Shibuda out

Yaani waswahili bwana, wamezoea udikteta wa mwenyekiti na katibu ktk chama la mafisadi sasa wakiona watu wanakubaliana kutokubaliana kidemokrasia wanasema kuna mgogoro. Ndo demokrasia hiyo!
 
Ee bwna ee!...mnataka kununua magari mitumba kutoka india?...mapya kutoka india tu sinunui!......hawa watu ni walewale,hamna kuwapa nchi.
 
WANA-CDM KUKOSOA VIONGOZI WETU NI WAJIBU KAMA KWELI TUNGEPENDA KUPATA DAIMA MATUNDA MAZURI NA ZAO LA DEMOKRASIA YA KWELI NDANI YA CHAMA LAKINI KATIKA
MADA HII NENO 'MGOGORO' UNAIBUA MKANGANYIKO MKUBWA ZAIDI


Sasa hapo penye kujadili mapungufu unayoyaona na hata kuyatolea suluhisho jinsi unavyoyaona yatuliwe vipi hapo NI SAHIHI KABISA tena ni wajibu wa JF kufanya hivyo iliviongozi wetu wajue na kuchukua hatua kwa mtu mmoja mmoja au kama kikundi tukiwa na lengo la kuboresha zaidi chama.

Walau mimi na wewe tukijibidisha kufanya hivyo tena kwa ujasiri kabisa basi walau tutakua tumefikisha viwango vyetu vya mijadala kuleee katika JF PREMIER LEAGUE kimjadala ili tukafananie na akina Malecela Mdogo (CCM), MMwanakijiji (CDM) na kwa kidooogo sana Waberoya (CCM / CDM).

Nasema katika kundi kubwa la wanachama 40,000 mtandao wa JF hadi leo, nakiri kwamba nimewaona wachache sana WENYE UWEZO kimtazamo na kimjadala WA KUPATA UJASIRI WA KUPONDA WANACHOKIPENDA NA HATA KUPAMBA WANACHOKICHUKIA; alimradi kimsingi nguvu ya hoja na mantiki inawaelekeza kuwa kufanya hivyo; nmiongoni mwa watu hao ni pamoja na watu hao hapo juu, pia Dingiswayo (CUF), Ganekai (CDM), Jasusi (CDM), Regia (CDM) na Dr Kitila Mkumbo (CDM).

Wakati nikijibidisha na mimi niweze kufikia huko kwenye viwango vyao, najihisi kuhitajika kufanya kazi zaidi. Ila yoote juu ya yote inaniwiia vigumu kununua wazo kwamba kutofautiana kwenye mijadala katika vikao tayari ni mgogoro.

Maadam katika lugha yangu hii ninayojivunia ya Kiswahili bado kinanipa uwanja mpana zaidi ki-misamiati, basi ningalikua ni mwandishi wa makala hayo hapo juu basi kwanza kidooooogo ningechelewa kutumia neno MGOGORO wakati jambo lenyewe lilikua ni tukio katika kikao kimoja na wala si mwendelezo na msururu wa matukio YANAYOUMANA KIMAUDHUI kiasi cha kuridhisha sana kushindikana kutatulika licha ya juhudi mbalimbali.

Kama ingalikua ni mimi ningalifikiria kwanza maneno kama vile; kwenye kikao cha CHADEMA kuliibuka 'Kucharukiana', 'Kupingana', 'Kuburuzana', 'Kupeana somo', na kadhalika.

Naongeza kwamba inawezekana mwandishi ameandika lakini bila kupata uhakika ka megemeo wooote wa mjadala ulikua ni Mgogoro au vinginevyo lakini naye mhariri bado akaenda mbele kidogo kutia muhuri mashaka hayo bila hata kuhoji ni kitu gani hasa kilijiri kwenye vikao husika.

Wenye kuelewa nashukuru watakua wameona kwamba kama neno kuu ni 'mgogoro' basi tusubiri makala mengine ya kuja kukamilisha picha zima kuthibitisha gogoro lenyewe kwa maana halisi ya neno hilo na mazingira yanayozungumzwa hapa.

Kwa lugha nyepesi nasema huenda huyu mwandishi hamudu vema lugha yetu hii (labda akaandike kwa kiingereza) ua kachipukia porini tu kwa kujichagulia juu ya nini kilichojiiri kwenye kikao cha CHADEMA hapo majuzi.

 

I second u
 
Mimi sioni tatizo la kumkosoa Mwy kiti. hii ndiyo Democrasia ya kweli siyo mpeleke mpeleke
 
Pamoja na kutokuaminika kwa Shibuda na zaidi Zitto, wangemuacha hadi kipindi cha uchaguzi.
Kuhusu hayo magari, nisuala la kukubaliana na kuhakikisha kwamba hakuna ufisadi. Kwa mfano wanaweza wakaamua kununua magari ambayo milage zake hazijazidi 50,000 km, haya bado yanakuwa katika hali nzuri.

Na nafikiri hili wamelifanya kwa nia nzuri ili waweze kupata idadi kubwa ya magari yakasaidie huko mikoani. Ila ni lazima wahakikishe kwamba wananunua kwa manufacturer mzuri e.g Toyota.

Lakini wakifanya makosa ya kununua e.g Mahindra kutoka India baada ya muda mfupi maintanance cost itakuwa kubwa hata kama yangekuwa mapya kabisa. Nawashauri watafute mtu mwenye idea ya magari awashauri hasa ukizingatia mutumizi yake ni kwa shughuli za vijijini kwa nchi kama TZ.

