Shibuda: CHADEMA nifukuzeni muone!

Kichama Shibuda hana nguvu, anaweza kuwekewa mkakati, akafukuzwa uanachama na kupoteza hata ubunge.

Kinachwapa watu maswali hapa ni, Shibuda anathubutu vipi kuwa na kiburi hiki? Je, kashajichukulia siri nzito za CHADEMA kiasi cha kuweza kubwabwaja bila kuogopa huku akijua kwamba inawawia vigumu CHADEMA kumfukuza kwa kuwa wanajua ana siri za uongozi wa juu wa chama?

Mkuu ni kweli jamaa ana kiburi, lakini mimi nakiita si kiburi bali ni kubuni mbinu kuchanganya akili za watu, huyu huyu alitishia kugombea urais apingane na JK watu wakahofu sana, akawachanganya watu kwa muda then akasema Hagombei tena.

Anajua wanaweza kumfukuzwa, sasa anachofanya ni kuwafanya watu wote tuwe attention tuumize vichwa vyetu kujiuliza hizi guts za kusema nifukuzeni muone kazipata wapi? kifupi jamaa hana lolote na nawaambieni kama kuwa fired atakuwa fired tu.


Na endapo ataanza kuitisha mikutano kukiponda chadema yatamkuta ya Mch. Mtikila alipotaka kutafuta umaarufu wa kutumia jina la marehemu Wangwe kujinadi - yaliyomkuta jukwaani Tarime hatakaa ayasahau hadi leo.



 
Huyu jinga sana,tupilia mbali kabisa akaliwe na mamba!shenz type zake!fukuzen kuku hilo,asituharibie chama
 
Wewe sema ukweli wa nafsi yako.........Haumuamini Prof. Safari kwan sababu ana jina la Kiislamu. Hata kwenye orodha yako ya watu wa kuaminiwa slaa, mbowe, mnyika, mdee, lissu wote ni WAKORINTHO!
sijui kama HALIMA mdee ni mkristo,..na sijamuweka kwenye list ili kubalance wakristo na waislam,ni kwa sababu ameonyesha utiifu mkubwa kwenye mapambano ya ukombozi...dhambi ya udini itawasumbua sana ccm,hamfanyi jambo bila kuhesabu idadi ya wakristo na waislam..shame on y'all ccm
 
Ni kweli kuwa cdm walizichanga karata vibaya hadi kujikuta wamelamba hili garasha. Ukweli ni kuwa cdm walishaliona siku nyingi, na naamini uelewa wao unakwenda mbali kuliko garasha lenyewe. Inaonekana kuwa jamaa anafanya vyovyote iwezekanavyo afukuzwe hivi sasa kwa swala lililotokea bungeni ili apate kinga ya mahakama kama ilivyokuwa kwa Jidawi. Nadahani kwa hili cdm wako sooo big, kiasi kwamba halitatokea kwa sasa, yeye ataendelea kutembea na 4 yake, hadi wakati mwafaka wanamwekea 0 na hapo ndio inakuwa arobaini yake. Ndio, itakuwa chali!
 
Namhurumia sana John Shibuda kwamba huko alikokimbilia ni sawa na mtu alikuwa anamkimbia simba akaamua kijificha kwenye pango lakini ghafla akajikuta amekanyaga kichwa cha nyoka akapata mtihani mgumu, je atoke nje ya pango aliwe na simba au abaki ndani ya pango agongwe na nyoka mwenye sumu kali?
Nadhani Shibubda angejua kwamba CDM ni sawa na nyoka mwenye sumu kali, katu asingeiomba imdhamini awe mbunge wa Maswa, hata hivyo, asihofu porojo za CMD kwani wapiga kura wa Maswa sio wajinga wanajua maana ya kuwakilishwa
 
Namhurumia sana John Shibuda kwamba huko alikokimbilia ni sawa na mtu alikuwa anamkimbia simba akaamua kijificha kwenye pango lakini ghafla akajikuta amekanyaga kichwa cha nyoka akapata mtihani mgumu, je atoke nje ya pango aliwe na simba au abaki ndani ya pango agongwe na nyoka mwenye sumu kali?
Nadhani Shibubda angejua kwamba CDM ni sawa na nyoka mwenye sumu kali, katu asingeiomba imdhamini awe mbunge wa Maswa, hata hivyo, asihofu porojo za CMD kwani wapiga kura wa Maswa sio wajinga wanajua maana ya kuwakilishwa[/QUOTE

unampotosha mwenzako.
 
Shibuda anatumia reverse spychology anajua akifukunzwa heshima yake itaisha kabisa ataonekana mwanaume malaya wa kisiasa,sasa anatumia maneno ya vitisho,kashfa na matusi lakini hajiudhuru kuondokana na chama cha mlenda ha ha huyu hana jipya huyo kuropoka tuu
 
Shibuda, CDM si mbowe, slaa na zitto tu, CDM ni zaidi ya unavyoijua nafikiri ulidandia tren kwa mbele, CDM ni taasisi yenye misingi imara.

na ni wengi tu wanafikiri issue ya wewe mropokaji na ile ya madiwani 3 wenye njaa kule arusha inaweza kuiyumbisha CDM - msahau milele.
 
