Shibuda sasa amvaa Dk Slaa, adai kuwatumia BAVICHA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shibuda sasa amvaa Dk Slaa, adai kuwatumia BAVICHA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwana Mpotevu, May 24, 2012.

 1. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #1
  May 24, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,294
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Na Aidan Mhando | Mwananchi
  23 May 2012

  MSUGUANO wa vijana wa Chadema (Bavicha) na Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki , John Shibuda, umezidi kuongeza joto la kisiasa ndani ya chama hicho baada ya mbunge huyo kumrushia kombora Katibu Mkuu, Dk Willibrod Slaa, akisema ndiye anayewatumia vijana hao kumhujumu.

  Tayari Shibuda ameigawa Bavicha baada ya Mwenyekiti wake, John Heche kupingana hadharani na makamu wake, Juliana Shonza kuhusu msimamo wa baraza hilo dhidi ya hatua ya mbunge huyo kutangaza dhamira ya kuwania urais mwaka 2015 ndani ya Nec ya CCM na kumwomba Mwenyekiti wa chama hicho tawala, Rais Jakaya Kikwete awe kampeni meneja wake.

  Wakati kauli zake hizo ndani ya Nec ya CCM zikitarajiwa kumweka katika hatari ya kufukuzwa ndani ya Chadema kipindi hiki ambacho amekuwa katika uangalizi maalum, Shibuda jana aliliambia Mwananchi kwamba, yuko tayari kwa lolote na wakati wowote tena kwa asilimia 100.

  Shibuda alifafanua kwamba anatuhumiwa kukihujumu chama huku akiwa hajawahi kukiuka maagizo yoyote ya Kamati Kuu ndani ya Chadema , lakini amebaini kuna baadhi ya watu wanatumiwa na viongozi wa juu wa chama hicho akiwamo Dk Slaa kwa lengo la kumfanyia fitina na hujuma.

  Alisema kitendo cha Dk Slaa kukalia kimya shutuma zinazoelekezwa kwake na vijana hao wa Chadema kinampa fursa ya kuamini kwamba vigogo wa chama hicho wako nyuma yao na kumtaka sasa Dk Slaa aeleza hadharani uovu wake huo ili Watanzania wafahamu ukweli kuhusu sakata hilo.

  "Mimi sina kosa lolote ila ninachofikiria ni kwamba Bavicha wanatumiwa na viongozi wa juu wa Chama ili kutaka kuniharibia lakini cha msingi ni vyema Katibu Mkuu wetu (Dk Slaa), akaweka hadharani maovu yangu ili Watanzania wajue makosa yangu ni yapi," alisema Shibuda na kuongeza:

  "Ni wakati wa Chadema kupitia viongozi wake wakuu kueleza ubora wake wa kuwaongoza wananchi uko wapi kwani kama mtu anatangaza nia na kuonekana ameenda kinyume, sidhani kama kuna uongozi thabiti."

  Kitisho cha kufukuzwa

  Akizungumzia kitisho cha kuweza kufukuzwa Chadema, Shibuda alisema kwa sasa yupo tayari kwa asilimia 100 kupokea jambo lolote litakalotokea dhidi yake ndani ya chama hicho na kwamba kinachotakiwa ni kuonyeshwa makosa yake.

  "Kwa asilimia 100, kutoka moyoni nasema nipo tayari kwa lolote litakalotokea kwangu ndani ya Chadema, kwani mimi natambua wazi sina kosa nililolifanya na kama nina makosa basi yaanikwe hadharani ili wananchi nao watambue," alisema.

  Akizungumzia kupewa barua ya karipio kali, Shibuda alisema kwamba, hata siku moja hajawahi kupewa barua yoyote ya karipio kali na hafahamu chochote juu ya suala hilo.

  "Sikiliza ndugu mwandishi, mimi sijawahi kupewa barua yoyote ya karipio kali na sifahamu chochote juu ya suala hilo labda hao walionipa barua hiyo wangeeleza lini walinipa," alisema.

  Kauli ya Dk Slaa

  Akizungumzia tuhuma hizo za Shibuda, Dk Slaa alisema asingependa kuingizwa katika mjadala huo kwani hajawahi kumzungumzia Mbunge huyo kuhusu jambo lolote wakati wowote tangu mjadala wake na Bavicha ulipoanza.

  Alisema haoni suala la Shibuda kama ni jambo la kuzungumzia kwa sasa kwani halina msingi na kuna mambo mengi ya kujadili ili kuliwezesha taifa kupambana na umasikini.

  "Mimi nisingependa kuhusishwa na suala la Shibuda kwani sijawahi kuzungumza chochote kumhusu yeye na kwamba, nina mambo mengi ya kuangalia na sio Shibuda," alisema Dk Slaa na kuongeza:

  "Sipendi kuzungumzia kauli za watu hata kidogo kwani tunakazi kubwa ya kupambana na kuwakomboa wananchi kutoka katika umasikini."


  MY Take: Hivi kuna ugumu gani CHADEMA kuchukua maamuzi magumu kwa mtu huyu????
   
 2. chitalula

  chitalula JF-Expert Member

  #2
  May 24, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,307
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  We unaona kuna ugumu hapo? Aliyosema Slaa ni ya msingi
  " Alisema haoni suala la Shibuda kama ni jambo la kuzungumzia kwa sasa kwani halina msingi na kuna mambo mengi ya kujadili ili kuliwezesha taifa kupambana na umasikini."
   