Na mwisho huyo mtu aliyekuja na hoja ya kununua magari kutoka India, atoe sababu za kutosha ni kwanini siyo Japani?
 
nilishasema tangau hapo awali kwamba CDM ni chama kinachowahada watanzani, wanachokiongea sicho wanachokiamin ,uthibitisho ni huu upuuzi wa kutaka kununua magari machakavu wakati huo huo wanapinga serikali kufanya hivyo hii ni aibu kwa chama kinachojiita chama makini
 
kutofautiana ni muhimu kwa uhai wa chama ila tofauti zisivuke mipaka.
Katika kundi la watu ni lazima mutofautiane ila swala ni kwa maslahi ya wanani?
 
Kwa kweli Huyu Zitto haeleweki, kila controversial ya CDM lazima ahusike. Isije ikawa amepandikizwa kuiua CDM.
Zitto kama binadamu yoyote anaweza kuwa na matatizo yake, ila ukweli ni kwamaba mwnyekiti CDM anaipeleka CDM kaburini. Uwezo waka kama mwnyekiti wa chama kikukbwa ni wa kutia shaka mwnye CV yake atupatie ndio mtajua ninachosimami, kama si kosei ndiye mwenyekiti peke wa vyama vyenye wabunge ambae hana shahada ukimwondo mzee kwa kiraracha
 
Ushirika wa lema na Mbowe utakiua hiki chama
 
Mwenzenu huwa ni mfuatiliaji sana wa vyombo vya habari.Huyu mwandishi wa mwananchi aliyeandika hii habari ni mfuasi mkubwa wa Zitto Kabwe.Ana tabia ya kushabikia migogoro pale anapoona kuna mvutano wa hoja ndani ya Chadema.Nilishangaa kuona gazeti makini kama mwananchi kuandika habari kama gazeti la uhuru,lakini nilipoona mwandishi aliyeandika hiyo habari wala sikuhangaika kuisoma na kuimalizia.Wenye kumbukumbu wakati wa kususia hotuba ya Rais bungeni watafute huyu mwandishi alikuwa anaandika vitu gani kuihusu Chadema kwenye gazeti lake.
Ushauri:Namshauri mhariri wa gazeti la mwananchi awe makini na habari za huyu mwandishi hasa zinazoihusu Chadema.Tunaliamini sana gazeti hili habari za kishabiki zitalichafua hili gazeti....
 
mbowe na zito kaeni chini mfikirie chama kwanza badala ya kujenga makundi kwa sasa kwani ndiyo yanaimaliza ccm
 
CDM hampendi kusikia habari za upande mwingine kuweni wavumilivu hata kama habari husika sio nzuri upande wenu
 

Hizi ni mbinu za Zitto mwenyewe kuspin story, ili aonekane safi. Ukweli ni kuwa alikiuka katiba kumpa Shibuda ukaimu m/kiti, kwa kuwa si mjumbe wa sekretarieti ya mkoa. Wajumbe tu ndo wanastahili kushika nafasi. Alikuwa ana aje da ya kupanga safu yake. Na ndicho alichohoji Lema.
 
Heh.lakini katika jamii lazima watu kama hao wawepo.
 

Umekosea Chini ya uongozi wa Mbowe CDM imepata mafanikio ambayo kipofu pekee hataweza kuona, Sipati picha kama Zitto angekuwa mwenyekiti migogoro angekigawa chama kutokana na kukosa dhamira na mapenzi ya kweli aliyokuwa nayo awali, ingawa Mbowe anautawala wa kimla lakini napendezwa na dhamira na mapenzi yake kwa chama na hii yuko sawa kwa sasa kutokana na hali ya chama kipindi hiki ambacho maadui ni wengi tena ndani na nje ya chama
 
Mawazo yako ni vinyu. Tafakari tena. Ama una utindio wa Ubongo.
 
Kama umekubali kuwa Mbowe ana utawala wa kiimla hyo ni sifa amabao si njema kwa chama kinachokuwa, ni vizuri basi mkaitisha uchaguzi mapema ili kuinusuru CDM kwani uwezo wake kwa sasa huendani na majukumu ya cdm( jivueni gamba) kabla ya matatizo kuwaelemea. Inashangaza cdm mna wasomi kibao lakini hili hamlioni .
 
Mbona malumbano kati ya Shyrose na Makamba kwenye UVCCM yalijadiliwa? Kwani CDM yenyewe ni exceptional kiasi gani mpaka taarifa zikitolewa ziwe zinachambua vya kuwajulisha watu na vya kufanya siri?? Acha hizo banaa...!
 
SAFIIIII,UKWELI UTAKUWEKA HURU DAIMA
Wana Cdm tukubali kuwa kunakipindi ni lazima tuwe tayari kwa kila kitu,si kila siku CDM itakuwa ktk khali ya furaha na kicheko,
nakubaliana na mtoa hoja kwa kuweka kila alichokiona ama kukisikia kutokana na chanzo chake,Mh Lema amekuwa muwazi zaidi tofauti na baadhi ya washabiki humu JF wanaopenda kuficha mambo haswa yale yanayohusu Cdm,
Tatizo letu tunataka tujadili yale Mazuri tu ya CDM ila mabaya hatutaki kuyaona

tunapenda kujadili mabaya ya CCM inapokuja mabaya ya chama chetu CDM Hatutaki kuyasikia walakuyaona huo ni udogo wa SIASA vichwani mwenu ni lazima tubadilike sasa

Lema safiiiiiiiii,ukweli utakuweka huru
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…