameshamuuma sikio huyu Mh. Shibuda, juu ya kitu kilichopo kwenye report ya kamati inayoshughulikia mambo yake ndio maana ameamua kunyea kambi kabisa. Tuvute subira washikadau
 
ni mtazamo tu,msihamaki,chama cha demokrasia na....,demokrasia ni pamoja na uhuru wa mawazo.kama mmoja alivyoamua kukaa rumande
 
Mnamwonea tu Shibuda, mh.Selasini wa Rombo naye alisema kabisaaaaaa bungeni kuwa posho ni ndogo sana na wanaopinga wana ajenda zao za siri pia kina Regia na wengine wengi wa CDM posho wanazitaka sana ila wanasemea chini chini. Shibuda ni muwazi.
Kwahiyo na wewe unawaunga mkono?
 
Haya sasa ni matusi ya nguoni yaani iyo iliyoongeazwa kwake pia anaiona ni ndogo!
Namshauri atupe mchanganuo wa udogo wa iyo posho kwa kuweka hadharani matumizi ya kila siku then k wa mwezi alafu afanye comparative analysis na sample ya watu anaowawakilisha maisha wanayoishi
 
Shibuda is real.hakuna unafiki pale anasema kile anachomini.he is a great guy.
Ila hilo suala la posho asee hata mi napingana nalo saana tu.imefika wakati sasa hawa wanasiasa tuwaweke mahali wanastahili IN HELL
 
Dah...nimesahau kitu..shibuda ni tunu ya taifa hakuna mwingine kama yeye hio tunu chadema msiitupe.
Huh...!!
 
si kila mtu ana access na unachoona, ni vyema ukapanga hoja na kuleta habari kamili kama wanavyofanya wakubwa zako akina superman, BAK, Ruta nk.

Unakurupuka kama umeumwa na siafu na habari nusu.......... cant you even give a little background umeona nini kilichotokea ili wengine nao waelewe unasema nini??

C'moon hivi MTM ni kipi ambacho hujaelewa kiasi kwamba unadai eti mtoa habari analeta habari nusu-nusu,! Hivi kwan ni ww peke yako ndo unaeweza kusoma katikati ya mistari?
Mbona kuna comments kibao ambazo zinatoa picha kuwa watu wameelewa thread.
Mijitu kama MTM mnakera sana na haijalishi hata kama ni JF senior expert member, unaweza ongea upupu tu.
Kwa kheri!
 
Huyu mzee ni tatizo, katika hoja yake anamsema mwenyekiti wake kakataa shangingi la serikali lakini anapanda mashangingi yake binafsi.

Mzee Shibuda usizeeke vibaya - acha wivu na wewe kanunue shangingi lako - ulichagua siasa kuwatumikia watu na si POSHO, kama unategemea kuendesha maisha yako kwa kutumia POSHO za mjengoni mzee utakufa maskini, anza ujasiliamali kama mimi.
 
Nimemsoma vizuri SHIBUDA sasa hivi. Kujiunga Chadema licha ya ubunge alitarajia kupata nafasi nyingine katika uongozi wa chama kitaifa. Kama mtakumbuka ndoto zake tangu bunge lililotangulia alitaka kugombea urais kumtelemsha Kikwete. Alipogonga mwamba na kuishia kutiwa kapuni huko Maswa kwenye ubunge, tegemeo lake lilikuwa Chadema angeweza kuibuka na kuwa pekee mwenye kauli na hivyo kuwa na tegemeo la kupata nafasi ya uongozi kitaifa na kisha kuteuliwa kugombea urais. Kwa sasa hali inavyoonyesha ndoto hizo zimeyeyuka na kinachoendelea ni kutapatapa kwa mfa maji.
yes, nawashauri CDM just to ignore this person na wasonge mbele ya mambo yako, kinachonipa faraja ni kwamba jamaa hana cheo chochote na hatakaa apewe. The guy is confused.

Ukifungua milango kuruhusu ukuaji wa chama basi tegemea popo, panya na mijusi kuingia pia - cha msingi ni kutumia mbinu za medani kuwaondoa mmoja baada ya mwingine.

Kwa hili CDM sina wasiwasi nalo kabisa, wanakua ku-deal na hivi vitu.
 
Katika hali ya kushangaza mbunge wa maswa John Shibuda-chadema amewalaani vikali watu wote wanaopinga nyongeza ya posho ya wabunge na kuwafananisha wote hao wanaopinga na madomokaya na wahuni.

Shibuda ameendelea kusema kwamba nyongeza hiyo ni kidogo sana na watanzania waendelee kuiomba serikali iwajali wabunge wake.Shibuda amesema wanaopinga ni wanafiki wakubwa,wasaliti na waropokaji.

Source: Shibuda aliongea na waandishi jana na kunukuliwa na baadhi ya magazeti leo kama Tanzania daima na majira

huyo mwacheni, anahitaji kuhurumiwa. unapoona mtu mzima na mvi kichwani, akikaa na kufikiri nini aongee ndo anatoa maneno kama hayo ujue either anakamilisha mwisho au yu ktk mwanzo wa mwisho.

nawahurumia walio mchagua. ni bora kuwa na mwakilishi anayekaa kimyaaaaaaaa, kuliko anayeongea vizuri kama mheshimiwa shibuda
 
Katika hali ya kushangaza mbunge wa maswa John Shibuda-chadema amewalaani vikali watu wote wanaopinga nyongeza ya posho ya wabunge na kuwafananisha wote hao wanaopinga na madomokaya na wahuni.

Shibuda ameendelea kusema kwamba nyongeza hiyo ni kidogo sana na watanzania waendelee kuiomba serikali iwajali wabunge wake.Shibuda amesema wanaopinga ni wanafiki wakubwa,wasaliti na waropokaji.

Source: Shibuda aliongea na waandishi jana na kunukuliwa na baadhi ya magazeti leo kama Tanzania daima na majira

Du huyu hajatumwa na Magamba kuleta mtafakaruko ndani ya cdm, yafaa cdm mmwe makini na huyu mtu maana atakuja kuwaaribia kama madiwani waarusha
 
Kati ya watu CDM imechemsha ndo huyu,hivi hata haon huruma ya wananchi wa jimbo lake walivyo na maisha magumu?Shibuda akapimwe akili na apelekwe Mirembe

Huyu akili timamu anazo ila anachofanya ndicho alichotumwa na makamba na ndicho anachotekeleza
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom