Shibuda sasa amvaa Dk Slaa, adai kuwatumia BAVICHA

Shibuda sasa amvaa Dk Slaa, adai kuwatumia BAVICHA

Huyo anamatatizo fulani, nafikiri ni wa kumuangalia kwa makini. inawezakana ni matatizo ya kisaikolojia. Sasa atashambulia kila mtu. Kaeni kimya mumuinjoy.
 
Huyu Mzee anazidi kuchanganyikiwa, alidhani kauli na matendo yake ya kujikomba sisiem vingeleta mtafaruku kakuta chama makini kinaendelea na shuguli za kujijenga na kumuacha amebakia kwenye dust bin hivyo anatafuta namna ya kukuza mgogoro. Watu makini wamemwambia hawashuguliki na watu.

Alipokuwa CCM alitangaza nia mapema zaidi watu wakamuwekea bifu wakampora na ubunge wake, aishukuru CDM kwa kumuokoa alipobambikiziwa kesi ya mauaji akasaidiwa vinginevyo angekuwa ananyea debe.

Kitendo cha Shibuda kumrukia Dr ni sawa na shoga akiwa kwenye harakati za kutafuta mtu wa kumshikisha ukuta, huwa anaparamia kila kidume kutafuta attention maana muwasho huwa hauvumiliki!
 
Wana Chadema tuachane na hilo li Shibuda kwa maana hata anachogombea, anacholilia, akijulikani kama shida ni kuwa Rais na achukuwe fomu ajaze aombe huo urais cha kushanghaza siji unapatikana kwao tu pale Maswa au Tanzania nzima wenzake wanaimarisha chama wanawaanda wapiga kura wao 2015 lenyewe linalopoka lipoka ovyo tuachane nalo tu sisi tusonge mbele Chadema kaikuta.Mujwahuzia
 
Dr.Slaa amefanya vizuri.Tangu mwanzo nilisema Dawa Shibuda ni kumpuuza...That's it!

This is the safe, standard,prepackaged rhetorical frippery. If the hypocrisy or intellectual laziness that actuates these thoughtless,simplistic sound bites didn ’t have far-reaching consequences for our continued existence as a political party
and, in fact, our very survival as a people, one would simply yawn in silence and ignore them.

Huwezi kucheza mziki alioulipia mtu na kumuweka DJ wake.Siasa za kujadili watu badala ya sera ni siasa mufilisi.Chadema iko juu ya Hili. Watu wanapenda kujadiliwa na kututoa katika ajenda ya msingi.
 
Kazi ya Katibu Mkuu ni kukemea Raisi Kikwete alivyomaliza billioni 6.5 US$ alizoacha Raisi Mkapa kwenye reserve yetu kwa safari za kuenda kumbebea ulaya
Deni la Taifa kufikia trilioni 16 katika kipindi cha miaka mitano tuu
trillioni 50 kutumika kwa magari ya serikali
bilioni 300 kuliwa na watendaji wa serikali
asilimia 90 ya watoto wa sekondari kufeli
asilimia 75 wanawake kuzalia kwa wanganga wa kienyeji
asilimia 80 ya fedha za mradi wa maji kuliwa na mawaziri
pato la taifa kushuka chini

hao watu mkuu unawapotezea kama Dr ananvompotezea shibuda,
huyu yupo kiachama zaidi mkuu si kitaifa asikuumize kichwa!
 
Sioni haja ya kumfukuza kwasasa kwani dawa yake ipo 2015. Haihitaji uwe na PHD usijuwe Shibuda katumwa na CCM kuivuruga CDM. Tutulie tujenge chama kwa manufaa ya Watanzania kwani Shibuda si Chadema bali ni mbunge kupitia tiketi ya Chadema isiwape taaaaaaaaaaaaaabu sana wana wa Magwanda.
 
Mwenye cv ya Shibudam tafadhali aiweke hapa ili tumwelewe zaidi ya hapa tulipofikia.
 
Unachemka tena!