 3. Anheuser

  Anheuser JF-Expert Member

  #3
  May 24, 2012
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 1,962
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Ukisikia habari za uongo na udaku ndio hizi.

  Mbunge wa CHADEMA akaingia kwenye kikao cha Nationa Executive Committe ya Chama Cha Mapinduzi umeanza lini utaratibu huo? Na akaongea kama nani??? Magazeti yetu mbona yamekaa kidaku daku hivi???
   
 4. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #4
  May 24, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Huyu Mzee anazidi kuchanganyikiwa, alidhani kauli na matendo yake ya kujikomba sisiem vingeleta mtafaruku kakuta chama makini kinaendelea na shuguli za kujijenga na kumuacha amebakia kwenye dust bin hivyo anatafuta namna ya kukuza mgogoro. Watu makini wamemwambia hawashuguliki na watu.

  Alipokuwa CCM alitangaza nia mapema zaidi watu wakamuwekea bifu wakampora na ubunge wake, aishukuru CDM kwa kumuokoa alipobambikiziwa kesi ya mauaji akasaidiwa vinginevyo angekuwa ananyea debe.

  Kitendo cha Shibuda kumrukia Dr ni sawa na shoga akiwa kwenye harakati za kutafuta mtu wa kumshikisha ukuta, huwa anaparamia kila kidume kutafuta attention maana muwasho huwa hauvumiliki.
   
 5. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #5
  May 24, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,640
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Hili ni pigo lingine kwa shibuda.
  Dawa ya watu kama hawa ni kuwapuuza tu. Kaandaa disco kaona hakuna turn up hata kidogo, ni aibu sana.
   
 6. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #6
  May 24, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,815
  Trophy Points: 280
  Mkuu fuatilia mambo usikimbilie mambo. Shibuda aliingia kwenye NEC ya CCM akiwa kama mjumbe wa APRM iliyokuwa ikiwasilisha mada kwenye kikao hicho.
   
 7. M

  Molemo JF-Expert Member

  #7
  May 24, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Ni kweli mkuu naona kakasirika baada ya viongozi wakuu kumpuuza
   
 8. Anheuser

  Anheuser JF-Expert Member

  #8
  May 24, 2012
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 1,962
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Unachemka tena!

  Shibuda, Mbunge wa CHADEMA, hawezi kuingia kwenye National Executive Committee ya Chama Cha Mapinduzi. Period!

  Nyinyi ndio waandishi wa kibongo ninaowaambia kila siku hapa ni wabovu!

   
 9. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #9
  May 24, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,694
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  I wonder, what is this fuss all about? BAVICHA wamejiingiza kwenye ubishani usio na maana hata kidogo. Huyu jamaa anatafuta publicity dawa ilikuwa kumchukulia kama alikuwa "anafanya utani".
   
 10. k

  kagame Senior Member

  #10
  May 24, 2012
  Joined: Dec 6, 2008
  Messages: 159
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Uongo na udaku ndo huu uliouandika weye, kama ulikuwa hujui haya mambo ya shibuda kuzungumza nia yake ya kugombea urais cdm akiwa kwenye NEC (CCM) ni aheri ungeomba kujuzwa kuliko kufanya judgement kuwa ni habari ya udaku!
   
 11. D

  DUNIANGUMU JR Member

  #11
  May 24, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wamuchukulie maamuzi magumu ndugu shibuda kwa dhambi gani aliyofanya? kama kutangaza kuwania urais 2015 yeye si wa kwanza hata zitto kabwe aliwahi kujitambulisha hivyo sasa iweje zitto hakuchukuliwa hatuwa na shibuda achukuliwe?
   
 12. k

  kijiichake JF-Expert Member

  #12
  May 24, 2012
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 285
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Chibuku chibuda shibuda. Kaambulia patupu mwishowe naona atajitia kitanzi shingoni ajinyonge mwenyewe.
   
 13. M

  Mnyonge Namba1 JF-Expert Member

  #13
  May 24, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 402
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Sitajadili ugonjwa wa mafua wa taifa(shibuda) hali nchi inaumizwa na kansa ya ubongo(ufisadi/ubadhirifu)
   
 14. P

  PakavuNateleza JF-Expert Member

  #14
  May 24, 2012
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 957
  Likes Received: 513
  Trophy Points: 180
  Shibuda atachukuliwa hatua when the time is right.
   
 15. Kumbakumba

  Kumbakumba JF-Expert Member

  #15
  May 24, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 222
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi sioni kama kauli zake zina madhara kwa chama..yeye aendelee kuropoka..
   
 16. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #16
  May 24, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  dawa yake ni kumpuuza tuu yaani asijibiwe wamwache alolome hadi achoke
   
 17. B

  BigMan JF-Expert Member

  #17
  May 24, 2012
  Joined: Feb 19, 2007
  Messages: 1,097
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  habari ingefafanua jinsi ya shibuda alivyoingia katika nec ya ccm kwani ninavyofahamu hata waandishi wa habari hawaruhusiwi ni kikao cha ndani
   
 18. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #18
  May 24, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Huyu mie namjua ni comedian mzuri na ni mtu wa U-Turn
   
 19. nashy

  nashy JF-Expert Member

  #19
  May 24, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 679
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Acha ubishi wa kijinga, tamko alitoa akiwa NEC ya ccm
   
 20. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #20
  May 24, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ndo uzuri wa mtu ukiwa ni phd holder ya darasani na si ya kudondokewa na zali.heko dk.w.p.slaa
   
Loading...