Kusema ukweli Chadema ilichemsha kumakaribisha huyu mtu kwenye chama...

Binafsi sidhani kama CHADEMA walikosea kukaribisha hili 'KARAI'. Ila maadam zege limeisha wanaweza sasa CHADEMA kulitupa hili karai anytime. Nasema hivi kwa sababu, Shibuda alipata ubunge, na wananchi wengi waliomchagua (kama sio wote) walimpa kura pia mgombea wa urais wa CHADEMA. Sasa kumbuka ruzuku kwa vyama vya siasa huendana na % ya total votes za ubunge & urais. Vile vile kumbuka wasukuma ni wengi (population wise) hivyo kupitia Shibuda, CHADEMA walipata kura na ubunge ambao kimsingi unachangia kiasi fulani kuengezeka kwa financial strength ya chama. Kwa sasa wakimtimua hakuna impact yeyote kwa chama sana sana ni vijimaneno vya huyu Shibuda ambavyo hata waliompa kura hawatasikiliza. Ndio maana namfananisha Shibuda na karai maana if he thought aliwatumia CHADEMA naye akumbuke CHADEMA nao wamemtumia vilivyo and he is not of any use kwa sasa.

Na nina hakika uchaguzi ukirudiwa leo jimboni kwake Shibuda kama hakupitia CHADEMA hawezi kupita. They only option kwa Shibuda kama anataka kuwa bungeni ni CHADEMA au ateuliwe na Rais but he will never win kupitia chama kingine chochote. Tatizo la la huyu bwana anafikiri bado anaweza kufanya umamluki. Zama hizi za science & technology ni ngumu sana kuendeleza tabia za undumi la kuwili na sasa anakaribia political death kwa sababu hataki kusoma au haelewi akisoma alama za nyakati. Kubwa zaidi, akirudi CCM ataenda kundi gani? la Lowassa, au la Kikwete au la Sitta? He's in big trouble!

As for ARUSHA, ni kweli huyu CCM-clerk alienda Arusha. Sijui kama ana familia Shibuda maana mwanaume mzima kuwa kibaraka inatia aibu kweli!

CHADEMA jipangeni kwa uchaguzi, mtimueni huyu. Kelele zake ni sawa na mwendawazimu. don't mind him oooooo!
 
Chadema wanamuogopa Shibuda kwa kuwa wanahofia nyadhifa zao katika chama zilizokaa kikabila na kikanda. Shibuda ni zaidi yao wote kwa siasa, hawamuwezi.
Mbona CCM walimtimua kama hapo red ni ukweli??
 
Chadema wanamuogopa Shibuda kwa kuwa wanahofia nyadhifa zao katika chama zilizokaa kikabila na kikanda. Shibuda ni zaidi yao wote kwa siasa, hawamuwezi.
Shimbunda sijui asahibuda ni nani kwani, si kaja kakuta chama huyo alichegama mvua sasa anaona kumekucha anatafuta namna ya kusepa. Hatuitaji vilaza kama anaona CDM hapamfai njia nyeupe, asituletee mifarakano huyo mwanasiasa uchwara!!!!!!!!!! Mtu amebebwa ametunzwa shukurani yake ni kunyea kambi!!!!!!!!!
 
Nakumbuka wakati wa uchaguzi mwaka jana Chadema ilionywa na baadhi ya watu humu kuhusu kuchukua mabaki ya vyama vingine. Kama kawaida wale mashabiki ambao hawaangalii mbele wa kureason wakatetea. Kuna baadhi ya members walionya specifically kuhusu Shibuda lakini wale fuata upepo wakamuita Shibuda "kamanda", "mpiganaji", "mwanamapinduzi" nk. Leo hii watu hao hao wamemgeuka kitu kinacho thibitisha kwamba humu ndani kuna wengi tu ni bendera fuata upepo na hawana uwezo wa kupingana na wengi ao uwezo wa kufikiria wenyewe.

Anyway ishu ya Shibuda Chadema ilijikoroga yenyewe. Sasa tuone watakavyo deal na hii ishu. Ila ukweli ni kwamba kuna watu walisema Shibuda ni shushushu na kama anatishia kwamba wakimfukuza Chadema watakiona inawezekana kasha tengeneza profile kubwa kuhusu Chadema tayari kulitumia dhidi yao.

Msikurupuke, nyie mtengenezee mazingira ya kukiuka sera ambazo sheria yake ni kufukuzwa. Ataingia kwenye mtego tu. Then mnamaliza kazi
 
hujasikia jana lema akisema>>>kama siku moja tukibahatika kuchukua dola mambo yatakuwa ivi ivi........akichangia bajeti ya maendeleo ya jamii.

yaani kuchukua dola ni kubahatika?????
 
Msikurupuke, nyie mtengenezee mazingira ya kukiuka sera ambazo sheria yake ni kufukuzwa. Ataingia kwenye mtego tu. Then mnamaliza kazi

relax mkuu, wewe lini ulisikia CDM huwa inakurupuka? - nyie tuongee mambo ya umeme maana taifa lipo gizani - huyu mropokaji asitupotezee muda wetu.
 
Back
Top Bottom