Shibuda kugombea uenyekiti CHADEMA

Shibuda kugombea uenyekiti CHADEMA

Shibuda hajasema lolote, TUWE MAKINI HAKUNA LOLOTE LA KUJADILI KWA KIPINDI HIKI HOJA ZA KUWAHAMISHA WACHANGIAJI KWENYE LENGO LA MSINGI (mfano mauaji ya wanaharakati nk) TUSIZIJADILI POEZEA MBALI
 
Ni haki ya member yeyote kugombea cheo chochote ndani ya chadema. Hata mimi naweza kugombea kwani si ndiyo demokrasia? Lkn je nakubalika? Nna mbinu za kuendesha chama kama chairman? Niko chamani kwa matakwa yangu au ya wananch? Atapata kura 1 yake.
 
Ili chadema kionekana ni chama cha kidomokrasia ni vizuri kumwachia agombee vizuri tu
 
nafikiri wakati wa Mwalimu Nyerere kigezo cha kuingia USALAMA wa Taifa kilikuwa ni akili nzuri,sasa kama aina ya Mwami Shibuda ndiyo wenyewe huhitaji shahada wala uelewa wa msingi kujua matokeo ya kazi za watu wa akili hiyo
 
shibuda akae pemben hii siyo ngoma ya kisukuma unachezacheza tu kuwapiga roba magamba siyo mchezo yeye acha akae pemben hii ngoma lazma ujipange kama kutoa pepo ivi
 
Nakunya kutoka hapa dom hadi dar,ikishndkana akiwa mwenyekt narudi ccm nijue mojaaaa tu'
 
Dah,hadi mtu kama Shibuda anazua mjadala?
Aachwe agombee tu kwani hakuna atakaye mpa kura.
 
KARIBU SHIBUDA AU MTU MWINGINE YEYOTE YULE UWE MWENYEKITI WETU CHADEMA ENDAPO UTAFUZU KUKIDHI HAYA MAPENDEKEZO YETU NEC

Ni jambo iliyo dhahiri kabisa kwamba haya mafanikio makubwa ambayo CHADEMA kimepata hadi leo ni matokeo ya kubahatika kupata viongozi bora, wachapa kazi na wenye kuaminika wakati wote na kutukuka bila ya hata mmoja wao kujikweza mbele ya jamii ya Tanzania.

Ukweli huo hapo juu hakika ni zaidi ya tunu maalum ambalo si kila chama kimebahatika kujaliwa nalo katika historia ya taifa letu tangu mfumo wa vyama vingi uanze huko 1992.

Hivyo basi, hii ndio maana NEC CHADEMA sikuzote humulika sana tena sana juu ya kuzingatia misingi mema ya malezi bora kuandaa viongozi chipukizi katika chama chetu kimchakato zaidi.

Sasa ni kutokana na hiyo misingi mizuri CHADEMA iliyotuimarisha kama chama na kukifanya chama hiki kuonekana kuwa ndicho pekee kioo na kiwakilishi cha sauti ya wanyonge nchini ndio maana baadhi ya wanachama tumesukumwa kupendekeza njia mbali mbali za kuzingatiwa siku za usoni ili kuhakikisha ya kwamba CHADEMA tunaendelea kutunda hili tunu la uongozi bora na makini kwa njia endelevu zaidi.

Hivyo sisi wanachama wa kawaida ambao hasa ndio wenye chama chenyewe, tunaomba usikivu wa NEC CHADEMA kufanyia tathmini mawazo haya na kuyazingatia (to adopt them), endapo itaonekana inafaa, vigezo vya msingi vya kuzingatia katika michakato yote jinsi gani ya kupata viongozi wetu.

Mwanachama yeyote (akiwemo Mzee Shibuda) awe huru kugombea nafasi yoyote katika chama chetu CHADEMA ilmradi tu iwe ni kwamba anakidhi matakwa yote ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na vigezo binafsi vya ndani ya chama chetu kama vile:

1. Awe amedumu ndani ya chama kwa kipindi kisichopungua;

i) Walau kipindi cha Chaguzi Kuu tatu endapo anatafuta kiti chochote ngazi ya taifa.
ii) Walau kipindi cha Chaguzi Kuu mbili endapo anatafuta kiti chochote ngazi ya mkoa.
iii) Walau kipindi cha Chaguzi Kuu moja endapo anatafuta kiti chochote ngazi ya wilaya.
vi) Walau nusu kipindi cha uchaguzi mkuu mmoja endapo anatafuta kiti chochote ngazi ya kata.
v) Walau robo kipindi tangu uchaguzi mkuu upite endapo anatafuta kiti chochote ngazi ya mashinani.