Shibuda, Mbunge wa CHADEMA, hawezi kuingia kwenye National Executive Committee ya Chama Cha Mapinduzi. Period!

Nyinyi ndio waandishi wa kibongo ninaowaambia kila siku hapa ni wabovu!


Watanzania bwana hivi kwanini hamuelewi?
Shibuda alikwenda nec ya ccm coz ni mjumbe anayewakilisha Aprm bungeni na wako wawili na Martha umbulah wa ccm,na alichaguliwa na wabunge wote.Povu jingi wakati hamuelewi hata Aprm ni nini.
 


IBARA ya 18(i) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inampa Mtanzania yeyote fursa ya kutoa maoni yake kuhusu jambo lolote, kupitia chombo chochote, na vilevile kuwa na haki ya kutoa maoni yake na haki ya kutoingiliwa katika mawasiliano yake, ila tu asivunje sheria za nchi. Basi.

Vyama vyote vya siasa hapa Tanzania vimebebwa na katiba zake. Hakuna chama kilichosajiliwa Tanzania bila kuwa na katiba inayoeleweka. Ni juu basi ya kila Mtanzania, hususan anayejiunga na chama chochote cha siasa, kuisoma, kuielewa, kuiamini, kuiheshimu na kuilinda katiba ya chama alichoamua kujiunga, huku akifuata kanuni zake na kuwa mwanachama mwenye nidhamu.
Naiandika makala hii kwa tahadhari kubwa nikiwa na lengo moja tu: ndugu yangu John Shibuda (Mbunge wa Maswa Mashariki) anielewe kwamba sote tunahitaji mabadiliko Tanzania na pia tuko katika mpambano mkali wa kubomoa dari ili tujenge paa. Hakuna zaidi.

Hivi karibuni Shibuda amekaririwa na vyombo vya habari akitangaza ‘azma’ yake ya kugombea urais Tanzania (mbele ya NEC ya CCM huko Dodoma) katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na akaenda mbali zaidi kumuomba Rais Jakaya Kikwete (ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa), awe meneja kampeni wake.

CHADEMA haina utaratibu mbovu wala tambo za hovyo sampuli hii! Niseme tu mapema, kwa tafsiri ya namna yoyote ile, huu ni upuuzi na utovu wa nidhamu katika chama na bila shaka uko na ujumbe mzito nyuma yake. Kama una macho ona!

Waandishi na wachambuzi wengi kwa nyakati tofauti wamelielezea tukio hili kwa namna tofauti. Kuna waliokubaliana na Shibuda na uhuru wake wa kusema kila analofikiri linafaa, kuna waliomponda Shibuda kwa kuanzisha hoja ambayo sio kipaumbele cha CHADEMA, na kuna ambao wako katikati hawajui kama Shibuda kateleza aua lah! Nitajadili mtindo huu wa Shibuda kuibuka na hoja ‘gongana’ kwa mtindo ninaouona na mimi unafaa.

John Shibuda alijiunga CHADEMA akitokea CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 baada ya kushindwa kupenya katika kura za maoni kupata wagombea ubunge wa CCM, na mpaka sasa haieleweki vizuri sababu iliyomsukuma kugombea ubunge Maswa Mashariki kupitia CHADEMA chama ambacho na yeye aliamini ni cha upinzani, pengine kwa harakaharaka naweza kutoa tafsiri ya spidi ya Shibuda kuibukia CHADEMA ilikuwa ni ‘kulikomboa jimbo lake’.

Nasema hili nikiamini ni vigumu kabisa kusema moja kwa moja kwamba ni uzalendo ndiyo uliomsukuma kujiunga na CHADEMA kwa maneno matamu matamu kwamba ni chama makini chenye kutoa fursa sawa kwa kila mwanachama mwenye vigezo.
Haieleweki kama Shibuda alipata muda wa kuvichambua vyama vyote vya upinzani na kuamini kutoka moyoni mwake kwamba CHADEMA ndilo chaguo sahihi kabisa, laini pia hadi sasa haieleweki kama Shibuda alisoma katiba ya CHADEMA na kuielewa sawa sawa.