2. Mgombea wa kiti chochote ndani ya CHADEMA atahitajika kuwa na rekodi ya nidhamu ya hali ya juu hivyo;

i) Awe ni mtu ambaye hajawahi kuadhibiwa na chama kwa kipindi kinachozidi miezi 6.
ii) Hajawahi kuwa sehemu na kisababishi cha mitafaruku na migogoro yenye viashirio kali kukidhoofisha chama.
iii) Awe ni mtu ambaye hajawahi kuwa ni sehemu na au kisababishi cha mazingira ya rushwa / ufisadi nchini.
vi) Awe ni mtu ambaye chini ya mikono yake, maelekezo au usimamizi wake hajawahi kumwaga au kusababisha kumwagwa damu ya raia yeyote wa Tanzania.
v) Awe ni mtu ambaye katika historia yake yote ndani ya chama hajawahi kulaza ada yoyote na au mchango.

3. Mgombe wa nafasi yoyote ya uongozi ndani ya CHADEMA atahitajika kuwa na UZOEFU WENYE TIJA kwa chama

i) Awe amewahi kushika nafasi ya uongozi katika ngazi yoyote ndani chama au sawa yake kwingineko yenye ufanano huo huo walau kwa kipindi cha miaka:

a. Miaka 8 ili kugombea kiti ngazi ya taifa;
b. Miaka 6 ili kugombea kiti ngazi ya Mkoa;
c. Miaka 4 ili kugombea kiti ngazi ya Wilaya;
d. Miaka 2 ili kugombea kiti ngazi ya Kata;
e. na walau Mwaka 1 ili kugombea kiti ngazi ya Mashinani;

... na kuweza kukidhi vema matakwa ya MKATABA WA UTENDAJI KAZI NDANI YA CHAMA (aliyotiliana sahihi na Katibu Mkuu wa CHADEMA au kiongozi yeyote sawa yake nje ya chama) na kupata cheti safi ya utendaji.

Kwa mtaji wa mapendekezo haya kwa uongozi wetu sikivu NEC Taifa hakika naamini kwamba CHADEMA kitakua chama imara cha kupigwa mfano, chenye demokrasia sawa kwa wanachama wake wote wenye nidhamu na utendaji uliotukuka.

Kwa lugha nyingine, kwa mtaji wa maapendekezo haya endapo yatazingatiwa vema, CHADEMA kitakua kimejiwekea uzio madhubuti wa kuondokana na kichwa kuuma kwa baadhi ya (1) walevi wa madaraka, (2) mamluki wanaopandikizwa chamani na kesho kutegemea kuibuka viongozi wa ngazi za juu kabla ya kukiuza chama.

Na (3) vile vile kuondoa minunguniko yaa hapa na pale maana utaratibu wa kuwapata viongozi utakua unajulikana wazi kwa kila mmoja huku kigezo cha utendaji uliotukuka na nidhamu zikipewa kipaumbele zaidi.
 
Nimezipata kutoka ndani ya CHADEMA, sasa kuna mtafaruku unaendelea ndani ya CHADEMA baada ya mkakati wa mbunge wa maswa bwana Shibuda kutaka kugombea uenyekiti akipigiwa kampeni na kambi ya Zitto Kabwe
Acha uzushi. Zito na Shibuda ni wanasiasa wasiona ushirikiano. Mzee wa Posho (Shibuda) anamuona Zito ni mpinzani wa maslahi bora ya wabunge.
 
Kila la heri SHIBUDA, nasi Kanda ya ziwa tuongoze CDM, labda kitapata mafanikio, hawa jamaa wa kaskazini siasa zimewashinda
Nakumbuka namna shibuda alivyoandamwa na marehemu shekh yahaya kipindi ametangaza kugombea urais ccm mwaka 2000,watu tulimwonea huruma sana na alipohamia CDM na kushinda ubunge,wapenda haki tulishangilia na kusema UOVU umeshindwa na haki imejidhihiri.leo nikiangalia mambo anayoyafanya CDM namshangaa sana,lkn malipo ni hapa hapa duniani.
 
KATIBU NA MTENDAJI MKUU CHADEMA (DR SLAA) TAFADHALI TUPE RIPOTI YA MAREJESHO YA UTENDAJI KAZI BORA WA VIONGOZI WETU ILI TUPATE KUBAINI MBEGU ZA 'VIONGOZI BORA' NA WALE 'BORA VIONGOZI'

Baada ya mapendekezo ya UTARATIBU GANI KUFUATA KUPATA VIONGOZI ndani ya CHADEMA, sasa naomba nichukue fursa hii kumpa changaamoto Katibu Mkuu wetu Dr Slaa kwamba awe anachapisha magazetini ripoti ya MAREJESHO YA VIONGOZI WA CHADEMA NA UBORA WA UTENDAJI WAO KAZI walau mara moja kwa mwaka.