Na mwisho sina hakika kama Shibuda alijiunga na CHADEMA kutokana na umaarufu wa chama chenyewe au jina tu lilimvutia. Ni siri yake.

Kauli ya kuutaka urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CHADEMA kwa kukampeniwa na Rais Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa CCM aliyoitoa John Shibuda ilipokelewa kwa namna tofauti na kila Mtanzania mwenye kuifikirisha akili yake vizuri. Wengi walipigwa butwaa na kushindwa kuamini walichokisikia kutoka kwa mwanasiasa huyu nguli na kada mzuri wa CCM.

Kuna walioilaani na kuikemea hadharani na kuna waliokubaliana naye kwamba ametimiza haki yake kwa mujibu wa Katiba ya nchi. Angefanya nini sasa?

Kauli kama hii ya kuutaka urais amewahi pia kuitoa mwaka 2010 alipojikuta peke yake akipingana na taratibu na kanuni zao (CCM) huku akiwa mwanachama wake. Shibuda alitangaza kuchukua fomu ya kugombea kuteuliwa ili agombee urais mwaka 2010 sambamba na Rais Jakaya Kikwete aliyekuwa akikitetea kiti chake. Maajabu ya Mussa. Nia yake na ndoto zake za kuutaka urais wa Tanzania wakati huo akiwa CCM, huku akijua kwamba kila mtu alikuwa akimshangaa, bila shaka zilifuatiwa na rungu toka NEC na hatimaye Shibuda akajikuta kaachwa kijiweni, wote wakimshangaa, na hivyo kuamua kutimua mbio kukimbilia CHADEMA ambako imedhihirika amepwaya na haendani na nidhamu na imani ya chama.

Siwezi kuilaumu CHADEMA kwa kumkaribisha na kumpokea Shibuda akitokea CCM kwa kuwa kama nilivyosema hapo juu haieleweki Shibuda alifuata nini CHADEMA, hakusema.

Na kwa kuwa ni vugumu mno mtu kuyatambua mawazo ya mwingine, CHADEMA iliishia kukubaliana tu na ujio wa Shibuda na kumuona kama mwanachama mwingine yeyote. Kumbe Shibuda ana yake, na sasa yameanza kufumka. Njia ya maji haipandwi mbigili.

Kwa kauli za rejareja anazopenda kutoa mbunge Shibuda hasa zenye kila tafsiri ya kukomoana ni dhahiri kwamba ama Shibuda ameichoka CHADEMA au ana ajenda yake nyuma ya pazia: pandikizi.

Mnyukano wa mawazo sasa unainyemelea CHADEMA na sasa upo ushahidi baadhi ya viongozi wake wameamua kuanza malumbano kupitia vyombo vya habari kuhusu uhalali wa Shibuda na hekaya yake ya urais 2015 kwa msaada wa CCM.

Je, hii itupe maana kwamba viongozi wetu huko CHADEMA wameshindwa kurekebishana kwa kupitia vikao na njia nyingine sahihi kwa mujibu wa katiba na kanuni za chama? Busara imeachwa.

Mgongano wa mawazo unaofukuta baina ya Mwenyekiti wa Baraza la Vijana CHADEMA, John Heche, dhidi ya Makamu wake Joliana Shonza kuhusu uhalali wa Shibuda ni kama kupoteza muda tu.

Ni lazima viongozi wetu hawa wa Baraza la Vijana CHADEMA waende hatua kumi mbele kutafakari mzozo, unaoanza kuwatafuna na kuwagawa, kwa busara na hekima badala ya kila mmoja kuegemea upande wake ama kwa kusaka umaarufu wa kisiasa au kwa kutofahamu na pengine kwa kujionyesha umahiri wa kujua kila jambo hata lile lisilokuhusu.

Bavicha lazima litambue kwamba umma wa Watanzania walioamua kuikubali CHADEMA una mtazamo tofauti karibu kwa kila jambo linaloonekana kukivuruga chama. Potelea mbali kwamba katika jeshi la ukombozi wasaliti hawakosi.
Kila Mtanzania anao uelewa tofauti kabisa na mwingine. Hata kama kati ya hawa mafahari wawili wanaokinzana mmoja yuko sahihi na mwingine amekengeuka, suala linabaki palepale kwamba ni lazima wote hawa wawe na kauli moja, mpishano wa maneno uwe siri yao na kamwe usihusiane kabisa na misingi ya utendaji wa kazi zao, usihusiane na chama.

Hii itazidi kuwapa moyo vijana wengi walioamua kuwaamini.Na ni lazima Bavicha iweke akilini kwamba migogoro ndani ya chama iliyozaliwa kwa msuguano kama huu wanaouanzisha huishia kuharibu mwenendo wa chama na mwisho Watanzania kudharau dhana nzima ya mabadiliko. Hilo tu.

Ukiangalia ni nini wanachohitilafiana, eti kauli ya Shibuda.

Hivi Heche na Shonza wanaweza kuwadhihirishia vijana wenzao na Watanzania kwa ujumla kwamba hawawezi kukumbuka kauli tata na vitendo visivyoendana na falsafa ya CHADEMA ambavyo Shibuda amekwishavifanya tangu awe mbunge wa Maswa Mashariki kupitia CHADEMA? Kama alikuwa sahihi katika yote isipokuwa hili basi ni sawa, na ndiyo maana sikuwasikia wakisema wala kuanzisha zogo, lakini kama alikosea je, walianzisha mtafaruku kama huu wanaouigiza?

Sio Shibuda huyuhuyu aliyepingana waziwazi na mtazamo wa CHADEMA juu ya posho za wabunge?

Huku CHADEMA ikihuzunika na kuuhurumia umma maskini wa Watanzania walala hoi wasiojua kesho watakula nini, Shibuda alisema angependa apewe shilingi za Kitanzania 500,000 kwa kila siku akiwa bungeni bila kujalisha kama amechangia, hakuchangia, au amesema lolote kwa niaba ya watu wake.

Haihitaji elimu kubwa kuelewa siasa za Shibuda. Niseme wazi tu katika suala la kutamani posho kubwa kinyume na hoja ya CHADEMA, wengi tuliishia kucheka tu tuliposikia mbunge wetu kaja na mapendekezo yasiyofikirika.
Kwa Shibuda ilikuwa sahihi yeye kuchangia mjadala huo wa posho ya namna hiyo, pengine tuamini pesa zilizokuwa zinalipwa hazikuwa zinamtosha, ana majukumu mengi.

Na kama tujuavyo Shibuda ni mtunga sheria na kwa hakika katika hilo la posho angeweza kusema kirahisi tu kwamba CHADEMA iache ubabe kwa kuwa yeye alienda sambamba na ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hakuvunja sheria. Kwa mtindo huu wa kutafsiri kifungu hiki vibaya unaweza siku moja kutamka bungeni hoja ya kutaka mbunge kupigiwa saluti na maafande wetu ukasema hilo ni wazo lako na uheshimiwe kwa kuwa hukuvunja Katiba. Tanzania ina vioja!

Nchi hii inayumba na kuna mengi ya kuzungumza zaidi ya hoja isiyoeleweka. Badala ya kuhitilafiana na CHADEMA katika sera na mtazamo wake na kupoteza muda mwingi katika malumbano yasiyo na tija kwa taifa wala chama, Shibuda angeenda kwa wapiga kura wake kuwaelimisha namna nzuri ya kutoa maoni yao siku tume ya kukusanya na kuratibu maoni kuhusu Katiba mpya itakapowatembelea.
Watu wa Maswa Mashariki wangefurahi kumsikia mbunge wao akikemea msimamo mbovu wa CCM katika mchakato wa uundwaji wa Katiba mpya maana unaminya uhuru halisi wa kutoa mawazo.