Huko tuendako, endapo CHADEMA tutazingatia mapendekezo kwenye mchango namba 70 ndani ya uzi huu hapa, watu tutaanza kusikia SIASA ZA KOO ZA 'UTENDAJI ULIOTUKUKA' na SIASA ZA UKOO WA 'UADILIFU USIO NA MAWAA' taratibu zikichukua nafasi za SIASA ZA KIZAMANI KULE CCM ambazo siku zote ni SIASA ZA 'KUBAHATIKA KUZALIWA KATIKA KOO TEULE ZA UONGOZI NCHINI' na zile siasa za 'UNAMJUA NANI NEC TAIFA NA UNAYO KILO NGAPI YA KUWEZA KUHONGA' au wakati mwingine tu ni kuzingatia SIASA VIWANGO VYA KUFUZU UPIKAJI MAJUNGU, FITINA, NA KUWAPORA WATANZANIA RASLMALI NA HAKI ZAO ZA MSINGI eti kwa jina na faida ya chama - CCM.

Watu tunakusudia kuondoka huko na kuleta mpambazuko mpwa wa siasa za HAKI, UTENDAJI ULIOTUKUKA na UADILIFU USIO MAWAA kwa kuzingatia njia za kupimika kisayansi na rekodi ambazo kamwe hazitowekwa SIRI KUU kwa macho ya Vikao vya NEC tu jinsi wenzetu CCM wanavyofanya hivi sasa.

Sasa ili Katibu Mkuu wa CHADEMA aweze kuonekana kuwa FAIR katika kutangaza wazi RIPOTI YA MAREJESHO YA UBORA WA UTENDAJI KAZI WA VIONGOZI WETU CHAMANI NA NDANI YA 'SERIKALI YA CHAADEMA', itakua ni vema kwake kuzingatia MIJUMUISHO MITATU ya ripoti za utendaji wa kila kiongozi na kuitengeneza kuwa ripoti moja inayozingatia vipindi 3 tofauti ili ndio picha halisi iweze kujiweka wazi kwetu sisi wanachama wa kawaida na Umma wa Tanzania kwa ujumla wake.

Naam, ninachokisema hapa ni kwamba mathalan tuchukulie kwamba kila kiongozi wa CHADEMA wa hivi sasa ameingia MKATABA WA UTENDAJI KAZI BORA na kwamba tathmini ya utendaji kazi wa afisa huyo husika hupimwa kila baada ya miezi mitatu ofisini kisha RIPOTI YA MAREJESHO YA TATHMINI YA UTENDAJI KAZI WAKE (CHADEMA Public Officer Quarterly Performance Appraisal Report - inayoainisha vigezo mbalimbali ndani mle) kutolewa na yeye kupewa nakala; itakua ni jukumu la Katibu Mkuu kutoa marejesho pia kwa wenye chama ambao ni sisi wanachama wa kawaida na umma wa Tanzania kwa ujumla wetu ili tupate kujua kama kweli tunaye kiongozi wa kutumainika katika ngazi husika au ni mzigo wa kuni tu.

Kwa namna hii ya chama kuwa na utaratibu wa wazi na unaopimika kisayansi kupiga chekecha maafisa wake, vivyo hivyo serikali itakayozaliwa na chama cha siasa chenye mfumo kama huu itaakua ni serikali yenye watendaji madhubuti na waadilifu wenye dalili zote za kuweza kutufikisha huko tunakodhamiria kwenda KIUCHUMI, KISIASA na KIJAMII. Kwa lugha nyingine, kwa utaratibu kama huu SIASA NCHINI TANZANIA ITAKOMA KUENDELEA KUWA PANGO LA WANYANG'ANYI ambako mfisi wote katika jamii hukimbilia kwa utajiri wa kimapepo.

Great Thinkers, sasa karibu tukosoleane na au kuboreshana mawazo hapa ili na sisi huku CHADEMA tukija kushika dola mnamo 2015 mambo yasije yakawa ni yale yale tunayoyakataa leo endapo utaratibu unaopimika kutekeleza wajibu chamani na ndani ya serikali haitokwepo.

Remember, mine is a real fight for a change of systems and structures on the way we operate as a government that is down-bent to benefit tax-payers at all costs throught varifiable checks and balances,and not merely making aa change of political faces that are heavily armed with lethal streak of arsenals of trendy unrealistic honey-sweet political slogans (Maisha bora kwa kila Mtanzania na kuishia na Bora maisha kwa kila Mtaanzania) that bears no impact to the masses of this country.

Ndio, mine is a brutal fight for a change that face-lifts the way we operate and carry ourselves in public office in a manner that easily predictable to trickle down benefits to citizens and not syphoning public finance from public coffers to a heavenly-safe Swiss bank that only facilitates job creation outside our borders.
 
Mkuu tafadhali usituache kwenye giza hivi;

hizo kura 3 atakazozipata 'Mheshimiwa Rais na Mwenyekiti Mtarajiwa - CHADEMA' huyu Ndugu Yohana Shibuda atakua amezibahatisha kutoka kwa akina nani hao?????????


Atapata kura tatu tu.
 
Back
Top Bottom