Shibuda angetenda haki kama angefanya mikutano ya hadhara jimboni kwake kuwaelimisha Watanzania wenzetu jinsi serikali ilivyo taaban na jinsi inavyoshindwa kudhibiti mfumko wa bei na jinsi CHADEMA walivyojipanga kuyarekebisha haya.
CHADEMA inapaswa kulichukua suala hili kama chanzo cha mgogoro wa muda mrefu.

Ni lazima Shibuda ashughulikiwe kwa mujibu wa katiba na kanuni halali za chama.
Kumlea Shibuda na ukinzani wake ndani ya CHADEMA kutakigharimu chama, kama sio leo basi kesho.

Hakuna Mtanzania atakayekuwa na wazo kama la kwangu kwamba kauli ya Shibuda haiwezi kuchukuliwa uzito kwa kuwa ana haki kwa mujibu wa Katiba. Mbegu ya ubaya kamwe haizai wema, kama akithibitika kutenda kosa, aadhibiwe kwa mujibu wa kosa lake na sio kukumbushia kauli tata zilizopitwa na wakati. Ni afadhali CHADEMA ikameza pini kwa kuliweka rehani jimbo moja kuliko kupoteza imani ya Watanzania.

CHADEMA haiwezi kwenda mwendo wa kuchechemea au kuogopa mtu, itaonekana dhaifu. Lakini CHADEMA pia haiwezi kukaa kimya isilishughulikie jambo hili mapema; itaonekana imeogopa.
Na kama CHADEMA ikilichukulia suala hili kwa jazba, itaonekana ni chama cha kibabe na nina imani tutasikia mengi ya ajabu.


h.sep3.gif
​

godfrey120@hotmail.com 0786 546 555

Source: Tanzania Daima 23/05/2012

[TD="bgcolor: #FFFFFF"]
Na Godfrey Kassanga

[/TD]
 
Mkuu fuatilia mambo usikimbilie mambo. Shibuda aliingia kwenye NEC ya CCM akiwa kama mjumbe wa APRM iliyokuwa ikiwasilisha mada kwenye kikao hicho.

sasa kwanini asinge ongelea mambo ya APRM badala yake akaongelea mambo ya siasa? Asinge ongelea siasa nani angemfuatilia?
 
kuendelea kujadili upuuzi wa SHIBUDA ni kumpandisha chati bure, aachwe aseme atakavyo na hata akitaka kugombea kuteuliwa kugombea urais, aachwe tu maana sidhani kama ataweza kupata uungwaji mkono ndani ya CDM. hivo kuliko kuonekana ananyimwa nafasi, aachwe na wakati ukifika agombee tuone atapata kura ngapi dhidi ya wengine watakaojitokeza ndani ya CDM.

vinginevyo, ni kuingia katika mtego wa CCM kichwa kichwa ambacho siku zote kinatumia watu aina ya shibuda kuleta vurugu

Mkuu si salama kuliacha tu hivi hivi, lazima lishughulikiwe vingenevyo tutatilia mashaka sana umakini wa viongozi wetu. Kauli hizi zinatakiwa zikemewe kwa nguvu sana kwani pamoja na ukweli kuwa Shibuda ni mpuuzi fulani lakini hizi kauli zake zinatutoa kwenye lengo la ukombozi. Huyu si mpiganaji ni lazima akemewe ili kuweka presidency kwa wapuuzi wengine wa aina yake.
 
mimi naamini watanzania wana matatizo mengi sana ila huwezi kuandaa chama ambacho kinaenda kushughulkia watu huku ndani yake ukiwa na wapotoshaji wengi na wenye misamiati isiyoeleweka mithili ya huyu SHIBUDA huyu anafanya kazi maalum ya kutaka CDM nao waonekane hawako serious na HECHE YUKO SAHIHI KABISA katika kumpa tahadhari sasa huyu SHONZA yeye anatumikia visenti mpaka lini? sasa wapi na wapi tena SLAA aonekane ni saiz ya shibuda
 
Ukisikia habari za uongo na udaku ndio hizi.

Mbunge wa CHADEMA akaingia kwenye kikao cha Nationa Executive Committe ya Chama Cha Mapinduzi umeanza lini utaratibu huo? Na akaongea kama nani??? Magazeti yetu mbona yamekaa kidaku daku hivi???

Aliingia NEC akiwa kama mjumbe wa bodi ya APRM ambao walikuwa wanatoa mada katika semina ya NEC, hakuingia mle kama Chadema
 
Methali zinamaana nyingi katika jamii. Kwa yeyote mwenye kufamu methali atakubaliana na mimi. Kuna methali moja inasema '' MFA MAJI HAISHI KUTAPATAPA'' methali hii ina maana sama. Napenda kuanza na methali hii ili kuwaonyesha watu sifa za mfa maji. Katika siku za karibuni tumeshuhudia jinsi Mhesimiwa Shibuda anavyo jaribu kuivuruga CDM bila sababu. Wengi wetu tunajua kwamba Shibuda ni Gamba katika CDM. Wengi ambao hawafahamu ama si wadadisi hawajui hilo!!!. Kama nilivyotangulia kusema Shibuda aliingia katika CDM si kwa kuipenda bali kukimbilia madaraka!! Nani asiyejua hilo?!!! Sasa Mbinu zake zimeshindwa baada ya viongozi wa CDM kumstukia na kumtenga katika Masuala mengi nyeti ameamua KUFA MAJI yaani anatapatapa. MUACHE ATAPETAPE Atakula Jeuri yake. CDM kuweni makini maana watakuja magamba wanajifanya wanajiunga cdm kumbe wanakuja kuvuruga
''' ONYO''
Nawaonya ndugu na wapenzi wote wa CDM kama mimi wajiandae kusikia yafuatayo yatakayo zushwa juu ya chadema na Mh Shibuda endapo atatemwa na CDM ama ataamua kurudi CCM;
YEYE SHIBUDA AU WATU WA JINSI YAKE WAKIVULIWA UANACHAMA WA CDM KWA UMAMLUKI WAO WATAKUJA NA KAULI ZIFUATAZO:
>> Oooo CDM ni Chama cha Kidini!
>> OOO CDM ni Chama cha Kaskazini!
>> Viongozi WQengi wa CDM ni Madikteta!
>> CDM haina Demokrasia!
>> CDM ni Gamba Jipya!
>> CDM bado wachanga kuingia ikulu!
>> CDM ni Chama cha Wachaga!
>> CDM wanampngo wa kupindua nchi!
>> CDM wanampango wa siri kuanzisha jamhuri ya Kaskazini!
>> CCM ndo cha THABITI!
>> CDM walikuwa wanasema CC ni magamba kumbe wao!

Chonde chonde wapenda maendeleo na mageuzi mkisikia kauli hizi msitishwe maana tushazisoma!
 
Viva dr. Slaa Rais wa ukweli kwani umefunika kombe wakati muafaka ili huyo mwanaharamu shibuda apite. Sisi tusonge mbele na kwa watu kama hawa ni vitanzi vya umma 2 ndipo vitakavyoamua.
 
I like the post. Ni kweli kbs, tupo kwenye mpambano mkali wa kubomoa dari ili tujenge paa. Hakuna zaidi.
 
Aliingia NEC
Hawezi kuingia NEC!

Period!


na alichaguliwa na wabunge wote.
"Alichaguliwa na wabunge wote" kuwa nani, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi?

Ridiculous!


Acha ubishi wa kijinga, tamko alitoa akiwa NEC ya ccm
Kama mimi ni mjinga basi I am the proudest mjinga in the world because ninakataa kwa confidence thabiti kwamba Shibuda, Mbunge wa CHADEMA, hawezi kuingia Halmashauri Kuu ya CCM. Such a gullible audience!

Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ni kikao. Wanaoingia kwenye kikao cha NEC nafasi zao ziko fixed, written in stones, Shibuda hayumo!
 
Back
Top Bottom